Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Tumeshuhudia mwaka jana, viongozi fulani wazito tu wa CCM baada ya kukosa nafasi ya kugombea kwa tiketi ya CCM wakajiunga na CDM. Je, ukweli ni kwamba walifuata itikadi ama fursa ya kupata ubunge wakiamini kuwa wanakubalika na jamii? CCM kuwakataa ilikuwa ni kuvua magamba ya wanzo yaliyovaliwa na CDM (mf. Shibuda). Sasa kuna magamba ya pili yanavuliwa, je, haya nayo si yatavaliwa na CDM? Kwa maana hakuna pengine pa kwenda..........
 
- Kumshitaki kwa umma kiongozi aliyepumzika na siasa ni dalili za siasa za Desparation za kutaka kumuingiza kila mtu kwenye siasa za kuropoka ropoka, ili kujipatia attention kwa mshitaki, sasa kama unaijua vizuri siasa unajua kwamba huyu sasa amefika mwisho hana agenda tena sasa anajaribu kuanzisha agenda isiyokuwepo ili kuendelea na zile 15 minutes of fame ambazo sio siri kwamba sasa zimefika mwisho. Kwa mwendo huu mpya wa Slaa hata neno fisadi linakosa maana kabisa mkuu, ingawa ni hadithi nzuri kwa media, elewa kwamba wananchi sio wajinga na hizi siasa za kulipua mabomu hata kama hayapo haziwezi kuisaidia Chadema kwenda mbele.

- Well kwa mwendo huu wa Slaa ni kwamba ni fair kila mwanasiasa kukurupuka na kuanza maneno ya kizushi, ili mradi yashile the media attention, mimi mkuu ninasema hivi Tanzania hatuna sheria ya Political finance Campaign kwa hiyo ni sawa kwa chama cha siasa kupokea pesa toka mahali popote pale, however kama unamshitaki kiongozi yoyote kwa wizi wa benki basi ni lazima uwe na karatasi linaloonyesha kwamba amesaini na zile pesa kuchukuliwa, lakini ukisema chama cha yule kiongozi kilipewa hela ndio hapo sasa unakuja mtego wa Political Campaign Finance Laws ambazo bongo hatuna, kwa sababu huwezi with a straight face kusema vyama vyote vya siasa Tanzania vinapokea hela safi kisheria na ukichunguza ukagundua ukweli wa uchafu wake basi viongozi wote wa kile chama ni mafisadi, please Mkuu chadema wanapewa hela na ile Charity ya Tony Blair ambayo pia ndio wanaompa hela Tshangarai kule Zimbabwe, sasa kweli unasema ukizichunguza hizo hela zitakuwa na usafi 100%? Na zisipokuwa basi viongozi wote wa Chadema sio wasafi? Pleasee!

- Malecela atakuwa mwendawazimu kwenda kumjibu Slaa anywhere kwa sababu atakuwa anajiingiza kwenye mtego wa Slaa wa kujitafutia umaarufu kwa nguvu hata kama time imekwisha, Malecela sio kiongozi wa taifa tena hahitaji kwenda popote, isipokuwa ni haki yangu kujadili anything humu JF kama mwananchi wa Tanzania, na ndicho ninachofanya hayo mengine ni yako mkuu!
- Ha! ha! hapa imenibidi nicheke kwamba kwa vile Chadema hawajaenda mahakamani basi sio lazima na Malecela asiende mahakamani, hilo limenivunja mbavu mkuu na sina la kuongeza zaidi!

William @ NYC, USA.

The problem ni kwamba wewe unaonekana ni mmoja wa wale mlionufaika na wizi wa familia zenu. I don't think kama unaamini maneno unayasema au ni kujikosha kwenye JF, by the way you have the right diffend yourself. Unachodai ni ushahidi ambao familia zenu mmekalia. Tangu lini nyie mnajua kitu kinachoitwa "Transparency"? Hata ukimuuliza mtoto wa Gadaffi leo kwamba baba yako ni dikteta off course ataruka na kutoa maneno lakini akienda kulala na kutafakari wanajua kweli baba ni mbovu. Kitu mnataka kutueleza watanzania kwamba nyie ccm na familia zenu mmekaa hii miaka yote hamkujua umuhimu wa campaign finance laws au umuhimu wa kuwa na Strong Independent Judicial System in Tanzanis? Kikwete, Mwinyi au Mkapa na hata Malecela hawajawahi kupanda pipa na kwenda nje kuona democrasia zinaendeshwa vipi au hata kuuliza maswali kwenye vikao kwamba how do your country get this far. Majority ya viongozi wa ccm tangu miaka ya nyuma wamepata exposure ya ajabu na benefits nje ya nchi na wengi wao wamesoma nje na kufanya kazi nje. What happened to the education, knowledge and skills? Its useless if you thinking about it mhhhhh. Tafadhari usije na excuse yeyote ya kusema kwamba Malecela na wengine walifanya kazi au Kikwete ni mtu mzuri kati ya kundi la magangsters wote NEC.

Dr Slaa na viongozi wengine wa upinzani wanatumia hizi platforms kuwajulisha wananchi jinsi gani tumeumizwa na jinsi gani tunaendelea kuumizwa mpaka "Katiba" yenye mamlaka kwa Watanzania itengenezwe na kupitishwa na Watanzania wenyewe. Huko unaishi nje ya nchi lakini kilichokupeleka huko sio matatizo ya Tanzania yalioletwa na mafisadi ccm sio? Kama maisha na uchumi ni mzuri Tanzania si ungekuwa na kazi maybe private sector au kujiajiri mwenyewe Tanzania. Kuna upungufu mwingi katika opinions zako na unahaki ya opinions zako ila usimlaumu Dr Slaa kama kiongozi wetu anaziumiza familia zenu. Things are changing in Tanzania nyie pia mngeweza ku-stand up mbele ya familia zenu na kuwa against all crimes na violations zinazoendelea Tanzania chini ya hiki chama kinachokufa ccm, you are wellcome to join the revolution. Chadema wanatumia hii nafasi kuwafahamisha na ku-mobilize wananchi kufuatilia kila jambo na kama uchaguzi mlivyoiba mtataka tuwape ushahidi sio? Ushahidi utapatikana tu pale "Katiba" na "Tume huru ya uchaguzi" itakapopitishwa na wananchi sio na dikteta kikwete au NEC.
By the way Hujafahamu Impact ya Chadema, Aliesimamisha Katiba bungeni ni nani? Aliwaelimisha Watanzania Kupinga hii mipango ya Katiba ya ccm ni nani? Aliua ccm dodoma ni nani? I think you are intelligent enough to figure out the facts. Let me leave you with this news from Egypt.

"Egypt’s ex-president Hosni Mubarak, detained pending an investigation into corruption and state violence, may be jailed or hanged if found guilty of ordering the killing of demonstrators, state media said today. The state-owned newspaper Al-Ahram quoted the head of Cairo’s appeals court, Zakaria Shalash, as saying that Mubarak may face execution after a trial he expected to last at least a year."
Daily Nation: - Africa |Mubarak

"Tunisian authorities have prepared 18 legal cases against former president Zine El Abidine
Ben Ali, including "voluntary manslaughter" and "drug trafficking", the state TAP news agency reported."
Tunisia files cases against Ben Ali - Africa - Al Jazeera English

Sasa Utueleze Nani Alitabiri Haya Egypt na Tunisia? Tukiingia Serikalini Chadema Tunauhakika Tutawakea Wote Mafisadi Jela, Hii Ndio Hofe Yenu
 
Tarehe 17 April watu walielekeza masikio yao mkoani Tabora wakisubiri list ya mafisadi itakoyo somwa na Dr Slaa(Padri Mstaafu) ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema anae lipwa 12 Milioni kwa Mwezi. Padri Mstaafu pasipo kujua nyakati akamtaja Dr Magufuli kuwa ni fisadi! Tofauti na matarajio yake na CDM mwitikio wa jamii juu ya Magufuli nae ajulikane kama Fisadi imekua ngumu kuingia akilini kwa Watanzania! Kinacho zungumzwa na wadadisi wa mambo ni mbinu ya Dr Slaa kuanza kumchafua Magufuli kwani ni Mwanasiasa anaekubalika kwa sasa na Watanzania! Dr Slaa siasa inatakiwa kujipanga zaidi kwa hili la Magufuli haliingii akilini kwa Watanzania!

Jaribu basi ku-edit post yako na uondoe neno 'padri mstaafu' maana halina uhusiano na mada yako. Hoja inaanza kunuka udini mapema, kwani hata huyo Magufuli unayemshabikia anaenda kutubu kwa mapadri hao hao.
 
kwani huyu jamaa humjui? huyu ndio majimshindo aka malaria sugu watu washamzoea , sijui nani anamlipa kuja kuongea upuuzi hapa
 
Tarehe 17 April watu walielekeza masikio yao mkoani Tabora wakisubiri list ya mafisadi itakoyo somwa na Dr Slaa(Padri Mstaafu) ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema anae lipwa 12 Milioni kwa Mwezi. Padri Mstaafu pasipo kujua nyakati akamtaja Dr Magufuli kuwa ni fisadi! Tofauti na matarajio yake na CDM mwitikio wa jamii juu ya Magufuli nae ajulikane kama Fisadi imekua ngumu kuingia akilini kwa Watanzania! Kinacho zungumzwa na wadadisi wa mambo ni mbinu ya Dr Slaa kuanza kumchafua Magufuli kwani ni Mwanasiasa anaekubalika kwa sasa na Watanzania! Dr Slaa siasa inatakiwa kujipanga zaidi kwa hili la Magufuli haliingii akilini kwa Watanzania!

Hata ukishinda siku nzima una-post na kuandika utumbo kama jitihada zenu mpya za kutoka dodoma, watanzania sio wajinga kama bibi na babu yangu. Wanajua upuuzi wenu. Kinachoonekana wazi mnamwogopa sana Dr Slaa. Dr Slaa is our president now.
 
Tarehe 17 April watu walielekeza masikio yao mkoani Tabora wakisubiri list ya mafisadi itakoyo somwa na Dr Slaa(Padri Mstaafu) ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema anae lipwa 12 Milioni kwa Mwezi. Padri Mstaafu pasipo kujua nyakati akamtaja Dr Magufuli kuwa ni fisadi! Tofauti na matarajio yake na CDM mwitikio wa jamii juu ya Magufuli nae ajulikane kama Fisadi imekua ngumu kuingia akilini kwa Watanzania! Kinacho zungumzwa na wadadisi wa mambo ni mbinu ya Dr Slaa kuanza kumchafua Magufuli kwani ni Mwanasiasa anaekubalika kwa sasa na Watanzania! Dr Slaa siasa inatakiwa kujipanga zaidi kwa hili la Magufuli haliingii akilini kwa Watanzania!

---------------------------hapa umeandika pumba tupu!!!
 
Thanx God ukombozi umefika hadi huku kwetu Kaliua. Kimsingi tumechoshwa na ubabe wa Kapuya na mwanae Baraka Kapuya anayejiita "full boss". Wamekuwa wakiihandle Kaliua kama miungu watu, hata kwenye kampeni za mwaka jana yeyote aliyethubutu kuuliza maswali ya kumbana Kapuya alifutwa palepale alipo na kupata kichapo kutoka kwa mabaunsa.
Tuliitumainia CUF kama our future saviour but the way thing goes baada ya ndoa ya CUF na CCM, tulijua hatuna mkombozi tena. But thanx god kwa kuileta CDM coz kutokana na commitment yao tunayoiona we hope dat enzi ya Kapuya na CCM imefikia ukingoni.
THANX CDM, THANX Dr. SLAA (PhD) AND YOUR TEAM AND MAY GOD BLESS YOU.
 
Kafiribangi,

Ni dakika chache tu nimeingia kutoka Kaliua na Urambo. Tumekuwa na mikutano mitatu ya hadhara, tumefungua ofisi na matawi ya Chama. Hivyo si kweli kuwa Chadema inalipiza kisasi kwa CCM.

1)Kwanza inaelekea wengi hawafahamu malengo ya mikutano ya vijijini, na hasa kwa kuwa wanapata magazeti, wanatazama TV wanaamini Watanzania wote wanafanana. Lengo la Chadema katika hatua hii siyo kuwaambia CCM mbinu ya kuleta maendeleo wala kuwapa mikakati ya maendeleo. Ikumbukwe kuwa Chadema haikusanyi kodi yeyote ya wananchi na hivyo katika kipindi katika ya Uchaguzi kazi ya Chama cha siasa ni kujijenga kwa uchaguzi ujao,kukosoa Serikali iliyoko madarakani katika sera,Ilani na utekelezaji wa sera na ilani hiyo,kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuelewa udhaifu wa Chama hicho Tawala ili katika uchaguzi ujao tuiondoe. Hii ndiyo kazi yetu ya kikatiba. Chama cha siasa chenye kujua wajibu wake hakiwezi kuwa wasindikizaji tu. Sisi si washauri wa Serikali kwa kuipatia mbinu za kuongoza au mikakati ya kuongza na kuleta maendeleo. Kama yuko anayefikiri hivyo ni vema arejea vizuri majukumu ya vyama vya siasa.

2)Sisi tunaofika vizuri ndio tuko kwenye mazingira ya kutafsiri nini kizungumzwe katika kijiji fulani tofauti na kingine. Hii inatokana na uelewa unaotofautiana. Katika kijiji kingine hata ajenda iliyokwisha kuzoeleka kwa watu wa vijijini kama Listi of Shame iliyotolewa 2007 inabidi itolewe upya kwa kuwa wananchi hawajawahi kujua ni kwanini nchi yeny utajiri mkubwa kama TZ inaweza kuwa maskini, au inakuwaje wako wanaoogelea katika utajiri mkubwa wakati wao hawana zahanati, maji, wanakula mlo mmoja bila kujua kuwa inatokana na rasilimali nyingi kutafunwa na mafisadi. Najua wako ambao wanaumia kwa sababu zao kila tunapowataja mafisadi, lakini katika mazingira kama hayo Mwanasiasa makini ni yule anayejua mahitaji ya wananchi wake. Hivyo, Msishangae wana JF kuona tunayarudia yale yale. Mtakuwa wabinafsi iwapo hamtapenda watanzania wenzenu wayajue mnayoyajua nyie.

3) WanaJF wako katika jamvihili wanaoishi dunia yao wenyewe, au kwa kutaka au kwa bahati mbaya. Mathalan, nimestuka sana, kama niliyoelezwa Kaliua ni ya kweli Tanzania kuna ndugu zetu wanaishi bado Tanganyika ni si mwaka 47. Kaliua mtu mmoja aliyetajwa kama Baraka,mtoto wa Kapuya amekuwa tishio kwa wana Kaliua wote.Wanakaliua wanapigwa,wanachomewa nyumba, wanauawa na wakilalamika polisi nao inafyata kutokana baba Baraka kuwa tishio. Katika mazingira kama hayo usifikirie utazungumzia maendeleo zaidi ya kuwajengea ujasiri,mbinu za ukombozi na hata kuwafafanulia ufisadi mkubwa katika Jimbo kama hilo. Haiingii akilini mwa yeyote, kwa umaskini mkubwa tulioona Kaliua, na bado 72 Millioni zimetafunwa kwa jina la au kupitia kasma ya Mishahara (mishahara hewa, mishahara kulipwa kwa watumishi waliofariki, waliofukuzewa watoro n.k.) Kwa bahati mbaya hata tunapokuwa na Waandishi wa habari katika ziara mazingira na hotuba kama hizo hazipati nafasi kwa sababu yeyote ile, au hata kwa vile tu mwandishi anachagua anayotaka yeye.

Hali inatisha, ndiyo maana Chadema tumedhamiria kutoa elimu katika vijiji mbalimbali kati ya sasa na 2015. Wanaoumia na hiyo waumie tu. Wananchi wengi vijijini ndicho wanachohitaji kwa CCM siku mmoja haitawapa elimu hiyo. Wilaya/Jimbo Maskini kama Kaliua haingii akilini inapotokea Halmashauri inashindwa kutumia Tshs 659,697 Millioni katika mwaka wa Fedha, na hatimaye isionekane katika B/F kwa kuwa mfumo wa uhasibu wa almashauri hauna utaratibu huo. Matokeo yake hakuna anayejua fedha hizo zimeenda wapi. Kama Madfiwani wa Kamati ya Fedha hawajapangia matumizi ni nani anapangia matumizi. Kama Chadema hatutakemea ufisadi wa namna hiyo nani akemee. Ikumbukwe hii ni wilaya iliyokuwa hadi mwaka wa ukaguzi yaani Juni 30, 2010, mawaziri wawili na Spika wa Bunge.

Ndugu zangu wengine kwenye jamvi hili wanazungumza tu nadharia bila kujua hali halisi ya nchi yetu, au kwa makusudi tu wanataka kutuondoa kwenye ajenda zetu. Hatoki mtu hapa "ngo"(kwa lugha ya kina Kombani. Atakuwa mwanasiasa wa ajabu ambaye anahutubia mbele ya Ofisi ya "Spika" iliyojengwa Urambo, wakati Urambo haina Bunge na hivyo haina Spika. Hii ni ofisi iliyojengwa kwa milioni zaidi ya 300 na kuwekewa fenicha ya zaidi ya 170 Millioni, katika jimbo ambalo hakuna zahanati, vituo vya afya n.k. Mwanasiasa atakayeacha kutaja Ufisadi huu kwa kuwa wanaJamvi wachache wadhani wamechoka kusikia habari ya ufisadi atakuwa siyo mwanasiasa Makini. Kafiribigiri,naamini nimeeleweka.

Tushuke chini, tusidhani maisha ndani ya jamvi hili ndivyo yalivyo vijijini. Hata kama sisi tuna maisha mazuri, tuwafikirie wazazi wetu,shangazi zetu,wajomba zetu ambao bado wanaishi nyumba za tembe na majani, ambao mlo wa siku ni shida, ambao wameacha kula nyama kwa kuwa bei haishikiki nakadhalika. Hizi ni ajenda za kudumu na ndiyo namna ya kuondoa umaskini wa wananchi wetu kwa kuikaba serikali ngazio zote iache ufisadi na ielekeze rasilimali zote kuwahudumia wananchi badala ya kujijengea mahekalu, kutembelea mashangingi ya millioni 500. Hii ndiyo ajenda,inaewzerkana wewe huipendi lakini vijijini ndiyo mambo yenye "mshiko"

someni hii kitu dr aliyokuja nayo hapa jamvini
 
Nape: Orodha ya mafisadi ni mchezo wa kuigiza Send to a friend
Sunday, 17 April 2011 21:08

Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye

Ramadhan Semtawa, Dar na Salma Said, Zanzibar
SIKU moja baada ya Chadema kutangaza orodha mpya ya watu, kinachodai kuwa ni mafisadi ndani ya CCM, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye amesema orodha hiyo ni sawa na mchezo wa kuigiza.

CCM katika vikao vyake vya Nec na Kamati Kuu vilivyofanyika Dodoma wiki iliyopita, kilifanya mageuzi makubwa ya uongozi na maazimio kadhaa yenye lengo la kuwaondoa wote wenye tuhuma nzito za ufisadi na ukosefu wa maadili katika kile inachokiita kujivua gamba. Lakini juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alirusha kombora jingine akiongeza orodha ya watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho.

Akizungumza kabla na baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Zanzibar, Nape alisema; "Huo ni sawa na mchezo wa kuigiza. Hatua hiyo haina lolote katika mchakato wa kung'oa mafisadi ndani ya chama chetu tena nawaambia wanachofanya ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli."

"Bahati nzuri tumeshajua mipango yao yote ya kujaribu kuendesha kampeni ya kuchafua watu wasafi ndani ya chama akiwamo Rais na familia yake.""Tunajua wamepanga kutumia baadhi ya vyama

vya siasa vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi. Kwa hiyo hata hiyo orodha mpya tunajua ni sehemu ya mchezo huo."

Nape alisema mkakati huo wa kuwachafua makada wa CCM na Rais Kikwete hautafanikiwa akisema kila kitu kiko wazi."Ni mchezo wa kuchafua watu tu lakini nawaambia mkakati huo hautaweza kukigharimu chama wala kukifanya kiachane na mchakato wa kuwashughulikia mafisadi ndani ya CCM ," alisisitiza Nape.

Mkutano wa hadhara
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kisonge, Mjumbe huyo wa Nec ya CCM alisema, uamuzi uliochukuliwa na chama hicho wa kujivua gamba ni mgumu na ulihitaji ujasiri mkubwa.

Alisema uamuzi huo ni sawa na mwenge ambao umewashwa Dodoma na kwamba utazunguka nchi nzima na kumulika maeneo yote ili kurejesha imani ya wananchi na wanaCCM ambao kwa muda mrefu wamekata tamaa na chama chao ambacho kinazuliwa mambo mengi machafu ikiwamo madai kuwa ni chama cha mafisadi na chama cha matajiri jambo ambalo halina ukweli.

Aliwataka wanachama wa CCM Zanzibar, kurejesha matumaini kwa chama chao huku akisisitiza kwamba uamuzi wake wa kujisafisha, unawalenga wote wenye kukidhoofisha hivyo kuwataka wale wote wenye shutuma wajitose wenyewe kabla hawajatoswa kwani wakichelewa watatoswa kwa lazima ili boti iendelee na safari yake.

"Tunawaambia kabla boti yetu haijaondoka wale wote wanaotuhumiwa ndani ya chama chetu tunataka watoke. Kama hawataki basi tutawatosa kabisa ili sisi tuendelee na safari," alisema Nape.

Akifafanua sababu za kutoa miezi mitatu, kwa wale wote wanaotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa mbalimbali za ufisadi zilizokitia doa chama hicho, Nape alisema lengo la uamuzi huo ni kuwapa nafasi ya kujitathmini wenyewe.

Alitoa mfano wa hatua hiyo kwamba ni ; "Sawa na pweza unapotaka kumla lazima umpige na michanga hivyo miezi hiyo mitatu ni kujisafisha kabla ya kuliwa."

Kwa upande wake, Katibu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Januari Makamba, amesema chama hicho hivi sasa kitaendeshwa kisiasa kwa lengo la kujiimarisha vyema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Alisema hivi sasa chama hicho kimepata wataalamu na wenye kufanya mipango kisomi zaidi kuliko kilivyokuwa mwanzo, hivyo hakuna sababu ya vijana kuvunjika moyo hasa kwa kuzingatia kuwa ndiyo waliopewa majukumu ya kukiendesha.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema moja ya majukumu yake ni kukiunganisha na kukiimarisha chama hicho. Aliwataka wanachama wanaokwenda kwake kupeleka maneno yenye kukijenga na siyo fitina na majungu.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema mabadiliko hayo yana lengo la kukirejesha chama katika mstari lakini akiwataka wananchi kuridhika na uamuzi huo mgumu ambao alisema hakuna chama kingine ambacho kinaweza kuiga mfano huo
 
Hamna tofauti kati ya Samaki la Gufuli na Fisadi la Slaa. Zote ni gimmicks tu (i.e., wote wawili ni Wasanii waliobobea na ma-PhD yao obsolete.)
 
The problem ni kwamba wewe unaonekana ni mmoja wa wale mlionufaika na wizi wa familia zenu. I don't think kama unaamini maneno unayasema au ni kujikosha kwenye JF, by the way you have the right diffend yourself. Unachodai ni ushahidi ambao familia zenu mmekalia. Tangu lini nyie mnajua kitu kinachoitwa "Transparency"? Hata ukimuuliza mtoto wa Gadaffi leo kwamba baba yako ni dikteta off course ataruka na kutoa maneno lakini akienda kulala na kutafakari wanajua kweli baba ni mbovu. Kitu mnataka kutueleza watanzania kwamba nyie ccm na familia zenu mmekaa hii miaka yote hamkujua umuhimu wa campaign finance laws au umuhimu wa kuwa na Strong Independent Judicial System in Tanzanis? Kikwete, Mwinyi au Mkapa na hata Malecela hawajawahi kupanda pipa na kwenda nje kuona democrasia zinaendeshwa vipi au hata kuuliza maswali kwenye vikao kwamba how do your country get this far. Majority ya viongozi wa ccm tangu miaka ya nyuma wamepata exposure ya ajabu na benefits nje ya nchi na wengi wao wamesoma nje na kufanya kazi nje. What happened to the education, knowledge and skills? Its useless if you thinking about it mhhhhh. Tafadhari usije na excuse yeyote ya kusema kwamba Malecela na wengine walifanya kazi au Kikwete ni mtu mzuri kati ya kundi la magangsters wote NEC.

Dr Slaa na viongozi wengine wa upinzani wanatumia hizi platforms kuwajulisha wananchi jinsi gani tumeumizwa na jinsi gani tunaendelea kuumizwa mpaka "Katiba" yenye mamlaka kwa Watanzania itengenezwe na kupitishwa na Watanzania wenyewe. Huko unaishi nje ya nchi lakini kilichokupeleka huko sio matatizo ya Tanzania yalioletwa na mafisadi ccm sio? Kama maisha na uchumi ni mzuri Tanzania si ungekuwa na kazi maybe private sector au kujiajiri mwenyewe Tanzania. Kuna upungufu mwingi katika opinions zako na unahaki ya opinions zako ila usimlaumu Dr Slaa kama kiongozi wetu anaziumiza familia zenu. Things are changing in Tanzania nyie pia mngeweza ku-stand up mbele ya familia zenu na kuwa against all crimes na violations zinazoendelea Tanzania chini ya hiki chama kinachokufa ccm, you are wellcome to join the revolution. Chadema wanatumia hii nafasi kuwafahamisha na ku-mobilize wananchi kufuatilia kila jambo na kama uchaguzi mlivyoiba mtataka tuwape ushahidi sio? Ushahidi utapatikana tu pale "Katiba" na "Tume huru ya uchaguzi" itakapopitishwa na wananchi sio na dikteta kikwete au NEC.
By the way Hujafahamu Impact ya Chadema, Aliesimamisha Katiba bungeni ni nani? Aliwaelimisha Watanzania Kupinga hii mipango ya Katiba ya ccm ni nani? Aliua ccm dodoma ni nani? I think you are intelligent enough to figure out the facts. Let me leave you with this news from Egypt.

"Egypt's ex-president Hosni Mubarak, detained pending an investigation into corruption and state violence, may be jailed or hanged if found guilty of ordering the killing of demonstrators, state media said today. The state-owned newspaper Al-Ahram quoted the head of Cairo's appeals court, Zakaria Shalash, as saying that Mubarak may face execution after a trial he expected to last at least a year."
Daily Nation: - Africa |Mubarak

"Tunisian authorities have prepared 18 legal cases against former president Zine El Abidine
Ben Ali, including "voluntary manslaughter" and "drug trafficking", the state TAP news agency reported."
Tunisia files cases against Ben Ali - Africa - Al Jazeera English

Sasa Utueleze Nani Alitabiri Haya Egypt na Tunisia? Tukiingia Serikalini Chadema Tunauhakika Tutawakea Wote Mafisadi Jela, Hii Ndio Hofe Yenu

- Well, I guess huu wako ni ushahidi mzito sana kwamba Malecela anahusika na EPA, sawa sawa mkuu kwa kweli una ushahidi mzito sana!

William @ NYC, USA.
 
Wananchi wengi hatujasahau kwamba Mwalimu Nyerere alitunga Kitabu kumsema Waziri Mkuu Malecela na Raisi Mwinyi,wakati ule walipoachia Ikulu ikawa sebure ya wafanya biashara haswa wenye asili ya Kihindi,lakini vilevile tunajua Mzee Male sio Fisadi kihivyo,Lakini alikuwa Makamu mwnyekiti wa CCM kwa kipindi cha miaka kumi kwa hiyo alijua michoro yote ya uporaji wa fedha
za EPA kutokana na nafasi yake ni vizuri wananchi wakajua kwamba na yeye akisaidia wengine kuwa mafisadi hata kama yeye si Fisadi

Kutoa mabomu kumesaidia kwa kiwango fulani kwa kutafuta njia za kujikwamua utasemaje Mabomu ya Dr Slaa ni sawa na Mrema ,wakati CCM munaimba wimbo huo huo wakuwapa siku 90 mafisadi waondoke kwenye chama,Kama sio mabomu imekuwaje sekretariati ikalazimishwa kujiuzuru,imetokea wapi mivugano kati ya waliotajwa mafisadi na hao wanaojiita masafisha ufisadi,kampeni zimeanza TBC ya kupiga mapambio ya kujivua magamba ili wananchi tuone kwamba CCM wanapiga vita ya Mafisadi nadhani uko kwenye denial ni jambo la kawaida hakuna mtoto atakayekubali mzazi wake awe na kashfa

- Mkuu heshima sana maana huu ni ushahidi mzito sana kwamba Malecela anahusika na EPA, keep it up mkuu!

William @ NYC, USA.
 
Tarehe 17 April watu walielekeza masikio yao mkoani Tabora wakisubiri list ya mafisadi itakoyo somwa na Dr Slaa(Padri Mstaafu) ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema anae lipwa 12 Milioni kwa Mwezi. Padri Mstaafu pasipo kujua nyakati akamtaja Dr Magufuli kuwa ni fisadi! Tofauti na matarajio yake na CDM mwitikio wa jamii juu ya Magufuli nae ajulikane kama Fisadi imekua ngumu kuingia akilini kwa Watanzania! Kinacho zungumzwa na wadadisi wa mambo ni mbinu ya Dr Slaa kuanza kumchafua Magufuli kwani ni Mwanasiasa anaekubalika kwa sasa na Watanzania! Dr Slaa siasa inatakiwa kujipanga zaidi kwa hili la Magufuli haliingii akilini kwa Watanzania!

Kutumia lugha chafu hakuwezi kufanya hoja yako ikawa na nguvu.It's the content that counts.

Tangu lini umekuwa msemaji wa Watanzania?Tatizo lenu mkishatoka kwenye vinywaji haramu mnaanza kujifanya wawakilishi wa umma,just because hapo kwa mama muuza ulisikilizwa kwa makini.Kama kichwa chako ni tofali unategemea hoja gani itaingia akilini mwako?Hoja ya ufisadi wa Magufuli imekuwa ngumu kuingia akilini mwa Watanzania wapi hao?Simply kwa vile imekuwa vigumu kuingia akilini mwako-kwa sababu zilizo wazi kabisa-doesnt mean haiwezi kuingia akilini mwa wenye akili timamu.

Ni upumbavu kumlaumu Dkt Slaa kuwa anamchafua Magufuli ilhali wewe mwenyewe unatumia lugha ya kashfa dhidi ya Dkt Slaa.Hii sio double standard bali mtindio wa ubongo.Hivi sio huyo Magufuli unayedai anakubalika kwa Watanzania aliyeumbuliwa na Kikwete hadharani kwa boboma bomoa zake?Mbona hukumlaumu Kikwete kwa hilo?

Mmeishiwa na hoja hata za kuokoteza,sasa mnakurupuka na lolote lile linalowaijia akilini.Sasa akili yenyewe nayo inapokuwa na mapungufu ndio inakuwa shida kweli kweli.MMEROGWA?
 
- Well, I guess huu wako ni ushahidi mzito sana kwamba Malecela anahusika na EPA, sawa sawa mkuu kwa kweli una ushahidi mzito sana!

William @ NYC, USA.

- Mkuu heshima sana maana huu ni ushahidi mzito sana kwamba Malecela anahusika na EPA, keep it up mkuu!

William @ NYC, USA.

Unahitaji ushahidi gani zaidi ya Mzee Malecela kutajwa hadharani kuwa ni fisadi?Mbona ulimpongeza Kikwete kwa maamuzi yake ya kuwatimua mafisadi (japo Kikwete hakuweka ushahidi hadharani) lakini linapokuja suala la babayako unataka ushahidi?Rejea ile post yako kwenye facebook wall yako kuhusu "giving credit where it's due..."

Nimejaribu kukushauri umshauri mzee wako aende mahakamani lakini nadhani umeona ushauri huo hauna maana.Sasa badala ya kutetea kwa maneno matupu kuwa Malecela sio fisadi,tupe ushahidi kuwa sio fisadi.Sie kama jamii ushahidi wetu ni kauli ya Dkt Slaa/Chadema.Wewe je?

Halafu nahofia utetezi kwa baba yako unaweza kupelekea hasira za wanyonge waliofisadiwa na genge la akina MALECELA.Yaleyale ya Saif Gaddafi kuwakashifu wanaokandamizwa na mfumo dhalimu.Watu wameibiwa kisha watoto wa majambazi hao wanaleta zao za kuleta!!!!!
 
Hamna tofauti kati ya Samaki la Gufuli na Fisadi la Slaa. Zote ni gimmicks tu (i.e., wote wawili ni Wasanii waliobobea na ma-PhD yao obsolete.)

Sijui JF isingekuwa hewani viumbe kama wewe mngeondolea wapi frustration zenu binafsi
 
HTML:
[quote="Mlalahoi, post: 1869091"]Unahitaji ushahidi gani zaidi ya Mzee Malecela kutajwa hadharani kuwa ni fisadi?Mbona ulimpongeza Kikwete kwa maamuzi yake ya kuwatimua mafisadi (japo Kikwete hakuweka ushahidi hadharani) lakini linapokuja suala la babayako unataka ushahidi?Rejea ile post yako kwenye facebook wall yako kuhusu "giving credit where it's due..."
- Ya Facebook yabaki kule kule hapa ya hapa, CCM wametimua mafisadi sio JK, unaposema Malecela anahusika na EPA, unatakiwa kuonyesha evidence za makaratasi aliyoyasaini na kuwezesha kuchotwa kwa hela za wananchi benki, kama huna huo ushahidi na wewe unakua fisadi kwa kusema uongo na kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao ni hewa! JF haiwezi kugeuka kijiwe cha walevi mkuu kwa sababu amesema Slaa tu hapana, Sophia Simba hana ushahidi kwamba Chadema wanapewa hela kutoka nje so is Slaa hana ushahidi wa Malecela au Mangula kuhusika na EPA msishushe hadhi ya Forums kwa sababu amesema Slaa tu! ha! ha! ha!

HTML:
Nimejaribu kukushauri umshauri mzee wako aende mahakamani lakini nadhani umeona ushauri huo hauna maana.Sasa badala ya kutetea kwa maneno matupu kuwa Malecela sio fisadi,tupe ushahidi kuwa sio fisadi.Sie kama jamii ushahidi wetu ni kauli ya Dkt Slaa/Chadema.Wewe je?
- Ha! ha! ha! ha! sikutegemea hata siku moja unaweza kushuka this low duh yote nini amesema Slaa basi zidumu! ha! ha! ha!

HTML:
Halafu nahofia utetezi kwa baba yako unaweza kupelekea hasira za wanyonge waliofisadiwa na genge la akina MALECELA.Yaleyale ya Saif Gaddafi kuwakashifu wanaokandamizwa na mfumo dhalimu.Watu wameibiwa kisha watoto wa majambazi hao wanaleta zao za kuleta!!!!!
- Mkuu ninakushuru sana na ushahidi wako wa EPA kuhusika na Malecela, ukweli ni kwamba una ushahidi mzito sana kuliko hata Slaa mwenyewe, UBARIKIWE SANA BRO!

William @ NYC, USA
 
Sijui JF isingekuwa hewani viumbe kama wewe mngeondolea wapi frustration zenu binafsi

Aloo. Mimi nilikuwa hewani kabla hata web browsers hazijagunduliwa: wakati huo Mosaic, Netscape Navigator 1.0 na Internet Explorer 1.0 zilikuwa bado hazijazaliwa. I've been through 'em all since then, kuanzia TANZANET hadi JF and everything in between kama YA, DARHOTBOARDS, BSCTIMES.COM, TANZATL.ORG, you name it. What's more: huyo demi-God wako Slaa pia namfahamu vizuri, at a more or less personal level, kabla hajaenda Italia kusomea madigrii yake ya Sheria za Kanisa, na hata baada ya kurudi Bongo: prior to and after he became Secretary General of TEC. So basically, you got nothing to tell me dude!
 
Nyangomboli,

Ndiyo maana kwa watu wanaoangalia tu haraka haraka si rahisi kuelewa na wanavutika na "kuvua Gamba". The Ufisadi issue is much deeper than most people understand. Ukisema hawa wazere hawana kitu ni "safi" basi ni vema mkatueleza Vijinoti "messages" za hawa wazee zilizotoa fedha kwa Balali zilikuwa za nini. Kama mtu haelewi kitu si vema kujitumbukiza kwa utetezi. Kumbukeni nilishaambiwa "nitapelekwa mhakamani" hjadi leo hakuna badala yake wao ndio wako mahakamani japo ni cosmetic tu.

Niliambiwa "nisali" nina dakika chache za kuishi. Nadunda hadi leo lakini mastokeo wao wenyewe wamepeana siku 90 za kujiondoa kwenye uongozi. Ndugu zangu wengi wanajadili kwa ushabiki. Kama mtu haelewi mtuachie tunaoelewa undani na tulio na ushahidi wa kina. Wala usituambie tuweke hapa, kuna mahali tukitakiwa tutapeleka lakini si jamvini na sababu zinajulikana. Ila ieleweke,

i) Wenzetu wanavua Gamba ndani ya CCM. Lakini fedha zilizoibiwa ni za CCM hivyo siyo issue ya CCM tu. Consequences za kuvua Gamba lazima ziende nje ya CCM i.e. kama ni mbunge ajivue, kama ni kiongozi serikalini ajivue.

ii) Watanzania ndio tulioibiwa, hivyo mtu asiojaribu kamwe kutufunga mdomo. Tulianzisha ngoma hii tutaicheza hadi mwisho, nchi itakaporudi kwenye njia sahihi. Wanaoogopa mchezo huu wakae mbali. Lakini Watanzania wasio na hofu na wenye uchungu na nchi yetu kamwe hatutanyamazishwa na yeyote yule, wala na kitendo cha CCM kujivua Gamba.

Asilani, wamekubali sasa wenyewe wanaimba "wimbo wetu" mchezo ndio umefika patamu.

Mkuu Dr. Slaa

Hapa inatakiwa Chadema kucheza Chess na sio Checkers. EL, RA & Chenge ni watu ambao ni Mafisadi Papa, pesa walizonazo ni nyingi na EL ni kama amepagawa yeye anataka urais 2015 utadhani ameambiwa atafariki bila kukamilisha hilo. Chadema wasubiri damage na mpasuko mkubwa unaokuja utakaosababishwa na hii move. Unaposema Mangula, Malecela, Magufuli ni mafisadi unaongeza nguvu kwa kina EL na kuwafanya wananchi ambao wanampenda Magufuli kuanza kuquestion Chadema Motives.

All in all, dhamira ya kutaka hawa watu waondolewe ubunge nk ni nzuri, lakini subirini kwanza mpaka JULY, CCM ikiwatema tu, then Chadema waanze kudai lazima wapelekwe mahakamani na ubunge watoswe. Hapo kutakuwa na hoja ya msingi.

After JULY, then unaweza kuja na hii hoja kuwa CCM wafisadi wako wengi nk, lakini muda huo Chadema itakuwa kwenye wakati mzuri sababu kina EL nao watakuwa wanaiattack CCM direct kwa kutumia watu wao serikali, vyombo vya habari, CCM nk. Kuna siri nyingi sana tutajuwa wakishatoswa.

Chadema itapata hasara sana kama CCM watashindwa kuwatosa hawa watu watatu.
 
Si mchezo!
Demokrasia imegeuzwa Domokrasia!
Freedom of Speech imegeuzwa Freedom of Kuropoka!
Tuna safari ndefu sana!

Kwa nini tusijaribu kuvumiliana pale itikadi zetu zinapokinzana? Hakuna haja ya kutukanana wala kukoseana heshima!

- Sawa sawa hapo mkuu, hakuna la kuongeza!

William @ NYC, USA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom