Kwa kweli Slaa anatia huruma, nilimsikiliza jana alivyokuwa anahaha na Kigwangalla (MB) tu nikasema sasa huyu Mkuu akianza kunishughulikia mimi, nani atamshughulikia Rais wa CCM, nikajiuliza au mimi MB wa CCM ni sawa na mgombea URAIS wa CDM aliyegaragazwa? Kwa kweli Slaa hana jipya yule Mzee, labda ma-think tank wa CDM (kama hata mpo!) mtafute agenda nyingine, na siyo ufisadi, kwa ajili ya kuibeba CDM la sivyo itapotea kabla ya 2015. yaani ameishiwa sera na hoja. Kwa mtindo huu basi kasi ya kuporomoka kwa CDM, na Slaa itakuwa kubwa mno. Slaa - hadi kufikia 2015 atakuwa amepoteza prospects za kuingia Ikulu kwa kiasi kikubwa mno!
Sasa Mheshimiwa Kigwangala,tutegemee nini kutoka kwako zaidi ya shutuma na kebehi kwa Dkt Slaa na Chadema?Kutarajia umpongeze Slaa au Chadema ni sawa na kutarajia mwana JF mwenzetu aliye-"like" post yako W.J.Malecela awapongeze Chadema kwa kumtaja mzazi wake,John Malecela,kuwa ni miongoni mwa mafisadi.
Kwani Slaa alipoibua ishu za EPA alionekana ana jipya?Hivi sio Slaa huyu huyu aliyetishiwa kupelekwa polisi akathibitishe tuhuma hizo,lakini baadaye ikathibitika kuwa alichosema ni kweli?
Hivi sio Slaa huyu huyu aliyetaja List of Shame pale Mwembeyanga,watajwa wakatishia kumburuza mahakamani (hadi dakika hii hakuna hata mmoja aliyediriki kufanya hivyo),CCM ikatumia kila nguvu na raslimali ilizonazo kukebehi na kupinga tuhuma hizo,lakini hatimaye-na kwa vile njia ya mwongo ni fupi-mmelazimika kulamba matapishi yenu na kukiri kuwa ufisadi upo,na salama yenu ni kuuvua.
Sasa unaleta siasa za kudai oooh Dkt Slaa ameishiwa,ohh hatofika 2015!!Be careful what you wish for.Ripoti zinaeleza kuwa Chadema wameweka kambi kwenye jimbo lako,na mtu anayedai umempora jina lake amekuwa karibu na viongozi wa chama hicho.
Mnaweza kumkebehi kadri mtakavyo,mnaweza kumchukia kadri muwezavyo,lakini deep in your hearts you certainly know kwamba Dkt Slaa sio mwanasiasa wa kuchukuliwa lightly,hususan anapotoa public announcements.
Na kwa upeo wenu finyu mnawekeza nguvu nyingi kwa kuamini Slaa na Chadema ndio tatizo badala ya kuangalia jamii inayowazunguka,watu mnaowaongoza na kisha mngetambua umaarufu na kukubalika kwa Slaa/Chadema kunatoka wapi.
Halafu bado mnatuzuga mmejivua magamba ilhali fikra zenu bado ni zile zile za kifisadi.Mko uchi lakini mnataka umma uamini kuwa mmevaa suti,mnateleza lakini mnataka umma uwaone mmesimama.At the moment kuna mkanganyiko kuhusu the so-called magamba.How come Lowassa,Rostam na Chenge wawe wasafi Oktoba 2010 lakini leo wawe mafisadi?And how come you kept on refuting Chadema's claims that CCM was every fisadi's choice of a refuge,only for you to concede publicly that ufisadi was indeed a problem within the party,and some people were to go!
Walalahoi mnaowapuuza-ambao ni majority-ndio mtaji mkubwa wa Chadema.Hizo public announcements kuhusu mafisadi ni mazungumzo ya kawaida kati ya Chama hicho na wazalendo wenzake (walalahoi),ya kujulishana namna nchi inavyozidi kutafunwa,na nini kifanyike huko mbeleni.
Siku zenu zinahesabika