Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Wewe ndo mnafiki ukiendelee kutumika utajiua

usifikiri kila mtu ana mawazo kama yako , nimekwambia mafisadi wakihamia chadema chama kitakuwa salama??? Usiwe na mawazo kama ya babu loliondo !!! Ni lazima ujibu hoja!!!

Wapo watu wakihamia chadema hawana madhara , suala ni rostam kuhamia chadema , kama unajibu sema.

Suala la kukamatwa na kushitakiwa ni la kisheria!!!

Slaa ameshitakiwa na kesi yake ya kusingiziwa ipo arusha , je kikwete hajampeleka slaa mahakamani pamoja na yeye kuwa fisadi???

Kumbuka viongozi wete wote ,mbowe ,slaa wamekamatwa kwa amri ya kikwete na kufunguliwa mashitaka sasa kwa nini wewe hutaki rostam, lowasa na chenge wasikamatwe??? Huna akili wewe ni mbumbu tu???
 
Kwa kweli Slaa anatia huruma, nilimsikiliza jana alivyokuwa anahaha na Kigwangalla (MB) tu nikasema sasa huyu Mkuu akianza kunishughulikia mimi, nani atamshughulikia Rais wa CCM, nikajiuliza au mimi MB wa CCM ni sawa na mgombea URAIS wa CDM aliyegaragazwa? Kwa kweli Slaa hana jipya yule Mzee, labda ma-think tank wa CDM (kama hata mpo!) mtafute agenda nyingine, na siyo ufisadi, kwa ajili ya kuibeba CDM la sivyo itapotea kabla ya 2015. yaani ameishiwa sera na hoja. Kwa mtindo huu basi kasi ya kuporomoka kwa CDM, na Slaa itakuwa kubwa mno. Slaa - hadi kufikia 2015 atakuwa amepoteza prospects za kuingia Ikulu kwa kiasi kikubwa mno!

Tutafute ajenda zingine ili muundelee kuficha docs za watanzania. Kweli mwizi siku zote ni mwizi. Kama hamjaiibia Tanzania mbona hamtaki wananchi wajue mali zao zinakwenda wapi? Tuonyesheni revenues za nchi na expenses zake. Pigeni kampeni kuleta "transparency" hapo bungeni ili muone kama vyama vingine na wananchi hawataunga mkono. Tuonyesheni mnaipenda Tanzania kwa kuonyesha contracts zote za serikali na wamiliki wote wa biashara Tanzania. Kwanini kama mnajua umuhimu wa justice system mbona JK apigi kampeni ya kuwapa mahakama power za kuendesha kesi bila uingiliaji wa ofisi ya raisi au ccm? Tuonyesheni kura za uchaguzi wa uraisi zilipatikana vipi? Watu millioni 20 waliojiandikisha wanapiga kura millioni tano sio, hesabu za Harvard? Kinachoshangaza ni wananchi kama nyie mnafanya kazi kwa kuwaua watanzania wenzanu ili kunufaika na pesa za kujengea nyumba au kununulia gari, huu ndio umaskini wa hali ya juu na uuaji. Siku imekariabia na Mungu anawaona nyote nyie.

"Haki na democratic reforms hata mara moja hazitaletwa na mafisadi, wananchi wenyewe watazipigania mpaka zipatikane"
 
Francis Jr,
Tatizo ni kutokufanya utafiti. Nilishiriki katika hatua zote za kuandaa MOU kati ya CSCC na Serikali ya URT, wakati huo nikiwa Katibu Mkuu wa TEC. Kwa vile niko safarini sitaenda kwa undani lakini kama wako wengi wanaotaka kujua ukweli juu ya jambo hili, nitakuwa tayari kuwawekea mtiririko wote hapa jamvini. Hakuna ufisadi wowote ni moyo wa kuwatumikia watanzania bila kijali rangi,itikadi au imani ya dini ndiyo iliyotutuma kutoa huduma hizo.Ukijenga hospitali, shule zenye kupokea watoto wote wa kitanzania hakuna ufisadi wowote. Tatizo uelewa na uvivu wa kufanya utafiti wa kina.

Udini tu unawasumbua!Mbona ufisadi wa MOU ya mwaka 1992 ya makanisa na serikali mbona hausemi! au kwa kuwa wanapewa wakristo wenzake! Serikali haina dini iweje iwe inawapa wakristo tu na wengine hawapati!
 
- Sema wewe muhogo! ha! ha! ha! Hivi kuiba mke wa mtu sio ufisadi? Ha! ha! ha! ha! ha!

William @ NYC, USA.

Kama DR Slaa aliiba mke. Je masifadi wa ccm wangapi wanaukimwi na kutibiwa nje? Wao si wanabaka kwa kutumia vyombo vya dola vya wananchi? Huu sio ukiukaji wa haki za wanawake? Mwinyi alioa mtoto wa miaka mingapi tena Dar? Malecela yeye hajawahi kutafuta wanawake mitaani au kuwa na kimada? Kama mnataka kwenda kwenye ethical issues, you guys don't have any standards, low and nasty. Wangapi JK ametembea nao? Wangapi Sumaye anao? Wasichana wangapi Tanzania wamepata ukimwi kupitia wasanii wa ccm kwa kutumia pesa za wananchi? Talk ethical sio. Dr Slaa hata kama anaishi na mwanamke alikuwa ameolewa at least he has one woman at home ukilinganisha na wasanii wa ccm. Hii ni ethical hapa chini sio, mnataka ethical ya aina gani?

gongo-la-mboto.jpg

Mbagala%2BMabomu.jpg

images

3940383859_73f48abf02.jpg

Which one best represent you and ccm?
 
Kwa kweli Slaa anatia huruma, nilimsikiliza jana alivyokuwa anahaha na Kigwangalla (MB) tu nikasema sasa huyu Mkuu akianza kunishughulikia mimi, nani atamshughulikia Rais wa CCM, nikajiuliza au mimi MB wa CCM ni sawa na mgombea URAIS wa CDM aliyegaragazwa? Kwa kweli Slaa hana jipya yule Mzee, labda ma-think tank wa CDM (kama hata mpo!) mtafute agenda nyingine, na siyo ufisadi, kwa ajili ya kuibeba CDM la sivyo itapotea kabla ya 2015. yaani ameishiwa sera na hoja. Kwa mtindo huu basi kasi ya kuporomoka kwa CDM, na Slaa itakuwa kubwa mno. Slaa - hadi kufikia 2015 atakuwa amepoteza prospects za kuingia Ikulu kwa kiasi kikubwa mno!

Mkuu Kwema?

Ni swali tu.
 
Sasa Mheshimiwa Kigwangala,tutegemee nini kutoka kwako zaidi ya shutuma na kebehi kwa Dkt Slaa na Chadema?Kutarajia umpongeze Slaa au Chadema ni sawa na kutarajia mwana JF mwenzetu aliye-"like" post yako W.J.Malecela awapongeze Chadema kwa kumtaja mzazi wake,John Malecela,kuwa ni miongoni mwa mafisadi.

Kwani Slaa alipoibua ishu za EPA alionekana ana jipya?Hivi sio Slaa huyu huyu aliyetishiwa kupelekwa polisi akathibitishe tuhuma hizo,lakini baadaye ikathibitika kuwa alichosema ni kweli?

Hivi sio Slaa huyu huyu aliyetaja List of Shame pale Mwembeyanga,watajwa wakatishia kumburuza mahakamani (hadi dakika hii hakuna hata mmoja aliyediriki kufanya hivyo),CCM ikatumia kila nguvu na raslimali ilizonazo kukebehi na kupinga tuhuma hizo,lakini hatimaye-na kwa vile njia ya mwongo ni fupi-mmelazimika kulamba matapishi yenu na kukiri kuwa ufisadi upo,na salama yenu ni kuuvua.

Sasa unaleta siasa za kudai oooh Dkt Slaa ameishiwa,ohh hatofika 2015!!Be careful what you wish for.Ripoti zinaeleza kuwa Chadema wameweka kambi kwenye jimbo lako,na mtu anayedai umempora jina lake amekuwa karibu na viongozi wa chama hicho.

Mnaweza kumkebehi kadri mtakavyo,mnaweza kumchukia kadri muwezavyo,lakini deep in your hearts you certainly know kwamba Dkt Slaa sio mwanasiasa wa kuchukuliwa lightly,hususan anapotoa public announcements.

Na kwa upeo wenu finyu mnawekeza nguvu nyingi kwa kuamini Slaa na Chadema ndio tatizo badala ya kuangalia jamii inayowazunguka,watu mnaowaongoza na kisha mngetambua umaarufu na kukubalika kwa Slaa/Chadema kunatoka wapi.

Halafu bado mnatuzuga mmejivua magamba ilhali fikra zenu bado ni zile zile za kifisadi.Mko uchi lakini mnataka umma uamini kuwa mmevaa suti,mnateleza lakini mnataka umma uwaone mmesimama.At the moment kuna mkanganyiko kuhusu the so-called magamba.How come Lowassa,Rostam na Chenge wawe wasafi Oktoba 2010 lakini leo wawe mafisadi?And how come you kept on refuting Chadema's claims that CCM was every fisadi's choice of a refuge,only for you to concede publicly that ufisadi was indeed a problem within the party,and some people were to go!

Walalahoi mnaowapuuza-ambao ni majority-ndio mtaji mkubwa wa Chadema.Hizo public announcements kuhusu mafisadi ni mazungumzo ya kawaida kati ya Chama hicho na wazalendo wenzake (walalahoi),ya kujulishana namna nchi inavyozidi kutafunwa,na nini kifanyike huko mbeleni.

Siku zenu zinahesabika
Mlalahoi, mimi ni mmoja wa wenye mtazamo kuwa single ya ufisadi ili hit kwenye list of shame ya Mwembeyanga, lakini sasa imepoteza mvuto, hoja ulizoweke kwenye hii post ni very convincing to make to think twice.

Thanks.

Pasco
 
Sumaye hakutajwa orodha ya mafisadi-CHADEMA

Na Tumaini Makene

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetoa ufafanuzi juu ya orodha mpya ya ufisadi na mafisadi nchini, iliyosomwa juzi Mjini Tabora na Katibu Mkuu wa
chama hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ile iliyotolewa mwaka 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.

CHADEMA kimelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari jana kumnukuu Dkt. Slaa akisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi nchini, kwa mujibu katika orodha hiyo mpya.

Akizungumza jana Dar es Salaam na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Bw. Kigaila Benson, alisema kuwa wamelazimika kufafanua jambo hilo kwani hawataki kumtuhumu mtu bila kuwa na ushahidi wa tuhuma hizo, kwani kufanya
hivyo haingekuwa sahihi.

"Hili suala tumeamua kulifanyia ufafanuzi kwa sababu hatutaki wala hatuwezi kumtuhumu mtu au watu bila kuwa na ushahidi, kama mnavyojua sisi tunapoamua kusema fulani na fulani ni fisadi huwa tunaweka ushahidi bayana, kwa maana kuutaja ufisadi
waliofanya, si maneno matupu.

"Sasa imeandikwa kuwa katibu mkuu wetu Dkt. Slaa amemtaja Sumaye kuwa ni mmoja wa walioko katika orodha mpya ya mafisadi, hii si kweli, katika orodha hiyo hatukumtaja...hatusemi kuwa Sumaye ni fisadi au si fisadi, tunachosema ni kuwa sisi hatujamtaja katika orodha yetu.

"Kama kuna mtu anao ushahidi juu ya ufisadi wake anaweza kumtaja, hata sisi siku tukipata ushahidi juu ya Sumaye tutamtaja ...asubuhi nimeongea na Dkt. Slaa na Marando
(Mabere) wanasema Sumaye hakutajwa katika orodha, mazingira ambayo Dkt. Slaa alimzungumza Sumaye hayakunukuliwa sahihi," alisema Bw. Benson.

Aliongeza kuwa Dkt. Slaa alitaja jina la Bw. Sumaye alipokuwa akisema kuwa mafisadi na ufisadi ambao ameutaja mara kwa mara haujali dini, uhusiano, kabila, rangi wala umri wa mtu, hivyo akatolea mfano jinsi alivyowahi kumshambulia waziri mkuu huyo
mstaafu ambaye anatoka naye eneo moja huko Arusha, wakati akiwa madarakani kwa kushindwa kudhibiti ufisadi serikalini.

Bw. Benson pia alizungumzia kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri ya Taifa (NEC) ya CCM, Bw. Nape Nnauye kuwa kuna vyama vya upinzani vimetumwa na mafisadi kumchafua Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, huku pia akidai kuwa kuna
wanasiasa wa upinzani wametumwa Tabora kufanya kazi hiyo hiyo.

"Unajua kitu kimoja ambacho mtu mwenye akili hawezi kuwaelewa CCM, hususan wanapoamua kutuhumu, wanaimba sana ngonjera. Unapoamua kusema kuwa kuna mafisadi wanatumia vyama vya upinzani kumchafua rais, ili ueleweke na kuaminika unawataja hao mafisadi
au huyo fisadi na vyama au chama kinachotumika.

"Ndiyo maana sisi tunapenda kuwaonesha njia sahihi ili wajikosoe vizuri, tukitaja mafisadi tunaonesha na ufisadi wao, hatubahatishi, sasa wao wanaimba tu ooh tunawapatia mafisadi siku tisini wajiuzulu lakini hawana ubavu wa kuwasema kwa
majina hao mafisadi ni akina nani na ufisadi wao uko wapi na wanachukua hatua gani za kisheria juu ya ufisadi wao.

"Tena sasa wanataka kuleta utamaduni mbaya sana ambao utatengeneza mwanya kwa watu walioko madarakani kufanya ufisadi maana wanajua wataambiwa wajiuzulu tu, hakutakuwa na hatua za kisheria juu ya yao, tulitegemea kwa chama chenye serikali kama CCM, kuiagiza serikali kuchukua hatua si kulalamika au kuimba ngonjera kama wanavyofanya sasa."

Bw. Benson alisema kuwa si sahihi watu wanaotuhumiwa ufisadi katika chama kinachounda serikali, huku wakiwa na dhamana ya uongozi sehemu zote mbili, kuachia nafasi zao ndani ya chama husika pekee, badala ya kuchunguzwa, kisha kufikishwa
mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.

"Alitakiwa ataje jina la huyo fisadi au mafisadi na hivyo vyama vya upinzani. Pia fisadi ni mwizi, amefilisi taifa, raslimali za nchi sasa unaposema ajiuzulu nini kinafuata sasa, mwizi anakamatwa, mwizi hasemwi tu, sisi hatuna serikali sasa, lakini
tumewataja, hawa wana serikali mbona hawachukui hatua."

Juzi katika mkutano wake wa ujenzi wa chama hicho mkoani Tabora, Dkt. Slaa akiwa na pamoja makada wengine wa chama hicho, wakiwemo wanasheria Profesa Abdalla Safari na Mabere Marando pamoja na baadhi ya wakurugenzi na maofisa wa chama hicho walitaja
orodha ya watuhumiwa wa ufisadi nchini.

Dkt. Slaa ambaye aliwahi kutoa orodha aliyoita ya aibu ya watuhumiwa 11 wa ufisadi mkubwa unaolifilisi taifa, mwaka 2007, juzi aliongeza majina mengine matatu, ambapo alimtaja Dkt. John Magufuli kuhusiana na uuzaji wa nyumba za serikali, Bw. Phillip Mangula na Dkt. John Malecela kuhusiana na Fedha za EPA, huku
akimtaja Rais Kikwete kwa kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, katika uuzaji wa nyumba za serikali bila kufuata utaratibu.

(source- Majira)
 
DU KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LEO WANAMKANUSHIA SUMAYE WAKATI MKOPO ULE MKUBWA WA sHIRIKA LA JAMII HAUJALIPWA, ACHILIA MASHAMBA ALIYAPATA WAPI WAKATI ALITOKEA kILOMBERO SUGAR,AKITOKEA UALIMU CHUO CHA UKIRUGULU WAKATI A KUUWANIA URAIS WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIJICHOTEA
NANI ASIYEFAHAMU MIRADI YA IFAD ALIWAWEKA NDUGU ZAKE HUKO SHINYANGA, ARUSHA NA DODOMA NA MIRADI IMEKUFA
TIME WILL TELL
 
chadema hawana ushaidi mkuu ndio maana wanasema kama mtu anaushahidi kama wewe hivi kashushe kwenye vyombo vya habari, lakini pia lakini pia hawajamkanushia kwamba ni fisadi au sio fisadi, nadhani chadema bado wako kwenye msitari, ina maana siku wakipata undani wa nyeti kama hizi unazosema wewe na wakawa na ushahidi watamtaja, hacha mambo ya ukabila, yawezekana huyo mkubwa hakuacha fingerprints sehemu yoyote, kwa hiyo inaweza kuwa ngumu kumuweka kwenye familia ya LIST OF SHAME,
hata mimi huo nahisia kwa huyo bwana alitukaanga, kivi anajua yeye!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
DU KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LEO WANAMKANUSHIA SUMAYE WAKATI MKOPO ULE MKUBWA WA sHIRIKA LA JAMII HAUJALIPWA, ACHILIA MASHAMBA ALIYAPATA WAPI WAKATI ALITOKEA kILOMBERO SUGAR,AKITOKEA UALIMU CHUO CHA UKIRUGULU WAKATI A KUUWANIA URAIS WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIJICHOTEA
NANI ASIYEFAHAMU MIRADI YA IFAD ALIWAWEKA NDUGU ZAKE HUKO SHINYANGA, ARUSHA NA DODOMA NA MIRADI IMEKUFA
TIME WILL TELL
 
Chadema wameamua kutoa jina la sumaye kwa vile ameomba kujiunga na chama hicho kikubwa cha siasa kinachoendana na jina lake. hata hivyo ukweli utabaki wazi kuwa sumaye ni fisadi, utakumbuka yeye ndiye alikuwa waziri mkuu na kubariki uuzaji wa nyumba za serikali kwa wahindi kwa bei ya bure, sumaye huyo huyo alisimamia kwa makini uuzaji wa masharika ya umma akiwa waziri mkuu wa serikali ya mkapa, na sumaye huyo akiwa waziri mkuu hakuweza kumshauri rais wake mkapa asijiuzie kiwanda cha kiwira hii inamaana kuwa waligawana mapato yote malipo ya makampuni ya serikali na kujilimbikizia mali.
 
hii imetokea lini mkuu, more data please
chadema wameamua kutoa jina la sumaye kwa vile ameomba kujiunga na chama hicho kikubwa cha siasa kinachoendana na jina lake. Hata hivyo ukweli utabaki wazi kuwa sumaye ni fisadi, utakumbuka yeye ndiye alikuwa waziri mkuu na kubariki uuzaji wa nyumba za serikali kwa wahindi kwa bei ya bure, sumaye huyo huyo alisimamia kwa makini uuzaji wa masharika ya umma akiwa waziri mkuu wa serikali ya mkapa, na sumaye huyo akiwa waziri mkuu hakuweza kumshauri rais wake mkapa asijiuzie kiwanda cha kiwira hii inamaana kuwa waligawana mapato yote malipo ya makampuni ya serikali na kujilimbikizia mali.
 
Kama sumaye ni fisadi pelekeni ushahidi ili naye aongezwe kwenye orodha ya mafisadi. Ccm waache propaganda za eti Dr. Slaa hajamtaja Sumaye kwa sababu wanatoka sehemu moja. Kama wao ccm wana ushahidi basi wawapatie cdm ili nae atajwe kama mojawapo ya mafisadi.
 
DU KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LEO WANAMKANUSHIA SUMAYE WAKATI MKOPO ULE MKUBWA WA sHIRIKA LA JAMII HAUJALIPWA, ACHILIA MASHAMBA ALIYAPATA WAPI WAKATI ALITOKEA kILOMBERO SUGAR,AKITOKEA UALIMU CHUO CHA UKIRUGULU WAKATI A KUUWANIA URAIS WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIJICHOTEA
NANI ASIYEFAHAMU MIRADI YA IFAD ALIWAWEKA NDUGU ZAKE HUKO SHINYANGA, ARUSHA NA DODOMA NA MIRADI IMEKUFA
TIME WILL TELL

Mkuu si uwapelekee ushahidi wako sijui kama umewaelewa, wanasema hawana ushahidi wa kutosha na kama kuna mwenye nao basi aupeleke. Tunalalama tu watz soma habari nzima mkuu sisome sentensi moja na kuingia tu kichwakichwa. Si kwamba Sumaye ni fisadi au si fisadi but hawana ushahidi! Unataka waropoke halafu washtakiwe kwa uzushi?
 
Ndugu yangu kama unavyojua kitendo cha kumuita mtu fisadi ni ujasiri mkubwa sana na huwezi kumuita mtu fisadi kama huna ushaidi wa kujitosheleza.
Nafikiri CDM wanalitambua hilo na liko kwenye mchakato wa kutafuta ushaidi ndipo waliweke hazarani.
Isitoshe DR hakusema hao aliowataja ndio mafisadi pekee wa TZ la hasha.
Na kama wewe ni kidume kweli na ushahidi unao , basi tema cheche tukujue na wewe u mpambanaji kwani kazi ya kuwaumbua mafisadi si ya DR peke yake ni jukumu letu sote
 
DU KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LEO WANAMKANUSHIA SUMAYE WAKATI MKOPO ULE MKUBWA WA sHIRIKA LA JAMII HAUJALIPWA, ACHILIA MASHAMBA ALIYAPATA WAPI WAKATI ALITOKEA kILOMBERO SUGAR,AKITOKEA UALIMU CHUO CHA UKIRUGULU WAKATI A KUUWANIA URAIS WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIJICHOTEA
NANI ASIYEFAHAMU MIRADI YA IFAD ALIWAWEKA NDUGU ZAKE HUKO SHINYANGA, ARUSHA NA DODOMA NA MIRADI IMEKUFA
TIME WILL TELL

Ndugu yangu chunguza kwanza kabla ya kunena. Mimi nina uhakika kuwa mkopo wa PPF (50) aliulipa ndani ya muda mfupi. Nilihakikishiwa na Mkurugenzi wa PPF kwa kuonyeshwa balance sheet kuwa Sumaye alilipa mkopo. Lkn pia mkopo una tofauti kubwa na Kagoda,EPA, Richmond na Dowans. Alafu, kama kweli hakutajwa, akaingizwa kwenye story na watu wenye nia (ya tuchafuke wote)? Kuna kosa gani kumkanushia?
 
Hivi hamfahamu kwamba sumaye na slaa ni kabila moja? Sidhani slaa ana ubavu wa kumsaliti sumaye kwa wa iraqw wenzake!!

Macinkus
 
DU KWELI DAMU NZITO KULIKO MAJI LEO WANAMKANUSHIA SUMAYE WAKATI MKOPO ULE MKUBWA WA sHIRIKA LA JAMII HAUJALIPWA, ACHILIA MASHAMBA ALIYAPATA WAPI WAKATI ALITOKEA kILOMBERO SUGAR,AKITOKEA UALIMU CHUO CHA UKIRUGULU WAKATI A KUUWANIA URAIS WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WALIJICHOTEA
NANI ASIYEFAHAMU MIRADI YA IFAD ALIWAWEKA NDUGU ZAKE HUKO SHINYANGA, ARUSHA NA DODOMA NA MIRADI IMEKUFA
TIME WILL TELL

Hujui unachosema!! Huwezi kumtuhumu mtu bila ushahidi, kwa sababu hii ina legal implications. Nashukru wewe unaushahidi wa Sumaye sasa mtangazde wewe au mpatie Dr. Slaa huo ushahidi ili wanasheria wauchambue na waweze mtangaza rasmi. CDM haitaki majungu, husema ukweli na kuusimamia. Punde ya Sumaye yakipata ushahidi-atatangazwa, vinginevyo, atabaki safiiiiiiii.
 
Hivi hamfahamu kwamba sumaye na slaa ni kabila moja? Sidhani slaa ana ubavu wa kumsaliti sumaye kwa wa iraqw wenzake!!

Macinkus

Ilogical argument; maana hata kama ni ukanda, na Lowasa wanatoka naye mkoa mmoja. Huwezi kumtuhumu mtu bila ushahidi, maana anaweza kukushita mahakamani na ukashindwa-it will be shame. Wewe yaelekea una ushahidi wa Sumaye, tupatie, na Dr.Slaa bila ajizi atamtangaza maana orodha haijafika mwisho. Ushahidi bado unatafutwa na kila unapopatikana watu anatangazwa. Ni jambo la kushukuru ukisaidia katika hili (evidence).
 
Francis Jr,
Tatizo ni kutokufanya utafiti. Nilishiriki katika hatua zote za kuandaa MOU kati ya CSCC na Serikali ya URT, wakati huo nikiwa Katibu Mkuu wa TEC. Kwa vile niko safarini sitaenda kwa undani lakini kama wako wengi wanaotaka kujua ukweli juu ya jambo hili, nitakuwa tayari kuwawekea mtiririko wote hapa jamvini. Hakuna ufisadi wowote ni moyo wa kuwatumikia watanzania bila kijali rangi,itikadi au imani ya dini ndiyo iliyotutuma kutoa huduma hizo.Ukijenga hospitali, shule zenye kupokea watoto wote wa kitanzania hakuna ufisadi wowote. Tatizo uelewa na uvivu wa kufanya utafiti wa kina.

E Mola, Kweli Dr Slaa inataka kuingia huku nako? Ni wazi hili jukumu la kutofanya utafiti ni fond ndugu la watanzania wote
 
Francis Jr,
Tatizo ni kutokufanya utafiti. Nilishiriki katika hatua zote za kuandaa MOU kati ya CSCC na Serikali ya URT, wakati huo nikiwa Katibu Mkuu wa TEC. Kwa vile niko safarini sitaenda kwa undani lakini kama wako wengi wanaotaka kujua ukweli juu ya jambo hili, nitakuwa tayari kuwawekea mtiririko wote hapa jamvini. Hakuna ufisadi wowote ni moyo wa kuwatumikia watanzania bila kijali rangi,itikadi au imani ya dini ndiyo iliyotutuma kutoa huduma hizo.Ukijenga hospitali, shule zenye kupokea watoto wote wa kitanzania hakuna ufisadi wowote. Tatizo uelewa na uvivu wa kufanya utafiti wa kina.

E Mola, Kweli Dr Slaa unataka kuingia huku nako? Ni wazi hili jukumu la kutofanya utafiti ni fond ndugu la watanzania wote
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom