Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Apr 16, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  TBC watarusha live? Si Wanajiendesha kwa kodi zetu bana. La sivyo nao wajumuishwe kwenye orodha ya mafisadi, wanatuibia kodi zetu

  Imeipata wapi?jibu ni humo humo ccm!sasa ni staili ya mwaga mboga nitupe ugali.
  Kazi ipo tusubiri majina.

  Saturday, 16 April 2011
  Fidelis Butahe

  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikijivua gamba kwa kuwataka wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe kwenye uongozi wa chama hicho, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa leo anataja orodha mpya ya mafisadi ndani ya chama hicho tawala ili nao waunganishwe katika orodha hiyo.

  Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Singo Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Dk Slaa atataja majina hayo leo mkoani Tabora katika mkutano wa hadhara kama alivyofanya mwaka 2007, katika Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam.

  Alisema katika mkutano huo, Dk Slaa akiwa na viongozi wengine wa Chadema, atataja majina hayo ya mafisadi ili kuipa CCM wakati mzuri wa kuwatambua na kuwachukulia hatua kama kweli ina nia njema ya kujivua gamba.

  Hii ni changamoto mpya kwa CCM ambayo tayari imenyooshea kidole genge la mafisadi lililoko ndani ya chama hicho na kuwapa siku 90 watuhumiwa hao kujiuzulu ili kukinusuru.

  Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa orodha hiyo mpya ya mafisadi inayotarajiwa kutajwa leo, ni kubwa kuliko ile ya mwaka 2007.

  “Ushahidi tunao ndiyo maana hata tuliowataja mwaka 2007 hadi leo hawajafungua kesi yoyote mahakamani. Wanasema kuwa wamejivua gamba. Gamba la CCM siyo uzee ni ufisadi,” alisema Bensoni na kuongeza: “Tutawakumbusha gamba wanalotakiwa kujivua ni lipi ili Watanzania watambue. Dk Slaa ataweka mambo hadharani katika mkutano huo akiwa pamoja Profesa Abdalah Safari na Mabere Malando.”

  Alisema licha ya CCM kutoa siku 90 kwa watuhumiwa wa ufisadi wanaotajwatajwa, wapo ambao hawajatajwa kati ya waliotakiwa kujiuzulu kwa tuhuma za hizo. “Hapa sasa ndiyo watajua mafisadi ni kina nani. Tunataka kuwakumbusha gamba ni lipi.”

  Alisema kuwa orodha hiyo ni mpya na ina tofauti na ile ya Mwembeyanga kwa kuwa tangu kipindi hicho mpaka leo kuna matukio mengi ya ufisadi yaliyoendelea nchini. “Ufisadi wa sasa ni mkubwa sana hivyo orodha itakuwa kubwa, ‘Ni ngoma nzito’ na tukimaliza kutaja orodha hiyo tutaendelea na mikutano yetu nchi nzima,” alisema Bensoni.

  Akizungumzia hatua hiyo ya Chadema, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Chadema wamefilisika kisiasa, walidhani wataitisha CCM kwa hoja ya ufisadi lakini sasa CCM ni chama safi. Kwa mabadiliko tuliyoyafanya, Chadema inatakiwa kucheza ngoma yetu (CCM) na siyo sisi (CCM) kucheza ngoma yao."

  Nape alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kukubali kurudisha muswada wa Katiba kwa wananchi na kuwapa fursa zaidi kujadili suala hilo.


  MAFISADI WAPYA HADI SASA NI ;
  1. John Kato mwajiriwa Caspian (KAGODA).
  2. Bharati Goda ni mwajiriwa caspian (KAGODA).
  3. John Samweli Malecela –EPA
  4. Philip Mangula – EPA
  5. John Magufuli – nyumba za Serikali.
  SAMAHANI SIJAWEZA KUIHARIRI ILA HAYO NDIO YANAENDELEA - NTAWAJUZA ZAIDI.

  PROF. SAFARI:


  Anasema kuwa ni wakati wa kudai nyumba za serikali kwa nguvu ya umma , kwani kwenda mahakamani sio muafaka kwani hata majaji wenyewe walijiuzia hivyo hawawezi kutoa haki.


  Zidaiwe kwa nguvu ya umma ndio njia pekee ya kupata nyumba hizo kwani viongozi wengi wanakaa hotelini.

  Udini:

  Wakoloni waliwagawa watu kwa njia za makabila ili wawatawale ,wakagawa watu kwa njia za udini mf.waingereza waliingiza dini na kjuweka watu wao serikalini , na waislamu wengi walikosa nafasi ya kusoma ndio maana hawakuingia serikalini mapema.

  Waislamu walipigania uhuru ila , kutokana na waingereza kuwabagua , ndio maana waliamua kupinga ukoloni ili waweza kuweka serikali ambayo haiwabagui, anasema ugomvi wa Nyerere na shehe takadir kuhusu waislamu kubaguliwa , na anasema kuwa ndani ya CDM hakuna udini ila ndani ya nchi kuna tatizo la kihistoria la kidini.

  Anasema kuwa ni mbinu ya serikali kuwagawa watanzania ili waweze kuwatawala.


  Alipojitoa CUF na kujiunga na CDM alifuatwa na mashehe wakimwambia kuwa yeye ameamua kujiunga na wakristo , yeye akajibu kuwa walitaka yeye aende kwenye chama gani? Mbona CCM sio ya waislamu kwani ukiondoka JK wengi waliopo serikalini.

  Anasema yeye hajabatizwa na pia Slaa sio yohana mbatizaji na amewataka waislamu kuungana pamoja ili kupigania haki za waislamu kwani CCM ndio ambao wanawakandamiza waislamu hivyo ni bora wakajiunga na CDM kwa wingi ili waweze kudai haki zao tangu awali na wasisubiri, waingie CDM tangu mwanzo ili wawe sehemu ya kupigania haki zao na njia nzuri ni kuhakikisha nkuwa wanajiunga ili kuingiza hoja zao kabla ya cdm kuingia serikalini na ni lazima waislamu wakitaka madai yao yasikilizwe wanapaswa kuingia sasa na sio wawasusie cdm kwa hoja za udini halafu baadae waje walalamike.

  Kuna haja ya kujiunga na CDM sasa.

  MARANDO:
  Ameanza kwa kusema Slaa alishinda ila kura zilichakachuliwa na hivyo ndio maana Slaa ameamua kuingia kazini rasmi kujenga chama ili kiwe imara na kuweza kujiandaa na uchaguzi ujao.

  Anasema yeye ataongelea mambo matatu; KATIBA, EPA NA MAGAMBA YA CCM

  KATIBA:


  Hii ilikuwa hoja ya CDM kwani iliyopo inawafanya mafisadi watamalaki, katiba ni maji, ni unga ni kila kitu ambacho kipo, ukishaweka katiba mengine yote yanawezekana.


  Anasema JK alishauriwa na watu kuhusu katiba , ila aliweza kjuipata muswada wa sheria kutokana na taaluma yake ya kishushu aliupata mapema na kuisambaza a kwani jk hakuwa tayari kupata katiba .


  Amewataka watanzania kuwa macho kwani nia ya ccm ni kuendelea na katiba iliyopo na sio kweli kjuwa wanataka katiba mpya.


  Tofauti ya CCM na CDM kwenye katiba ni kuwa CCM wanataka iliyopo iwekwe viraka , na CDM wanataka mpya .

  Cdm wanataka mambo yafuatayo kwenye katiba mpya:

  1. Kupunguza madaraka ya rais haswa ktk kuteua watu mbalimbali.
  2. Viongozi wa wilaya wapigiwe kura na sio kuteuliwa na rais…..
  3. Madini yalindwe na katiba
  4. Power of recall kwa wabunge na madiwani

  Kuhusu EPA na magamba ya CCM:

  CCM ndilo gamba la watanzania na tunapaswa kuliondoa hilo gamba CCM na sio wao waondoane wenyewe. CCM ndio gamba lenyewe na linapaswa kuondolewa moja kwa moja.

  Lissu amewafundishwa wabunge sheria. EPA ni ya JK kwani ndiyo ilimuingiza madarakani. Kikwete amesamehe wezi wa EPA wakati wezi wanapaswa kupelekwa jela.

  Slaa alipotaja mafisadi CCM walisema ni uongo kuwa hakuna mafisadi, JK juzi kakiri kuwa kuna mafisadi wengi ndani ya chama na walitaja listi yao ya mafisadi, Lowassa, Chenge na Rostam.

  JK sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .
  JK alishindwa hata kujua mafisadi DOWANS.

  Kagoda:

  Kuna visamaki vidogo vimeshitakiwa ila Kagoda haswa hawajapelekwa mahakamani, rais alisema hawajui wahusika wa Kagoda.

  Kemhondo William ni jina la bandia – John Kato mwajiriwa Caspian
  Francis Wiliam jina bandia – Bharati Goda na ni mwajiriwa caspian

  Aliweka majeshi yake kwa siku tatu na majina halisi ndiyo hayo.

  Na JK kama hawajui aende ofisini kwake atampa mpaka picha. Kama JK anataka atume watu ofisini kwake ili waende kuchukua picha.

  Anasema yuko tayari kama JK akimtaka kujitolea apewe jalada la Kagoda na atawafikisha mahakamani na wataishia Keko.
  Wengine wa Kagoda ni Malecela na Mangula.

  CDM tulimuita Safari ili aje aweze kutueleza ni jinsi gani tunaweza kiutatua matatizo ya waislamu na pindi tukiingia madarakani tutakuwa tayari kuzitekeleza kwani CCM kwa miaka 60 wameshindwa kutatua matataizo hayo.


  DR.SLAA.

  Ameanza kwa kuwataka maasikari kuacha siasa na haswa jana walipoamua kuzuia maandamano kwa madai kuwa hali ya nchi ni tete, amewataka polisi kuacha kufanya siasa. Hiyo hali wameipima hospitali gani mpaka kujua hali ni tete na pia pesa zimeibiwa ndani ya jeshi la polisi na hata mdhibiti mkuu amesema uozo wa polisi.


  Sababu ya pili waliyotoa polisi kuwa hoja yetu ya maandamano imefutwa na serikali ,hiyo sio kazi ya polisi kusema kuwa maandamano yamevunjwa .


  Polisi kuweni na uchungu na nchi hii kwani mama, baba , watoto wenu wanaumia sana kutokana na ufisadi wan chi hii, pia usalama wa taifa wanapaswa sasa kuamka na kulinda masilahi ya taifa na sio kulinda masilahi ya viongozi kama wanavyofanya sasa.


  Nchi haiwezi kutawalika ni mpaka mafisadi wote wakamatwe kwani haiwezekani kluwa na mafisadi na nchi ikaweza kutawalika.

  Wananchi wa Tabora kwa ujumla wenu mmefanywa kuwa wateja wa CCM kwani hii ni ngome yao ya kuvuna kura wakati hakuna hata barabara kwenye mkutano wenu.


  Hawezi kujibu vyama wanaozunguka kuisema CDM ila hoja yake ni maisha ya watanzania tuu na sio vinginevyo kwani maisha ni magumu kwa kila mwananchi bila kiujali vyama vyao.

  Maeneo waliyoikataa CCM kuna lami ila huku ambako kuna CCM hakuna barabara za kwenda Urambo, Bukene, Nzega … huku mmetelekezwa.

  Rais anaahidi kujenga viwanja vya ndege wakati cha Tabora hakitumiki sasa hivyo vipya anaweza?

  Kwa taarifa yenu mimi ni mwana Tabora kwani nilikulia na kusoma Itaga , wakati huo kulikuwa na viwanda vya nyuzi, maziwa n.k. na kwelina sababu nzito ya kuikataa CCM.

  Makisio ya kodi ya Tabora mwaka huu ni kulipa serikali kuu 9.9 bilioni, ila hakuna barabara. Je, kodi zenu zinapelekwa wapi?

  Anazungumzia juu ya nyumba za serikali na sasa muda umeisha wa kuendelea kuvumilia kuhusu nyumba za serikali lazima sasa zirejeshwe mara moja.
  Mkapa anahusika na uuzwaji wa nyumba za Serikali. Mkapa na Magufuli kwenye kuuza nyumba za serikali na wao ni mafisadi.

  Ndege za JK za kampeni zilitoka kwa watu walioiba EPA na ndio maana ameshindwa kuchukua hatua kwani anashirikiana nao.

  Kama JK kawapa mafisadi siku 90 ndani ya chama chake nay eye Tunampa JK na eye siku 90 ataje fedha za mabango yake dola 1.5 milioni aseme zilitoka wapi zilizotumwa CANADA kutengeneza 2010 election .na yeye anapaswa kujitoa kama atashindwa kuchukua hatua hizo.
   
 2. S

  Sobangeja Senior Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ni vema tukapata pia up to date list hasa kwa wale waliojificha kwa migongo ya mapapa na manyangumi fisadi.
   
 3. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamani CHADEMA ni chama makini,hata kama watu bado akili zimelala tuwasaidie ili tuinusuru nchi yetu. Hivi wabunge wote hao wa ccm akili zao zimevaa magamba? wananiudhi kweli mimi! Dr wa ukweli atataja wote na hakuna wa kwenda mahakamani.

  Mi nahisi majina matatu ya kwanza yatakuwa ni,
  1.JK
  2.EL
  3.RA
   
 4. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa hivi bado sijaona kilichofanyika kuhusu tuhuma za ufisadi, ina maana wale waliojiuzulu toka sekretarieti ndio mafisadi? mbona mi siwaelewi, na je kujiuzulu ndio kuchukuliwa hatua? Kama ni mafisadi kwanini hawashtakiwi?
   
 5. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watakao kuwepo watujuze
   
 6. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  haya ni ya zamani bana!
   
 7. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nape nnauye,,,, hamnazo huyu...................
   
 8. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Atakuwepo Salva rweyemamu, Ngeleja, Masha, Wasira
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Nape, ina maana unakiri mlikuwa mnacheza ngoma ya CHADEMA kabla ya kuvua magamba?
   
 10. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  CDM ni makini kuliko hata Serikali, ingekuwa hotuba yoyote ya Kikwete ingekuwa imeshavuja na tunayo wana JF kutokana na umakini wa CDM wana JF wanahisi labda
  1. JK
  2. RA
  3. EL
  Big up CDM
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Abdulrahman Kinana will be number 6.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wait a minute!
  Tabora ni nyumbani kwa Lipumba
  Lipumba ni Mkiti wa Kafu
  Kafu ni Mke wa ccm
  JK ni Mkiti wa ccm

  Kwa nini Chadema wanakwenda nyumbani kwa mke wa mtu kwenda kumwambia kuhusu mume wake alivyo fisadi? Je mume atakubali hili litokee? Basi tusubiri kuona polisi na TBC watakavyo handle hili
   
 13. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Anathibitisha kwamba walikuwa wanacheza ngoma ya CDM, ebu tumwone hiyo ngoma atakayoianzisha! Najua hilo haliwezekani ndani ya CCM! Kule ni kula, kula, kula ushibe uvimbiwe uwaambie wale wanaokusema kwamba wana wivu!
   
 14. M

  MBANINO Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili la kuwataja Mafisadi waliopo CCM na Serikalini ni la muhimu sana. Tusisahau ya kwamba CCM wanajaribu kutuonyesha ya kwamba kwa Sekretariati yake kujiuzulu na wajumbe wake kutorudishwa tena basi wapo safi. Au isidhani kwa viongozi wake wenye tuhuma nyingi kama Chenge, RA na EL kutokuwamo katika Kamati Kuu ya Chama hicho basi tena wapo safi, hii si kweli.

  Ufisadi umezidi kuongezeka na hali ya maisha ya Mtanzania imezidi kudorora. Kwa hili ni ishara ya wazi kabisa ya kwamba bado kuna viongozi wengi tu na wafuasi wao ndani ya CCM bado wanaendelea kufisadi mali ya umma. Hivyo kitendo cha Chadema kuamua kuwataja ni kuonyesha jinsi gani CCM inavyojaribu kufanya usanii ambao ni wa kitoto sana.

  Wanamdanganya nani ya kwamba sasa chama ni safi na kinapambana na ufisadi? Hivi hawaoni ya kwamba maisha yanazidi kuwa magumu kwa mwananchi wa kawaida? Hivi wanadhani wananchi hawaelewi ya kwamba kila kukicha miradi mingio ya maendeleo haimaliziki kwa sababu ya utafunaji wa fedha za miradi hiyo? Nani asiyejua ya kwamba hatuna dawa hospitalini? nani asiyejua ya kwamba wamechakachua huduma zote za kijamii kwa manufaa yao ya kisiasa?

  Lazima CCM ijue, michezo yake michafu na ya kitoto isiyo na manufaa kwa watanzania walio wengi inaonekana. Hawajajivua gamba, hili ni wazi kabisa, usanii mtupu.

  Hivyo kitendo cha Chadema kujiandaa kuwaonyesha wananchi ya kwamba kunamafisadi wengi tu ndani ya chama na si ajabu baadhi yao wapo katika Sekretariati mpya na Kamati kuu ya CCM ni kitendo kizuri kwa mustakabali wa taifa letu.
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  yaani sasa hivi wana haha kujua nani yumo ndani ya hiyo list.............nape nnauye namwonea huruma kweli....kuropoka kwingine hakuna maana
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  STEIN wakimuweka Wasira mi sitaelewa maana wasira ana nini tofauti na kutumika? Uyu mzee mlopokaji hana lolote! Labda ufisadi wa kutumika na wakubwa hapo sawa. Dr Slaa,tunasubiri utaje iyo orodha,ikumbukwe kuwa wewe ndo uliyekabidhiwa kazi na wananchi ya kuliongoza taifa,na kwa kuwa kila kitu ulichoelekeza wachakachuaji wametekeleza ikiwemo kuondoa muswada wa kijangili,sasa ni wakati muafaka wa kuwaelekeza ccm wamteme nani na nani. THANK U MR DR.
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  "Inatakiwa" na nani? ila chadema haitaki eeh? Nape analalama.
  Bold nyeusi. CCM ya Nape wameicheza ngoma ya Chadema kivitendo, hadharani tena baada ya "kujivua magamba"
  Wasubiri W.P.Slaa (PhD ya Ukweli) awape tune nyingine Tabora, sisiem wakacheze.
   
 18. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TUJIKUMBUSHE ORODHA YA 2007
  1. Dr. Daudi T.S. Balali
  2. Andrew J. Chenge
  3. Basil Pesambili Mramba
  4. Gray S. Mgonja
  5. Patrick P.R Rutabanzibwa
  6. Nazir Karamagi
  7. Nimrod Mkono
  8. Rostam Aziz
  9. Edward Lowassa
  10. Benjamin W. Mkapa
  11. Jakaya Mrisho Kikwete
   
 19. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM nawaonea huruma. Wakibanwa wanaachia. Kama hao mafasadi ambao wametajwa miaka yote waliendelea kuwakumbatia wakiwatetea kuwa hao ni watuhumiwa tu na hawajathibitishwa, leo wanapowatosa wamewathibitisha?

  Wanapodhani kwa kuwatosa mafisadi sasa CDM haina jipya la kufanya, si wangeanza kwanza kwa kukiri kwamba yaliyokuwa yamesemwa na viongozi wa CDM ni kweli? Walikana mwanzoni na sasa wanakiri kimyemela.
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huyo slaa angeanza kutaja mafisadi waliyomo ndani ya chama chake! Hii kukimbilia kujitia anajua sana mambo ya CCM ni kutafuta ujiko usio na mshiko!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...