Tabora: Anayeidai TRA Milioni 986, Ramadhani Ntuzwe adaiwa 'kujiua kwa risasi'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Snapinsta.app_417502753_18326493067189072_2413745782387798104_n_1080.jpg
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: MwanaHalisi
 
Mfanyabiashara Ramadhani Ntuzwe ‘Babu Rama’ aliyekuwa akipaza sauti katika vyombo mbalimbali vya habari kwa takriba miaka saba kwamba anaida fidia ya Sh 986 milioni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), anadaiwa kujiua kwa risasi leo Jumatano Machi 6, 2024 nyumbani kwake Urambo mkoani Tabora.

Meneja wa mfanyabiashara huyo, Msifuni Myava amethibitisha kutokea kwa kifo cha bosi wake na kudai kuwa amejipiga risasi ya kichwa na kupoteza maisha akiwa amejifungia dukani kwake.

Mfanyabiashara huyo kwa mara ya kwanza aliwasilisha kilio chake tarehe 28 Februari 2019 katika kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wafanyabiashara wa Ilala ikiwa ni
miezi saba tangu alipokutana na mkasa huo tarehe 30 Oktoba 2016 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma kuelekea Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Ntunzwe alieleza mikasa miwili iliyomkuta dhidi ya TRA; kwanza kushikilia mzigo wake kwa miaka mitatu kwa tuhuma za kukwepa kukodi huku yeye akidai
kukataa kutoa rushwa ya Sh2milioni na mkasa wa pili ni kuibiwa mali zake zenye thamani ya Sh986 milioni katika duka lililopo Kariakoo baada ya TRA kulifunga kwa madai ya kutotumia mashine ya EFD.

Chanzo: Mwanahalisi
Serikali isidhani inaendeshwa na maroboti.

Wahusika wote watagawana hii dhambi.

Hamuwezi kuua kisa mnadaiwa
 
Pole Kwa familia ya marehemu, yawezekana mzee wao alikuwa na mengi yanamsibu zaidi ya hiyo madai ya TRA.
Kwa Sasa hakuna wa kumlaumu ila marehemu aliechukua uamuzi mbaya dhidi yake na kusababisha simanzi ya mapema kwa familia, ndugu na jamaa.
 
Back
Top Bottom