Tabia na sifa za Paka ni za kushangaza

Tabia na sifa za Paka ni za kushangaza

Ahsante sana mkuu,mimi ni mdau sana wa paka,hata nikimkuta mgahawani ama poppte lazima nimnunulie maziwa au chakula.

Kuna pahala huwa hukaaga kula chips kariakoo nikifika pale nyau wakinifuata tu lazima niwanunulie mishkaki.

Wakiniona tu lazima waje.

Kuna mwingine nilikuwa namnunulia supu na chapati.
Watu hadi wakawa wananishangaa.


Aisee we kweli ni mdau wa hao viumbe. Sema paka hawapendi mtu fukara
 
Hawa paka ni waajabu sana, kuna vitu vingine ukijiuliza hupati jibu kabisa

Kwa mfano;
Maiti zao zinapotelea wapi?

Kingine wanapofanya mapenzi, kiuhalisia huwezi kuwaona wakifanya mapenzi hadharani, wanyama wengine kama mbwa, mbuzi, ng'ombe na wengineo angalau wengi wetu tumebahatika kushuhudia, ila kwa paka ni nadra sana.

Paka dume akimwaga mayai ukeni mwa paka jike, jike anagaragaza kabisa utafikiri kamwagiwa maji ya moto sehemu za siri huku akipiga kelele haieleweki kama anapata maumivu au la, hawa ndo paka ajabu sana.

Mimi huwa sipati picha kuhusu hawa paka, akijisaidia anafukia, wastaarabu sana

Najua wengine watashare vingi hapa...

Karibuni sana...

paka ni mswahili sana kama unapaka wako ukahamia mtaa unapaka wengi ujue tabia za paka wako zitabadilika
 
Paka katika masaa 24 ya siku analala masaa 13 yani zile dakika tano au mbili anazo lala na kuamka ukijumlisha unapata masaa 13
Kwa ujumla anafikisha zaidi ya asilimia 70 ya maisha yake akiwa usingizini! Ana uti wa mgongo mlaini sana ndio maana hawezi ruhusu kuangukia mgongo!
 
Paka hapotei njia hata siku moja
Kuna paka nilienda kumtupa mbali sana na nyumbani
Wakati wa kurudi nikapotea njia ila bahati nzuri nikamuona yule paka anapita
Nikaanza kumfuata nyumanyuma mwishowe nikajikuta nimetokea nyumbani
Ukimfungia kwenye gunia anapotea. Ila ukimbeba wakati anaona njia lazma arudi ata ukienda kumtupa bagamoyo!
 
Paka ndiyo nini tena mbona mimi najua tu kale kamnyama kapenda starehe kanalia nyau nyau unakakuta kako juu ya friji kanachapa usingizi mara kwenye sofa mara kitandani nahisi kuna watu wamerithi tabia ya Nyau starehe tu kazi hakuna mimi rafiki yako mkubwa ni MBWA wako wawili HOLO NA NGUSSA ndiyo marafiki zako hata ikitokea noma tunasaidizana ila hako kanyau kamo ndani kama pambo tu kulingana tabia zake
Ukiishi maeneo yenye nyoka wengi ma vidudu vingine hatar vitambaavyo ndio utaujua umuhimu wa paka!
Kwa kuongezea paka hafugiki ukikaa nae anajiona ana haki zote za matumizi ya nyimba yako na chakula chako kwa kifupi anakugeuza mtumwa wake!***** paka!
Unaweza kumfiga wewe akiona menyu zako hazieleweki anahamia kwa jirani mazima na kwenye familia anakuwa na washikaji -hampendi chiku lakini yuko bye na Anna na huyu George akinigusa nitampa mikucha hiyo mpka ashangae !
Yaani paka ana make friendship na uadui kama binadamu na ukimafnyia figisu hakusahau !
 
Ni mnyama Ninaye mpenda Sana mpk Sasa Nina paka 6
1. Paka ni mnyama anayejua kudekeza mwanae anaweza akazaa mizao 3 na wote wakanyonya kwa pamoja
2.paka hapendi Fujo, ni mnyama mstaarab Sana
Wewe tutaelewana, sio siri mi paka nampenda mno! Nilipokuwa mdogo nilikuwa nalala nae rum, akifungiwa nje anakuja kulia dirishan kwangu namfungulia. I really love cats as pets more than my love for dogs! Ingawa wote nimefuga pamoja
 
Ukiishi maeneo yenye nyoka wengi ma vidudu vingine hatar vitambaavyo ndio utaujua umuhimu wa paka!
Kwa kuongezea paka hafugiki ukikaa nae anajiona ana haki zote za matumizi ya nyimba yako na chakula chako kwa kifupi anakugeuza mtumwa wake!***** paka!
Unaweza kumfiga wewe akiona menyu zako hazieleweki anahamia kwa jirani mazima na kwenye familia anakuwa na washikaji -hampendi chiku lakini yuko bye na Anna na huyu George akinigusa nitampa mikucha hiyo mpka ashangae !
Yaani paka ana make friendship na uadui kama binadamu na ukimafnyia figisu hakusahau !
Hahah paka yuko live sana, hataki ufala!
 
Kuna jirani hapa paa lake lipo wazi sasa paka wameweka makazi siwapendi sasa paka mmoja akavizie akaingia jikoni nilivyomuona nikamfungia mlango nikaenda kutafuta fimbo kichekesho eti kajificha nyuma ya jiko eti ndo kajificha wakati yupo uchi nikaufungua mlango eti bado kajikunyata nilimfyatulia bakora aliruka huyoo
Ungeendelea kufunga mlango umchape kwa nusu saa mfululizo asione pa kutokea ungeipata shughuli yake! Try it someday ulete mrejesho.
 
We acha mi nikimuona mtu anamsifia paka na kutaka kufuga namshangaa ,kwani ulidhani ilianzaje paka aliletwa home akamate panya sasa akawaleta wenzake kwenye paa huyo paka sijui kakimbilia wapi saizi nimekapiga sana na hapo kwenye paa wameletana kibao ila kwa ukuda wangu wamekimbia wote wamebaki 2 vinganganizi vibishi ila nitakula nao sahani moja lazima watahama ,usiombe atokee dume moja kubwa lazima watapigana usiku kucha....ubaya wa paka lazima atakua na marafiki na hapo ndio tatizo huanzia
Ukimfungia ndani usiku hapati marafiki
 
my granny anawap3nda sana hawa viumbe , nlivyoenda moshi nliwakuta kama 4 hivi yaani wana share yao kwenye chakula kama watu, maziwa akikamua lita10, mbili za paka , tupo watano akienda sokoni ataleta samaki 9 au kumi, dagaa kila siku lazima wale sasa we uoshe vyombo usahau kuosha vyombo vya paka 😂😂😂 kelele zake hutorudia tena,.
alikuwa anawatrain since wameanza kut3mbea ani wakijisaidia ndani anawachapa na kuwalisha kinyesi chao a week wameacha kujisaidia ndani,
ni marafiki wazuri nimecheza nao sanaaa
 
Back
Top Bottom