Tabia na sifa za Paka ni za kushangaza

Tabia na sifa za Paka ni za kushangaza

Mleta mada analenga point zaidi ya moja. Anaigusia anaiacha. Mhhh kuhusu wachawi wanamfanya je? Mshana Jr.
 
Kuna paka wa mtaani walikuA na tabia wakitaka kugegedana wanakuja kufanyia dirishani kwangu, shida ni pale paka labda pair 3 zinagegedana hizo sauti ni zaidi ya sauti 12 za Lucifer kule mbinguni. Teh teh
Unaijua sauti ya Lucifer's?
 
Afu umezungumzia ishu za milio, ni kweli Paka ana milio ya kila dizain na kila mlio hautoi bure unakua na maana yake,
Mlio wa njaa,
Mlio wa kuumwa,
Mlio wa nyege,
Mlio wa kuona hatari au kitu kibaya,
Mlio wa mama kwa wanae akiwaita kula,
Mlio wa mama kwa wanae akiwa hawaoni,
Mlio wa mzee baba akimuita wife wake,
Na mingine mingi.

Kuna mdau kasema Paka akiona sijui mchawi anakua kimya, Wrong, analia sema tu ndio vile unakua huelewi na wengi wakisikia Paka wakilia usiku wanawaita wachawi kuuumbe wanakwambia nyumba yako ipo hatarini.

Je unajua kama Paka ukimpa chakula hua anashukuru?? Anza kuchunguza leo Paka wako ukimpa chakula akiwa anakula au akimaliza kula utaona anausimamisha mkia wake wima huku anauchezesha ukiwa vile vile umesimama basi jua anakushukuru.

Paka akikuona una huzuni anajua lazima atakua karibu na wewe akufariji wala hatokusumbua na ukiwa na furaha anajua basi atakufata ili mcheze.

Paka anaona zaidi usiku kuliko mchana ndio maana mchana hupenda kulala lakini usiku ndio anatembea pia hujikinga na maadui hasa watoto wanaopenda kuwapiga mawe pindi wakiwaona.
 
Yaan napenda sana Paka, Nampenda sana Paka wangu... ukiweza kuishi na huyu mnyama utaenjoy sana.
Ila ndio wana vituko hatari, hua 1.Ananiacha hoi ukimsema kwa jambo fulani ananuna siku nzima basi hali hata umuwekee nini hali ng'oo.

2.Anajua yeye ni sehemu ya familia na akija mgeni atamkarimu kama mwanafamilia.

3. Ana wivu balaa, akija mtoto akiona ninamjali sana yule kuliko yeye anaweza hata kumparua na kulia kila saa hakuishi.

4. Kuna siku anachagua chakula kama hataki dagaa ni hali mpk umpe samaki au nyama au kama kuna samaki halafu ukampa dagaa hali.

5. Akiumwa ana mlio wake anautoa unajua kua minyoo imepamba moto, na akiumwa hali mwenyewe mpk nimlishe tena mimi tu.

6. Siku akiamua kukaa na mimi room hata nimtoe vipi hatoki hasa akiona mgeni fulani fulani hivi (lol) ndio atakomaa rum hatoki mpk namuacha tu.

Ukitaka rafiki wa kweli basi ni Paka ila ukitaka Mlinzi basi ni Mbwa. The choice is yours.
[emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji250][emoji250][emoji250][emoji250][emoji250][emoji257][emoji257][emoji257]umenisaidia kuwasilisha mawazo yangu
 
Tatizo mmezoea paka shume huko uswahilini ,paka aliye lelewa vyema na kufundishwa swala la kudokoa mboga na kunya hovyo halipo kabisaa. Paka kama analishwa vyema na anafundishwa utampenda , ni sawa na mtoto wako usipo mfundisha maadili mema ataishia kuwa shoga na kibaka kama sio malaya

wanyama wafugwao hasa paka na mbwa nao wanahitaji malezi na mafunzo kama ambavyo una fanya kwa watoto wako kinyume na hapo tegemea mbwa koko na paka shume kama ambavyo usipo lea vyema wanao tegemea wavuta bangi na malaya wa kutupwa
Kabisa mkuu,shakuwa na paka hadokoi nyama
 
ujinga wa paka ni pale anapovuka barabara!!
-kweli anajua kuna magari, na ni hatari kuvuka bila kutazana pande zote
-husimama na kutazama kushoto kwa zaidi ya dk 5
-kisha hutazama na upande wa kulia zaid ya dk 5
-Kisha huvuka kwa madoido bila kutazama tena kushoto na gari imekaribia

Ghafla utasikia ..waaaaauuuu....! (kashabutuliwa na gari)

we wachunguze wanapovuka barabara
[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Nilikuwa nampiga kweli.na mpaka Leo uwa sipendi mazoea na paka.usiku kuna mwenzie alikuwa ana kuja.basi yanaanza kucheza kama yanapigana na wanalia milio ya ajabu ajabu.wanakera.nikiamka natafuta mawe yangu tu.
Sasa kesho akija mgeni ndo anafanya hivyo kumpokea na akikuona we we anakimbia.nia yake wewe uonekane mbaya kwa mgeni.kumbe yeye ndo anaanzaga kukuchokoza.kesha kula sana viporo vyangu vya nyama na samaki.
Mkuu Una bifu na paka?
 
Wanauzi ile tabia ya kuomba Chakula, anaomba wee huku anakutazama usoni , matonya cha mtoto. Anaweza omba mkampa cha kutosha tu, akija mgeni mbio anaanza kumuomba.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yani nimecheka mpaka balaa.
 
Wee jamaa wee umenifanya niangue kicheko Cha hatarii. Thanks so much bro
Hiyo ni kweli kabisa. mimi ninaye paka nyumbani, usiku watoto wakienda kulala chumbani na yeye anataka aingie kulala nao. Yaani na yeye ameshajiona kama ni mtoto. Paka ana wivu sana, nikiwapa watoto chakula na yeye anataka apewe hapohapo. Hadi natamani nikamtupe, ila amesaidia sana kuwaondoa panya.
 
Paka ni mnyama mwenye sura ya kuvutia sana. Anasura ya matumaini na kibrazamen au kistaduu.
Paka ni msafi hata kushinda baadhi ya watu mara nyingi hujilamba kama njia ya kujisafisha na kupunguza joto la mwili.
Paka hujisafisha usoni kwa mikono yake ya mbele baada ya kuilama na ulimi. Utakuta analamba mkono then anasafisha uso wake.

Paka hupenda mzaha/utani na michezo tofauti na mbwa ambaye hapendi sana sana.
Paka hutumia akili wakati mbwa hufuata Order au komandi. Paka anaweza akalia ukamwambia acha akakataa lakini mbwa ukimnyoshea tuu kidole aache ataacha mara moja.

Paka hupenda kudeka na kujikomba sana. Pia anaushawishi kwani huweza kukushawishi kwa sauti yake na kujikomba kwake akipita miguuni mkia ukikugusa gusa huku macho yake ya huruma yakikutizama. Kama unahuruma huwezi mnyima paka chakula.

Paka humpenda Baba mwenye nyumba kuliko mama mwenye nyumba. Na pia hupenda watu wanaovaa vizuri na wasionuka harufu za ajabu ajabu. Wanapenda watu wasafi na wacheshi na wenye mahaba.

Paka hapendi utani wa watoto na hawezi kuuvumilia wakati mbwa yeye huweza kuvumilia utani na watoto.

Paka hu-assume kuwa yeye ndiye mrithi wa nyumba husika na mlinzi wa nyumba kwani mara zote yeye ndio hubaki nyumbani na ndiye anayejua nini kinachoendelea ndani ya nyumba husika. Wakati mbwa yeye hutawala zaidi nje na wakati mwingine huweza kuchukuliwa kwa tripu za nje kama kuwinda, kwenda kwenye matembezi ya starehe wakimuachia paka nyumba.

Paka huyaamini masikio yake zaidi ya macho, ndio maana huweza kufumba macho lakini bado akajua kuna hatari imemkaribia. Paka hata akilala kuna uwezekano mkubwa masikio yake kufanya kazi.

Paka kabla hajalala hukariri na kupanga njia atakayo itumie kukimbilia endapo itatokea hatari yoyote.

Paka anatabia ya kukutukana kwa kutoa mlio kama utamsema vibaya. Pia paka unaweza kuongea naye ijapokuwa yeye atabakia na sauti yake ya nyau.

Binafsi nyumbani tulikuwa tunafuga wanyama karibu wote hivyo naelewa kwa kiasi kikubwa tabia zao
 
Usimtupe tafadhali,paka ni rafiki mzuri na mwema sana
 
Ahsante sana mkuu,mimi ni mdau sana wa paka,hata nikimkuta mgahawani ama poppte lazima nimnunulie maziwa au chakula.

Kuna pahala huwa hukaaga kula chips kariakoo nikifika pale nyau wakinifuata tu lazima niwanunulie mishkaki.

Wakiniona tu lazima waje.

Kuna mwingine nilikuwa namnunulia supu na chapati.
Watu hadi wakawa wananishangaa.
 
Back
Top Bottom