Jana, kwenye majira ya saa nane mchana, nikaingia Kisuma Bar pale Magomeni na kuagiza ugali nyama choma. Kama kawaida yao, paka wakanizingira ghafla na kuanza kunipigia kelele.
Safari hii sikuwatilia maanani. Nikaendelea kula bila kujali wanavyonihesabia matonge. Walipokata tamaa wakaamua kujilaza sakafuni na kuanza kuchezeana wenyewe kwa wenyewe chini ya meza.
Nikahusudu jinsi walivyopendana. Ndiyo kwanza nikabaini kuwa hawa paka walikuwa familia moja. Rangi zao zilirandana. Palikuwepo dume na jike waliokomaa, nikahisi ni wazazi. Palikuwepo pia wengine wanne waliopishana ukubwa. Nikabashiri kuwa watoto wao.
Vile walivyocheza pamoja, wakilambana kwa upendo na kunong'onezana kwa lugha yao, ikafanya niipende familia hiyo ya paka, nikaamua kuwashirikisha fahari ya chakula changu kwa kuwatupia vipande vya nyama. Kilichotokea sikuamini macho yangu!
Paliibuka vita ya kuogofya!
Paka waliraruana kwa makucha yao na kuungurumiana kwa chuki ya mauti. Dume likamchakaza jike kwa makofi mfululizo yaliyoambana na mchomozo wa kucha. Kisha akanyakua kipande cha nyama na kujitenga mbali.
Jike nalo likawararua wale wadogo kwa hasira na makelele ya "myaauuuuuu" yakatibua utulivu wa eneo hilo.
Hawa wadogo pia wakashambuliana kwa zamu kikatili kabisa bila kuhurumiana.
Sasa kikabakia kipaka chenye umbo dogo na afya dhaifu. Hicho hakikuambulia kitu. Kikabaki kinapepesa macho na kujilamba kwa uchu wa kinyonge. Niliwafukuza wale wakubwa kwa mateke ndipo nikafanikiwa kukipatia walau finyango moja. Hakikuamini!
Wakati nakitazama jinsi kinavyopambana na kile kipande cha nyama, akili yangu ilienda mbali sana...
* * * *
Kuna watu tunaishi nao lakini wana haiba halisi ya paka wa baa. Wao wanaweza kuwa marafiki, ndugu au jamaa zetu wazuri katika kipindi chote. Lakini pindi inapoibuka fursa ya aina yoyote yenye maslahi ndani yake, husahau mara moja ujamaa na uswahiba wenu wa awali.
Kwenye maslahi wao wapo tayari kuua au kudhuru; wapo tayari kuvunja undugu na kufuta kabisa historia ya ujamaa wenu. Ni watu wanaodhani na kuamini kuwa wao pekee ndiyo wenye haki ya kupata zaidi kuliko wengine. Hata kinachotosha kwa wote, wao hutaka chote peke yao; tamaa yao ni kuhodhi kila kitu peke yao. Na watafanya kila mbinu chafu kuhakikisha hupati chochote. Na ukisogeza pua yako hawakawii kukufisha kama si kukutoboa macho!
Watu wa aina hii ni watu hatari sana. Ukiwa mwerevu utawang'amua mapema kabla hawajakudhuru. Ukiweza kuwatambua, usichangamane nao. Jitenge nao haraka.
Watu wenye hulka za paka wa baa ni watu wabinafsi na wenye tamaa kali. Wamejaa inda na choyo. Hawa watu, ni mfano wa mtu mwenye mbio kali sana. Kama mnakimbia pamoja naye, simama ghafla. Atapiliza. Kisha wewe badili mwelekeo, na asijue abadani ulipoelekea.
Masalkheri