Taasisi za Marekani, zamtambua Muhongo

Taasisi za Marekani, zamtambua Muhongo

Wakati dunia na mataifa ya Magharibi ya Ulaya na Marekani, yakifanya jitihada kubwa kukusanya wasomi wenye vipaji toka sehemu mbalimbali duniani, kwa ajili ya tafiti na vumbuzi ili kijipeleka mbele zaidi kisayansi na kiteknolojia;

na wakati wasomi wanaosaka maslahi zaidi kimaisha wakiendelea kukimbilia Ulaya na Marekani (Brain drain), Wabunge masilahi Tanzania wanafanya jitihada za kubwa kufukuza na kuwakatisha tamaa wachache wenye nyoyo za Uzalendo.

Profesa Muhongo, ni mmoja wa wanasayansi mahiri katika sayansi ya madini (Geologist), anayetambuliwa na kuheshimika na mashirika mbalimbali ya kisayansi na tafiti ulimwenguni.

Miongoni mwa taasisi zinazoaminika kimataifa zinazomtambua na kumtumia Profesa Muhongo katika uwezo wake wa utendaji wa Kazi ni pamoja na FGSA la Marekani, FGS la London, Uingereza: Hon FCAGS la London, Uingereza; Hon FCGS la China, na Chuo cha kuendelea Sayansi ya dunia (FTWAS).


(Source AL-HUDA)

Heading yako iko kishabiki zaidi. Kukosea au kuwa na kashfa hakufuti taaluma aliyo nayo mtu.
 
Kilicho mponza mhongo ni siasa; siasa ni mchezo mchafu; kamwe huwezi fananisha na taaluma zingine za kitaalamu; mtu kama prof. Mhongo haikuwa vema kumtumia katika siasa za nchi hii, na penginepo sehemu nyingi duniani, lazima mziki wa wanasiasa hasa ambao elimu ya shule ni ndogo ungemshinda.....si unajua kwenye siasa unaweza kuwa unajua kusoma na kuandika tu!!!!!!!!!! Ila kwakuwa mhongo anajitambua hawezi fedheheka sana, japo machoni pa watu wengi kwakweli alifedheheka..... Siasa waachiwe akina lukuvi na wengineo...
IPILIMO, kwa kiasi fulani unanishawishi lakini, wizara kama ile ya nishati na madini inahitaji kiongozi msomi, mzalendo kwelikweli na asiyetetereshwa na mafisadi. Sifa hizo Muhongo anazo na ninaamini JK alimpa nafasi hiyo kwa kulitambua hilo.
 
IPILIMO, kwa kiasi fulani unanishawishi lakini, wizara kama ile ya nishati na madini inahitaji kiongozi msomi, mzalendo kwelikweli na asiyetetereshwa na mafisadi. Sifa hizo Muhongo anazo na ninaamini JK alimpa nafasi hiyo kwa kulitambua hilo.

Naunga mkono hoja! Baba Riz analitambua sana hilo nadhani hadi sasa anajuta kumwondoa Jembe maana anajua makali ya Jembe. Miaka miwili na nusu Sekta hizo mbili zimekua na Adabu na Heshima sana sababu ya Muhongo! kwanza jana nimesoma kwenye blogs Wizara imepewa Tuzo sijui na Jarida gani. hebu ngoja niutafute uzi huo niulete hapa! Hata hayo mafanikio ya Tuzo ni wazi amechangia kwa kiasi kikubwa sana!
 
Yani wewe hadi leo hujui tu tatizo sio Utaalamu wake bali ni wanasiasa wenye chuki na visasi? wafanyabiashara wezi na warafi na mafisadi ndio wamesababisha? kama ni mfuatiliaji mzuri utagundua huyu Mzee hakuwa amekaa kianasiasa kama wanasiasa walio wengi. Mwanzo umeanza vizuri nashindwa kukuelewa kwanini umeshindwa kutegua kitendawili hiki! Na wewe changanya na akili zako. Nimeshakuona unashindwa sana katika hili!

Wafanyabiashara na mafisadi wanahusika vipi kuhusu yeye kutambua kuna pesa ya uma kwenye account ya escrow?
Au walimpa rushwa ikalemaza uwezo wake wa kifikiri? Au aliamua kwa hiari yake kushiriki wizi na kuwatetea?
 
Mtaendelea ku guess hivyo hivyo. Makamanda wanamkubali wala yeye haitaji kuingia JF, atafute nini kwanza! Tuseme sisi wachokaza mada!

nimejiridhisha wewe ni zero brain soospeter muhongo,bora ungekaa kimya.
 
Sioni logic katika hii comment yako. Issue si lini mtu kajiunga JF. Jenga hoja.

Atajengaje hoja wakati hajawahi kuwa na akili! Full kuchungulizia! a.ka. Kilaza mzee!
 
mkuu achana na muhongo,kapagawa baada ya kupigwa chini uwaziri na nguvu ya umma!

Nguvu ya umma upi? Kaondoka mwenyewe. Umma haujawahi kumtaka aondoke zaidi ya Magazeti yanayosambaza nakala dar es Salaam na Morogoro halafu yanabaki kila siku maana hayanunuliwi yote.

Nguvu za umma au hongo kwa Wanasiasa Waroho, wenye chuki na wazandiki?

Nguvu ya Umma au wapigaji wa rasilimali za nishati na Madini?

Rudi tena uka google sijui unatumia reference kutoka wapi?
 
nimejiridhisha wewe ni zero brain soospeter muhongo,bora ungekaa kimya.
.

Oyo oyoyoyoyoyoyoyoyo. Kijana rudisha hela za watu watakudai maana hujielewi unachoongea, maneno yako yote yakuuumbiwa kama Silabi!
 
nimejiridhisha wewe ni zero brain soospeter muhongo,bora ungekaa kimya.

Ndugu yangu Nyabhingi, matusi na kejeli hayakusaidii. Unajidhalilisha. Chuki zako personal kwa Muhongo pia hazibadilishi ukweli kwamba jamaa anakubalika na wengi hasa wapenda maendeleo. Tafakari na uchukue hatua sahihi, hujachelewa.
 
Wafanyabiashara na mafisadi wanahusika vipi kuhusu yeye kutambua kuna pesa ya uma kwenye account ya escrow?
Au walimpa rushwa ikalemaza uwezo wake wa kifikiri? Au aliamua kwa hiari yake kushiriki wizi na kuwatetea?

Hilo swali kamuulize Shangazi yako , kizaa mjomba, kizaa mpwa wako maana limechanganyikana sana, HAKIKA sikuelewii
 
chakutaka mbona huyo bwana hayupo kwenye status ya kusafishwa, nyakati za kumsafisha zliisha bila mafanikio na ndio maana kwa uchafu wake na wenzie Nchi imekosa ile asilimia ya bajeti ambayo hao unaosema wanamtambua wanahitaji yeye na wenzie kwanza waburuzwe mahakamani ndipo wa-realise hiyo fund, i wonder kama USA na UK wapo na double standards kama wakwere wa Lugoba.
 
Last edited by a moderator:
mkuu achana na muhongo,kapagawa baada ya kupigwa chini uwaziri na nguvu ya umma!

Nyabhingi, kwanini unawadhalilisha watanzania kwamba si wafuatiliaji wa mambo?! Ni lini Muhongo alipigwa chini uwaziri? Sote tulishuhudia Prof akijiuzulu mwenyewe wadhifa wake. Mwenzetu unatoa wapi taarifa hizo za uongo?
 
Back
Top Bottom