Swali: Hivi kwa sisi wazazi ukisikia mtoto wako wa kiume anavuta sigara, unamkanyaje?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,608
93,374
Tufanye wewe ni mzazi ambaye unainvest pesa nyingi kwa mtoto ambaye bado hajafika University, just yuko high school na ameanza uvutaji wa Sigara kwa siri unafanyaje?

Watoto mkae pembeni kwanza, nataka kusikia maoni ya Wazazi, maana Watoto wa sasa sijui tuwalee kwa style ipi?

Cc: Dr Lizzy say something.
 
Cc:
Aisee nakumbuka kaka yangu alivyomsumbuaga mama yangu tena yeye alikua anavuta bangi nachokumbuka walimuonya wakawa wanamuombea na wakamuhamishia mkoa mwingine na ilimsaidia yan alibadilika na kuacha hiyo tabia
 
Unatakiwa ukae nae chin au umpelekee Kwa daktari aelezwee athari zote za cgara na aonyeshwe na picha picha za baadhi ya watu waliothirika mapafu Kwa ajili ya uvutaji wa cgara..na ikishindikanaa alee viboko na ufukuzee akavutee ukoo na ada usilipee,,,haiwezekan kujaza maji Kwenye gunia
 
Nilimgundua mimi mwenyewe kwamba ameanza kuvuta sigara.

Nikamwita nikakaa nae kistaarabu kabisa nikamuuliza sigara mpaka uikimbilie unapata faida gani?.

Nikamuuliza mimi navuta sigara. Akasema hapana. Vipi babaako mdogo umewahi kuona anavuta?. Akakataa pia. Nikamuuliza vipi ktk familia yote yangu kuna mtu umewahi kumuona anavuta? Akakataa.

Nikamwambia basi ujue yapo mambo ya kuiga na yapo mambo lazima uone yakupite hasa ukiangalia sisi tuliokutangulia. Kama unaona tume-fail mahala ktk kuwaendeleza nyinyi kuanzia kuvaa,kula,kusoma n.k basi ujue ksbb tulikuwa hatuvuti sigara. Ila kama unaona tumefauru kwa kila hatua kuhusiana na nyie wote basi ujue ksbb tulikuwa hatuvuti sigara na pombe pia.

Leo nimekuambia kistaarabu. Siku nyingine haitakuwa kistaarabu kama hivi. Hutanishinda wewe. Kwa hiyo jua umeanzisha vita na mara zote tukuanza ligi mimi na wewe sikubali kushindwa. Kama una hamu na sigara ksbb umeona unakupa faida utavuta ukiwa kwako. Sio ukiwa kwangu. Jiulize mara mbili.

Sikuwahi kumuona tena na hicho kitu
 
Tufanye wewe ni mzazi ambaye unainvest pesa nyingi kwa mtoto ambaye bado hajafika University, just yuko high school na ameanza uvutaji wa Sigara kwa siri unafanyaje?

Watoto mkae pembeni kwanza, nataka kusikia maoni ya Wazazi, maana Watoto wa sasa sijui tuwalee kwa style ipi?

Cc: Dr Lizzy say something.
Mtafutie Jägermeister mpe anywe baada ya kula atakushukuru sana,
 
Mwalimu dunia ni Mbaya sana, anafundisha kwa njia ngumu sana ambazo mwanafunzi atapata uchungu kuliko wa mama yake aliyemzaa.
 
Mimi baba yangu ndie rafiki yangu mkubwa kabla sijafanya kuvuta sigara au bangi, alinambia hasara zake pia na stori zake za kuchekesha na kuhuzunisha.

Mzee una takiwa uanze kumhabarisha mtoto kwenye ukuwaji wake kipi kinafaa na kipi hakifai.

Kaa nae ongea nae mwambie hasara zake kwa afya na matumizi ya hela
 
Tafuta jukwaa la jokes, vijana wa hovyo hii thread mpite kimya kimya, mjifunze ni namna gani Wazazi tunaumia mnavyopotea pamoja na uwekezaji mkubwa wa pesa tunaowafanyia.

Tuliza mshono, stay away.

Tuache hayo

Ndio maana nikakwambia mpe Jägermeister anywe baada ya kula jioni atakushukuru unaniona Mimi wa hovyo

Sawa mimi wa hovyo but you can't stop him once in always in never quit, yeye ndio anajua nini anapitia na nini kimemfanya aingie kwenye uvutaji wa Sigara hili sio suala la peer group km unamuuliza muulize kwa upole na Jenga nae ukaribu sio kumkemea kemea km unakemea mapepo au kumsema sema vibaya, tengeneza closeness na yeye km kweli unataka aache, nicotine ikishaingia imeingia na withdrawal ya nicotine inauma balaa km ni muoga hawezi kuacha kirahisi rahisi lazima ataendelea kuvuta tu
 
Tufanye wewe ni mzazi ambaye unainvest pesa nyingi kwa mtoto ambaye bado hajafika University, just yuko high school na ameanza uvutaji wa Sigara kwa siri unafanyaje?

Watoto mkae pembeni kwanza, nataka kusikia maoni ya Wazazi, maana Watoto wa sasa sijui tuwalee kwa style ipi?

Cc: Dr Lizzy say something.
Ndugu hizo ni athari za makundi na malezi uvutaji wa sigara sio wake pekeake wapo wengi nyuma yake Cha muhimu ongea nae kirafiki akueleze shida na changamoto anazopitia ,chunguza marafiki na tabia zake binafsi then mpe muda ajitathmini baada ya hapo mmbadilishie mazingira
 
MImi wakat naanza, hata mimi nlikalishwa na kukanywa sana.
Lakini i feel like it was too late.
Nliendelea kwa kificho hadi nikawa mtu mzima. Hua nakataa nkiulizwa, lakini to be honest katika kitu kigumu kuacha ni nicotine.
Wakakomaa wakaniambia kama imeshindikana, bas at least wacha kuvuta ganja kwanza af uache na mafegi pia.
Nkaskiliza ushauri, nkaacha ganja (9 yrs sober as of now), baadae nkaacha pombe (4 yrs sober now), sigara nmeamua tu kua pindi mwanangu atAkapozaliwa sitavuta tena. Ni nadhiri nlijowekea kua sitaki anikute bado nachoma.
To be honest bwana Dr Matola PhD , jitahidi kwa nguvu zote kumkanya aache mapema kabla nicotine receptors hazijawa fully triggered. Ni ngumu kuacha chiga kuliko kuacha mitungi.
Cha muhim, wahi mapema, talk to him kistaarabu, tena ongea nae kama mtu mzima maana mostly watu wanaanza kuvuta fegi ili kupata ile feeling ya grandiosity among their peers, so ukiweza kuongea nae akaona kbsa kua umemconsider kama mtu mzima, then kias flan inaweza kusaidia kuacha mapema.
I wish you well mzee, hicho ni kipengele.
 
sigara nmeamua tu kua pindi mwanangu atAkapozaliwa sitavuta tena
Mzee umemwambia ukweli mtupu withdrawal ya nicotine inauma balaa ukiacha fegi km hujaamia kwenye GIN kukata maumivu ya withdrawal sijui emu tupe feelings za fegi wewe hua unajisikiaje ukivuta na je unapenda kuvuta ukiwa umeshiba chakula au ukiwa hauna kitu tumboni, unapenda kuvuta ukiwa umekaa, umesimama au unatembea? Ipi Sigara unayopenda kuitumia nyota, ubalozi, sm au ston?
 
Nafikiri kama mzazi kuna mistake ulifanya wakati kijana wako anakua, na hili kosa tunalifanya wazazi wengi sana. Mzazi unapaswa kua rafiki wa watoto wako, zungumza nao jambo lolote zuri na baya. Waeleze wanao madhara ya zinaa, pombe, sigara nk: na hii itawafanya watoto wajengeke kisaikolojia na watambue ubaya wa haya mambo mapema hata wakiwa mbali na nyumbani (wanakua na ile hali ya kwamba baba alinikataza hiki).
Ushauri:-
Kwakua tayari umegundua kijana ameanza matumizi ya sigara, basi muite kwa upole na ongea nae kwa kirefu huku ukimueleza madhara ya uvutaji wa sigara, pia mueleze ajue namna jamii itakavyo mtazama kwa tabia yake ya uvutaji wa sigara akiwa na umri mdogo.
Pia jaribu kuongea nae aepukane na aina ya marafiki alio nao kwa sasa na ikiwezekana muhamishe shule na umoeleke shule ambayo anaweza akapata udbibiti zaidi ya alipo.
Anza kuongea kuwasiliana nae mara kwa mara hata anaookua shuleni omba mwalimu uongee nae, hakikisha kila unapo ongea nae unamkumbusha na kumsiaitiza kuhusu uvutaji wa sigara ambao unaweza ukamuharibia afya na hata maisha yake iwapo atafukuzwa shule.
Mwisho kabisa, mfanye atambue kwamba haupendezwi na tabia alio ianza, na hakikisha anafaham kwamba iwapo ataharibu shule kwa ajili ya uvutaji wa sigara basi akae akijua kwamba mafasu yake haipo tena hapo nyumbani kwako (atafute pakwenda).
 
Tufanye wewe ni mzazi ambaye unainvest pesa nyingi kwa mtoto ambaye bado hajafika University, just yuko high school na ameanza uvutaji wa Sigara kwa siri unafanyaje?

Watoto mkae pembeni kwanza, nataka kusikia maoni ya Wazazi, maana Watoto wa sasa sijui tuwalee kwa style ipi?

Cc: Dr Lizzy say something.
Kuna vipindi katika makuzi lazima apitie.. Kikubwa asiharibikiwe
Kuna maendeleo yake shuleni je anafanya vizuri?
Kuna makundi mitaani, marafiki shuleni na watu anao intaract nao inabidi yote haya uyajue walau 70%
Ukaribu wako kwake ni muhimu sana
Mahusiano ya kifamilia
Nafasi yake katika familia!
Je unamjali kiasi gani? Unamheshimu kiasi gani!?
Je unayatambua madhaifu yake? Kushindwa kwake? Kushinda kwake?
Je anapendelea nini? Nyakati gani nknk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sigara ama kilevi chochote si kitu cha kujikuta tu ipo mdomoni. Ni vitu ambavyo kwa kiwango kikubwa kinachagizwa na makundi na matamanio.

Makundi haswa yana asilimia kubwa katika kushawishi mtu mwingine kuenenda katika njia hiyo. Kama anavuta sigara maana yake kuna wenzake wanavuta na yeye akawiwa kuijaribu. Kudanganyana kuwa unajisikia high ukivuta ndiyo haswa imewapoteza vijana.

Sasa, kwa kuwa umeshajua mapema, bila shaka huyo hajawa addictive. Uwezo wa kumbadilisha unao bado. Ukilega ndiyo utampoteza kabisa.

Hivyo, muweke mbali na makundi na hata mazingira yanayomshawishi kutumia vilevi hivyo. Mpige marufuku kuambatana na aina ya marafiki unaodhani wanamshawishi.

Msikilize haswa ni nini kilimvutia katika utumiaji huo wa sigara. Kisha crash matamanio yake kwa tahadhari na madhara ya uvutaji wa sigara na bangi pamoja na utumiaji wa vilevi.

Muombee kwa Mungu kama wewe ni muamini.

NB: Kama mzazi ni mtumiaji wa sigara (haswa wa kiume) ni ngumu sana kufanikiwa kumkataza mwanae uvutaji. Watoto wanaiga sana.
 
Back
Top Bottom