Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Salam Wakuu,

Katika malezi ni muhimu sana mtoto ajihisi kupendwa na wazazi wake ama na yoyote anayemlea. Ni ngumu kwa mzazi/mlezi kuwapenda watoto wote sawa, lakini ni muhimu kwa watoto wote kujihisi wanapendwa na kujaliwa na wazazi/walezi wao.

Mtoto anayepata mapenzi na upendo kutoka wa wazazi wake; kwanza anakuwa huru kueleza changamoto zake pale anapokwama, lakini pia ni rahisi kwa wewe mzazi kugundua mapema kama kuna tatizo kubwa linamsumbua hata asiposema, sababu tayari una ukaribu naye kiasi cha kuona tofauti pindi asipokuwa sawa.

Mtoto anafikisha mpaka miaka 15 hajawahi kusikia hata siku moja mama au baba yake wake anamwambia anampenda, mtoto huyu akikutana na mtu akaonyesha kumjali na kumpa upendo wa kuziba nafasi yako unafikiri atashindwa kumrubuni?

Na usitegemee kwamba wa kumrubuni anaweza akawa kwenye mazingira ya hapo karibu tu, mtoto wako anaweza kupata rafiki mtandaoni ambae ataona kuna mwanya huo akautumia vizuri. Mwanzo ataanza kumuonesha upendo na mapenzi, na mtoto akishamuamini ni rahisi kumfanyia chochote. Wengine wanaweza kwenda mbali kabisa mtoto akatekwa ukibahatika kumpata ni maiti, lakini hayo ilifikaje huko, ni kwa sababu mtu alipata mwanya ambao ni wajibu wako kuufanya akautumia vizuri.

Na ikishatokea hivyo mtoto wala hatakwambia kuwa nimekutana na mtu amesema moja, mbili, tatu kwasababu atakuwa mtu muhimu kwake anaemtendea vema kuliko wazazi wake, kwanini asimuamini zaidi na kuhamisha upendo, mapenzi na kumthamini mtu huyo kuliko wazazi wake?

Kibaya ni kwamba mtu huyo aliyeaminiwa anaweza kufanya ukatili kwa mtoto wako wala usijue, mpaka unakuja kushtuka unakuwa umechelewa, mtoto ameshaharibiwa kwa miaka na wewe upo hapo hapo, wakati ungetoa muda wako na kuonesha upendo kwa mtoto wako ungeweza kuepusha mambo mengi.

Kuna watu wapo azma yao ni kutafuta watoto kuwafanyia ukatili ama kuwafanya bidhaa kwa watu wengine wenye matamanio hayo maovu, wengine wanaweza kuwa ni wafanyabishara haramu ya viungo vya binadamu, anakuja kuziba nafasi yako vizuri, anampa mtoto upendo wako wote lakini lengo lake sio kusaidia, tuwe makini.

Mzazi unafurahi na kuhadithia kabisa, yaani mtoto wangu anampenda fulani kuliko mimi, nikimuacha kwake nafanya kazi zote hata hasumbui, JITAFAKARI. Wazazi hasa wanaume wanaona hili halina maana, tubadilike. Mtoto wako wa kike au wa kiume akijua baba na mama wananipenda unatengeneza ukaribu kati yenu na kufanya iwe ngumu kurubuniwa na watu wengine na kumuepusha na vitu vingine vibaya vinavyoweza kutokea, tuwe macho.

Narudisha swali kwenu wazazi na walezi, mara ya mwisho kumwambia mtoto wako unampenda ni lini?
 
Mi huwa sina muda huo wa kufanya undenzi kama mzazi. Badala yake wao wanajua mapenzi yangu kwao hata bila kusema ama kuwaambia.

Ikifika wikendi ama likizo kama salio lipo basi ni kutoka nao out, kuwaptia kile nafahamu wanahitaji, kuzungumza nao nini wanahitaji kwangu, kuwaambia nini sitaki wafanye, then kuwawekea malengo ya shule na kutimiza ahadi zangu kwao kwa alietimiza malengo yake tuliyowekeana.
 
Salam Wakuu,

Katika malezi ni muhimu sana mtoto ajihisi kupendwa na wazazi wake ama na yoyote anayemlea. Ni ngumu kwa mzazi/mlezi kuwapenda watoto wote sawa, lakini ni muhimu kwa watoto wote kujihisi wanapendwa na kujaliwa na wazazi/walezi wao.

Mtoto anayepata mapenzi na upendo kutoka wa wazazi wake; kwanza anakuwa huru kueleza changamoto zake pale anapokwama, lakini pia ni rahisi kwa wewe mzazi kugundua mapema kama kuna tatizo kubwa linamsumbua hata asiposema, sababu tayari una ukaribu naye kiasi cha kuona tofauti pindi asipokuwa sawa.

Mtoto anafikisha mpaka miaka 15 hajawahi kusikia hata siku moja mama au baba yake wake anamwambia anampenda, mtoto huyu akikutana na mtu akaonyesha kumjali na kumpa upendo wa kuziba nafasi yako unafikiri atashindwa kumrubuni?

Na usitegemee kwamba wa kumrubuni anaweza akawa kwenye mazingira ya hapo karibu tu, mtoto wako anaweza kupata rafiki mtandaoni ambae ataona kuna mwanya huo akautumia vizuri. Mwanzo ataanza kumuonesha upendo na mapenzi, na mtoto akishamuamini ni rahisi kumfanyia chochote. Wengine wanaweza kwenda mbali kabisa mtoto akatekwa ukibahatika kumpata ni maiti, lakini hayo ilifikaje huko, ni kwa sababu mtu alipata mwanya ambao ni wajibu wako kuufanya akautumia vizuri.

Na ikishatokea hivyo mtoto wala hatakwambia kuwa nimekutana na mtu amesema moja, mbili, tatu kwasababu atakuwa mtu muhimu kwake anaemtendea vema kuliko wazazi wake, kwanini asimuamini zaidi na kuhamisha upendo, mapenzi na kumthamini mtu huyo kuliko wazazi wake?

Kibaya ni kwamba mtu huyo aliyeaminiwa anaweza kufanya ukatili kwa mtoto wako wala usijue, mpaka unakuja kushtuka unakuwa umechelewa, mtoto ameshaharibiwa kwa miaka na wewe upo hapo hapo, wakati ungetoa muda wako na kuonesha upendo kwa mtoto wako ungeweza kuepusha mambo mengi.

Kuna watu wapo azma yao ni kutafuta watoto kuwafanyia ukatili ama kuwafanya bidhaa kwa watu wengine wenye matamanio hayo maovu, wengine wanaweza kuwa ni wafanyabishara haramu ya viungo vya binadamu, anakuja kuziba nafasi yako vizuri, anampa mtoto upendo wako wote lakini lengo lake sio kusaidia, tuwe makini.

Mzazi unafurahi na kuhadithia kabisa, yaani mtoto wangu anampenda fulani kuliko mimi, nikimuacha kwake nafanya kazi zote hata hasumbui, JITAFAKARI. Wazazi hasa wanaume wanaona hili halina maana, tubadilike. Mtoto wako wa kike au wa kiume akijua baba na mama wananipenda unatengeneza ukaribu kati yenu na kufanya iwe ngumu kurubuniwa na watu wengine na kumuepusha na vitu vingine vibaya vinavyoweza kutokea, tuwe macho.

Narudisha swali kwenu wazazi na walezi, mara ya mwisho kumwambia mtoto wako unampenda ni lini?
Ni leo asubuhi
 
Labda kila mtoto umwambie kwa wakati wake mkiwa wawili tu, kinyume na hapo ni kuwajengea chuki wao kwa wao.

Hata hivyo matendo yako tu kwao yatawaonyesha ikiwemo na viboko vya hapa na pale.
 
sijawahi kuambiwa na mzazi kuwa ananipenda lakini nimekuwa nikiamini miaka yote kuwa walikuwa wananipenda kwa dhati.

-Sijawahi kulala na njaa wala kukosa mahitaji yangu muhimu katika umri wangu nilipokuwa mdogo mpaka nimekuwa wa kujitegemea.

-nikikokesa nilikuwa nikirekebishwa kwa maneno makali na mara chache sana kwa fimbo (once nakumbuka nilifuata ngoma nikachelewa kurudi mpaka usiku - hapo nilikula kichapo lakini siyo kingi)

- nikipewa ushauri muafaka na baadhi ya wakati tulikwa tunazungumza mambo ya maisha kwa ujumla na nasaha kuhusu maisha.

Ila 'I love you, mwa mwaa....' haikuwepo na mpaka hii leo wazazi wangu marehemu lakini nawakumbuka kwa upendo.
 
Hizi tamaduni za kimagharibi zinatuharibu sana. Binafsi sijawahi kumwambia mtoto wangu yeyote kwamba ninampenda, bali watu wengine pamoja na mama yao ndio hua wananiambia kwamba ninawapenda sana watoto wangu.
Mkuu, upendo hauoneshwi bali huonekana.
 
Back
Top Bottom