Mtoto wa kiume jikaze, acha kulegea, mtoto wa kiume halii! Tusipobadilika tutawapoteza!

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Mtoto wa kiume amekuwa akipitia changamoto nyingi tu katika jamii kama mtoto wa kike, ila unakuta wao kusema inakuwa vigumu kwa sababu wameaminishwa kuwa wao Kidume, Nguzo ya Familia, akilia anaambiwa jikaze mtoto wa kiume halii, akionesha kuumia anachekwa anaambiwa acha kulegea, mwisho siku kila anachopitia anakiweka moyoni.

Kesi za watoto kiume kulawitiwa zimekuwa nyingi wakati huu tukilinganisha na zamani, wanapitia ukatili mkubwa lakini hawasemi. Unakuta mtoto anafanyiwa unyama anakaa kimya maana alishaambiwa mtoto wa kiume kujikaza usiwe unalialia kama dada yako, mpaka siku anakuja kusema hali inakuwa mbaya.

Haya yote wa kulaumiwa ni sisi wazazi na walezi, tunawajengea watoto hawa picha ambayo kiuhalisia inaharibu watoto, mzazi anaona fahari mtoto wake akiwa mbishi mbishi, mtundu, waswahili wanakwambia nunda kwamba huo ndio uanaume wanasahau kama ilivyo kwq watoto wakike, wakime nao wanahitaji kuongozwa na wewe mzazi ndio kioo chake, ukimpotosha mwanzo ni vigumu sana kuja kumyoosha akishakuwa mkubwa na kuweza kujisimamia.

Ndio hawa unasikia leo kampiga fulani, kesho kafanya vurugu kule, mara kila mtu anamwogopa hakuna anayetaka kumsogelea, tunajisahau kuwa tunatengeneza wazazi wa baadaye, sasa unatengeneza mzazi gani ambaye ambaye amezoea ukorofi, kutoonesha hisia, ubabe, kama tabia ya kawaida?

Ni muhimu kuwafundisha watoto wa kiume jinsi ya kudeal na hisia zao, kuongea zaidi wanayoyapitia, kusema pale wanapoona mambo hayapo vizuri, na kutovumilia aina yoyote ya unyanyaji, ili hata akiona mtoto mwenzake anafanyiwa awe wa kwanza kusema. Tusiache kutilia mkazo wa watoto wakike lakini pia tusijisahau kwa watoto wa kiume kiasi cha kuwapoteza kabisa na kuishia kujilaumu.
 
NAUNGA MKONO HOJA

TUFUNDISHE MADOGO WASIKAE KINYONGE, WAKAZE NA MAMBO YA KIPUUZI WAACHE...
 
Back
Top Bottom