Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Nje ya mada .
Mkuu naomba nikuulize kuhusiana na hiyo caption yako ya"house girl"
Vipi una experience yoyote kuhusiana na matendo wanayofanyiwa? Kwaninini umeichagua kama caption?


Sent using Jamii Forums mobile app
SUASO
 
Kwanza niwatakie heri ya Krismasi kwa JF Members wote. Ninatumai wote ni wazima wa afya, leo nimejaribu kutafakari baadhi ya mambo na kuamini ule msemo wa mfadhili "MBUZI UTAMLA MCHUZI" binadamu atakuudhi.

Nitazungumzia xperience yangu kuhusu the so-called friends and relatives

1. Kanda ya Ziwa.
Nikiwa Meneja wa Mkoa taasisi fulani ya fedha, niliwahi fuatwa na vijana wawili ambao walikuwa ni wahudumu wa hoteli kuomba niwasaidie as kiukweli japo kwa hali ndogo nilokuwa nayo ila nilisaidia wengi hasa nikikumbuka safari yangu ilivokuwa. Nakumbuka niliwapa nafasi ya kuwa Sales Reps na kwa kuwa walikuwa wanaishi pale hotelini na wafanyakazi wenzao, kuwarahisishia na kuwapa mwanzo mzuri niliwachukulia chumba nikalipa 6months rent, nikanunua kitanda, godoro, jiko, pasi etc and of course walishukuru sana. I personally trained those guys, gave support and invested much on them, mwisho they became the best in my branch. Wakatoka katika kulipwa 90,000/= per month na kuweza kupata minimum 1mil per month, in other words not less than 200k per week as commission. Of course was proud, ila kilichokuja tokea Mungu ndo anajua na ikanibidi niombe transferna kuhama mkoa. Ikatengenezwa figisu na ikaundwa team with my admin, vijana wakapikwa kidogo nifukuzwe kazi [emoji848] mwisho malipo ni hapa hapa duniani wote walifukuzwa na nilipohama tawi na mkoa mauzo yakadrop. Jana nimekutana na mmoja wapo ni Mchungaji now baada ya kupata malipo matakatifu, kuvunjika mguu, kukoswa kufungwa na kampuni kwa wizi, etc. Kaniomba samahani sana, nimemjibu nilishamsamehe muda mrefu sana na awe na amani.

2. Kanda ya Ziwa
Nilifatwa na kijana ambaye alihitaji kazi Ila kwa elimu yake hakukidhi vigezo, and the guy was passing through hell. Dah, roho yangu hii nikamuonea huruma nikamchukua na kununua bodaboda
nikampa mkataba 1yr malipo 70per week, kijana akaanza vzr na pesa alikuwa anadeposit bank na kuniletea slip. Kilichokuja kutokea siwezi kuelezea, mpaka nikatengenezewa kesi ambayo ni Mungu tu aliniokoa.. Yakafuata matukio ya kishirikina mpaka nyumba yangu nilojenga na nilokuwa nakaa ikabidi nihame kuhofia uhai wangu.

3. Kanda ya Kaskazini
Way back 2010 nikiwa nimejiajiri na nimefungua kampuni ikijishugulisha na fumigation, stationary services and supplies, music studio production audio and video, electronic money transfer. Nikamchukua mtoto wa ma mdogo nikamtrain jinsi ya kuproduce music kuanzia beat, vocal mixing etc, at first dogo akawa mtiifu sana, nikamuacha nikiwa nasimamia kazi ili nami nijigawe mambo yaende, dah nakumbuka ni siku moja nimesafiri Dar kufata mzigo na kuonana na my co director ambaye ndo aliwekeza capital, niliporudi sikukuta kitu maana alisafisha studio, ofisi za stationary na items zote. Nilipigiwa xm ucku nikiwa Dar, nilirudi nikiwa siamini ila nilipofika na kuona empty shelves and office, nililia sana na mwisho co director mwenzangu alitaka kunifunga, thanks to God alileta njia. Dogo nilikutana nae Dar kachoka vby, na alinitafuta yeye ila nimemsamehe toka moyoni.

4. Makazini
Nimewahi fanyiwa fitina na wasaidizi wangu kisa wivu na chuki, nikahamisha vituo na wao kuwa promoted kushika nafasi yangu ila within first quarter wote waliprove failure na kufukuzwa kazi baada ya ukweli kuja kugundulika..

Kwa kifupi nimepitia mengi sana kwenye maisha yangu, achilia mbali ajali, kuwa broke from a person who was well off financially, kuzulumiwa pesa nyingi sana na mwisho kutengwa, ila niwatie moyo wote ambao mna wakati mgumu au mnapitia magumu kamwe msikate tamaa, God is always in control.

Nikikumbuka nilipotoka na hapa nilipo, japo sijafika bado ambapo nilikuwa before ila namshukuru Mungu sana.

Kwa yeyote pia ambaye alifanya mema na kulipwa mabaya pls share with us, ili wengine wajifunze pia

Niwatakie sikukuu njema
Pole sana mkuu. Miaka ya 2007 nilimnunulia ndugu wa mbali gari ili aitumie kama taxi lengo kuu ni kuisaidia familia ya kwao maana walikuwa na hali ya chini sana kiuchumi. Tulikubaliana kiasi fulani kiwekwe bank kwa ajili ya running costs kama insurance n.k. alifanya kwa miezi tu baadae nilipohoji kidogo nifungwe maana hata card ya gari alishabadilisha jina kwenda la kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka 2015 nadai laki 5 haki nilipitia kipindi kibaya sana kicuhumi lakini mdai wangu hata 30,000 hajantumia naona anapost biashara zake tu juzi, kuna siku akapost senene ndoo anauza.
Nikamfata nikamuambia basi naonba nitumie ndoo moja ya senene nitafune nipunguze machungu hakunijibu.
Imagine ndoo moja ya senene kwa laki 5

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka Kama mazuri vizuri..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Relief Mirzska,

Duh pole Mkuu..

Nilichojifunza ni kuwa ukiwa na roho nzuri sana daima hutoendelea, mi nilifungua ofisi ya welding Kigamboni and invested 2mil.. Alinifata jamaa ambaye anakaa karibu na Shemeji yangu (mke wa bro)

I gave that person 2mil, ambayo ilitosha kununua mashine 3 (grender, driller and cutter) jamaa cjui ilikuwaje nikamuamini kiasi kile, shida ikaja kwenye receipt za mashine ukizingatia nilikuambia ahakikishe ananua vyote dukani na alete receipts.

Mpaka tunapozungumza jamaa nimekuwa adui mkubwa Sana kwake, mashine anadai alinunua kwa mtu, nikamwuliza with whose permission!?

Out of 2mil, kanunua cutter 400k (ambayo alinambia kanunua 850k), drill machine 150k, grender it's nearly 3months now haijafika kwa madai aliyemtumia pesa yuko Zanzibar na hapatikani.

Inaenda miezi 3 na ofisi hajanipa hata kumi, awali nilidhani ni ugumu wa kazi ila kufuatilia nikagundua alifanya kazi ya msikiti akalipwa 700k, akafanya nyingine akalipwa 1.5m, and the last 1.2m, aisee nilishikwa na hasira mpaka kidogo pressure inipande.

Baada ya kuanza kufuatilia jamaa akaanza kuhamisha kazi anafanyia kwingine sababu pale ofcn nimeweka msimamizi na anambana,, kiukweli ninajuta sana.

Jana nimembana mpaka ndugu zake wameamua wauze kiwanja wanipe pesa yangu maana kiukweli nilikuwa namfunga, analia kama mtoto mdogo, mbaya pesa yangu ndo kaolea Nov 2019 mwishoni, yaani nikikumbuka mpaka roho inaniuma.

Ila nimeamua wanilipe maana walitaka wanipe kiwanja nikakataa, kwa hasira nilizonazo hazielezeki ila hakika Mungu atamlipa kabisa, tena naomba amlipe kabisa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16], show no love, love will get you killed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna msela mavi alifukuzwa kwa dada yake akaniomba hifadhi gheto akae kwa siku tatu, mimi nilikuwa silali huko gheto kwangu enzi hizo naanza kujitegemea kimaisha.
Baadae jamaa kageuka kama mtoto wangu anakuja kuomba hadi hela ya chakula ofisini kwangu.
Miezi haondoki kama alivyosema, hataki kazi ya kuajiriwa niliyomtafutia. Akaanza kuvaa nguo zangu bila ruhusa.
Mwisho wa siku msela mavi kaniibia kila kitu gheto hadi nguo za ndani na personal note books.
Hilo sengerema ni age mate, classmate, lilitaka nililee miaka kama mtoto wangu.
Liliacha kitanda, godoro na fridge tu, liliiba hadi vifaaa vyangu flani nilivyokuwa nimetunza gheto baada ya kufunga biashara yangu sehemu.

Waswahili maneno mengi wale wanakuambia mfadhili mbuzi utakula nyama au mfadhili mbwa anaweza kukulindia nyumba yako, sio binadamu majanga tu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu. Miaka ya 2007 nilimnunulia ndugu wa mbali gari ili aitumie kama taxi lengo kuu ni kuisaidia familia ya kwao maana walikuwa na hali ya chini sana kiuchumi. Tulikubaliana kiasi fulani kiwekwe bank kwa ajili ya running costs kama insurance n.k. alifanya kwa miezi tu baadae nilipohoji kidogo nifungwe maana hata card ya gari alishabadilisha jina kwenda la kwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16],show no love, love will get you killed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh!
Majuto nnayojuta mimi..hayaelezeki.
ni mengi..
Mbaya zaidi mpaka ndugu yako pekee tena wa toka nitoke..ndio anakuwa nyuma ya hayo...
Imenipa majeraha na maumivu..ya daima!
Si sote tunaoishi..humu... wengine ni frem. .
Binaadam sisi...kweli tulirithi dhambi ...
Jahhanam hii hapa...


Sent using Jamii Forums mobile app
tupe story moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unasema. Sisi tunajionea huku mume anahamia kwa mchepuko mazima, mke unabaki unagaagaa na upwa. Huo uvumilivu nivumilie labda anirudie bado akiwa "asset", sio maisha yamemgonga. Changamoto hazikosekani, ila tuzisolve mapema; sio hadi ujichokee maisha na afya ndo oooh mke wangu nimerudi, afu mimi ndo nianze kujisifia uvumilivu wangu sijui nini eeh. Furaha haiji kwa kuhesabu miaka ya ndoa tangu mfunge ndoa au kuitwa mke huku mume mwenyewe kakuhama.
ukipata mwanaume ambae hachepuki mheshimu sanaaaa,sababu anakuwa anaenda kinyume na nature yake kwa ajili yako,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule alikuwa zaidi ya usaliti halafu heartless. Mtu ambaye hata akuumize vipi hajui neno samahani....nilichogundua umalaya ukizidi unaondoa utu.
Siwezi kuishi bila Amani ya moyo kwakweli nikafupisha maisha yangu kwa mtu ambaye kwa upeo wake Hana mchango wowote kwangu kimawazo zaidi ya kunijazia stress.

Nisimulie kidogo kuhusu huyo mama...
may be na wewe upande wako ulikuwa una shida,angekuja na yeye kuongea hapa na yeye aongolee madhaifu yako ingekuwa vizuri,kila kitu kinatokea kwasababu ya reason

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ilikuwa mwaka 2014, nikiwa msimamizi mkuu wa kituo fulani hivi cha kutoa huduma kwa umma, nilimpokea dada fulani hivi akiwa ni new employee. nilimpokea na kwakuwa kulikuwa na uhaba wa nyumba basi nilimkaribisha (kwa hiyari yake) kuishi katika nyumba niliyokuwa nikiishi mimi (ya mwajiri). alikaribia na maisha yakaenda vizuri huku tukiheshimiana vema tu kama kaka na dada. usilolijua ni sawa na usiku wa giza!

siku moja aliniita na kuniambia kuwa kuna mgeni wake fulani (boyfriend) anakuja kumtembelea. aliniambia kama mwenyeji wake nilimkaribisha ndani. nikaona ni jambo jema tu, tena la kiheshima, kuniambia. nikamtoa wasiwasi na kumwambia kuwa asiwe na wasiwasi wowote alete tu shemeji nitampa ushirikiano. alikuja na kwakuwa yule dada alishanieleza hilo basi nikamchangamkia tu shemeji yangu vizuri tu huku nikishiriki matukio ya hapa na pale kama vile kuwapa taarifa za wapi kuku wanapatikana n.k.

alivyoondoka sasa yule jamaa (nakumbuka alikaa siku mbili), yule dada aliongea maneno mengi mno ya kunikashfu/ kunivunjia heshima. mara aseme alinishangaa jinsi nilivyomchangamkia mtu wake utafikiri alikuwa mgeni wangu mimi n.k. baadae sana akatangaza kuwa ninamtaka......sikuyajua haya yote maana sina stori sana na majirani ingawa tunaheshimiana sana. nilikuja kuambiwa karibu miezi minne hadi mitano tangu aanze kunichafua na aliyeniambia alinishangaa kuwa imekuaje sijui mpaka sasa wakati wao wanasahau tena habari hizo. nillikereka sana lkn kwakuwa lilishapita muda na nilimuona kama yule dada ni mshamba wa kupitiliza basi nikaamua kukauka tu lakini nilimwita na kumwambia kuwa hakufanya jambo jema. aliomba msamaha lakini binafsi nilijiapiza kamwe sitokuja kuishi na mfanyakazi mwenzangu mwanamke nyumba moja huku nikiwa boss wake. kamwe!!!! she is approaching 32 now!

ajabu sasa, yule dada amekuwa kama analaaniwa tu kutokana na mdomo wake, haolewi na wala hapati mwekezaji wa kueleweka.....wanatumia na kuondoka tu. amezakishwa mtoto mmoja lakini baba hajui tu kama ana mtoto!!!!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3], show no love,love will get you killed,ungekuwa kauzu yasingekukuta haya,ona sasa umeshavunjiwa heshima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimpenda kutoka moyoni mwangu nikajishusha mnoo, nikambadilisha kutoka kuwa mchafu mchafu hadi akawa mtu anayejua japo kuoga......maisha yake yalikuwa ya kijima kiasi kwamba hata akiwa na hela bado ni wale watanunua andazi la stend na kunywa na juice zile wanapitia ha bila kujali usafi... Sikutaka ionekane kwamba mwanamke ukiwa umemzidi ME elimu na exposure basi mahusiano hayawezekani. Mwanzo I ilikuwa ngumu lakini badae nikajikuta nshampenda na watu hawakuamini Kama tumeweza kuwa pamoja kwa kipindi kirefu. Kifupi nilikuwa deeply in love.
Siku zote watu watakunyima hela na chakula Ila hawawezi kukunyima neno. Wao walijua ni nini alikuwa anafanya Huko nje wakawa wanaongea mwisho waliopoona siwasikilizi wakanyamaza.

Mwisho nikaja kugundua hakustahili mapenzi yangu na alikuwa zaidi ya nilivyodhani kwa mambo ya ajabu aliyokuwa anafanya. Niliamua kulipa kibinadamu Ila mwisho nikaamua kumuachia Mungu anilipie.

Binafsi naona matajiri wapendane wao kwa wao, maskini wapendane wao kwa wao, wasomi wapendane wao kwa wao na wasio na elimu wapendane wao kwa wao. Maana unaweza ukawa na nia nzuri Ila unayempenda a siamini Kama inaweza kana. Haya mambo sijui ya true love tuwaachie wazungu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2007 nilimaliza mafunzo ya ufundi veta, nikawa nafanya kazi za mtaani mwaka 1 baadae nikakutana name bint mchaga sura nzuri had tabia .

Alitengetengeneza mazingira ya kumpenda na kweli ikawa hivyo.
Mwaka 2009 nilipanga chumba name kutoka Kwa mzee, bahati mbaya nae nyumbani kwao akawa hatakiwi maana alikuwa akiishi kwa baba yake alie Kuwait name mke mwingine.

Nilitafuta sehemu ya kwenda kukaa Kwa ninao wafahamu hatimae nikapata kwa dada 1 akakaa wake.

Ilibidi nizunguke pale mjini kutafuta kazi nilizunguka sana nikapata kampuni ya ukusanyaji wa ushuru maegesho ya Magari.

Miezi 3 baadae dada aliekua akikaa nae alimfukuza ikabidi nikaaongee name mzee wangu akaniruhusu nikakae nae yeye atamalizana na mzazi mwenzake.

Nikabeba mke jioni ya SAA moja jumamosi tarehe 12 mwezi wa 9 2009.


Hapo ndipo kizaa kilipo anza , nilikaa nae miaka mitatu. Ndani ya hio miaka 3 ndipo nilipojua wakati mwingine likuepukalo lina heri ndani yake.

Kwa ufupi Kwa kua alikua amesoma had kidato cha 4 na matokeo mazuri, nilianza kumtafutia college kuanzia ualimu unesi misitu mifugo computer veta kote huko akakosa, hiyo iligarimu mwaka na nusu.


Aliugua kifua kikuuu Kwa muda wa miezi nane ndio alipona, kipindi hiki kidogo kilinipa challenge Kwa kiasi kikubwa.
Miezi minne baadae mama yake mzazi aliugua na kufariki (R I P) hapa napo mziki wake ulikua si haba.

Miezi 3 baada ya hili nilifiwa na mlezi wangu alien nilea toka nikiwa na mwezi 1 hapa napo niliumia mno!

Baada ya haya ilibidi nimtafutie cha kufanya.
Dada mmoja akaniambie anafungua kibanda stand hivyo kama ataweza akakae hapo.
Alinipa kazi ya kutengeneza kibanda maana mimi ni seremala, akanipa hela nikanunue bidhaa ,nilitumia usafiri wa baiskel nilirudi mjini Mara 8 tena bado kidogo nigongwe na lori, mwishowe nikaenda kumchukua yeye mke wangu kuja dukani. Kumbe ndio nampeleke Kwa mume mwingine.


Alianza kurudi nyumban Saa nne tofauti na makubaliano.
Alikuwa akiwasifia watu wengine wanamaendeleo tofauti na Mimi.
Mwishoni akaniambia tuachane!

Kweli aliondoka na mimi nikabaki na maumivu name umaskini.

Miaka minne niliipoteza kwake lakini aliniacha kwenye Mata, na athari alizoniachia mpaka leo sijasimama kimaisha vizuri.
Lakini taarifa nilizonazo yeye yupo safi na nyumba wanayo.

Yote ni maisha name maisha yanaendelea , poleni wakuu Kwa mikasa mliokutana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom