Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

ilikuwa mwaka 2014, nikiwa msimamizi mkuu wa kituo fulani hivi cha kutoa huduma kwa umma, nilimpokea dada fulani hivi akiwa ni new employee. nilimpokea na kwakuwa kulikuwa na uhaba wa nyumba basi nilimkaribisha (kwa hiyari yake) kuishi katika nyumba niliyokuwa nikiishi mimi (ya mwajiri). alikaribia na maisha yakaenda vizuri huku tukiheshimiana vema tu kama kaka na dada. usilolijua ni sawa na usiku wa giza!

siku moja aliniita na kuniambia kuwa kuna mgeni wake fulani (boyfriend) anakuja kumtembelea. aliniambia kama mwenyeji wake nilimkaribisha ndani. nikaona ni jambo jema tu, tena la kiheshima, kuniambia. nikamtoa wasiwasi na kumwambia kuwa asiwe na wasiwasi wowote alete tu shemeji nitampa ushirikiano. alikuja na kwakuwa yule dada alishanieleza hilo basi nikamchangamkia tu shemeji yangu vizuri tu huku nikishiriki matukio ya hapa na pale kama vile kuwapa taarifa za wapi kuku wanapatikana n.k.

alivyoondoka sasa yule jamaa (nakumbuka alikaa siku mbili), yule dada aliongea maneno mengi mno ya kunikashfu/ kunivunjia heshima. mara aseme alinishangaa jinsi nilivyomchangamkia mtu wake utafikiri alikuwa mgeni wangu mimi n.k. baadae sana akatangaza kuwa ninamtaka......sikuyajua haya yote maana sina stori sana na majirani ingawa tunaheshimiana sana. nilikuja kuambiwa karibu miezi minne hadi mitano tangu aanze kunichafua na aliyeniambia alinishangaa kuwa imekuaje sijui mpaka sasa wakati wao wanasahau tena habari hizo. nillikereka sana lkn kwakuwa lilishapita muda na nilimuona kama yule dada ni mshamba wa kupitiliza basi nikaamua kukauka tu lakini nilimwita na kumwambia kuwa hakufanya jambo jema. aliomba msamaha lakini binafsi nilijiapiza kamwe sitokuja kuishi na mfanyakazi mwenzangu mwanamke nyumba moja huku nikiwa boss wake. kamwe!!!! she is approaching 32 now!

ajabu sasa, yule dada amekuwa kama analaaniwa tu kutokana na mdomo wake, haolewi na wala hapati mwekezaji wa kueleweka.....wanatumia na kuondoka tu. amezakishwa mtoto mmoja lakini baba hajui tu kama ana mtoto!!!!
 
Jambo Muhimu kwenye maisha ni kutenda mema kwa mtu ukitegemea vitu viwili either kulipwa ule wema au kutokulipwa hii itakusaidia kupunguza stress

Kwakuwa akikutendea wema kwa ulitegemea aiumi
Lakini pia akikutendea ubaya kwasababu ulitegemea pia hakuna tabu

Tunapokosea tunategemea kulipwa sana tukisahau kuto kulipwa ndio inapotokea kutokulipwa unaishia kumchukia mtu na kumdharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujitahidi kuishi kwa amani na upendo kama mtu unauwezo wa kusaidia mtu msaidie tu na kama huna basi mwambie tu ukweli.

Wema ni kama akiba kamwe haiozi itatudi tu.
 
Pole sana mkuu, ni bahati mbaya tuu usijumuishe.

Lakini ungekaza huo upepo mbaya upite Leo ungekua unaongea lugha nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nisingeweza kuvumilia zaidi kwa kuwa alichonifanyia ningemganda ningeumia zaidi, bora nilivyokubali kwamba mzoea punda farasi hapandi nkaamua kusonga mbele
 
Mrs Bishanga, hujasema alifanya nini?
Nilimpenda kutoka moyoni mwangu nikajishusha mnoo, nikambadilisha kutoka kuwa mchafu mchafu hadi akawa mtu anayejua japo kuoga......maisha yake yalikuwa ya kijima kiasi kwamba hata akiwa na hela bado ni wale watanunua andazi la stend na kunywa na juice zile wanapitia ha bila kujali usafi... Sikutaka ionekane kwamba mwanamke ukiwa umemzidi ME elimu na exposure basi mahusiano hayawezekani. Mwanzo I ilikuwa ngumu lakini badae nikajikuta nshampenda na watu hawakuamini Kama tumeweza kuwa pamoja kwa kipindi kirefu. Kifupi nilikuwa deeply in love.
Siku zote watu watakunyima hela na chakula Ila hawawezi kukunyima neno. Wao walijua ni nini alikuwa anafanya Huko nje wakawa wanaongea mwisho waliopoona siwasikilizi wakanyamaza.

Mwisho nikaja kugundua hakustahili mapenzi yangu na alikuwa zaidi ya nilivyodhani kwa mambo ya ajabu aliyokuwa anafanya. Niliamua kulipa kibinadamu Ila mwisho nikaamua kumuachia Mungu anilipie.

Binafsi naona matajiri wapendane wao kwa wao, maskini wapendane wao kwa wao, wasomi wapendane wao kwa wao na wasio na elimu wapendane wao kwa wao. Maana unaweza ukawa na nia nzuri Ila unayempenda a siamini Kama inaweza kana. Haya mambo sijui ya true love tuwaachie wazungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya mambo, inafaa kumwachia Mungu. Ni ngumu kusamehe na kusahau ila kisasi ni juu ya Mungu na sio sis wanadamu.
 
Kifupi nisiwachoshe.Nilitumikia mwaka mzima kusimamia kazi ya jamaa bila malipo.Japo nilipewa uhuru wa kutumia pesa ya manunuzi na dharura bila kuulizwa.Aliniambia tu hii pesa ni kwa ajili yangu na yako.Hapo pakiisha utapata ajira.Ukinikwamisha ni umejikwamisha mwenyewe.Mara chache siku za sikuku ananiambia chukua pesa ya sikuku.Nachukua 50k bila kupangiwa si zaidi ya hapo.

Mwaka ukakatika jamaa kafilisika.Pesa hana.Kazi hana.Ujenzi ukaishia kati.Mzee nimepiga mwaka mzima.mvua na jua,Usiku mbu na n'ge wangu.Nikaambulia laki 2.Mwaka mzima narudi sina pesa sina chochote.Sikuweza kununua hata godoro wa ule mtumbwi wangu.Nguo zote zilichakalia pale.Jamaa akanitelekeza hata alipopata kazi akunijali tena.Mawasiliano yakawa finyu.Fadhila,muda na uaminifu wangu haukua kitu tena(sijutii).Niliumwa anapita hata kuja kuniona hakuna.Urafiki ukafifia kama sio karibia kufa.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom