Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Son Of Almighty

Senior Member
Jun 28, 2017
123
428
Kwanza niwatakie heri ya Krismasi kwa JF Members wote. Ninatumai wote ni wazima wa afya, leo nimejaribu kutafakari baadhi ya mambo na kuamini ule msemo wa mfadhili "MBUZI UTAMLA MCHUZI" binadamu atakuudhi.

Nitazungumzia xperience yangu kuhusu the so-called friends and relatives

1. Kanda ya Ziwa.
Nikiwa Meneja wa Mkoa taasisi fulani ya fedha, niliwahi fuatwa na vijana wawili ambao walikuwa ni wahudumu wa hoteli kuomba niwasaidie as kiukweli japo kwa hali ndogo nilokuwa nayo ila nilisaidia wengi hasa nikikumbuka safari yangu ilivokuwa. Nakumbuka niliwapa nafasi ya kuwa Sales Reps na kwa kuwa walikuwa wanaishi pale hotelini na wafanyakazi wenzao, kuwarahisishia na kuwapa mwanzo mzuri niliwachukulia chumba nikalipa 6months rent, nikanunua kitanda, godoro, jiko, pasi etc and of course walishukuru sana. I personally trained those guys, gave support and invested much on them, mwisho they became the best in my branch. Wakatoka katika kulipwa 90,000/= per month na kuweza kupata minimum 1mil per month, in other words not less than 200k per week as commission. Of course was proud, ila kilichokuja tokea Mungu ndo anajua na ikanibidi niombe transferna kuhama mkoa. Ikatengenezwa figisu na ikaundwa team with my admin, vijana wakapikwa kidogo nifukuzwe kazi 🤔 mwisho malipo ni hapa hapa duniani wote walifukuzwa na nilipohama tawi na mkoa mauzo yakadrop. Jana nimekutana na mmoja wapo ni Mchungaji now baada ya kupata malipo matakatifu, kuvunjika mguu, kukoswa kufungwa na kampuni kwa wizi, etc. Kaniomba samahani sana, nimemjibu nilishamsamehe muda mrefu sana na awe na amani.

2. Kanda ya Ziwa
Nilifatwa na kijana ambaye alihitaji kazi Ila kwa elimu yake hakukidhi vigezo, and the guy was passing through hell. Dah, roho yangu hii nikamuonea huruma nikamchukua na kununua bodaboda
nikampa mkataba 1yr malipo 70per week, kijana akaanza vzr na pesa alikuwa anadeposit bank na kuniletea slip. Kilichokuja kutokea siwezi kuelezea, mpaka nikatengenezewa kesi ambayo ni Mungu tu aliniokoa.. Yakafuata matukio ya kishirikina mpaka nyumba yangu nilojenga na nilokuwa nakaa ikabidi nihame kuhofia uhai wangu.

3. Kanda ya Kaskazini
Way back 2010 nikiwa nimejiajiri na nimefungua kampuni ikijishugulisha na fumigation, stationary services and supplies, music studio production audio and video, electronic money transfer. Nikamchukua mtoto wa ma mdogo nikamtrain jinsi ya kuproduce music kuanzia beat, vocal mixing etc, at first dogo akawa mtiifu sana, nikamuacha nikiwa nasimamia kazi ili nami nijigawe mambo yaende, dah nakumbuka ni siku moja nimesafiri Dar kufata mzigo na kuonana na my co director ambaye ndo aliwekeza capital, niliporudi sikukuta kitu maana alisafisha studio, ofisi za stationary na items zote. Nilipigiwa xm ucku nikiwa Dar, nilirudi nikiwa siamini ila nilipofika na kuona empty shelves and office, nililia sana na mwisho co director mwenzangu alitaka kunifunga, thanks to God alileta njia. Dogo nilikutana nae Dar kachoka vby, na alinitafuta yeye ila nimemsamehe toka moyoni.

4. Makazini
Nimewahi fanyiwa fitina na wasaidizi wangu kisa wivu na chuki, nikahamisha vituo na wao kuwa promoted kushika nafasi yangu ila within first quarter wote waliprove failure na kufukuzwa kazi baada ya ukweli kuja kugundulika..

Kwa kifupi nimepitia mengi sana kwenye maisha yangu, achilia mbali ajali, kuwa broke from a person who was well off financially, kuzulumiwa pesa nyingi sana na mwisho kutengwa, ila niwatie moyo wote ambao mna wakati mgumu au mnapitia magumu kamwe msikate tamaa, God is always in control.

Nikikumbuka nilipotoka na hapa nilipo, japo sijafika bado ambapo nilikuwa before ila namshukuru Mungu sana.

Kwa yeyote pia ambaye alifanya mema na kulipwa mabaya pls share with us, ili wengine wajifunze pia

Niwatakie sikukuu njema
 
Mwaka huu wakati tukianza mwaka mpya kulikuwa na nafasi za kazi kwenye company yetu. Kama kawaida zilitakiwa zijazwe, niliamua kwa dhati kabisa kutafuta vijana wenye sifa kutoka humu jukwaani (JF).

Mchakato ulifanyika na hatimae nkaajiri vijana watatu kutoka humu humu ambao mmoja alikuwa na experience kidogo na wawili are straight from school wamemaliza pale UDSM 2018. Mmoja yule mwenye experience baada ya muda mchache aliamua kuacha kazi baada ya kuomba salary increment na mimi kukataa hilo ombi kwa sababu haikuwa hata na miezi 4 kazini, kilichoniudhi ni namna alivyoondoka, alidanganya kwamba anaenda kumuangalia mzazi wake mgonjwa, na pia alichukua baadhi ya vifaa vya ofisini. Tulitegemea angekaa na Sisi ila ndio hivyo.

Wa pili kati ya hawa watatu ni kijana mmoja anaetoka kanda ya ziwa. Much know kwa sana, he considers himself the most knowledgeable and best employee out of all we have. Alikuwa akim criticise supervisor wake kwenye staff meeting in front of all other staff. Sio mara moja sio mara mbili. Nidhamu yake ni mbaya sana, alifikia mpaka kumtongoza one of the manager (foreigner) from the same office. At first alikuwa akiniheshimu/kuniogopa mimi tu because he knew I was making the calls. I went out of my way in helping him establish his life, salary ikikata mnamo tarehe 20 I would give him loans or my personal money. Baada ya kurudi one of my trip around August this year supervisor wake akanieleza mashakil yake. Nikaanza kukata all favors alizokuwa akipata from me. Akaona I was no longer a friend to her, I was only a boss at work and nothing more. As long as he could do his job and not insult anyone, everything was okey for me. At last, he had to go, and he had to go himself, what happened mpaka akaondoka mwenyewe sitaki kusema hapa but yeah he had to leave kwa kejeli na dharau na shutma kubwa dhidi yangu. Shutma moja ni kwamba mimi nimemchawia na namfanyia uchawi, usiku akilala ananiona namkaba🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Sijui why hakumtafuta Mshana Jr hahaahahahahha

Huyu kijana wa tatu bado nipo nae, he is doing good and he is my friend, he loves talking to me about Manchester United and would joke to me about Arsenal. He thinks I am the best boss in the world and may be he is reading this hahahaahahahah.

Sijisifii lakini humu jukwaani nimeshawasaidia watu si chini ya 10 msaada wa maana sio hizi 10,000 au 15,000 ila sasa nimeacha.

Ndio maana the other time nkamwambia Cresida be careful.

cc: SweetieLee and Karma
 
Relief Mirzska,

Duh pole Mkuu..

Nilichojifunza ni kuwa ukiwa na roho nzuri sana daima hutoendelea, mi nilifungua ofisi ya welding Kigamboni and invested 2mil.. Alinifata jamaa ambaye anakaa karibu na Shemeji yangu (mke wa bro)

I gave that person 2mil, ambayo ilitosha kununua mashine 3 (grender, driller and cutter) jamaa cjui ilikuwaje nikamuamini kiasi kile, shida ikaja kwenye receipt za mashine ukizingatia nilikuambia ahakikishe ananua vyote dukani na alete receipts.

Mpaka tunapozungumza jamaa nimekuwa adui mkubwa Sana kwake, mashine anadai alinunua kwa mtu, nikamwuliza with whose permission!?

Out of 2mil, kanunua cutter 400k (ambayo alinambia kanunua 850k), drill machine 150k, grender it's nearly 3months now haijafika kwa madai aliyemtumia pesa yuko Zanzibar na hapatikani.

Inaenda miezi 3 na ofisi hajanipa hata kumi, awali nilidhani ni ugumu wa kazi ila kufuatilia nikagundua alifanya kazi ya msikiti akalipwa 700k, akafanya nyingine akalipwa 1.5m, and the last 1.2m, aisee nilishikwa na hasira mpaka kidogo pressure inipande.

Baada ya kuanza kufuatilia jamaa akaanza kuhamisha kazi anafanyia kwingine sababu pale ofcn nimeweka msimamizi na anambana,, kiukweli ninajuta sana.

Jana nimembana mpaka ndugu zake wameamua wauze kiwanja wanipe pesa yangu maana kiukweli nilikuwa namfunga, analia kama mtoto mdogo, mbaya pesa yangu ndo kaolea Nov 2019 mwishoni, yaani nikikumbuka mpaka roho inaniuma.

Ila nimeamua wanilipe maana walitaka wanipe kiwanja nikakataa, kwa hasira nilizonazo hazielezeki ila hakika Mungu atamlipa kabisa, tena naomba amlipe kabisa
 
Aisee mara nyingi watu unaowasaidia kipindi kigumu wanakuja kukutenda vibaya hii inanitokea sana mimi.

Kipind niko chuo nikawa nime invest mtaji almost 2m na msimamizi akiwa ni binamu yangu(alikuwa kamaliza diploma ya uwalimu na yuko jobless).
Tuliubaliana atasimamia ile kazi mpaka tuone matokeo mazuri.Ee bwana haujaisha hata mwezi kumbe kapata tempo na ofisi kanambia kafunga!.nilivurugwa hatari na auliza mauzo mara hoo nilitumia nitakupa.
Nilipata hasira nikamwambia hamisha vitu vipeleke home a nauli nilimtumia.

Akapeleka baadhi ya vitu kumbe pc alibakiza aliendelea kuingizia nyimbo kwenye saluni ya jirani.Baadae akawa ana mtaji wa 500k sijui akajichanganya kwa demu wake wamelala akamchapa zote.Jamaa alichapka balaa akarid kupakia tofali kwenye malori lakin hola.Ilifika hatua kodi ya ya nyumba 15000 ikawa inamshinda maana walifikishana hadi kwa balozi na mwenye nyumba akapewa wiki moja alipe au la afurushwe
Ikabd anirudie kuomba msaada,nikamgomea akalia wee ikabd nimchane namna alivyonifelisha lakini mwisho nilimsamehe ikabd nimpe hela 100k asave jahaz.lakin nayo mpaka leo hakumalizia kunilipa.

2.Kuna dogo wakati nahama dsm nilitaka hamisha vyombo vya geto nije navyo mkoa.Kanililia naomba niachie geto hela nitakupa mwakani(alikuwa kakosa mkopo)
Bahat nzuri mwaka uliofatia akapata mkopo lakini mpaka leo hii hela yangu hajanipa ananipiga viswahili tu.
Nimegundua mwisho kusaidia hawa watu ni ukuda tu mwisho wanang'ang'ania wakuumize wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee na mungu huwa anajua kuwaadhibu haichukui mda.wanatiaga huruma wengine mpaka huja kuomba msaada tena.
Kimsingi huruma inatuponza sana wenye mioyo ya kusaidia.
Mie kuna kisa cha kima mmoja nikiandika hapa pilau ntashindwa kulila! Hata kinywaji hakitapanda!kifup usiwe mwema sana!

Erasto kitu ulichonifanyia sitasahau! Na madhila unayoyapata ss hv najua ni kofi!dadeq!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom