Mwaka 2007 nilimaliza mafunzo ya ufundi veta, nikawa nafanya kazi za mtaani mwaka 1 baadae nikakutana name bint mchaga sura nzuri had tabia .
Alitengetengeneza mazingira ya kumpenda na kweli ikawa hivyo.
Mwaka 2009 nilipanga chumba name kutoka Kwa mzee, bahati mbaya nae nyumbani kwao akawa hatakiwi maana alikuwa akiishi kwa baba yake alie Kuwait name mke mwingine.
Nilitafuta sehemu ya kwenda kukaa Kwa ninao wafahamu hatimae nikapata kwa dada 1 akakaa wake.
Ilibidi nizunguke pale mjini kutafuta kazi nilizunguka sana nikapata kampuni ya ukusanyaji wa ushuru maegesho ya Magari.
Miezi 3 baadae dada aliekua akikaa nae alimfukuza ikabidi nikaaongee name mzee wangu akaniruhusu nikakae nae yeye atamalizana na mzazi mwenzake.
Nikabeba mke jioni ya SAA moja jumamosi tarehe 12 mwezi wa 9 2009.
Hapo ndipo kizaa kilipo anza , nilikaa nae miaka mitatu. Ndani ya hio miaka 3 ndipo nilipojua wakati mwingine likuepukalo lina heri ndani yake.
Kwa ufupi Kwa kua alikua amesoma had kidato cha 4 na matokeo mazuri, nilianza kumtafutia college kuanzia ualimu unesi misitu mifugo computer veta kote huko akakosa, hiyo iligarimu mwaka na nusu.
Aliugua kifua kikuuu Kwa muda wa miezi nane ndio alipona, kipindi hiki kidogo kilinipa challenge Kwa kiasi kikubwa.
Miezi minne baadae mama yake mzazi aliugua na kufariki (R I P) hapa napo mziki wake ulikua si haba.
Miezi 3 baada ya hili nilifiwa na mlezi wangu alien nilea toka nikiwa na mwezi 1 hapa napo niliumia mno!
Baada ya haya ilibidi nimtafutie cha kufanya.
Dada mmoja akaniambie anafungua kibanda stand hivyo kama ataweza akakae hapo.
Alinipa kazi ya kutengeneza kibanda maana mimi ni seremala, akanipa hela nikanunue bidhaa ,nilitumia usafiri wa baiskel nilirudi mjini Mara 8 tena bado kidogo nigongwe na lori, mwishowe nikaenda kumchukua yeye mke wangu kuja dukani. Kumbe ndio nampeleke Kwa mume mwingine.
Alianza kurudi nyumban Saa nne tofauti na makubaliano.
Alikuwa akiwasifia watu wengine wanamaendeleo tofauti na Mimi.
Mwishoni akaniambia tuachane!
Kweli aliondoka na mimi nikabaki na maumivu name umaskini.
Miaka minne niliipoteza kwake lakini aliniacha kwenye Mata, na athari alizoniachia mpaka leo sijasimama kimaisha vizuri.
Lakini taarifa nilizonazo yeye yupo safi na nyumba wanayo.
Yote ni maisha name maisha yanaendelea , poleni wakuu Kwa mikasa mliokutana nayo.
Sent using
Jamii Forums mobile app