Haya majanga tunayo wengi sana,
Nilimfungulia mdogo angu wa tumbo moja biashara mtaji wa ml2, na nilimwambia yeye achague aina ya biashara na frem ilikua tayari, akanunua vitu km redio, tv, deki na vingi vya dizaini hizo, kwa kipindi hicho hiyo biashara ndio ilikua inaenea kwa kasi sana mitaani, tulikua tunauza sana kwa siku tunaenda mjini mara mbili, ndani ya mwaka mtaji ushafika ml10, nktamtafutia msaidizi huku mimi nikiendelea na mishe zangu,
Yaani baada ya mwaka duka limeisha enzi zile za deci washamla ml3 yake akisubiri kuvuna ndio ikafa, nilipata hasira nkalifunga akawa hana kazi mama analalamika namwachaje mdogo angu hivyo, kwa hasira nkampa kiduka kilikua uswazi ila mtaji tu vingine kama friji makreti na vingine aviache, mwisho wa siku na hilo kala kamaliza na ela ya mama laki 7 alimpa aongeze mtaji ikaishia hapo...
Baada ya miaka mi3 karudi kuomba msamaha baada ya kukosa kuuwawa akiwa anapokonywa bodaboda nkamsamehe nkamfungulia tena biashara iliyogharimu ml3.5 baada ya mwaka na nusu nilienda apo nikakuta imefungwa hadi leo sijui iliishia wapi...
Na majanga ya kumlelea watoto wake wa3 kaniachia.
Kipindi hicho nahangaika kutafuta ela mtaji mdogo jamaa yangu tunaishi karibu nkawa namuazima ela, kila laki1 baada ya mwezi nampa laki na kumi, nikichukua laki 3,4, 5 ni hivyohivyo, baada ya mambo yangu kua mazuri yeye ndio akawa ananiazima ela nkawa nampa tena bila riba yoyote baadae 1.6ml ilifia kwake hadi sa hivi hapokei simu yangu.
Kuna watu tumeumbwa kua daraja la wengine kufanikiwa ila hawajitambui hata kidogo mwisho wa siku chenga tupu
Sent using
Jamii Forums mobile app