Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Na mimi nilitaka nimuulize vizuri huo ushujaa wa mke wa ndoa ni kumpokea mume ambaye kashajichokea maisha na kuchokwa na bi mdogo au? Hapo unashindwa hata kujua kuwa amerudi kwa mke wa ndoa kwa sababu ni kweli amegundua makosa yake au kwa sababu maisha yamemchapa. Mtu u-fight na kuvumilia mume arudi akiwa bado anadai, sio mtu anajirudisha mwenyewe akiwa apeche alolo mwingine na maradhi juu afu ndo useme umeshinda. Huo ushindi me siutaki khaa
Apeche alolo. 🤣🤣🤣🤣

Heaven nakusalimu
 
Wewe unasema. Sisi tunajionea huku mume anahamia kwa mchepuko mazima, mke unabaki unagaagaa na upwa. Huo uvumilivu nivumilie labda anirudie bado akiwa "asset", sio maisha yamemgonga. Changamoto hazikosekani, ila tuzisolve mapema; sio hadi ujichokee maisha na afya ndo oooh mke wangu nimerudi, afu mimi ndo nianze kujisifia uvumilivu wangu sijui nini eeh. Furaha haiji kwa kuhesabu miaka ya ndoa tangu mfunge ndoa au kuitwa mke huku mume mwenyewe kakuhama.
Maga gaa na upwa hali wali mkavu lakini 😀😀😀😀😎😎😎😎😎
 
Wapo wacha Mungu. Waaminifu walioamua kutulia kwenye ndoa zao. Kama ni mchepukaji Sio kuchepuka Kwa madharau na kumtelekeza mke asee. Afiche kiasi kwamba hata mke akiambiwa asiamini. Hapo sawa nisijue Ila nikijua awe tayari kumuacha.
Sasa jamani si Bora tu nioe mke wa pili kuliko kuchepuka kusiko kwa madharau??

By the way, wanaume inabidi tujifunze kuwa na heshima kwa wenzi wetu, mtu ukizidiwa usichepuke kwa madharau
 
Daaah nimeamini ni kweli kaka/dada zetu wanatupiga sana tafu ila sisi madogo sometime tunazingua.
Nakumbuka ile nimetok chuo mwaka jana 2018. Nimerui maskani broo wangu (mwajiliwa wa serikali) akanambia niraute biashara ila mtaji usizid 2mil. Ila kutokana na mawenge niliyokua nayo nikamwambia broo ngoja kwanza nipambane kitaaa ikiwezekana nichapike sanaa, ili akili ikiniingia nitajua nini cha kufanya kwenye biashara. Nilikua naogopa nicije nikaingia kichwakichwa na kufeli.
Baadae nimamuomva mtaji wa kama laki tano hiv kuna biashara nilitaka niianzishe ilikua nikodi mashine ya kutobolea mawe (compressor machine) ila mambo yakaenda kombo baada ya mwenye mashine kuingia mitini na nusu ya hela 280k. iliyobaki nikajikuta naitumia tu kwa matumizi mengine bila kufanya nilichopanga. Ila nilipomueleza broo hakuchukia na alinijibu kwa ukarimu mpaka nikajikuta nahuzunika.
Baadae nkamueleza nahitaji kuanzinza mradi ila mtaji ni kama milioni 18 ambapo nimekadiria faida itakua almost 2mil kwa mwezi (na zaidi ya hapo) ila hiyo ni standard profit not minimum or maximum (kama sijakosea maana mm sio mchumi, ni mwalimu wa historia by professional). Na kikubwa ni kuinunua hiyo compressor mashine ili nipigie kazi mwenyewe, akagoma kua ni pesa kubwa sana.
Baadae broo alinunua gari mwezi wa 7kwa milioni 12, nikamuomba tena anisaidie nitimize malengo yangu ya mradi maana nimetafura watu wengi sana wote wananichomolea kikubw Nachokumbana nacho ni kuwa hawaniamini wanaogopa nisije nikaingia mitini. Lkn broo amekua sitaki nataka maana aliniambia nisubir afikirie, baadae akanambia atakopa benk toka mwezi wa 8 mpka now ananiambia atakopa. Lkn nahic anaogopa nisine nikamlostisha akai gia deni. Na nahic laki tano aliyonipa nikafeli ndo i amfanya asiniamini sana kwa hela kubwa kiasi hicho.
Ila kuna rafiki yake niliwahi kumueleza kuhusu huo mradi akaupenda baadae akamwambia broo kama hawezi basi wachangiane wanipe hiyo mashine lkn broo kagoma kwa madai kya yeye peke ake anaweza kukopa na kunipa hiyo mashine.
Ko nimevaki tu njia panda natamani afanye hivyo. ila namuheshimu sana maana kanisomesha advance na university. Wito wangu kwa sie madogo tuwaheshimu sana mabroo na ma sister zetu, Wanajitolea sana kwetu ila tu vile tunalungukiwaga na uelewa tunaona kama vile wanatuendesha au kutupelekesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezo wake milioni 2

Wewe unataka 18

Dogo utasubiri sana

Usawa huu nani akukopee mil 18 ambazo zinaweza kwenda na maji abakie kukatwa deni miaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu sio ushujaa

Ni ujinga tu kama ujinga mwingine


Huyo mwanaume ana bahati kuoa mke asiyetambua thamani yake

La.sivyo angekula alipopeleka mboga
Huyu mama alichukuliwa kutoka kijijini kwa lengo la kupatiwa kazi baada ya malengo take ya Kuwa mtawa kushindikana.

Kaletwa kwa mume aside mjua wakaishi wakafunga ndoa wakazaa mtoto wa 1,2 name 3.

Mume anakazi serikalini tena kipindi kile cha shirikisho la Africa mashariki.

Miaka fulani mume kapata kabint cha kidato cha pili akazaa nacho Mke akajua akarudi kijijini kwa wazazi lakini wakapatanishwa akarudi kwa mume.

Mumeakazaa name yule binti tena motto wa pili, hapa mke akalipa akazaa na jamaa mmoja hivi.

Mke alikua ana kaa na mdogo wake, mume akatembea na mdogo wa mke akazaa nae.
Kesi zikaamuliwa mke akatulia.

Yule binti baada ya uzao wa pili akajengewa nyumba name alisomeshwa mpaka kawa daktari wa binadamu.
Alifunguliwa duka la dawa
Baba yake alijengewa nyumba
Watoto wake walisoma mpka vyuo vya ulaya huko.


Mke wa ndoa aliendelea kubaki mama wa nyumbani, akishuhudia huduma bora Kwa mke mdogo.
Watoto wa mke Mkubwa aliesoma sana kidato cha nne.

Nyumba aliokua akikaa ni kota.

Matokeo Leo hii mume hana hata mia
Mke mdogo aliolewa na mume mwingine
Mume hana hata ramani Kwa hio anaishi Kwa hisani ya mke wa ndoa na mke wa ndoa amempokea mumewe Kwa Upendo na kumsamehe na wanaishi kama hakuna kilichotokea.

Kwa sasa mke Mkubwa ndie shujaa alivumilia changamoto ngumu ya usaliti salsa hivi yeye ndie mshindi.

Ndio maana nikasema kwako wewe ingekuwa bora sana kama ungevumilia ule upepo mbaya upite japo sijajua ni baya kiasi gani lakini hakuna baya chini ya Juan lisiloisha name kusameheka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa jamani si Bora tu nioe mke wa pili kuliko kuchepuka kusiko kwa madharau??

By the way, wanaume inabidi tujifunze kuwa na heshima kwa wenzi wetu, mtu ukizidiwa usichepuke kwa madharau

[emoji23][emoji23][emoji23]hata ukioa wa pili bado utamchoka tu maana shida ni tamaa ya kuonja kila kipya kilicho mbele.

Ila waliovumilia walirudi uzeeni baada ya kuchoka na meno kung'oka.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hata ukioa wa pili bado utamchoka tu maana shida ni tamaa ya kuonja kila kipya kilicho mbele.

Ila waliovumilia walirudi uzeeni baada ya kuchoka na meno kung'oka.
Swali ni je, ntamchoka baada ya muda gani?? Na baada ya muda huo kweli zile desires za mke wa tatu zitakuwepo?? There are number of factors to be considered.
 
Haya majanga tunayo wengi sana,
Nilimfungulia mdogo angu wa tumbo moja biashara mtaji wa ml2, na nilimwambia yeye achague aina ya biashara na frem ilikua tayari, akanunua vitu km redio, tv, deki na vingi vya dizaini hizo, kwa kipindi hicho hiyo biashara ndio ilikua inaenea kwa kasi sana mitaani, tulikua tunauza sana kwa siku tunaenda mjini mara mbili, ndani ya mwaka mtaji ushafika ml10, nktamtafutia msaidizi huku mimi nikiendelea na mishe zangu,
Yaani baada ya mwaka duka limeisha enzi zile za deci washamla ml3 yake akisubiri kuvuna ndio ikafa, nilipata hasira nkalifunga akawa hana kazi mama analalamika namwachaje mdogo angu hivyo, kwa hasira nkampa kiduka kilikua uswazi ila mtaji tu vingine kama friji makreti na vingine aviache, mwisho wa siku na hilo kala kamaliza na ela ya mama laki 7 alimpa aongeze mtaji ikaishia hapo...

Baada ya miaka mi3 karudi kuomba msamaha baada ya kukosa kuuwawa akiwa anapokonywa bodaboda nkamsamehe nkamfungulia tena biashara iliyogharimu ml3.5 baada ya mwaka na nusu nilienda apo nikakuta imefungwa hadi leo sijui iliishia wapi...
Na majanga ya kumlelea watoto wake wa3 kaniachia.

Kipindi hicho nahangaika kutafuta ela mtaji mdogo jamaa yangu tunaishi karibu nkawa namuazima ela, kila laki1 baada ya mwezi nampa laki na kumi, nikichukua laki 3,4, 5 ni hivyohivyo, baada ya mambo yangu kua mazuri yeye ndio akawa ananiazima ela nkawa nampa tena bila riba yoyote baadae 1.6ml ilifia kwake hadi sa hivi hapokei simu yangu.

Kuna watu tumeumbwa kua daraja la wengine kufanikiwa ila hawajitambui hata kidogo mwisho wa siku chenga tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna Watu Tunatamani tupate Mabro wa Namna hii, wengine Wanachezea Nafasi


Tuna Bro Wetu yuko Vizuri Hataki kusaidia wadogo zake tunataabika yeye ni mtu Wa Show Off kununulia washikaji bia na kuapangisha mademu na kuwanunulia vitu vya ndani na kuwapa Mitaji,.
 
Mwaka 2007 nilimaliza mafunzo ya ufundi veta, nikawa nafanya kazi za mtaani mwaka 1 baadae nikakutana name bint mchaga sura nzuri had tabia .

Alitengetengeneza mazingira ya kumpenda na kweli ikawa hivyo.
Mwaka 2009 nilipanga chumba name kutoka Kwa mzee, bahati mbaya nae nyumbani kwao akawa hatakiwi maana alikuwa akiishi kwa baba yake alie Kuwait name mke mwingine.

Nilitafuta sehemu ya kwenda kukaa Kwa ninao wafahamu hatimae nikapata kwa dada 1 akakaa wake.

Ilibidi nizunguke pale mjini kutafuta kazi nilizunguka sana nikapata kampuni ya ukusanyaji wa ushuru maegesho ya Magari.

Miezi 3 baadae dada aliekua akikaa nae alimfukuza ikabidi nikaaongee name mzee wangu akaniruhusu nikakae nae yeye atamalizana na mzazi mwenzake.

Nikabeba mke jioni ya SAA moja jumamosi tarehe 12 mwezi wa 9 2009.


Hapo ndipo kizaa kilipo anza , nilikaa nae miaka mitatu. Ndani ya hio miaka 3 ndipo nilipojua wakati mwingine likuepukalo lina heri ndani yake.

Kwa ufupi Kwa kua alikua amesoma had kidato cha 4 na matokeo mazuri, nilianza kumtafutia college kuanzia ualimu unesi misitu mifugo computer veta kote huko akakosa, hiyo iligarimu mwaka na nusu.


Aliugua kifua kikuuu Kwa muda wa miezi nane ndio alipona, kipindi hiki kidogo kilinipa challenge Kwa kiasi kikubwa.
Miezi minne baadae mama yake mzazi aliugua na kufariki (R I P) hapa napo mziki wake ulikua si haba.

Miezi 3 baada ya hili nilifiwa na mlezi wangu alien nilea toka nikiwa na mwezi 1 hapa napo niliumia mno!

Baada ya haya ilibidi nimtafutie cha kufanya.
Dada mmoja akaniambie anafungua kibanda stand hivyo kama ataweza akakae hapo.
Alinipa kazi ya kutengeneza kibanda maana mimi ni seremala, akanipa hela nikanunue bidhaa ,nilitumia usafiri wa baiskel nilirudi mjini Mara 8 tena bado kidogo nigongwe na lori, mwishowe nikaenda kumchukua yeye mke wangu kuja dukani. Kumbe ndio nampeleke Kwa mume mwingine.


Alianza kurudi nyumban Saa nne tofauti na makubaliano.
Alikuwa akiwasifia watu wengine wanamaendeleo tofauti na Mimi.
Mwishoni akaniambia tuachane!

Kweli aliondoka na mimi nikabaki na maumivu name umaskini.

Miaka minne niliipoteza kwake lakini aliniacha kwenye Mata, na athari alizoniachia mpaka leo sijasimama kimaisha vizuri.
Lakini taarifa nilizonazo yeye yupo safi na nyumba wanayo.

Yote ni maisha name maisha yanaendelea , poleni wakuu Kwa mikasa mliokutana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pole sana, nahisi maumivu uliyopita aisee
 
Kwanza niwatakie heri ya Krismasi kwa JF Members wote. Ninatumai wote ni wazima wa afya, leo nimejaribu kutafakari baadhi ya mambo na kuamini ule msemo wa mfadhili "MBUZI UTAMLA MCHUZI" binadamu atakuudhi.

Nitazungumzia xperience yangu kuhusu the so-called friends and relatives

1. Kanda ya Ziwa.
Nikiwa Meneja wa Mkoa taasisi fulani ya fedha, niliwahi fuatwa na vijana wawili ambao walikuwa ni wahudumu wa hoteli kuomba niwasaidie as kiukweli japo kwa hali ndogo nilokuwa nayo ila nilisaidia wengi hasa nikikumbuka safari yangu ilivokuwa. Nakumbuka niliwapa nafasi ya kuwa Sales Reps na kwa kuwa walikuwa wanaishi pale hotelini na wafanyakazi wenzao, kuwarahisishia na kuwapa mwanzo mzuri niliwachukulia chumba nikalipa 6months rent, nikanunua kitanda, godoro, jiko, pasi etc and of course walishukuru sana. I personally trained those guys, gave support and invested much on them, mwisho they became the best in my branch. Wakatoka katika kulipwa 90,000/= per month na kuweza kupata minimum 1mil per month, in other words not less than 200k per week as commission. Of course was proud, ila kilichokuja tokea Mungu ndo anajua na ikanibidi niombe transferna kuhama mkoa. Ikatengenezwa figisu na ikaundwa team with my admin, vijana wakapikwa kidogo nifukuzwe kazi [emoji848] mwisho malipo ni hapa hapa duniani wote walifukuzwa na nilipohama tawi na mkoa mauzo yakadrop. Jana nimekutana na mmoja wapo ni Mchungaji now baada ya kupata malipo matakatifu, kuvunjika mguu, kukoswa kufungwa na kampuni kwa wizi, etc. Kaniomba samahani sana, nimemjibu nilishamsamehe muda mrefu sana na awe na amani.

2. Kanda ya Ziwa
Nilifatwa na kijana ambaye alihitaji kazi Ila kwa elimu yake hakukidhi vigezo, and the guy was passing through hell. Dah, roho yangu hii nikamuonea huruma nikamchukua na kununua bodaboda
nikampa mkataba 1yr malipo 70per week, kijana akaanza vzr na pesa alikuwa anadeposit bank na kuniletea slip. Kilichokuja kutokea siwezi kuelezea, mpaka nikatengenezewa kesi ambayo ni Mungu tu aliniokoa.. Yakafuata matukio ya kishirikina mpaka nyumba yangu nilojenga na nilokuwa nakaa ikabidi nihame kuhofia uhai wangu.

3. Kanda ya Kaskazini
Way back 2010 nikiwa nimejiajiri na nimefungua kampuni ikijishugulisha na fumigation, stationary services and supplies, music studio production audio and video, electronic money transfer. Nikamchukua mtoto wa ma mdogo nikamtrain jinsi ya kuproduce music kuanzia beat, vocal mixing etc, at first dogo akawa mtiifu sana, nikamuacha nikiwa nasimamia kazi ili nami nijigawe mambo yaende, dah nakumbuka ni siku moja nimesafiri Dar kufata mzigo na kuonana na my co director ambaye ndo aliwekeza capital, niliporudi sikukuta kitu maana alisafisha studio, ofisi za stationary na items zote. Nilipigiwa xm ucku nikiwa Dar, nilirudi nikiwa siamini ila nilipofika na kuona empty shelves and office, nililia sana na mwisho co director mwenzangu alitaka kunifunga, thanks to God alileta njia. Dogo nilikutana nae Dar kachoka vby, na alinitafuta yeye ila nimemsamehe toka moyoni.

4. Makazini
Nimewahi fanyiwa fitina na wasaidizi wangu kisa wivu na chuki, nikahamisha vituo na wao kuwa promoted kushika nafasi yangu ila within first quarter wote waliprove failure na kufukuzwa kazi baada ya ukweli kuja kugundulika..

Kwa kifupi nimepitia mengi sana kwenye maisha yangu, achilia mbali ajali, kuwa broke from a person who was well off financially, kuzulumiwa pesa nyingi sana na mwisho kutengwa, ila niwatie moyo wote ambao mna wakati mgumu au mnapitia magumu kamwe msikate tamaa, God is always in control.

Nikikumbuka nilipotoka na hapa nilipo, japo sijafika bado ambapo nilikuwa before ila namshukuru Mungu sana.

Kwa yeyote pia ambaye alifanya mema na kulipwa mabaya pls share with us, ili wengine wajifunze pia

Niwatakie sikukuu njema
Tabia ya kusamehe ndo inakuharibia, hakikisha unalipa kadri ya inavostahili
 
Back
Top Bottom