Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Story: Ulitenda mema na kulipwa mabaya please share

Toka 2015 nadai laki 5 haki nilipitia kipindi kibaya sana kicuhumi lakini mdai wangu hata 30,000 hajantumia naona anapost biashara zake tu juzi, kuna siku akapost senene ndoo anauza.
Nikamfata nikamuambia basi naonba nitumie ndoo moja ya senene nitafune nipunguze machungu hakunijibu.
Imagine ndoo moja ya senene kwa laki 5

Sent using Jamii Forums mobile app

Aki nimechekaaa🤣
 
Mwaka 2007 nilimaliza mafunzo ya ufundi veta, nikawa nafanya kazi za mtaani mwaka 1 baadae nikakutana name bint mchaga sura nzuri had tabia .

Alitengetengeneza mazingira ya kumpenda na kweli ikawa hivyo.
Mwaka 2009 nilipanga chumba name kutoka Kwa mzee, bahati mbaya nae nyumbani kwao akawa hatakiwi maana alikuwa akiishi kwa baba yake alie Kuwait name mke mwingine.

Nilitafuta sehemu ya kwenda kukaa Kwa ninao wafahamu hatimae nikapata kwa dada 1 akakaa wake.

Ilibidi nizunguke pale mjini kutafuta kazi nilizunguka sana nikapata kampuni ya ukusanyaji wa ushuru maegesho ya Magari.

Miezi 3 baadae dada aliekua akikaa nae alimfukuza ikabidi nikaaongee name mzee wangu akaniruhusu nikakae nae yeye atamalizana na mzazi mwenzake.

Nikabeba mke jioni ya SAA moja jumamosi tarehe 12 mwezi wa 9 2009.

Hapo ndipo kizaa kilipo anza , nilikaa nae miaka mitatu. Ndani ya hio miaka 3 ndipo nilipojua wakati mwingine likuepukalo lina heri ndani yake.

Kwa ufupi Kwa kua alikua amesoma had kidato cha 4 na matokeo mazuri, nilianza kumtafutia college kuanzia ualimu unesi misitu mifugo computer veta kote huko akakosa, hiyo iligarimu mwaka na nusu.

Aliugua kifua kikuuu Kwa muda wa miezi nane ndio alipona, kipindi hiki kidogo kilinipa challenge Kwa kiasi kikubwa.
Miezi minne baadae mama yake mzazi aliugua na kufariki (R I P) hapa napo mziki wake ulikua si haba.

Miezi 3 baada ya hili nilifiwa na mlezi wangu alien nilea toka nikiwa na mwezi 1 hapa napo niliumia mno!

Baada ya haya ilibidi nimtafutie cha kufanya.
Dada mmoja akaniambie anafungua kibanda stand hivyo kama ataweza akakae hapo.
Alinipa kazi ya kutengeneza kibanda maana mimi ni seremala, akanipa hela nikanunue bidhaa ,nilitumia usafiri wa baiskel nilirudi mjini Mara 8 tena bado kidogo nigongwe na lori, mwishowe nikaenda kumchukua yeye mke wangu kuja dukani. Kumbe ndio nampeleke Kwa mume mwingine.

Alianza kurudi nyumban Saa nne tofauti na makubaliano.
Alikuwa akiwasifia watu wengine wanamaendeleo tofauti na Mimi.
Mwishoni akaniambia tuachane!

Kweli aliondoka na mimi nikabaki na maumivu name umaskini.

Miaka minne niliipoteza kwake lakini aliniacha kwenye Mata, na athari alizoniachia mpaka leo sijasimama kimaisha vizuri.
Lakini taarifa nilizonazo yeye yupo safi na nyumba wanayo.

Yote ni maisha name maisha yanaendelea , poleni wakuu Kwa mikasa mliokutana nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu hii imeniuma Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka 2015 nadai laki 5 haki nilipitia kipindi kibaya sana kicuhumi lakini mdai wangu hata 30,000 hajantumia naona anapost biashara zake tu juzi, kuna siku akapost senene ndoo anauza.
Nikamfata nikamuambia basi naonba nitumie ndoo moja ya senene nitafune nipunguze machungu hakunijibu.
Imagine ndoo moja ya senene kwa laki 5

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]umenichekesha kishenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, sijui hata nianzie wapi, nimelizwa sana kwa kujidai najua kuangalia matatizo ya watu. Mpaka muda huu napitia crisis kubwa kiuchumi, na hakuna wa kumwambia akaweza kunisaidia.......... Inanisumbua sana, nashindwa hata kuandika, ila Mungu anajua, nimemuachia yeye.
 
Meneja wa taasisi ya fedha simu unaandika xm? usiku unaandika ucku? Tuna shida kubwa sana kama Taifa
Kwanza niwatakie heri ya Krismasi kwa JF Members wote. Ninatumai wote ni wazima wa afya, leo nimejaribu kutafakari baadhi ya mambo na kuamini ule msemo wa mfadhili "MBUZI UTAMLA MCHUZI" binadamu atakuudhi.

Nitazungumzia xperience yangu kuhusu the so-called friends and relatives

1. Kanda ya Ziwa.
Nikiwa Meneja wa Mkoa taasisi fulani ya fedha, niliwahi fuatwa na vijana wawili ambao walikuwa ni wahudumu wa hoteli kuomba niwasaidie as kiukweli japo kwa hali ndogo nilokuwa nayo ila nilisaidia wengi hasa nikikumbuka safari yangu ilivokuwa. Nakumbuka niliwapa nafasi ya kuwa Sales Reps na kwa kuwa walikuwa wanaishi pale hotelini na wafanyakazi wenzao, kuwarahisishia na kuwapa mwanzo mzuri niliwachukulia chumba nikalipa 6months rent, nikanunua kitanda, godoro, jiko, pasi etc and of course walishukuru sana. I personally trained those guys, gave support and invested much on them, mwisho they became the best in my branch. Wakatoka katika kulipwa 90,000/= per month na kuweza kupata minimum 1mil per month, in other words not less than 200k per week as commission. Of course was proud, ila kilichokuja tokea Mungu ndo anajua na ikanibidi niombe transferna kuhama mkoa. Ikatengenezwa figisu na ikaundwa team with my admin, vijana wakapikwa kidogo nifukuzwe kazi [emoji848] mwisho malipo ni hapa hapa duniani wote walifukuzwa na nilipohama tawi na mkoa mauzo yakadrop. Jana nimekutana na mmoja wapo ni Mchungaji now baada ya kupata malipo matakatifu, kuvunjika mguu, kukoswa kufungwa na kampuni kwa wizi, etc. Kaniomba samahani sana, nimemjibu nilishamsamehe muda mrefu sana na awe na amani.

2. Kanda ya Ziwa
Nilifatwa na kijana ambaye alihitaji kazi Ila kwa elimu yake hakukidhi vigezo, and the guy was passing through hell. Dah, roho yangu hii nikamuonea huruma nikamchukua na kununua bodaboda
nikampa mkataba 1yr malipo 70per week, kijana akaanza vzr na pesa alikuwa anadeposit bank na kuniletea slip. Kilichokuja kutokea siwezi kuelezea, mpaka nikatengenezewa kesi ambayo ni Mungu tu aliniokoa.. Yakafuata matukio ya kishirikina mpaka nyumba yangu nilojenga na nilokuwa nakaa ikabidi nihame kuhofia uhai wangu.

3. Kanda ya Kaskazini
Way back 2010 nikiwa nimejiajiri na nimefungua kampuni ikijishugulisha na fumigation, stationary services and supplies, music studio production audio and video, electronic money transfer. Nikamchukua mtoto wa ma mdogo nikamtrain jinsi ya kuproduce music kuanzia beat, vocal mixing etc, at first dogo akawa mtiifu sana, nikamuacha nikiwa nasimamia kazi ili nami nijigawe mambo yaende, dah nakumbuka ni siku moja nimesafiri Dar kufata mzigo na kuonana na my co director ambaye ndo aliwekeza capital, niliporudi sikukuta kitu maana alisafisha studio, ofisi za stationary na items zote. Nilipigiwa xm ucku nikiwa Dar, nilirudi nikiwa siamini ila nilipofika na kuona empty shelves and office, nililia sana na mwisho co director mwenzangu alitaka kunifunga, thanks to God alileta njia. Dogo nilikutana nae Dar kachoka vby, na alinitafuta yeye ila nimemsamehe toka moyoni.

4. Makazini
Nimewahi fanyiwa fitina na wasaidizi wangu kisa wivu na chuki, nikahamisha vituo na wao kuwa promoted kushika nafasi yangu ila within first quarter wote waliprove failure na kufukuzwa kazi baada ya ukweli kuja kugundulika..

Kwa kifupi nimepitia mengi sana kwenye maisha yangu, achilia mbali ajali, kuwa broke from a person who was well off financially, kuzulumiwa pesa nyingi sana na mwisho kutengwa, ila niwatie moyo wote ambao mna wakati mgumu au mnapitia magumu kamwe msikate tamaa, God is always in control.

Nikikumbuka nilipotoka na hapa nilipo, japo sijafika bado ambapo nilikuwa before ila namshukuru Mungu sana.

Kwa yeyote pia ambaye alifanya mema na kulipwa mabaya pls share with us, ili wengine wajifunze pia

Niwatakie sikukuu njema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Relief Mirzska,

Duh pole Mkuu..

Nilichojifunza ni kuwa ukiwa na roho nzuri sana daima hutoendelea, mi nilifungua ofisi ya welding Kigamboni and invested 2mil.. Alinifata jamaa ambaye anakaa karibu na Shemeji yangu (mke wa bro)

I gave that person 2mil, ambayo ilitosha kununua mashine 3 (grender, driller and cutter) jamaa cjui ilikuwaje nikamuamini kiasi kile, shida ikaja kwenye receipt za mashine ukizingatia nilikuambia ahakikishe ananua vyote dukani na alete receipts.

Mpaka tunapozungumza jamaa nimekuwa adui mkubwa Sana kwake, mashine anadai alinunua kwa mtu, nikamwuliza with whose permission!?

Out of 2mil, kanunua cutter 400k (ambayo alinambia kanunua 850k), drill machine 150k, grender it's nearly 3months now haijafika kwa madai aliyemtumia pesa yuko Zanzibar na hapatikani.

Inaenda miezi 3 na ofisi hajanipa hata kumi, awali nilidhani ni ugumu wa kazi ila kufuatilia nikagundua alifanya kazi ya msikiti akalipwa 700k, akafanya nyingine akalipwa 1.5m, and the last 1.2m, aisee nilishikwa na hasira mpaka kidogo pressure inipande.

Baada ya kuanza kufuatilia jamaa akaanza kuhamisha kazi anafanyia kwingine sababu pale ofcn nimeweka msimamizi na anambana,, kiukweli ninajuta sana.

Jana nimembana mpaka ndugu zake wameamua wauze kiwanja wanipe pesa yangu maana kiukweli nilikuwa namfunga, analia kama mtoto mdogo, mbaya pesa yangu ndo kaolea Nov 2019 mwishoni, yaani nikikumbuka mpaka roho inaniuma.

Ila nimeamua wanilipe maana walitaka wanipe kiwanja nikakataa, kwa hasira nilizonazo hazielezeki ila hakika Mungu atamlipa kabisa, tena naomba amlipe kabisa
Mkuu hyo ofisi ipo maeneo gani kigamboni uniachie mm kwa maelewano maana nilikuwa nawaza kufungua ofisi fani yangu hyo mm
 
Daaah nimeamini ni kweli kaka/dada zetu wanatupiga sana tafu ila sisi madogo sometime tunazingua.
Nakumbuka ile nimetok chuo mwaka jana 2018. Nimerudi maskani broo wangu (mwajiliwa wa serikali) akanambia nitafute biashara ila mtaji usizid 2mil. Ila kutokana na mawenge niliyokua nayo nikamwambia broo ngoja kwanza nipambane kitaaa ikiwezekana nichapike sanaa, ili akili ikiniingia nitajua nini cha kufanya kwenye biashara. Nilikua naogopa nicije nikaingia kichwakichwa na kufeli.
Baadae nikamuomba mtaji wa kama laki tano hiv kuna biashara nilitaka niianzishe ilikua nikodi mashine ya kutobolea mawe (compressor machine) ila mambo yakaenda kombo baada ya mwenye mashine kuingia mitini na nusu ya hela 280k. iliyobaki nikajikuta naitumia tu kwa matumizi mengine bila kufanya nilichopanga. Ila nilipomueleza broo hakuchukia na alinijibu kwa ukarimu mpaka nikajikuta nahuzunika.
Baadae nkamueleza nahitaji kuanzinza mradi ila mtaji ni kama milioni 18 ambapo nimekadiria faida itakua almost 2mil kwa mwezi (na zaidi ya hapo) ila hiyo ni standard profit not minimum or maximum (kama sijakosea maana mm sio mchumi, ni mwalimu wa historia by professional). Na kikubwa ni kuinunua hiyo compressor mashine ili nipigie kazi mwenyewe, akagoma kua ni pesa kubwa sana.
Baadae broo alinunua gari mwezi wa 7kwa milioni 12, nikamuomba tena anisaidie nitimize malengo yangu ya mradi maana nimetafuta watu wengi sana wote wananichomolea kikubw Nachokumbana nacho ni kuwa hawaniamini wanaogopa nisije nikaingia mitini. Lkn broo amekua sitaki nataka maana aliniambia nisubir afikirie, baadae akanambia atakopa benk toka mwezi wa 8 mpka now ananiambia atakopa. Lkn nahic anaogopa nisije nikamlostisha akainga deni. Na nahic laki tano aliyonipa nikafeli ndo inamfanya asiniamini sana kwa hela kubwa kiasi hicho.
Ila kuna rafiki yake niliwahi kumueleza kuhusu huo mradi akaupenda baadae akamwambia broo kama hawezi basi wachangiane wanipe hiyo mashine lkn broo kagoma kwa madai kua yeye peke ake anaweza kukopa na kunipa hiyo mashine.
Ko nimebaki tu njia panda natamani afanye hivyo. ila namuheshimu sana maana kanisomesha advance na university. Wito wangu kwa sie madogo tuwaheshimu sana mabroo na ma sister zetu, Wanajitolea sana kwetu ila tu vile tunapungukiwaga na uelewa tunaona kama vile wanatuendesha au kutupelekesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaa imewahi nitokea nilikaa na jamaa nilikua namsaidia sana majibu, jamaa namfunulia achungulie mwenyewe lkn bado anauliza tu mpaka ananishtua kwa mkono mgogongoni, lecture akamuona akaja akachukua karatasi zetu na kupunguza maksi 5. ile test ilikua na marks 25 baada ya kupunguzwa nikawa nmepata 17. iliniuma balaa yaani.
Pole sana Relief, ndiyo binadamu walivyo ni lazima tuishi nao kwa akili..!!

Ngoja nitoe story tofauti kidogo, nakumbuka tukiwa chuo, lecturer akaingia, halafu ghafla ikaandikwa quiz, halafu huwa yupo very serious..! Aiseeh' niliskia kudata jamani,

Luckily, swali la kwanza nikawa nalijua kasoro tu mwanzoni nikawa nimesahau panaanzaje, kuna binti yupo next chair ana kidaftari, huwa ni wale mabingwa wa kuchabo, nikamuuliza zaidi ya mara mbili huwezi amini akanichunia! Akajikausha kabisa na ananisikia huku anaendelea kuperuzi, nikam mind ila nikampotezea!
While Sir anaendelea kutiririka maswali huko mbele nikageuka nikamuuliza mtu mwingine, ile kaanza tu kuniambia nikamuambia stop, nimeshakumbuka yooote! Yanayofuatia nikatiririka nayo kama maji..!!

Dakika chache baada ya Sir kumaliza namie nikawa nimemaliza, huwa sipendi kuonekana nimemaliza haraka hivyo ikabidi niendelee kuzuga zuga na wengine wamalize ndo ninyanyuke!

Mungu si Athumani, baada ya Sir kugeuka yule binti wa kuchabo akashindwa kuendelea kuigia hivyo maswali yote yaliyobaki yakawa yamemshinda, mind you nishamaliza ila nasubiri wengine wamalize malize ili nipate company.!!

Kahangaika weeh', mwishowe uzalendo ukamshinda ikabidi aniite Mimi tena aliyekuwa amenichunia nimsaidie, namie nilivyo mjinga tu by nature nikaanza kumsaidia, swali la kwanza lote mpaka akalimaliza, akauliza tena lingine ile naanza kujibu nikadakwa, yeye hakuonekana, sababu aliniona naongea, ila hakujua naongea na nani.!! Nikaitwa mbele,

Mimi nikabisha hatari kuwa nilikuwa siongei, maana ukhalisia nilikuwa nishamaliza! Sasa yule binti alivyo maandazi pori akaja mbele akajileta bila kuitwa!! Jamani, jamani nilitamani nimkule!! Nilimtazama kwa khasira mpaka nikaskia kutetemeka.!

Sir akawa ashapata jibu, hivyo akachukua zile karatasi akazichana tukatolewa nje! Nilimind sababu marks nishazikosa, aliyesababisha ni huyu furushi aliyegoma kunisaidia mwanzoni! Kubwa zaidi nishawekwa alama Mimi ni cheater! Nikaona bora ningelala zangu hostel tu.!!

Lastly, ikajaga next exam, Sir kamaliza tu kuandika kakaa, dakika chache mbele, nikainuka nikaenda kusanya mpaka akashangaa, halafu nimempiga maswali yote! Ndo ikawa tabia yangu, Kuanzia hapo sasa ndo nikawa jembe lake, akaja kujua kumbe mimi sio kiazi kama alivyodhani.! Heshima ikawepo mpaka namaliza chuo.!

Bahati mbaya yule binti hakufanikiwa kumaliza chuo, sup na carry zilimzidi maskiini! Sijui hata yuko wapi siku hizi!!

'tenda wema ila hakikisha usizidi uwezo'..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo paragraph ya pili kutoka mwisho imenipa simanzi sana, hakuna kitu kinauma kama mtu kukuharibia maisha yako halafu yeye yupo somewhere na mtu mwingine wanaishi maisha safi kabisa as if nothing happened

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu. Nashukuru Mungu siumii kumuona ameendela, ningeumia kama angekua maisha mabaya.
Zaidi mno namshukuru Mungu na kumuomba aniepushe kuwa sababu ya maumivu kwa wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule alikuwa zaidi ya usaliti halafu heartless. Mtu ambaye hata akuumize vipi hajui neno samahani....nilichogundua umalaya ukizidi unaondoa utu.
Siwezi kuishi bila Amani ya moyo kwakweli nikafupisha maisha yangu kwa mtu ambaye kwa upeo wake Hana mchango wowote kwangu kimawazo zaidi ya kunijazia stress.

Nisimulie kidogo kuhusu huyo mama...
Huyu mama alichukuliwa kutoka kijijini kwa lengo la kupatiwa kazi baada ya malengo take ya Kuwa mtawa kushindikana.

Kaletwa kwa mume aside mjua wakaishi wakafunga ndoa wakazaa mtoto wa 1,2 name 3.

Mume anakazi serikalini tena kipindi kile cha shirikisho la Africa mashariki.

Miaka fulani mume kapata kabint cha kidato cha pili akazaa nacho Mke akajua akarudi kijijini kwa wazazi lakini wakapatanishwa akarudi kwa mume.

Mumeakazaa name yule binti tena motto wa pili, hapa mke akalipa akazaa na jamaa mmoja hivi.

Mke alikua ana kaa na mdogo wake, mume akatembea na mdogo wa mke akazaa nae.
Kesi zikaamuliwa mke akatulia.

Yule binti baada ya uzao wa pili akajengewa nyumba name alisomeshwa mpaka kawa daktari wa binadamu.
Alifunguliwa duka la dawa
Baba yake alijengewa nyumba
Watoto wake walisoma mpka vyuo vya ulaya huko.

Mke wa ndoa aliendelea kubaki mama wa nyumbani, akishuhudia huduma bora Kwa mke mdogo.
Watoto wa mke Mkubwa aliesoma sana kidato cha nne.

Nyumba aliokua akikaa ni kota.

Matokeo Leo hii mume hana hata mia
Mke mdogo aliolewa na mume mwingine
Mume hana hata ramani Kwa hio anaishi Kwa hisani ya mke wa ndoa na mke wa ndoa amempokea mumewe Kwa Upendo na kumsamehe na wanaishi kama hakuna kilichotokea.

Kwa sasa mke Mkubwa ndie shujaa alivumilia changamoto ngumu ya usaliti salsa hivi yeye ndie mshindi.

Ndio maana nikasema kwako wewe ingekuwa bora sana kama ungevumilia ule upepo mbaya upite japo sijajua ni baya kiasi gani lakini hakuna baya chini ya Juan lisiloisha name kusameheka.

Mchumba havumiliwi. Kwangu ulikuwa uchumba tu Ila wenye mizizi.
Lakini pia haina maana raha na matanuzi afanyiwe mwingine halafu ukichoka ndo unarudi.....sina huo moyo asee. Moyo wangu wa spongy sio wa jiwe
 
Na mimi nilitaka nimuulize vizuri huo ushujaa wa mke wa ndoa ni kumpokea mume ambaye kashajichokea maisha na kuchokwa na bi mdogo au? Hapo unashindwa hata kujua kuwa amerudi kwa mke wa ndoa kwa sababu ni kweli amegundua makosa yake au kwa sababu maisha yamemchapa. Mtu u-fight na kuvumilia mume arudi akiwa bado anadai, sio mtu anajirudisha mwenyewe akiwa apeche alolo mwingine na maradhi juu afu ndo useme umeshinda. Huo ushindi me siutaki khaa
 
Mchumba havumiliwi. Kwangu ulikuwa uchumba tu Ila wenye mizizi.
Lakini pia haina maana raha na matanuzi afanyiwe mwingine halafu ukichoka ndo unarudi.....sina huo moyo asee. Moyo wangu wa spongy sio wa jiwe
OK kama ilikua ni uchumba saw a, ndio maana kuna hatua hizo tatu katika mahusiano ndoa uchumba na urafiki.
Lakini pia kama ilikua ni uchumba usingesubiri mpaka uumizwe hivyo.
Ila Kwa jumla hakuna ndoa nyepesi labda huyo mwenzi awe ni mcha Mungu. Hebu dhani umeolewa na uko name miaka 25 ya ndoa mime akaanza kutembea name watu wengine na huduma wanapewa wao na wewe umri umeenda,utafanyaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mama alichukuliwa kutoka kijijini kwa lengo la kupatiwa kazi baada ya malengo take ya Kuwa mtawa kushindikana.

Kaletwa kwa mume aside mjua wakaishi wakafunga ndoa wakazaa mtoto wa 1,2 name 3.

Mume anakazi serikalini tena kipindi kile cha shirikisho la Africa mashariki.

Miaka fulani mume kapata kabint cha kidato cha pili akazaa nacho Mke akajua akarudi kijijini kwa wazazi lakini wakapatanishwa akarudi kwa mume.

Mumeakazaa name yule binti tena motto wa pili, hapa mke akalipa akazaa na jamaa mmoja hivi.

Mke alikua ana kaa na mdogo wake, mume akatembea na mdogo wa mke akazaa nae.
Kesi zikaamuliwa mke akatulia.

Yule binti baada ya uzao wa pili akajengewa nyumba name alisomeshwa mpaka kawa daktari wa binadamu.
Alifunguliwa duka la dawa
Baba yake alijengewa nyumba
Watoto wake walisoma mpka vyuo vya ulaya huko.

Mke wa ndoa aliendelea kubaki mama wa nyumbani, akishuhudia huduma bora Kwa mke mdogo.
Watoto wa mke Mkubwa aliesoma sana kidato cha nne.

Nyumba aliokua akikaa ni kota.

Matokeo Leo hii mume hana hata mia
Mke mdogo aliolewa na mume mwingine
Mume hana hata ramani Kwa hio anaishi Kwa hisani ya mke wa ndoa na mke wa ndoa amempokea mumewe Kwa Upendo na kumsamehe na wanaishi kama hakuna kilichotokea.

Kwa sasa mke Mkubwa ndie shujaa alivumilia changamoto ngumu ya usaliti salsa hivi yeye ndie mshindi.

Ndio maana nikasema kwako wewe ingekuwa bora sana kama ungevumilia ule upepo mbaya upite japo sijajua ni baya kiasi gani lakini hakuna baya chini ya Juan lisiloisha name kusameheka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mke wa ndoa ni wa kuvumilia shida zake, akiwa kwenye raha wakuspend ni michepuko?
 
Back
Top Bottom