Leo huyu legs alikuwa kapaka supa glue, ikabidi nisim read tu.
Kuna vitu umeongea ambavyo ni ukweli mtupu, hasa kwa mdada aliyekulia kwenye maisha yenye ratiba almost fixed.
Ukishajitegemea na kuwa kwako, kuna vitu inabidi kujifunza kubadilika, kama.hukuwa social sana inabidi kujifunza. Si lazima kwenda club au bar, lakini kuna jumuia zingine unaweza kujiunga nazo si lazima sababu unahitaji msaada, but just to get to know people.
Hata ukiwa na mme na watoto, still unahitaji kuhusiana na watu. Na si lazima kila siku utoke out ili kuhusiana na watu. Sehemu ya kazi ni sehemu ya kwanza kujifunza kufahamiana na watu. Bado kuna sehemu kama kanisani, kuna vikundi mbalimbali waweza kujiunga navyo just to kill boredom, mwisho wa siku unajikuta umefahamiana na watu.
Kitu cha kwanza huanza na kubadili attitude yako mwenyewe. Na mara kadhaa huhitaji kuwa na marafiki weeengi, hata wakiwa wachache lakini muwe na interest za kufanana.
Suala la kujilinganisha na watu wengine nalo linaweza kuua confidence ya mtu kabisa. Kujifunza kuishi.maisha yako kama yalivyo inasaidia. Nimewahi kuona mdada akiteseka sana kwa kutafuta ndoa kama 'kazi', matokeo yake hakuipata. Huwa nasema ndoa hailazimishwi hata kama uko kwenye mahusiano, haya ni maridhiano ya watu wawili.
Kwani ndiyo wewe expert wa ku-read between the legs?