Mimi sio mgeni hapa JF ila nimeamua kuja na ID nyingine coz mhusika wa story hii anajua ID yangu nyingine.
Mimi ni mke, lonely heart , ila sasa nimepata mtu hapahapa JF. Kwa muda nimekuwa nikitamani sana kuwa mwenzi seriously, sio mtu wa kula nae ujana tu, kupotezeana muda, no seriously kuanzisha familia, dad, mom, ndani ya ndoa iliyobarikiwa kabisa, inapendeza sana jamani, asikudanganye mtu.
Mara nyingi nikiona couples na watoto wao nafurahi ila roho inauma pia coz na mimi natamani kuwa na wangu. Kusoma nimesoma weee, kazi nimefanya weeee sasa ni wakati wa kuwa na familia but nothing happens, sasa nifanyeje coz kwa mke ni ngumu kumwambia mme nakupenda au nioe hata kama unampenda.
Maisha yangu mie ni monotonous kazi - home - kazi - church- kazi - safari ya kikazi and all that, no social life at all, niko mbali sana na home and jinsi nilivyolelewa sikufundishwa kwenda kwenda kwa watu hovyo hovyo yani umetoka kazini hodi jirani blah blah, hodi hapa yidi yada yidi, no, nilivyolelewa mimi routine ilikuwa home - shule - home - church/ mafundisho etc.
Hakuna kucheza nje, so sijajifunza ku socialize na watu, ukiniweka kwenye group la watu drinking whatever they drink and talk loudly, I wouldn't know what to say, sana sana nitakuwa very bored or I would be very very boring coz nitakuwa mkimya sana then ntaanza kuwaghasi friends it's getting late, tuondoke, tuondoke, so my solution is stay at home, only that my home is empty, hata house girl halali hapo.
So accidentally and out of complete boredom nika join JF, siku hiyo nakumbuka nilikuwa nasubiri updates za matokeo ya uchaguzi wa 2010 and all the TV stations hazikuwa zinaniridhisha na matokeo waliyokuwa wakitoa, umeme nao ulikuwa hovyo sana, nika google matokeo ya uchaguzi and eventually I was led to JF.
Mwanzo nilikuwaga nasoma habari za siasa tu then one day kuna tangazo la mtu kutafuta mke likanivutia, nikaanza mawasiliano nae. daaaaahh, majanga. Ile tunakutana for the first time akatangaza kupeleka posa home, desperation y