Spika Tulia: Tusichanganye Maadili ya Mtanzania na Imani za kidini. Lipi kosa la walimu waliosimamishwa kazi Kwa kucheza muziki? Warudisheni kazini

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,610
17,818
Amesema hayo akihoji kuhus Njia iliyotumika Kuwasimamisha walimu hao,Bila ya kufuata utaratibu wa kinidhamu wa kiutumishi,Hata hivyo ameongeza na kusema kuwa lisionewe kundi fulani tu kwani hata baadhi ya wabunge pia nao wanacheza miziki hiyo..

"Wapo mawaziri humu ndani na sisi wabunge huwa tunacheza mziki na hao wanafunzi, Tufafanuliwe hapa ili watu wajue nini cha kufanya la sivyo tutaendelea kucheza huo mziki na watoto wakiwepo shuleni alafu tutawapomza wale ambao watatakiwa kuchukuliwa hatua ,kwahiyo ni muhimu muwe na hatua zaidi ya hapa ili watu wote wawe na uelewa ni miziki gani inachezwa na ipi haichezwi itasaidia sana,Lakini tusiingize Huko hisia za kidini tusichanganye Imani ya dini na maadili ya mtanzania tusivichanganye" amesema Dkt tulia Ackson spika wa bunge la Muungano leo bungeni

hata hivyo aliendelea kumhoji waziri Njia iliyotumika kuwasimamisha walimu wao kazi na akasema kuwa njia hiyo haikuwa na usawa hivyo ameomba warudishwe makazini na njia sahihi zifuatwe



Screenshot_20231106-145638.png
 
Siyo kila nyimbo inapigwa kila mahali, watoto wanapaswa kufundishwa maadili mema, Maudhui ya ile nyimbo yanafaa watu walioko kwenye ma-bar na magenge mengine ya wahuni
Kma umemuelewa alishindwa kusema moja kwa moja kwamba kwanini hawakuanza na Zuchu mwenyewe halafu wakafata walimu halafu na wwngine wakafata kuonea upande mmoja haifai wanatakiwa wawarudishe waalimu halafu zuchu ale Ban ya kwenda halafu ndo ziendelee mishe zingine
 
Back
Top Bottom