Spika wa Bunge Tulia Ackson atoa onyo la mwisho kwa vyombo vya habari vinavyotoa taarifa za upotoshaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 43 leo Juni 8, 2023.



Tatizo la Walimu kuhama Vituo vya vya Kazi Halmashauri ya Tunduru
- Wizara ya TAMISEMI Ofisi ya Rais kupitia Waziri Simbachawene, yaahidi kutafuta suluhu ya kuwa na mfumo mzuri kwa tatizo la walimu kuhama vituo vyao vya kazi mara baada ya kupangiwa katika Halmashuri ya Tunduru.

Changamoto ya huduma shuleni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
- Akijibu swali la Mbunge Asha Juma, Naibu Waziri Wizara ya TAMISEMI Ofisi ya Rais, Ridhiwani Kikwete aagiza Wakaguzi wa Ubora wa Shule wapite katika shule ndani ya halmashauri kuhakiki kama mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalum yamezingatiwa.

Ufafanuzi kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Pendekezo la kuridhiwa Mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini - Spika wa Bunge, Tulia Ackson

- Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau uliyofanyika siku ya Jumanne tar. 6 June, 2023 Dodoma ambapo Kamati ilipokoea maoni ya wadau waliofika, Kamati ya pamoja bado inaendelea kupokea maoni ya wadau ambao hawakuweza kufika, ambapo maoni ya wadau yanapokelewa kwa njia ya Posta na Baurua pepe.

- Taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ikiwemo magazeti ya The Guardian na Nipashe ya Tar 7 June, 2023 zikidai Azimio hilo limesharidhiwa na bunge, si za kweli. Azimio husika kwa sasa bado lipo katika ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni, na mara baada ya kamati kumaliza yake, azimio hilo limepangwa kuingia bungeni tar. 10 June, 2023 kwa ajili ya mjadala na kutipishwa na bunge.

- Wito kwa Waandishi wa Habari na Wanamitandao kuzingatia maadili kwa kuhakikisha kwamba wanajiridhisha na wanaata taarifa sahihi kutoka kwa mamlaka zinazohusika kabla ya kutoa taarifa ili kuepusha taharuki na usumbufu kwa umma.

Kitendo kilichofanywa na vyombo vya habari husika ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 34 Fasili ya 1(a) cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, ambacho kinaeleza; ni kosa Kisheria kuchapisha habari za uongo au zinazolenga kwa namna yoyote ile kupotosha kwa makusudi jambo lolote linalohusu uendeshwaji wa shughuli za bunge na kamati zake.

- Onyo la mwisho kwa vyombo vya habari wanaotoa taafifa za upotoshaji zinazohusu bunge; chombo kitakachofanya upotoshaji kitashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria.


Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria juu ya Muswada wa Tume ya Mipango wa Mwaka 2023 - Mashimba Ndaki

Sehemu ya kwanza (iIbara ya 1 - 3) ya muswada inaweka masharti ya utangulizi

Kwa ujumla Kamati inakubaliana na mapendekezo ya muswada katika ibara hizo isipokuwa kwa tafsiri ya neno moja tu la 'Mipango Mkakati.' Kamati ilipata shaka na tafsiri ya maneno hayo kwakuwa hayajatumika katika muswada na kupendekeza maneno 'Mpango Mkakati' ndio yatafsiriwe kwakuwa ndio yaliyotumika katika muswada. Pendekezo hili lilikubadiliwa na serikali.

Sehemu ya pili ya muswada (Ibara ya 4 - 10) inaweka masharti kuhusu tume ya mipango
Ibara ya 4, 5, 6 na 7 zinaweka masharti ya uanzishwaji wa tume, muundo, majukumu ya tume, na mamlaka mtawalia - Kamati ilibaini kuwa ibara ya 5 kifungu kidogo i(c) cha muswada hakijaweka masharti ya uteuzi wa mjumbe kutoka sekta binafsi katika uteuzi wa wajumbe wengine 4 wa tume ili kuendana na sera ya nchi kuwa naushirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi - Baada ya majadiliano na serikali walikubaliana ibara hii ibaki kama ilivyopendekezwa kwakuwa uteuzi wa wajumbe umewekewa sifa za kitaalamu na uzoefu katika ibara 5 kifungu kidogo cha iii.

- Tume imepewa mamlaka ya kumualika mtu yoyote kushiriki vikao vya tume na kutoa utaalamu wake kadri tume itakavyoona inafaa

- Kamati inashauri katika kutekeleza ibara hii, uteuzi wa mjumbe kutoka sekta binafsi uzingatiwe

Uchambuzi wa kamati kuhusu ibara ya 6 kifungu kidogo (i) imebaini kuwa, maneno 'Katika mfumo husika' yanasomeka mwishoni mwa ibara hiyo yana utata ukilinganisha na maudhui ya ibara hiyo na kupendekeza maneno hayo yaendolewe. Baada ya majadiliano serikali ilikubaliana na mapendekezo hayo.

Ibara ya 6 imeeleza majukumu ya tume - kwa kurejea historia ya tume na majukumu yake inayokusudia kuyatekeleza Kamati imependekeza sheria inayopendekezwa iweke ulinzi wa mipango ya maendeleo itakayoandaliwa na tume ili iweze kubadilishwa tu pale inapotokea ulazima kwa lengo la kuiboresha. Serikali imekubaliana na ushauri wa kamati

Ibara ya 8,9, na 10 za muswada zinahusu mwenendo wa tume - kwa kiasi kikubwa Kamati inakubaliana na mapendekezo ya serikali, kamati ilipendekeza kufutwa kwa maneno ya pembeni (marginal notes) ya Ibara ya 8 yanayosomeka 'mwenendo wa tume' na kuweka maneno fasaha yanayohakisi maudhui ya ibara hiyo. Serikali ilikubali mapendekezo hayo.

Pia kamati ilipendekeza ibara itaje idadi ya chini ya vikao vya tume kwa mwaka kwakuwa angalau vinne kama ilivyo kwenye sheria mbalimbali zenye bodi au tume - baada ya majadiliano na serikal ilikubalika ibara ibaki kama ilivyopendekezwa katika muswada ili kuwezesha tume kuwa na vikao kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Sehemu ya 3 (Ibara ya 11-15) ya muswada inaweka masharti ya utawala
Katika ibadara ya 12 Kamati ilibaini kuwa ibara haijaeleza idadi na sifa za Naibu Makatibu Watendaji wa Tume wanaokusudiwa kuteuliwa. Kamati ilipendekeza ibara iboreshwe kwa kuwekwa idadi ya Naibu Makatibu Watendaji pamoja na kuanisha sifa zao kwa lengo la kuweka uwazi katika mchakato wa uteuzi na kupata watendaji wenye sifa stahiki. Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya kamati

Pia kamati ilipendekeza kuondoa wajibu wa tume kushauriana na waziri wa fedha kuanzisha jukwaa la mashauriano ili kumpatia waziri wa fedha nafasi ya kutosha katika masuala ya fedha. Baada ya majadiliano na serikali ilikubalika ibara iboreshwe kuakisi na kuleta maana iliyokusudiwa.

Sehemu ya 4 (ibara ya 16 - 21) inakusudia kuweka masharti yanayohusu masuala ya fedha
Kwa kiasi kikubwa kamati inakubaliana na mapendekezo ya masharti ya ibara hizi, lakini kamati ilipendekeza kufutwa kwa vyanzo vya fedha katika ibara ya 16(i)b na c kwa hofu kuwa tume itaanza kujikita katika kutafuta misaada, michango na fedha za taasisi badala ya kujikita katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya kuandaa, kusimamia na kufatilia mipango ya maendeleo. Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya kamati.

Kamati ilipendekeza pia kuboreshwa kwa ibara ya 21 kwa kuondoa maneno ya pembeni yanayosomeka 'na Mikataba ya utendaji' yanayopatikana baada ya maneno 'Taarifa za mwaka' kwakuwa maneno hayo hayaakisi katika maudhui ya ibara hiyo. Serikali ilikubaliana na pendekezo hilo.

Sehemu ya 5 (ibara ya 22 - 26) inaweka masharti ya jumla kuhusu muswada
Kwa ujuma Kamati ilikubaliana na mapendekezo.

Sehemu ya 6 (ibara ya 27 - 34) inaweka masharti ya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kuweka ufanisi wa utekelezaji wa sheria hizo na sheria ya tume ya mipango inayopendekezwa.

Ufafanuzi wa sheria zinazorekebishwa ni kama ifuatavyo;
  • Sheria ya bajeti sura ya 439
  • Sheria ya mikopo, dhamana na misaada ya serikali sura ya 134
  • Sheria ya viapo rasmi sura ya 266

Maoni na mapendekezo ya kamati
- Tume imepewa mamlaka ya kuwa chombo cha juu cha kiserikali katika kushauri kuhusu masuala yote ya mipango ya maendeleo kamati inashauri serikali kutoa elimu kwa wizara na taasisi zote za umma kuhusu mamlaka ya tume katika kuandaa, kusimamia na kutoa miongozo ya mipango ya maendeleo - Hii itasaidia kufangamanisha mipango inayoandaliwa na taasisi hizo na ile inayoandaliwa na tume ili kuihamisha mipango ya kisekta katika mamlaka hizo ya mipango ya tume.

- Elimu kwa umma itawezesha wadau wote kushiriki katika kuiwezesha tume katika kuipatia taarifa zitakazowesha uwandaaji na ufatiliaji wa mipango ya maendeleo.

- Kumalizika kwa dira ya maendeleo ya taifa mwaka 2025 kunaashiria kubadilishwa kwa sera mbalimbali ili ziendane na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 - 2050 kwa sababu hiyo Kamati inashauri sera mbaimbali zichambuliwe na kuangaliwa upya ili ziendane na mipango na dira mpya ya maendeleo ya taifa.

==

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa wa mwaka 2023 wasomwa kwa mara ya pili.
Maoni ya Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala, katiba na sheria kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa sura ya 406

Katika Ibara ya 2, Kamati ilipendekeza kufutwa kwa neno 'Tanzania' na kutumika kwa neno 'United Republic' ili kuweka usawa (uniformity) wa matumizi ya msamiati huo kama ilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. - Serikali ilikubaliana na maoni ya kamati.

Katika Ibara ya 3 (C) Kamati ilipendekeza kuongeza neno 'all necessary service' mara baada ya neno 'establishment' kwenye tafsiri ya msamiati 'vital installations' kwa nia ya kulinda vifaa au miundombinu mbalimbali inayotumika wakati wa utekelezaji wa shughuli za idara. - Serikali ilikubaliana na maoni ya Kamati.

- Katika Ibara ya 5 (A) inayohusu utoaji ulinzi kwa viongozi, Kamati ilipendekeza mpangilio wa orodha ya viongozi waliowekwa katika kifungu hicho kifuate itifaki sahihi kwenye mpangilio wa viongozi na kuwaongeza Wanasheria Wakuu wa Tanzania na Tanzania Zanzibar. Pia kamati ishauri kufutwa kwa neno 'in' kwenye ibara ya 5 (A)(xiv) na kuandika neno 'upon' ili kuweka ulazima kwa Mkurugenzi Mkuu wa idara kufanya mawasiliano na Rais kabla ya kuongeza mtu mwingine kwenye hadhi ya kupewa ulinzi wa idara. - Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya kamati.

- Ibara ya 7 (B) inakusudia kufanya marekebisho kwa kuweka masharti yanayozuia Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuajiriwa au Kuteuliwa katika nafasi yoyote ya Utumishi Serikalini baada ya kutumikia nafasi hiyo - Kamati ilishauri kuwa, katazo hilo liondolewe kwani linakinzana na Masharti ya Ibara ya 9 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997. Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya Kamati na kufuta ibara hii.

- Katika Ibara ya 8, Ibara ndogo ya 3 inayohusu sifa ya kumteua Naibu Mkurugenzi Mkuu, Kamati ilipendekeza kuweka sifa ya mtu ambae atateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu Bara awe na asili ya kutoka Tanzania Bara kama ilivyo kwa Tanzania Zanzibar. - Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya Kamati.

- Katika Ibara ya 11 (A) inayohusu Mkurugenzi Mkuu kuwa ni Mamlaka ya mwisho ya nidhamu na maamuzi yake kuwa ya mwisho, Kamati ilipendekeza kuwa Ibara hii ilieleze kuwa kutakuwa na Mchakato wa Kisheria (Due process) na kufuta maneno 'final and conclusive' yanayoonekana katika Ibara hiyo na badala yake ibaki tu kuwa 'Mkurugenzi Mkuu atakuwa mamlaka ya nidhamu kwa Watumishi wa Idara kwa kuzingatia Masharti ya Kifungu cha 12 cha Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa.' - Serikali ilikubaliana na ushauri wa Kamati na kufanya mabadiliko hayo.

- Katika Ibara ya 18 ni maoni ya Kamati kuwa Serikali ilikusudia kuongeza Ibara ndogo ya 3 na sio kuifuta kwakuwa haipo kwenye Sheria Mama, hivyo Kamati ilipendekeza kufuta maneno 'deleting subsection 3' na 'Substituting for it' na badala yake kuandika maneno 'adding immediately after subsection 2' ili kuleta maana iliyokusudiwa na Serikali. - Serikali ilikubaliana mapendekezo hayo.

- Katika Ibara ya 22 (B) Kamati ilipendekeza marekebisho ya kiuandishi kwa kufuta neno 'carving' na kuweka neno 'carrying' ili kuleta maana iliyokusudiwa. Serikali ilikubaliana na mapendelezo ya Kamati na kufanta marekebisho.

===

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali yatokanayo na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 wasomwa kwa mara ya pili
 
  • Thanks
Reactions: RNA
TOFAUTI YA KIKAO NA MKUTANO NA UPI?

Mkutano umekutanwa mara nyingi kuliko kikao? kiaje sijaelewa😅😅😂😂
 
Back
Top Bottom