JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Baadhi ya Wachangiaji ndani ya JamiiForums wamezua Mjadala kuhusu 'Homeworks' nyingi wanazopewa Watoto toka Shuleni hasa kipindi cha likizo
Ikiwa wewe ni Mzazi, Mlezi au Mwalimu ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika leo Desemba 2, 2021 kupitia Clubhouse.
Kushiriki mjadala huu bonyeza link
Wanafunzi kuendelea na Masomo wakati wa Likizo - JamiiForums
With Ummy Mwalimu, Carol Ndosi and 10 others, hosted by JamiiForums
www.clubhouse.com
BAADHI YA MAONI NA MAWAZO YALIYOTOLEWA NA WADAU WAKATI WA MJADALA
Baraka (Mwalimu): Mtaala wetu wa Elimu una mambo mengi ndio maana unasababisha Walimu wengi kutomaliza wanayotakiwa kufundisha hivyo kuanzisha mfumo wa masomo ya ziada.
Tunatakiwa kurahisha Mfumo wa Elimu yetu. Tuna mambo mengi Wanafunzi wanafundishwa ambayo hayana maana kwetu.
Bazo Komu: Aliyetangulia kuongea amesema point za Msingi sana. Natamani tamko la Waziri lisifanye kazi kwenye Shule za Serikali tu bali Shule zote.
Watoto siku hizi hatuwajengi bali tunawabebesha mizigo ili mambo yaende. Mtoto wa darasa la 5 anabeba begi ambalo mimi siliwezi.
Bazil Komu: Tunawadumaza Watoto badala ya kuwajenga. Mtoto anahitaji kujifunza mambo ya kidunia, kidini na ku-refresh mind. Siku hizi wanapata Elimu ya darasani na kula.
Akirudi ana homework na anawahi school bus asubuhi. Hatujengi kizazi cha kupambana na changamoto za Dunia.
Simon Msenga: Tunaposema tusitishe huduma ya Masomo wakati wa likizo lakini inabidi tuangalie na namna ya kuwasaidia hawa Wanafunzi.
Sio Madarasa yote huwa yanabaki Shuleni ila unakuta ni Madarasa yale yenye mitihani. Shule za Serikali hazifanyi vizuri sana kwenye matokeo.
Zawadi Mkweru: Nizungumzie Enlish medium, kuna changamoto kubwa watoto huwa wanapewa kazi nyingi sana. Inawezekana walimu wana lengo zuri lakini zile kazi zinakuwa nyingi sana.
Unakuta likizo inapokaribia kuisha watoto wanaanza kustruggle kuzimaliza.
Zawadi Mkweru: Mfumo wa Elimu una mambo mengi sana, hata mimi nakumbuka kuna vitu vingi nilivisoma lakini sivitumii hivi sasa
Kuna mambo mengi ya muhimu ambayo nilipaswa kufundishwa lakini sikuyapata. Kwa hiyo iangaliwe namna ya kupunguza masomo.
Glory Tausi: Glory Tausi: Kuna shughuli nyingi za kijamii tunazoweza kufanya ambazo zitafanya watoto wawe bora zaidi kuliko hizo 'Homework'
Pia watoto wanahitaji kupata muda wa kuwa watoto kwa kucheza, kuna wakati tunataka kusafiri na watoto wetu kwenda kwa babu/bibi ili ajuane na ndugu wengine.
Sultan: Vijana wa siku hizi wamekuwa na kauzito kwenye kushika yale wanayofundishwa hivyo inabidi Mwalimu aende taratibu ili kuwapata Wanafunzi wote
Wanafunzi wengi akishasogea darasa la mbele anasahau vitu vyote vya darasa la nyuma. Pia, Walimu wana mambo mengi ya kufundisha.
Sultan: Nadhani tunaweza kupunguza muda wa hizi 'tuition' wakati wa likizo. Labda badala ya kufundisha Mwezi mzima iwe wiki 2
Vijana wanaangalia vitu vingi kwenye Jamii na Television jambo linalofanya Ubongo uwe mzito kushika vitu Darasani. Mzazi anaacha Mtoto anaangalia 'Series'.
Abdul Nondo: Maamuzi haya yanaegemea upande mmoja ambayo yanaenda kutatua matatizo yanayotokea maeneo tofauti. Maamuzi yamefanyika kana kwamba kuna tafiti iliyofanya kuonesha hii ni changamoto kwa wanafunzi wote.
Mimi nimesoma Kigoma, nilipata division 3 huku wanafunzi wengine wakiwa wamepata 4 na 0, shuleni hakukuwa na vipindi vya ziada. Mimi nilipambana ninavyojua, kwa hiyo wanaokubali suala la likizo inategemea na maeneo yao, sio suala la nchi nzima.
Abdul Nondo: Tamko la Waziri ni zuri na linaonesha Moyo wa Uzazi. Lakini hakuna tafiti iliyofanyika Tanzania nzima kufahamu haya Masomo ya likizo yameleta athari kwa kila sehemu.
Mimi nilipata division III, hakukuwa na 1 wala 2 kwasababu hatukuwa na 'remedial classes'.
Abdul Nondo: Siku 164 ambazo Wanafunzi wanatakiwa kuwepo Shule huwa hazitimii kwasababu huwa kuna sikukuu humo katikati
Huku Kigoma Wazazi wenyewe wamekubali hizo tuition na Walimu wako tayari. Kuna Wanafunzi akisikia neno likizo ndio anasahau kila kitu kabisa.
Justine Kakoko: Watoto huendelea kusoma hata wakati wa likizo ni kwa sababu tunaamini sana katika kufundisha kuliko kujisomea. Hii hofu ni changamoto kwa kuwa tunaamini watoto hawawezi kujisomea.
Justine Kakoko: Hofu ya mtoto kushindwa kujisomea kwa kuwa hatujajenga tamaduni ya kujifunza wenyewe bila mtu kusimama mbele yao.
Wazazi hawana muda wa kukaa na watoto hata wakati wa likizo, wazazi wanaamini shuleni ni sehemu salama ya mtoto kukaa.
Justine Kakoko: Kuna baadhi ya shule wazazi hulilia watoto wabaki shuleni, sio mara zote kuwa shule inalazimisha watoto kubaki shuleni.
Kuna watoto pia hubaki shule kama njia ya kufanya masoko hasa kwa shule binafsi, wazazi hupenda kuona shule inasoma muda wote.
Justine Kakoko: Masomo yana mambo mengi kiasi cha kuhitaji muda wa ziada kumaliza mambo yote. Madarasa ya mitihani yana mitihani mingi, hivyo wamiliki huona njia ya maandalizi ni kuwabakisha shule.
Justine Kakoko: Tunahitaji kuwapima watoto kwa njia zote tatu na kujenga nidhamu binafsi. Kipimo pekee kinachotumika ni kutumia mitihani ambapo tunashindwa kupima masuala mengine yanayohusu kuendelea kwa mtoto
Justine Kakoko: Wazazi wajengewe uwezo wa kuweza kusimamia watoto wakiwa nyumbani. Shule zinaweza kutengeneza semina au kwenye vikao vya wazazi kwa kuwa kusimamia sio kufundisha, mtu anaweza kufundisha hata kama hana uwezo wa kusoma na kuandika.
Godfrey Boniventura (Haki Elimu): Kiukweli mitihani inachangia woga kwa Wanafunzi, Walimu na Wazazi hasa kwa madarasa ya mitihani. Mitihani kwa sasa huonekana ni kila kitu, Wazazi hujiuliza itakuwaje mtoto akifeli
Boni wa Haki Elimu: Shule za binafsi zinafanya biashara hivyo hulazimisha sana watoto kufaulu. Kwa kuwa watoto wakifaulu huvutia zaidi biashara, na hii huleta changamoto kubwa.
Godfrey Boniventura (Haki Elimu): Shule za blBinafsi zinafanya biashara hivyo hulazimisha sana watoto kufaulu. Kwa kuwa watoto wakifaulu huvutia zaidi biashara, na hii huleta changamoto kubwa.
Godfrey Boniventure (Haki Elimu): Nashauri watoto wafanyiwe Assessment sio Examinations. NECTA wafanye Assessment ili kuondoa woga kwa hawa watoto. Pia, tuachane na kusema shule ipi ya kwanza shule ipi ya mwisho.
Alpha: Mfumo wa Elimu unamtaka Mwanafunzi atoke shuleni akiwa amefaulu mtihani sio kuwa ameongeza maarifa. Suala la kufaulu mitihani ndio hufanya Walimu wabakishe Watoto shuleni.
Assah: Mwalimu bora ni yule anayeweza kufundisha watoto ndani ya muda halisi ambapo wale wanaelewa kwa haraka kupata faida ya kujifunza mara mbili.
Kuhakikisha darasa zima wanaelewa kwa hiyo hakuna maana ya kutetea muda wa ziada ambapo watoto hupaswa kupumzika.
Ummy Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Ummy Mwalimu: Mimi kama Waziri, kauli yangu ililenga katika kutekeleza maelekezo ya kisera kutoka kwa mawaziri kisekta.
Marufuku ya wanafunzi kubaki shuleni wakati wa likizo ilitoka kwa Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako.
Ummy Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Elimu sio vita mtoto apate muda wa kupumzika. Kama kuna tatizo lolote linalohitaji siku za ziada Shule au Mamlaka italazimika kuomba kibali kutoka kwa Kamshna wa Elimu.
Umm Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Sisi kama TAMISEMI tumeandaa kalenda ya mtaala inayonesha mwanafunzi atafundishwa kitu gani ndani ya siku zinazoelekezwa. Ndani ya siku 194 tunajua tuliyoyapanga kufundishwa yatamalizika.
Umm Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Sisi kama TAMISEMI tumeandaa kalenda ya mtaala inayoonesha mwanafunzi atafundishwa kitu gani ndani ya siku zinazoelekezwa.
Ndani ya siku 194 tunajua tuliyoyapanga kufundishwa yatamalizika.
Ummy Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Sio tu likizo hata siku za kawaida watoto wanajifunza mpaka Jumamosi wanakosa muda wa kujifunza mambo mengine. Kwa mamlaka yangu kama Waziri wa TAMISEMI naagiza shule zote ziheshimu likizo za Wanafunzi.
Ummy Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Kwa sasa umezuka mchezo mbaya, shule ikifanya vibaya Afisa Elimu kata na Halmashauri wanashushwa vyeo. Nimepiga marufuku tabia hii kwa wakurugenzi kwa kuwa kabla hujamshusha cheo lazima uangalie ulimuwezesha kiasi gani.
Ummy Mwalimu (Waziri wa TAMISEMI): Kwa sasa umezuka mchezo mbaya, shule ikifanya vibaya Afisa Elimu Kata na Halmashauri wanashushwa vyeo. Nimepiga marufuku tabia hii kwa Wakurugenzi kwa kuwa kabla hujamshusha cheo lazima uangalie ulimuwezesha kiasi gani