Spika Ndugai haya uliyosema kuhusu Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa mbona mwaka 2017 hukuyasema wabunge wa CUF walipotimuliwa?

Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?

Umesema vyema. Lakini mimi niko kwenye kipengere hiki...

Unasema angeomba uthibitisho wa "kufukuzwa kwao". Uthibitisho gani wakati anayo barua mkononi mwake?

Chama kinatoa taarifa kwa Spika, na si vinginevyo kama anavyonwabwaja kuwa sijui walete hiki na kile nk nk..

Uthibitisho hutolewa mahakamani. Na wenye uhalali wa kuomba uthibitisho (uhalali wa mchakato wa kufukuzwa kwao ni hawa wabunge 19, siyo Spika) kupitia mahakama kama wakitaka...

What Mr Speaker is doing is stupidity with ignorance in it...!
 
Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?
jamaa alitaka siku ya kikao angekuwepo ili ahakikishe akidi kama imetimia na maamuzi yapi yamefikiwa - huyu ndiyo kiongozi wa chombo kikubwa kabisa cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali nchini kwetu.

Pole Tanzania hawa ndiyo wanaukuzika ukiwa mzima.
 
Ndugai kaa fikiria, suala la katiba halina uzoefu we fuata tu, hata kama unakinga ya kuto shitakiwa, uoni aibu? Waliofukuzwa wanajijuwa hawana chama wewe na naibu wako mnapishana mara hakuna taarifa mara kwa karatasi hii sio ya kuichukulia hatua, kumbuka ulie kuwa unashauriana ujinga huo hayupo tena, huko peke yako ukiendeza ujinga, acha!
 
Inashangaza taifa ambalo katiba yake imetamka wazi kuwa ni taifa linaloheshimu misingi ya demokrasia haki na utii wa sheria alafu linakuwa na spika asiyejitambua. Hii ni aibu kwa karne hii ambayo kila mtu anatambua umuhimu wa kuheshimu sheria.

Kama spika unayejitambua basi ungesoma ibara ya 8(1)(a) alafu ukawaomba msamaha watanzania kwa jinsi ulivyokengeuka na kuisigina katiba inayotoa mamlaka ya kutawala.

Kwa kuwa katiba ndio inatoa mamlaka ya kutawala na mamlaka hayo yapo kwa watu wanaounda taifa la Tanzania basi ulipaswa kuacha mara moja kuikanyaga katiba maana madhara yake ni makubwa.

Ibara ya 71(1)(e) ya katiba ya jamhuri ya Tanzania ipo wazi na haihitaji ufafanuzi. Ukomo wa mbunge utatokea pale uanachama wake utakoma kwenye chama alichochaguliwa kuwa mbunge.

Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?

Kwa kuwa katiba ni sheria mama na ndio inayotoa mamlaka ya kutawala na mamlaka haya yapo mikononi mwa wananchi basi tambua hii nchi ni mali ya watanzania. Hivyo usifanye maamuzi kwa utashi wako bali zingatia kaiba inasema nini.

Unaliabisha taifa letu kwa kuleta ubabe usio na maana.
Hayo si ndio ameyaomba? au hiyo taarifa yake hujaipata?
 
Kuna wakati unajiuliza kwanini mungu alimtoa Mahiga ama Ndulu katika hùu ulimwengu na kumuacha mtu wa hovyo kama huyu Ndugai. Kuna binadamu kama akina Kijazi walitakiwa wawepo sio huyu.
Mkuu maneno huumba na ndicho kilichotokea kwa mwendazake. Tena yeye mwenyewe alivyo spana mkononi!
 
jamaa alitaka siku ya kikao angekuwepo ili ahakikishe akidi kama imetimia na maamuzi yapi yamefikiwa - huyu ndiyo kiongozi wa chombo kikubwa kabisa cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali nchini kwetu.

Pole Tanzania hawa ndiyo wanaukuzika ukiwa mzima.
Akipewa muhtasari atataka picha za kikao.
 
Amekiri kupokea barua ya CHADEMA lakini alipuuza hakuijibu. Angewajibu kwa barua rasmi CHADEMA kwamba barua yao ilikuwa 'kipeperushi'. Badala yake amejibu kwa ngonjera za bungeni! Kwani yeye halazimiki kufuata utaratibu rasmi wa mawasiliano kati ya ofisi yake na CHADEMA?
Kwa kitendo hiki yeye Ndugai hajawadhalilisha bungeni na mbele ya jamii wanawake anaojigamba anawalinda hata kwa kudharau maamuzi na barua ya CHADEMA kuhusu masuala yao binafsi na chama chao?
Anaposema "wanalindwa" anamaanisha bunge zima limeamua wazi kupingana na CHADEMA juu ya masuala ya ndani ya chama hicho?
Spika anatakiwa kuwa neutral katika BUNGE vinginevyo litakuwa kama kamati ya CCM.
 
Nafikiri wakati mwingine tunatakiwa kuwa wakweli pale ambapo kila kitu kiko wazi. Tusingoje kuabishwa. Pamoja na mimi kutopenda kususia uachaguzi, lakini hiyo ni hiari ya chama cha siasa. Kususia uchaguzi kunakuja na faida au hasara zote za kususia. Tokeo kubwa la kususia ni kupoteza nafasi zote ambazo zingipatikana na huo uchaguzi. Kwa maana hiyo unaposusia huwezi susia nusu nusu. Kwa kifupiwaliposusia walipoteza haki ya ubunge wa vitu maalum.

Hata kama CHADEMA wangeamuwa kususia nusu nusu, ni lazima taratibu za kujaza hizo nafasi zifuatwe. Mimi nasikitika chombe kikubwa kama bunge kwa ushauri mbovu wa Ndugai wanaweza kukubali wabunge toka CHADEMA, ambao CHADEMA ilisema haikuwateua. Kama hawakuteuliwa, hiyo inatosha kuwaondoa buneni, kwa sababu hawana kigezo chochote cha kuwaruhusu kuwa wabunge, kwa sababu sponsor wao CHADEMA amewakana.

Tatizo lingine, ni pale mwanachama anapokuwa amefukuzwa chama. Ukifukuzwa kwenye chama, huwezi kuendelea kuwa mbunge unaotegemea uteuzi wa chama husika. Hawa tayari si wanachama, kwa hiyo hawawezi kuendelea kuwa wabunge kwa sababu tayari wamekosa sifa baada ya kufukuzwa.

Mimi mara nyingi namuona Ndugai anaendesha chombo muhimu kihuni. Bunge siyo sehemu tunayotegemea kutakuwa na uvunjaji wa katiba. Bunge linatakiwa kuilinda katiba. Kuilinda katiba ni pamoja na kuhakikisha wabune wote walioapishwa au watakaoapishwa wako bungeni kisheria kwa kuwa na sifa zote za kuwa wabunge. Kama ndugai hana hakika ni juu yake kutafuta ushauri wa kisheria kuhusu hilo.

Mwisho, namuomba Ndugai aheshimu bunge na kiti chake. Aache uzandika na matani ambayo hayana tija. Matani na uzandiki na ishara tosha kuwa huyu Bwana kiti cha Uspika kimempwaya, ndiyo maana anafanya maamuzi ya ovyo na inaonekana hana msimamo. Ndugai alikuwa ni kati ya wabunge ambao walikuwa wanampigia Magufuli, lakini leo hii utamuona anajaribu na yeye kujionyesha ana mawazo yake, ndiyo maana akachomekea ishu ya bandari ya Bagamoyo, huku huko nyuma alikuwa nyuma ya ishu. Nafikiri huyu ni mtu wa kujipendekeza, na hakuna mtu wa hatari kama mtu wa kujipendekeza.
Lakini hii sio mara ya kwanza bunge kuwa na watu wa aina hiyo, hata akina Zitto waliwahi kusurvive bungeni kwa njia hiyo. Chadema walisusa inawabidi wakae kimya hawawezi kulalamika kwa niaba ya wapiga kura wote, kwani akina Halima hawakuikosea chadema bali katiba na walipa kodi wote. Nia ya cdm lazima waiweke wazi. Je, wanataka kuyatambua matokeo na kupeleka watu wao bungeni, je, wana uchungu na hela za walipakodi wanazolipwa akina Halima, je, nini hasa?
 
Mkuu kavulata, kwanza asante kwa bandiko hili, naunga mkono hoja.
  1. Kwanza ni kweli Chadema walisusa, kwa maoni yangu, huu ni ujinga tuu. Chedema ilikuwa inafanya ujinga. Very fortunately sio wana Chadema wote ni wajinga, hivyo Halima na kundi lake la wabunge 19, waliukataa ujinga huo wa Chadema. Hawa ni mashujaa.
  2. Ni kweli Kina Halima wamefukuzwa kwa vivu tuu na ujinga, ila pia kufukuzwa kwao ni batili kwasababu Chedema haikufuata sheria, taratibu na kanuni zao wenyewe walizo jiwekea. Chadema walizoea Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
  3. Chadema inasumbuliwa na wivu tuu wa inda!. Kitu wewe hukitaki, akikipata mwingine, unakasirika!
  4. Hili la kuyakubali matokeo ndio mpango mzima, hata mimi niliwashauri CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao
  5. Huu pia ni kuwaonea wivu tuu.
  6. Hizo njia kina Halima walizotumia ndio issue. Kwa vile nafasi za wabunge wa viti maalum, zinatolewa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama kuna mbinu zozote zilizokwenda kinyume cha sheria, taratibu na kanuni katika kuwapata, then huu ni ubatili. Tusikubali Bunge letu liendeshwe kwa ubatili.
  7. Nafasi hizo ni za Chadema kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, haziwezi kugaiwa CCM, zingebaki wazi.
  8. Kwa vile kutoyatambua matokeo ni ujinga, uliosababishwa na kuchanganyikiwa na matokeo. Sasa akili zimeanza kuwakaa sawa and doing the right thing kwa kuyatambua matokeo.
  9. Huu sasa ndio mpango mzima, ila ni kama kawaida yao, sio tuu watapeleka wake zao, kwasababu kumpeleka mke bungeni ni heshima, ila watapeleka sio wake tuu, hadi vimada na vidumu!.
P
Hoja ya cdm kwenye malalamiko yao ni nini? Je, wanataka kuyatambua matokeo na kupeleka watu wao bungeni? Je, wanataka kuokoa hela zetu wananazolipwa akina Halima kimakosa? je, wanalalamikia Spika kuvunja katiba ya nchi kuruhusu wabunge waliofukuzwa kwenye chama kilevi, Je, wanalalamikia mchakato wa kuwapata akina Halima? au nini?

Nadhani hoja yao kama cdm iliishia pale walipoyakataa matokeo na walipowafukuza uwanachama akina Halima, full stop!
 
1. Haijalishi waliteuliwa kihalali au siyo kihalali wakishafutwa uanachama wanapoteza sifa ya ubunge na hili limekuwa likifanyika mara kwa mara kuna wabunge nane wa CUF walifukuzwa na Lipumba na kesi ikiwepo Mahakamani Ndugai aliwaondoa bungeni akiwa South Africa.

2. Speaker anapaswa kupewa taarifa na siyo minutes za vikao hata sheria ya uchaguzi iko wazi juu ya hilo.

Ni kuulize hivi Spika anatumia sheria ipi kuomba mihutasari ya vikao vya CHADEMA ?

Kamati kuu ina mamlaka ya kuwafukuza uanachama mwanachama yeyote hata Mbowe hilo Baraza kuu wewe unalitaka la nini ?

CHADEMA wameshaandika barua ya kuwa wao hawakufanya mchakato wa uteuzi wa hao wabunge na kwa taarifa yako katika hao 19 wawili walikuwa ni wajumbe wa kamati kuu ya chama hivyo vikao vya kuwateua vilifanyika wapi ?
Kwani alitumia sheria gani kuwabakiza akina Zitto kwenye ubunge hadi mwisho wa uhai wa bunge? Mbona wakati ule wa akina zito Bawacha hawakuimba mapambio kama wakati huu. Njaa kitu kibaya sana.
 
Wewe umeshiba kweli au??!!-----Hao kina Halima ni Wanachama wa chama kipi cha siasa??, je inaruhusiwa na sheria mtu kuwa mbunge bila Chama??.

Chadema imewafutia uanachama hao akina Halima, moja kwamoja na ubunge wao unakoma.

Yeye Spika mambo ya ndani ya Chadema yanamuhusu nini??, mambo ya ndani ya Chadema ni kati ya hao waliofukuzwa uanachama na uongozi wa chama na suala hilo laweza pia kupelekwa Mahakamani, kamwe Spika hawezi kuwa hakimu wa mgogoro huo wa kisiasa.
Sikatai hilo hata mimi, lakini hoja kama hiyo sio ya chadema tena, wao walishayakana matokeo hadi sasa na wamesema wamewafukuza uwanachama akina Halima, shida ya cdm ni nini hapo? Waache watu wengine walalamike lakini sio chadema.
 
Sikatai hilo hata mimi, lakini hoja kama hiyo sio ya chadema tena, wao walishayakana matokeo hadi sasa na wamesema wamewafukuza uwanachama akina Halima, shida ya cdm ni nini hapo? Waache watu wengine walalamike lakini sio chadema.


Spika anasema hao kina Halima ni Wanachama wa Cdm na ndiyo maana ya wao kuendelea kuwa wabunge kwa tiketi ya cdm, Cdm inasema hao sio tena wanachama wao na imepeleka barua kwa spika kumjulisha jambo hilo.

Ni hivi, kama spika angesema hao kina Halima sio wanachama wa chama chochote hivi sasa basi hapo cdm isingekuwa na haki ya kulalamika isipokuwa kesi ingebaki kwa spika kuvunja katiba kwa kuwaruhusu Watu wawe wabunge bila kupitia chama cha siasa lakini hivi sasa cdm inayo haki ya kulalamika kwasababu chama chao kinatumika kuhalalisha ubunge wa kina Halima kinyume na katiba ya nchi na kinyume na maamuzi ya chama chao kwani hao kina Halima wamefukuzwa chamani.

Ndugai ni spika wa ajabu sana, historia itamuandika hivyo.
 
Back
Top Bottom