Spika Ndugai haya uliyosema kuhusu Wabunge wa CHADEMA waliofukuzwa mbona mwaka 2017 hukuyasema wabunge wa CUF walipotimuliwa?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
2,078
2,000
Bila aibu wala kuona soni unadiriki kusema kuwa ili uamini kuwa hao akina Mdee na wenzake 18 lazima upewe muhtasari wa kikao kilichowafukuza? Mbaya zaidi unaongea bila aibu kuwa ili wewe upate uthibitisho kuwa hao akina Mdee walifukuzwa unataka uthibitisho kuwa natural justice ilizingatiwa. Hivi una mshipa wa aibu kweli?

Kama natural justice haukuzingatiwa mbona walikata rufaa? Kama kulikuwa hakuna kikao halali mbona walikata rufaa?

Mwaka 2017 mwezi julai ulipokea barua toka kwa Lipumba juu ya wabunge wa CuF waliofukuzwa. Na wewe bila mashariti yoyote unayotoa sasa hivi uliridhia kuwafukuza. Iweje kwa hawa akina mama 19 ndio uwe na masharti?

Tumia akili na utambue kuwa katiba ni sheria mama.

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,363
2,000
Tangia Uhuru Tanzania haijawahi kupata spika wa hovyo kama dikiteta ndugai, nimeshangazwa na huruma na busara aliyoonyesha kwa hawa covid19, Vp alishindwaje kuitumia kwa kina mama 8 wa cuf? Au wale si wanawake au kipindi hicho mfumo dume haukuwepo?
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,176

Sidhani kama ni dikteta, mpaka kaongea hivyo inawezekana wenye CCM yao wameshaamua hii fedhea na aibu kukomaa nayo mpaka 2025, yeye kama yeye hawezi kutema shombo lote hilo bila baraka za mihimili mingine. Otherwise wawe wanamtega.
 
ngutesha

Member
Nov 13, 2018
90
150
Bila aibu wala kuona soni unadiriki kusema kuwa ili uamini kuwa hao akina Mdee na wenzake 18 lazima upewe muhtasari wa kikao kilichowafukuza? Mbaya zaidi unaongea bila aibu kuwa ili wewe upate uthibitisho kuwa hao akina Mdee walifukuzwa unataka uthibitisho kuwa natural justice ilizingatiwa. Hivi una mshipa wa aibu kweli?

Kama natural justice haukuzingatiwa mbona walikata rufaa? Kama kulikuwa hakuna kikao halali mbona walikata rufaa?

Mwaka 2017 mwezi julai ulipokea barua toka kwa Lipumba juu ya wabunge wa CuF waliofukuzwa. Na wewe bila mashariti yoyote unayotoa sasa hivi uliridhia kuwafukuza. Iweje kwa hawa akina mama 19 ndio uwe na masharti?

Tumia akili na utambue kuwa katiba ni sheria mama.
View attachment 1772141
Spika ni dhahihiri hauko hufuata sheria.Unalazimisha,hata waliotimuliwa Chadema wanajua wamefukuzwa kihali.Unawatetea sana.Haya mambo yatakuwa na mwisho mbaya kwa kitiu chako.Sidhani kama rais wa nchi hilo jambo lina afya kwke.
 
Roy Logan

Senior Member
Jan 22, 2021
143
1,000
Nilichogundua pamoja na Mwendazake kutuachia Nchi yetu na kwenda kusikojulikana, CCM bado inatumia mbinu za Mwendazake kupambana na CDM, Ndugai na Tulia ni viongozi wa hovyo sitatamani hata kuwaambia wajukuu zangu kwamba hawa walikuwa viongozi wa Bunge.
 
binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,822
2,000
Kiukweli kabisa, hili la hawa wabunge litaleta shida sana, ni labda tuachane nao au tushinikize maamuzi magumu. Kwasababu hawa wapinzani bungeni wanahitajika ili kutumiza masharti fulani fulani ndio maana wanawang'ang'ania.

Kwahiyo ni either waachwe au bunge livunjwe tufanye uchaguzi upya kupata balance ya upinzani bungeni. Walioiba uchaguzi hawakuwa smart enough kulifikiria hili matokeo yake ni huu mvutano.
 
mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,606

Dah! Huyu Ndugai ataenda katika historia ya nchi hii kama Spika wa ovyo kabisa tangu historia ya nchi hii ianze!
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,678
2,000
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura?
Naona unalazimisha mabwana kinguvu, maana kila uzi unaanguka mbele ya wanaume kifudifudi, hamna shida, utapata mti muda si mrefu.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,150
2,000
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura?
Wewe ni darasa la Sana. Lisu katika wapi hapa.
 
Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,514
2,000
Inashangaza taifa ambalo katiba yake imetamka wazi kuwa ni taifa linaloheshimu misingi ya demokrasia haki na utii wa sheria alafu linakuwa na spika asiyejitambua. Hii ni aibu kwa karne hii ambayo kila mtu anatambua umuhimu wa kuheshimu sheria.

Kama spika unayejitambua basi ungesoma ibara ya 8(1)(a) alafu ukawaomba msamaha watanzania kwa jinsi ulivyokengeuka na kuisigina katiba inayotoa mamlaka ya kutawala.

Kwa kuwa katiba ndio inatoa mamlaka ya kutawala na mamlaka hayo yapo kwa watu wanaounda taifa la Tanzania basi ulipaswa kuacha mara moja kuikanyaga katiba maana madhara yake ni makubwa.

Ibara ya 71(1)(e) ya katiba ya jamhuri ya Tanzania ipo wazi na haihitaji ufafanuzi. Ukomo wa mbunge utatokea pale uanachama wake utakoma kwenye chama alichochaguliwa kuwa mbunge.

Sasa kama watu walishafukuzwa Chadema, na chama chao kikakuandikia barua kuwa walishafukuzwa wewe kwa nini hutaki kuamini kuwa walishafukuzwa? Ok kama huamini kwa nini usiombe uthibitisho kuwa walifukuzwa na vikao halali?

Kwa kuwa katiba ni sheria mama na ndio inayotoa mamlaka ya kutawala na mamlaka haya yapo mikononi mwa wananchi basi tambua hii nchi ni mali ya watanzania. Hivyo usifanye maamuzi kwa utashi wako bali zingatia kaiba inasema nini.

Unaliabisha taifa letu kwa kuleta ubabe usio na maana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom