Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

wabunge wetu wangeacha kuwa wanafiki kuliko unafiki ulivyo. kama ni wazalendo kweli wakubali kukatwa fedha kama wengine wanavyokatwa waache unafiki hawa watu.
 
Uko sahihi
Maisha yanaendelea kama kawaida. Mwenye kujiamini haogopi kufanya anachokiamini eti kwa sababu kifo kipo.

Anakufa imamu, anakufa Papa, anakufa mzee anayeheshimiwa na jamii!.

Cha muhimu hapa duniani tuheshimiane tusitake kupandana juu ya vichwa. Mtu asitake ku-blackmail ufanisi wa mtu eti kwa kitisho cha kifo!.

Maisha yote kwa ujumla wake ni neema tu.
 
Mheshimiwa Job Ndugai amewataka watanzania kutoa mbadala ili tujenge nchi. Ukweli japo sisi watanzania tunazo kwikwi juu ya ulipaji Kodi ukilinganisha na nchi zingine. Binafsi sitoi mbadala Ila nitoe marekebisho njia Bora kwetu sote kama watanzania kuenenda Sawa.

Kwa Kodi hii ya kizarendo naomba Kwanza viwango vishuke kidogo ili watanzania japo tujipe uzoefu Ila ili kuziba pengo tuweke tozo kwenye mishahara ya wabunge mawaziri na Raisi Kwa kuwa ni kundi linaloongoza japo kuwa vizuri kuliko makundi mengine ya watanzania.

Nadhani kama viongozi tutakuwa tumeonyesha njia badala ya kuwa nyampara na tutawaelewa zaidi.
 
hata saa mbovu huwa unaonyesha wakati sahihi mara mbili kwa siku. Hatimae Mzee wa Mirembe katumia tone la fikra zake zilizobaki. Ila huyu mwamba hakawii kubadilika akakanusha kuwa ameeleweka vibaya.

Kwa mtazamo tofauti pia, huyu Mama anapaswa ajiongeze kuzingatia waliomzunguka. Maana ni kama vile wanamkaanga hadharani.
 
Mheshimiwa Job Ndugai amewataka watanzania kutoa mbadala ili tujenge nchi. Ukweli japo sisi watanzania tunazo kwikwi juu ya ulipaji Kodi ukilinganisha na nchi zingine . Binafsi sitoi mbadala Ila nitoe marekebisho njia Bora kwetu sote kama watanzania kuenenda Sawa. Kwa Kodi hii ya kizarendo naomba Kwanza viwango vishuke kidogo ili watanzania japo tujipe uzoefu Ila ili kuziba pengo tuweke tozo kwenye mishahara ya wabunge mawaziri na Raisi Kwa kuwa ni kundi linaloongoza japo kuwa vizuri kuliko makundi mengine ya watanzania. Nadhani kama viongozi tutakuwa tumeonyesha njia badala ya kuwa nyampara na tutawaelewa zaidi.
Tumuulize faida ya kodi ni nini?
Nani ananufaika na hiyo kodi?
Pasipo kodi yeye anapata hasara gani?
Hiyo kodi inampa faida gani?
Nani mwenye wajibu wa kulipa kodi na kwanini?
Nani hapaswi kilipa kodi na kwanini?
Nani anayestahili kunufaika na kodi bila kulipa kodi na kwanini?
 
1: Viongozi wote walipe kodi.
2: Marupurupu yapunguzwe.
3: kodi zielekezwe kwenye shughuli za muhimu na za maendeleo sio kulipa wabunge wake spika (hawana majimbo sio wawakilishi)
4: Nafasi nyingine zipunguzwe ili kupunguza matumizi ya hizo kodi mf. Wabunge wa viti maalumu n.k n.k
(Kuna lundo la vyeo ambavyo havina hata cha maana zaidi ya kutafuna tu kodi)
 
Maswali mazuri Sana haya sina uhakika yanaweza kumfikiaje
 
Mheshimiwa Job Ndugai amewataka watanzania kutoa mbadala ili tujenge nchi. Ukweli japo sisi watanzania tunazo kwikwi juu ya ulipaji Kodi ukilinganisha na nchi zingine . Binafsi sitoi mbadala Ila nitoe marekebisho njia Bora kwetu sote kama watanzania kuenenda Sawa. Kwa Kodi hii ya kizarendo naomba Kwanza viwango vishuke kidogo ili watanzania japo tujipe uzoefu Ila ili kuziba pengo tuweke tozo kwenye mishahara ya wabunge mawaziri na Raisi Kwa kuwa ni kundi linaloongoza japo kuwa vizuri kuliko makundi mengine ya watanzania. Nadhani kama viongozi tutakuwa tumeonyesha njia badala ya kuwa nyampara na tutawaelewa zaidi.
Hii post ni maneno ya ndugai au ni wewe ndo umetoa mtazamo wako mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1: Viongozi wote walipe kodi.
2: Marupurupu yapunguzwe.
3: kodi zielekezwe kwenye shughuli za muhimu na za maendeleo sio kulipa wabunge wake spika (hawana majimbo sio wawakilishi)
4: Nafasi nyingine zipunguzwe ili kupunguza matumizi ya hizo kodi mf. Wabunge wa viti maalumu n.k n.k
(Kuna lundo la vyeo ambavyo havina hata cha maana zaidi ya kutafuna tu kodi)
Na na vieite umeyasahau yote yakizingatiwa kama nchi tutapaa
 
Jamaa wanaupiga mwingi!wanacheza kama Brazil ya enzi zile! Huku mama, pale Mwigulu, pembeni Ndugai!! Naona mama atakuwa anachekea tumboni!! huku akisema litazameni hilo!!! Wenye akili zao wameshajua kinachoendelea! Wanaosubiri mtu atumbuliwe watasubiri sana!! Mpira ukirudi kwa mama anaupoza kidogo watu wapumue kidogo kisha anatoa pande na mashambjlizi yanaendelea!! Burundi kutatuhusu tu, tutake tusitake!!
 
Mheshimiwa Job Ndugai amewataka watanzania kutoa mbadala ili tujenge nchi. Ukweli japo sisi watanzania tunazo kwikwi juu ya ulipaji Kodi ukilinganisha na nchi zingine . Binafsi sitoi mbadala Ila nitoe marekebisho njia Bora kwetu sote kama watanzania kuenenda Sawa. Kwa Kodi hii ya kizarendo naomba Kwanza viwango vishuke kidogo ili watanzania japo tujipe uzoefu Ila ili kuziba pengo tuweke tozo kwenye mishahara ya wabunge mawaziri na Raisi Kwa kuwa ni kundi linaloongoza japo kuwa vizuri kuliko makundi mengine ya watanzania. Nadhani kama viongozi tutakuwa tumeonyesha njia badala ya kuwa nyampara na tutawaelewa zaidi.
Ni uzwazwa kutaka kujenga nchi kwa kutukamua wananchi wakati nchi ina resources nyingi kuliko nchi zilizotuzunguka. Tuna dhahabu, almasi, chuma, ruby, tanzanite, gas asilia, bahari, bandari, makaa ya mawe, mlima kilimanjaro, ngorongoro crater, serengeti, manyara, tarangire, na vivutio vingi sana.

Lakini serikali inataka kutuambia kuwa imeshindwa kumobilize matumizi ya hizi resources wakati kuna nchi wana madini aina moja tu lakini yamejenga barabara za uhakika, watoto wanasoma bure, huduma za afya bora kabisa. Hivi tumerogwa au?
 
Hii post ni maneno ya ndugai au ni wewe ndo umetoa mtazamo wako mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuatilia Jana Ndugai alipaza sauti kuwa hizo tozo za miamala zimepita bungeni ili nchi ipae by 2025 so akatuimba watanzania tutoe mbadala ili tupate ahueni kwenye hiyo miamala so huo ndo mbadala wangu na naomba umfikie
 
Ana haki ya kuunga mkono wananchi kukamuliwa kwa sababu kupitia ukamuaji huo amewahi KUKODI HOSPITALI NZIMA KULE INDIA kwa miezi kadhaa
 
Anaandika Diwani wa Kata ya Kongolo- Magu na Mwanafalsafa Herbert Faustine
_________________________

NDUGAI JIFUNZE KUKUNJA MIGUU SHUKA INAPOKUWA FUPI.

Hatuwezi kuwa taifa la kukejeliana, kudharauliana au kufanyiana kebehi. Hatuwezi. Na wala misingi ya taifa hili haina jiwe la aina hiyo. Tunaruhusu kutofautiana kipato kama ambavyo Ndugai ana kipato kikubwa lakini haturuhusu utu wetu nao uwe na daraja la I, II, III.

Ndugai amesema manung'uniko juu ya tozo ya miamala yanatokana na sheria ya bajeti iliyopitishwa kwahiyo hata wanune sheria hii lazima itekelezwe. Kwa akili ya haraka haraka Ndugai anasema sheria za Bunge lake ni irrevocable. Hata Mheshimiwa Rais aliyesema tozo hizi ziangaliwe upya ni sehemu ya wanaonuna Ndugai kasema lazima sheria itekelezwe.

Maoni ya Watanzania sasa yanajibiwa kwa mipasho. Manung'uniko ya Watanzania sasa yanajibiwa na dhihaka. Kwanini tumefika hapa? Kila kukicha idadi ya walevi taifa hili inaongezeka.

Afadhali ya walevi kundi la kwanza wanaolewa bia, hao ni sehemu ya wajenga nchi. Ulevi wa kundi hili hauna athari ya kuligawanya taifa. Kundi la pili la ulevi ni hili la watu kuona nafasi zao ni immortal na wao wenyewe kujiona infallible. Ni hatari sana.

Yaani badala ya kusema bunge tumesikia kilio cha Watanzania, majibu unaambiwa hata unune tozo lazima. Hapa tunasumbuka na watu ambao hawajui hata menu ya M-pesa, Tigo-pesa wala Airtel-money.

Kanuni ya matumizi ya shuka wakati wa baridi inasema kama shuka ni fupi kunja miguu. Hizi kelele za wananchi na makampuni ya simu dhidi ya tozo ni ishara kwamba shuka ni fupi na Ndugai na bunge lake wanatakiwa wakunje miguu. Ajabu Ndugai ananyoosha miguu.

Ukimtazama Ndugai kama Spika kwenye kauli ile kuna vitu unaweza kukosea. Kwanini? Utamtazama kama Spika. Usifanye hivyo. Mtazame kama mwakilishi wa jimbo la Kongwa. Hili la tozo ni uwakilishi wa mawazo wa wananchi wa Kongwa.

He might be not the best Speaker we wanted, however, he is the only speaker we have.
HUYO NDIE NDUGAI.. MWENYE FILE MIREMBE...
 
IMG-20210719-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom