Spika Ndugai: Asiyetaka tozo ya kizalendo atupe njia mbadala ya kupata fedha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,923
141,889
Spika Ndugai amesema wabunge wameshapitisha tozo ya kizalendo kwenye miamala ya simu na sasa ni sheria hivyo asiyeitaka atupe njia mbadala ya kutufikisha 2025

Roho wa Bwana akamshukia mtumishi wake Jerry Slaa mbunge wa Ukonga naye akajibu; Wabunge tuanze kulipa kodi.

Labda kama Spika ana swali lingine....lakini sidhani.

Ijumaa kareem?

---
Baada ya mijadala mingi kuhusiana na tozo ya miamala ya simu hususani kwenye mitandao ya kijamii ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameibuka na kudai kuwa tozo hizo ni halali na kwamba fedha hizo zitachagiza masuala ya maendeleo ikiwemo huduma za kijamii kama vile shule,hospitali na maji.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu huku akipigilia msumari kwenye tozo hizo kwa kudai kuwa Bunge ndio limepitisha na kwamba wanaopinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike huku akisisitiza lengo ni ifikapo 2025 Tanzania iwe Taifa tofauti katika suala la Maendeleo.

Akizungumza mapema leo Julai 23,2021,katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,Spika Ndugai amesema "Sisi kama Bunge tulikaa kwa pamoja na kujadiliana kisha tukaamua kuwa na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi,"amesema na kuongeza;

"Tumepitisha na tukatunga sheria , tunataka kuliona hilo,sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofaut,CCM hoyee,nimemaliza,"amesema Spika huyo.

Chanzo: Malunde
 
Huyu Pimbi mfupi mi msumbufu sana Gibril hayupo mbali na kiviiile
Tatizo nyie mnawaza watu wafe tu hivi nyie mna mkataba na mungu?

Na nyie kwa roho zenu za kinyama na kigaidi kwa nini msife?

Kutofautiana kimawazo ni kutafuta njia mbadala na sio kuwazia watu wafe.

Nyie mna faida gani kwenye hili taifa?

Tuonyeshe ni mtu gani wa upinzani anaeongoza kuchangia kodi kubwa hapa tanzania?

Bosi wenu mbowe mwenyewe ni mkwepa kodi

Kodi ta miamala hakuna anayeipenda na kila mtu ametoa maoni yake kwa ustarabu na jambo liatashughulukiwa na tuataka wafanye haraka na sio kuchelewa na ikiwezekana wazuie huu utaratibu kuanzia sasa.

Lakini sio kuombeana vifo

Kuombeana vifo ni uzwazwa na ugaidi.
 
Tatizo nyie manawaza watu wafe tu hivi nyie mna mkataba na mungu?
Na nyie kwa roho zenu za kinyama na kigaidi kwa nini msife?
Kutofautiana kimawazo ni kutafuta njia mbadala na sio kuwazia watu wafe.
Nyie mna faida gani kwenye hili taifa?

Tuonyeshe ni mtu gani wa upinzani anaeongoza kuchangia kodi kubwa hapa tanzania?

Bosi wenu mbowe mwenyewe ni mkwepa kodi,
Kodi ta miamala hakuna anayeipenda na kila mtu ametoa maoni yake kwa ustarabu na jambo liatashughulukiwa na tuataka wafanye haraka na sio kuchelewa na ikiwezekana wazuie huu utaratibu kuanzia sasa.

Lakini sio kuombeana vifo,
Kuombeana vifo ni uzwazwa na ugaidi.
Bora kufa kuliko kuishi kama digidigi.
 
Mkuu afadhali umekemea huu upumbavu. Umejaa sana humu jukwaani haswa baada ya kifo cha JPM. Wanavyoombea watu wafe utadhani wao kwa sasa wanaishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja.

Ni aina fulani ya mawazo ambayo ni ya kipuuzi sana.
 
Nchi imeshaharibika. Kitendo cha kuruhusu biashara ya mkononi na kwenye meza ndo kifo cha kodi Tz. Nchi zilizoendelea hata karanga zinafungwa kwenye mfuko na kuwekwa barcode. ushuru unakuwa mdogo kiasi kwamba mfanyabiashara haumii lakini kila mfanya biashara analipa kodi. Sasa uongozi wetu umeona fahari kuruhusu biashara ziendeshwe kwa mtindo wa kuagiza mzigo wa kichina na kuwakabidhi machinga, sahau mapato ya serikali. Vijana badala ya kutumika kufanya kazi za uzalishaji wanafanya kazi ya kusaidia kuchepusha kodi na serikali imebariki.
 
Huyu Pimbi mfupi mi msumbufu sana Gibril hayupo mbali na kiviiile

1627048364763.png
1627048412950.png
 
Back
Top Bottom