Soko la Karume lateketea kwa moto usiku

Soko la Karume lateketea kwa moto usiku

Pole kwa waathirika wote! Ila laiti wangekuwa wamesikia na kutekeleza kuwa walitakiwa wahame na kwenda maeneo waliyotengenezewa yasingewakuta haya. Pale hapajaandaliwa kibiashara, hivyo kama kuna janga lolote latokea pale kutokana na miundo mbinu yake, hasara itegemewe. Hamna maeneo ya kupita vizuri, vyoo, vibanda vya mbao (vinashika moto kiurahisi) na mengine mengi. Hivyo nawapa pole wote walioathirika kwa njia moja au nyingine (nami nikiwepo maana nanunuaga vitu hapo), ila ni muda muafaka nao wamachinga waache UBISHI. Waende machinga complex. Watu watapazoea tu. Mbona zamani stendi wa mabasi ya mkoa wakati yaamishwa toka Kisutu kwenda Ubungo tulilalamika sana ila sasa tumezoea? Waende pale, TUTAZOEA tu, na kama likitokea janga pale, kutakuwa na wa kumlaumu.

Best Comment!
 
Wamachinga itakuwa imewakata pakubwa! Bima zenyewe hawana! Hapo lazima warudie misoto maeneo wawaachie mabwanyenye.
 
umejibu kipengele kimoja bidada,,,,twende cha uhamishaj wa masoko

Uhamishaji wa masoko una uhusiano upi na moto? Serikali inapotaka kuhamisha soko hailichomi moto. Inawapa ilani ya kuondoka kama hamjaondoka inawaondoa, mfano wake ni kama huo niliokupa hapo wa nyumba yako wakihitaji eneo.

Kumbuka Tanzania hakuna anaemiliki Ardhi mpaka sasa, ni Serikali na sisi ni wapangaji wa Serikali tu.
 
Nawapa pole sana vijana ambao mtapoteza mitaji na mali na hata hasara lukuki kutokana na hili tukio,ILA NAWAPA POLENI KUBWA ZAIDI KWA KUENDELEA KUICHAGUA NA KUIAMINI CCM, ENDELEENI NA MOYOYO HUO HUO, MPAKA SIKU MTAKAPOAMBULIA MABUA NDO MTATIA ADABU.
 
Kwa kweli tunarudishana nyuma, kwa hiyo kitengo cha polisi wa kuzima moto wanafanya kazi gani?!
 
Uhamishaji wa masoko una uhusiano upi na moto? Serikali inapotaka kuhamisha soko hailichomi moto. Inawapa ilani ya kuondoka kama hamjaondoka inawaondoa, mfano wake ni kama huo niliokupa hapo wa nyumba yako wakihitaji eneo.

Kumbuka Tanzania hakuna anaemiliki Ardhi mpaka sasa, ni Serikali na sisi ni wapangaji wa Serikali tu.

So kama sisi ni wapangaji wa serikali, serikali ni nani!!!!!????
 
Hakuna boksi hapo wala pakacha, janga la moto limetokea hata haujazimika mnakuja na siasa majitaka, yaani hata waliounguliwa kwenu ni chambo cha siasa majitaka, hamna hata ubinaadam kiduchu?

Kuna punguani mwingine, sijui ilikuwa wewe? hata mvua zilizotokea akazihusisha na CCM, eti kwanini hawakuzizuwia mapema. Huko ndio kufikiri nje ya boksi?

'Blaming nature can, of course, be very consoling and comforting. It can be of great use especially to those in positions of power and responsibility. Comfortable inaction is, however, typically purchased at a very heavy price - a price that is paid by others, often with their lives. (Dreze and Sen, Hunger and Public Action 1989, 47)'

'No one person suffers a lack of shelter without a social failure to organize shelter in such a way that it is accessible to each and every person. And no one person suffers unemployment without a system or political economy that fails to safeguard against that possibility. (Judith Butler, For and Against Precarity, 2011).'

Notice that vulnerability resides in the pre-hazard precarity of people. Vulnerability is,by definition, the social precarity found on the ground when hazards arrive. It does not fall from the sky. While there is no disaster without hazard, without vulnerability, hazard is nil (Blaikie et al 1994; Ribot, 2014).

Also, Margaret Lock observed that efforts to reduce suffering have habitually focused on control and repair of individual bodies. The social origins of suffering and distress, including poverty and discrimination, even if fleetingly recognized, are set aside.Politicians and those in power tend to ignore social causes of precarity, which is their own making.

Wakati mvua zimenyesha na kuvunja barabara, kuharibu miundo mbinu, Rais alituambia hiyo ni kazi ya Mungu. Serikali siyo iliyoleta mvua, hivyo haina cha kufanya na isilaumiwe. Wewe pia unaonekana kuwa na mtazamo huo. Kwa janga hili la moto pia mnataka kumsingizia Mungu. Lakini tafiti zinatufundisha vinginevyo.You are as usual trying to ignore the social causes of precarity. Si tatizo lako wala Rais. You both lack the requisite knowledge. Try and study vulnerability writings. These writings are normally dense but with some help, you should be able to pick up some concepts.
 
Poleni sana wahusika,,hapo kuna watu wamerudishwa nyuma sana kimaendeleo
 
Baada ya kufanikiwa kuwaondoa wamachinga pale Mwenge kwa kutumia mbinu mpya, kali na ya kisasa kabisa.., naona mmefanikiwa tena kuwaondoa pale Karume.., tena kwa kutumia mbinu iliyoboreshwa na ya uhakika zaidi kuliko hata ile iliyotumika pale Mwenge. Hivi ndivyo serikali inabidi iwe.., mnatakiwe muendelee kuwa wabunifu zaidi especially kwa ile kero ya muda mrefu kabisa pale ubungo ambapo sasa pamekuwa kama gulio la kule Igunga considering lile ni lango la jiji. Kuweni wabunifu zaidi ili tuone mafanikio pale ubungo.., safi sana!

Aiseee! Kama ni kweli, basi wewe na serikali hii nyote mna roho mbayaaa!
 
wonders shall never end, cdhani kama serikali can do that

Wewe Mategenani kakudanganya, waulize waliowahi kung'olewa makucha na meno bila ganzi watakueleza. Chezea $ wewe.
 
Last edited by a moderator:
'Blaming nature can, of course, be very consoling and comforting. It can be of great use especially to those in positions of power and responsibility. Comfortable inaction is, however, typically purchased at a very heavy price - a price that is paid by others, often with their lives. (Dreze and Sen, Hunger and Public Action 1989, 47)'

'No one person suffers a lack of shelter without a social failure to organize shelter in such a way that it is accessible to each and every person. And no one person suffers unemployment without a system or political economy that fails to safeguard against that possibility. (Judith Butler, For and Against Precarity, 2011).'

Notice that vulnerability resides in the pre-hazard precarity of people. Vulnerability is,by definition, the social precarity found on the ground when hazards arrive. It does not fall from the sky. While there is no disaster without hazard, without vulnerability, hazard is nil (Blaikie et al 1994; Ribot, 2014).

Also, Margaret Lock observed that efforts to reduce suffering have habitually focused on control and repair of individual bodies. The social origins of suffering and distress, including poverty and discrimination, even if fleetingly recognized, are set aside.Politicians and those in power tend to ignore social causes of precarity, which is their own making.

Wakati mvua zimenyesha na kuvunja barabara, kuharibu miundo mbinu, Rais alituambia hiyo ni kazi ya Mungu. Serikali siyo iliyoleta mvua, hivyo haina cha kufanya na isilaumiwe. Wewe pia unaonekana kuwa na mtazamo huo. Kwa janga hili la moto pia mnataka kumsingizia Mungu. Lakini tafiti zinatufundisha vinginevyo.You are as usual trying to ignore the social causes of precarity. Si tatizo lako wala Rais. You both lack the requisite knowledge. Try and study vulnerability writings. These writings are normally dense but with some help, you should be able to pick up some concepts.

Wadanganye ambao hawajasoma. Nimeanza chuo wakati wewe hata chekechea ulikuwa hujui kama ipo aka ulikuwa haujazaliwa.

Hapo inaongelewa "lack" of shelter. Hakiongelewi majanga ya moto. Au huelewi maana ya "lack of shelter"? Punguani wahed.
 
Mtu akisoma comments za huu uzi kuanzia mwanzo atagundua kuwa ni wazi watu ni wataalamu wa kutengeneza uongo usio na msingi kabisa na kila jambo wana ligeuza ni mtaji wa kisiasa.

Yani mtu anasema wazi kuwa serikali ndio imechoma mali za wamachinga hili waondoke pale lakini anashindwa kujiuliza kwanini wamachinga wa makoroboi-Mwanza hawakuchomewa hili waondoke?
Ni serikali gani yenye akili za kijinga namna hii kama wengi mnavyo jaribu kutuaminisha?

Hakuna serikali inayoweza kutumia njia hii wakati inajua fika mzigo wa ajira utarudi kwake, hivi kama ni swala la kuhama wangeshindwa kuwatoa kama walivyo watoa wengine hapa Dar na Mwanza?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hivi kwani serikali ingewapa siku mbili za kuondoka pale wangeweza kukataa kama serikali haiwataki pale kwa kipindi hiki?

Kila mtu anajua fika hawa wamachinga ingefika kipindi wangeondoka pale lakini serikali haiwezi kuchoma mabanda yao hata siku moja.

Sasa nimenza kufikiri upya kuna uwezekano watu hapa wasio hitakia mema serikali wakachoma ili kuibebesha lawama halafu kwao ni mtaji wa kisiasa na hili tukio limekuja baada ya kuondolewa wamachinga Makoboi mwanza.

Inasikitisha sana watu wamepoteza mali zao lakini kusema serikali ndio wamehusika
ni ujinga wa hali ya juu:

Tunajua kupitia hili tukio wale wataalam wa siasa za matukio watapata pa kutoea lakini inabidi tujiulize kwanini kusiwepo na uwezekano wa jambo hili kutekelezwa na watu baki wakijua lawama zitakwenda kwa serikali na kwao ni mtaji?.
 
So kama sisi ni wapangaji wa serikali, serikali ni nani!!!!!????

Sasa inabidi ufunguwe nyuzi nikupe darsa la "serikali ni nini", hapa panaongelewa janga la moto lililotokea Karume. Haya funguwa nyuzi, ntakuja.
 
mnaniboaaaaaaa mnavyoingiza serikaliiiii aasshhhh hivi lini mtaanza kusolv matatizo bila kusingizia serikali na chama tawala?????????

vibanda vya pale ni mbao???nguo zimerundikna kuns majereta yamefungiwa mle ndani moto ukianza pale ni vigum kuudhibiti WAMACHINGA WENYEWE WANAKIRI HIVYO
sehem yoyote moto kuzuka ni rahisi ndo maana tunapaswa kuwa na vifaa vya zima moto ndani sasa issue inakua kuudhibiti

kwa jographia ya pale moto ulianzia kule mwisho
HIVI GARI LINGEPITAJE????

SERIKALI SI WANGESE KUWAJENGEA MACHINGA COMLEXX

HIVI LINI TUTA SAPOTI WAKIFANYACHO SERIKali???????nilawama tu aaasrrrrrr

JIJI LAZIMA LIWE NA STRUCTURE INAYOELEWEKA

LAKINI SERIKALI INA UWEZO WA KUTUMIAMBINU NYINGI LAKINI SIO KUCHOMA MOTO MALI ZA WALALA HOI

mwisho siasa za ki kkk namna hii zinanifanya niamini serikali ya chama tawala

upinzani tuache kuaminisha jamii uongoo
kama una evidrnce nenda mahakamani
 
Haya hamieni machinga complex alaaa!!! Mnaleta za kuleta hapa ..... Hamia complex hamtaki.... Hamia hamtaki... Ah poleni sana ndo nchi yetu hii!!
 
Wadanganye ambao hawajasoma. Nimeanza chuo wakati wewe hata chekechea ulikuwa hujui kama ipo aka ulikuwa haujazaliwa.

Hapo inaongelewa "lack" of shelter. Hakiongelewi majanga ya moto. Au huelewi maana ya "lack of shelter"? Punguani wahed.

Lord have mercy. Nimekuonya kuwa tulizana usome na kuelewa. Vulnerability writings are dense. Lakini, unakimbilia kujibu matusi. This is not helping. Punguza emotions. Usipende kutoa uninformed opinions. Huna sababu za kufanya hivyo. And this is not Chadema vs CCM. This is an effort to expose you to a new body of knowledge. Clearly, you do not understand vulnerability as a concept. You cannot even define hazard, let alone disaster. Eti hapo inaongelewa lack of shelter, hakiongelewi majanga ya moto. Seriously? Yaani hata post yangu hukusoma, lakini umeijibu. Why are you doing this? Hili sasa ni ombi. Tafadhali jipe muda wa kusoma na kuelewa jambo kabla ya kujibu ili kustawisha mijadala hapa JF. Zaidi, ili uweze kujifunza. Na kama jambo hulifahamu, huna haja ya kujifanya unalifahamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom