Soko la Karume lateketea kwa moto usiku

Soko la Karume lateketea kwa moto usiku

Habari wana jf,soko la uhuru maarufu kama mchikichini au karume limelipotiwa kuungua kwa moto ambao ulizuka ghafla,mashuhuda wa tukio hilo wamesema huenda moto huo umesababishwa na shock ya umeme...kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia vyombo vya habari.

Hapo ndio unaona umuhimu wa bima ya moto ,sasa na hiyo mikopo sijui watu watalipaje,halafu ingine nchi nyingine ingechunguzwa chanzo cha moto na kama ni kutokana na tatizo la umeme ,kampuni ya umeme ingelipa lakini kwa hapa hiyo ni ndoto
 
Me nawapa pole wale wote walioathirika na moto huo pamoja na ndugu zao.

NAIOMBA SERIKALI IWAPE KUFUTA JASHO AU KIANZIO CHA MTAJI WA ANGALAU MILLION 5 KILA MFANYABIASHARA WA SOKO HILO ILI KUPUNGUZA MACHUNGU. WANAWEZA KUFANYA HIVYO KUPITIA VYAMA VYAO AU KWA NAMNA ITAKAVYOFAA. HILI NI JANGA LA KITAIFA KAMA YALIVYO MAJANGA YA MAFURIKO, TETEMEKO NA KADHALIKA. TUWE NA HURUMA KWA WATANZANIA WENZETU WALIOHARIBIKIWA NA TUACHE MALUMBANO YA KISIASA.

Ni ushauri tu. Na kama mimi ningekuwa president ningefanya hivyo.
 
Si ndio hao waliokuwa wamepanda nyuma ya Pikipiki siku ya muungano wakiishangilia chichiem au nakisea?.
 
Kwa kushabikia siasa tuu tunaweza sidhani kama nchi za jirani zinaujinga kama huu!poor Tz
 
Hata hivyo, vijana tuache kufanyia biashara zetu popote kiholela kwa kutumia visingizio rahisi, huu ni muda wa kufanya biashara na kazi zetu kitaalam sasa huku tukiwa na full vibali na bima za mioto na majanga mengine. Tuache uchama, udini, ukanda na uzawa. Haya ni maisha yetu, biashara kwenye njia za kupita kwa miguu hadi lini?
 
Kuna mambo ua kufikitri hapa ,soko la makoroboi linavamiwa usiku na mali za watu zinavunjwa usiku,wenye mali wanazuiwa kuchukua kitu chochote,wakati huohuo soko la machinga launfuzwa moti! Ukiunganisha doti serikali imehusika.Ni miaka mingi tjnambiwa zitajengwa machinga complex ambazi si rahisi kuwafanya wote wapate chumba na gharama za mtaji.
Mwaka 1972 Mwl nyerere alianzisha vijiji vya ujamaa vikiwa na lengo moja tu,kuwafikishia wananchi huduma bora ikiwemo maji ,shule,barabara ,siko nk.ni takribani miaka 42 sasa serikali hii sikivu bado inatafuta maeneo ya kuwapatia watu huduma bora!
Kutokana na sera mbovu za ccm zimewalazimisha watu kuhamia mjini jwa kuwa tu,vijiji hivi vya ujamaa vilitelekezwa na viongozi kuelekeza nguvu zai mijini,tulitaraji upatikanaji wa soko,barabara za lami,hospitali bora na wataalamu,shule nzuri zenye mahitaji muhimu ya kitaaluma kama vitabu,maabara,walimu,viwanja vya mipira bora na vitabu,
Viwanda pia vingejengwa kila mkoa ili vijana wamalizapo elimu zao kusingekuwa na haja za kukimbilia mkoa mwingine ,wangelima na kuuza hukohuko.
Hivi sasa majiji yanakua kwa sababu moja kubwa ,wananchi wa vijijini wametelekezwa, hakuna umeme,barabara mbovu ,mazao yao wakilima hawawezi kuyafikisha sokoni,hospitali hazina dawa,wala wataalamu,wanalazimika kuhamia mijini ambapo hata nyumba ya kupanga tu nayo mbovu na haina umeme,choo kizuri( squarter). Serikali hii kuonesha isivyowajali wananchi imelazimika tena mwaka huu kutenga bajeti kubwa ili kuboresha majiji.Mwl aliwahi kusema kwenye kitabu chake cha ujamaa na kujitegemea" maendeleo ya majumba,mabarabara,na magari mijini si maendeleo halisi,bali ni ya wachache sana" ccm inajinasibu kuwa ukiona magari,ghorofa nyingi ndio tumepiga hatua,umilikaji simu,madisco makubwa ndio maendeleo!!
Ccm haipimi maendeleo ya watu wake kwa kipato cha mwananchi mmoja mmoja,na lishe yake.tunasikia maiaha ya watu yametajwa na rais kuwa yameongezeka kwa 10% wakati watu wanakufa kwa magonjwa yanayozuilika,ukiwauliza madaktari wanasema,tatizo vifaa hawana!!
Kwa hali hii,nyie ccm bomu hili la machinga mmelitengeneza ninyi kwa sera mbovu,na kamwe suluhu haipatikani kwa mabavu,tunahitaji sera mbadala si za ahadi za machinga complex zilizoshinwa!!!
 
Habari ndugu zangu wa jf napenda kuchukua nafasi hii kuuliza kuwa hivi kuungua kwa soko kuu la karume ji ni mpango uliwekwa na serikali ili kuwaondoa wamachinga ambao walitakiwa kuondoka katika eneo hilo au kweli ni moto tu ulitokea kwa bahati mbaya maana bado sipati picha ya kwamba ule moto uliwaka tu pasipo kuwa na chanzo na mpaka sasa chanzo hakijajulikana pia kama si mpango wa serikali je kwanini kikosi cha zima moto kilifika na kuondoka katika eneo la tukio ilihali walifika mapema kwa sababu kwanza kulikuwa hakuna foleni maana moto uliwaka usiku pia kutoka fire mpaka karume sio mbali?? Ni hayo tu wakuu
 
Hekaya hii inanikumbusha MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Machinga waliokopa wanalia na kusaga meno.
 
Ukitaka kujua kuwa huwezi kuwaamisha wafanya biashara kiurahisi isipo kuwa kwa moto nenda kawaulize soko la songea,mwanjelwa mbeya. Hapo ndio utapata jibu ,na baada ya hapo soko limekiwaje?ni hayo tu.
 
Kaisaidie polisi sasa maana hata Mbowe alisema anamjua mlipua Bomu ila mpaka sasa hatoi ushirikiano
 
Serikali ipi mkuu maana kuna halmashauri ya jiji, manispaa na serikali kuu? kwa nini serikali ichome moto kwa nini wasivunje km walivyovunja kariakoo na kwingineko .serikal hapo haihusiki bali inawezakana ikawa hujuma ya mtu kwa mtu ndani ya soko na matokeo yake ikaathiri soko zima
 
wala msipate taabu serikari haiwezi kufanya hujuma ila masoko mengi hapa nchini yanaweza kuungua sababu miundo mbinu za umeme ndani ya masoko ni hovyo kabisa waya zinasambazwa kama waya za spika na tanesco wanajua
 
Hekaya hii inanikumbusha MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Machinga waliokopa wanalia na kusaga meno.

Ni kweli dalali lama ila sasa kwanza me nataka kujua chanzo kwanza cha moto vp mkuu umepata taarifa yoyote
 
wala msipate taabu serikari haiwezi kufanya hujuma ila masoko mengi hapa nchini yanaweza kuungua sababu miundo mbinu za umeme ndani ya masoko ni hovyo kabisa waya zinasambazwa kama waya za spika na tanesco wanajua

Hahahaha kweli kaka iyo inaweza kuwa ni tatizo
 
Serikali ipi mkuu maana kuna halmashauri ya jiji, manispaa na serikali kuu? kwa nini serikali ichome moto kwa nini wasivunje km walivyovunja kariakoo na kwingineko .serikal hapo haihusiki bali inawezakana ikawa hujuma ya mtu kwa mtu ndani ya soko na matokeo yake ikaathiri soko zima

Mkuu nikisema serikali nina maana ya kuanzia ngazi ya manispaa mpaka serikali kuu
 
Utasikia baadaye jiji linajenga soko la kisasa kama Mwanjerwa. Hivi Haiwezekani kawaondoa bila kuchoma moto?! Masoko yote kila baada ya kuungua either wafanyabiashara hawaruhusiwi tena mahali hapo au ujenzi mpya wa soko hufanyika. Poleni wamachinga, mwakani chagua mabadiliko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom