Hivi umekuja lini mjini? Nakushangaa unaposema Machinga Complex haikujengwa kwa ajili ya wauza mitumba.
Kwa taarifa yako na ukoo wako wote, Machinga Complex ilijengwa kwa ajili ya wauza mitumba ambao awali walitimuliwa mtaa wa Congo na kuamuliwa wakae kwa muda pale kwenye soko la Karume.
Uamuzi wa kupewa soko la muda ulikuja baada ya vurugu kubwa kutokea kati ya Wamachinga wa Congo na mgambo wa jiji na kupelekea mgambo watatu kuuawa na mtaa Huo kutopitika kwa saa 24.
Kwa kukusaidia zaidi, pale ambako soko la Karume lilipo, palikuwa na bustani ya maua na miti ya vivuli kwa ajili ya mapumziko kama ilivyo Mnazi Mmoja au Magomeni hospitali, hivyo ikaamuliwa na jiji kubadilishwa matumizi yake kwa muda ili Wamachinga wa Mtaa wa Congo wafanyie biashara hadi soko lao litakapojengwa.
Wakati Machinga Complex inajengwa ilichukua namba ya idadi ya wamiliki wa biashara walio kwenye soko la muda la Karume, lakini baada ya ujenzi kukamilika zikaanza sarakasi Za MaCCM.
Zungu na wenzake wakaanza kubadili mfumo wa ugawaji kwa sehemu iliyokuwa kwa ajili ya mfanyabiashara mmoja wakapanga wawekwe wanne kwa mtindo wa kama matundu ya wauza kuku, baada ya MaCCM kuchomeka majina yao katika list ya Wamachinga na kufanya idadi iongezeke.
Mwisho wa simu Wamachinga wakaligomea soko, ndo ikawa hivyo mpaka leo.
Ndio ilikuwa hivyo wewe bibi. Shika maneno ya Mtemvu aliposema usiizungumzie Dar es Salaam kama huijui, tuulize wenyeji.
Ova