Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 439
- 1,065
Moto mkubwa umetokea usiku wa kuamkia leo, Septemba 21, 2026 katika Soko la Machinga jijini Dodoma na kuteketeza vibanda pamoja na mali za wafanyabiashara, huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijajulikana.
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamesema walianza kuona moshi kabla ya moto kuzuka, ndipo walipoanza juhudi za kuokoa baadhi ya bidhaa zilizokuwa katika vibanda vyao.
Mmoja wa wafanyabiashara walioathirika amesema amepoteza takribani asilimia 95 ya mali zake kutokana na moto huo, huku akiomba Serikali kuwasaidia wafanyabiashara waliopata hasara.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma, Rehema Menda, amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, huku Jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama likiendelea na uchunguzi pamoja na hatua za kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama.
Aidha Menda amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuudhibiti moto huo kwa asilimia 99.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa katika tukio hilo.Senyamule amewataka wafanyabiashara kuondoka katika eneo hilo nyakati za usiku ili kutoa nafasi kwa vyombo vya usalama kuendelea na shughuli zao.