fiksiman
JF-Expert Member
- May 17, 2008
- 402
- 107
Hivi jamani huyo mengi msafi kweli mbona anajidai hivi? Kama kweli atueleze vita gani ya ufisadi anayopigana wakati yeye kasusa kutia mguu pale hotel ya kilimanjaro baada ya kunyimwa ulaji....mmh atueleze ni kweli utajiri alioupata umetokana na mtaji wa kuuza peni na karanga au baada ya kuwapua mabilioni ya walalahoi mwaka 1984 pale benki kuu maana kuna tetesi kuwa wao walihusika kuitia moto benki ile ili kupoteza ushahidi wa madeni yao na hata wale waliokuwa na vielelezo vya wadaiwa wote walipotezwa kimya kimya....mmh atueleze ni kweli alipompa katibu mkuu wa CCM mzee makamba pesa taslimu milioni 100 ili akasaidie uchaguzi huku ikijulikana fika ilikuwa hongo ya mzee huyo....atueleze madeni ya NBC anayodaiwa yamefikia wapi au ameshaipotezea kwa vigezo vya kisheria.....atueleze bwana huyo katika makampuni yake anayomiliki ameajiri watanzania wangapi maana asilimia 90 ya wafanyakazi wake ni vibarua na hata walioajiri wamepewa mikaba ya miaka miwili au mmoja...ajira nyingi zimeenda kwa wachaga na ndugu zake.....atueleze huyu bwana kisa cha kukimbilia kwenye vyombo vya habari kila anapoguswa huku akijua kuna vyombo vya kushughulikia masuala yake kwa mfano kama kweli yeye mwanachama halisi wa CCM na anakitakia mema iweje asitumie taratibu za chama chao kuwasilisha majibu yake kwa mama simba....atueleze alifanya vile kwa manufaa ya nani kama si kumtusi kisirisiri Rais wake na mwenyekiti wake wa chama kuwa viongozi wake aliowachagua hawafai na ni mafisadi.....huyo mzee ni nyoka kama si ndumilakuwili maana anagusika penye masilahi yake. Nasema anaatueleze bwana sio kuleta mbwembwe tuuu.