Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Mimi ninaona sasa nchi inakoelekea ni kubaya.

Hivi huyu Waziri tena mwenye jukumu kubwa hapa nchini la utawala bora mbona anaboronga na kupapukia mambo ambayo yakiletwa mbele ya hoja atashindwa kujibu? Hayo maswala kwamba harusi ya Malecela ni kibinafsi zaidi ni kama unayetaka kumvua mtu nguo? Na licha ya hivyo huyu mama toka awe mwenyekiti CCm kupitia tiketi ya kina mama ndiyo anagombana na kila mtu kwa kurushiana maneno?

Na hii na imetokana na kuchia mianya ya kumpa kila mtu uhuru wa kuongea mimi kwa mawazo yangu si lazima kila mtu aongee inabidi line of authority ichukue nafasi yake katika majukumu yanayoikabili na majibu ya hoja mbalimbali kwanini watu tunatafuta umaarufu usiyo na tija?
 
jamani naomba kuuliza maana kuuliza si ujinga

Hivi unapotaka kuanza New thread unakwenda vipi

1. Chagua jukwaa unalotaka mfano --- jukwaa la siasa.
2. Hapo juu kwenye upande wa kushoto kuna kitu kimeandikwa -- new thread
3. Kibonyeze na kitakuletea page ya kuanzisha new thread
 
Sophia Simba hafai kuwa Waziri wa Utawala Bora



pdidy.swi


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Mnyambi Simba, kwa mara nyingine tena amezua mjadala na kuamsha hisia za waliosinzia kuhusu utata wa utumishi wake ndani ya Serikali ya Awamu ya Nne chini ya mwamvuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ni mara nyingine kwa sababu huko nyuma amewahi pia kutoa kauli zenye ukakasi akimshambulia mfanyabiashara na mmoja wa wafadhili wa chama tawala kilichomweka waziri huyo madarakani.
Ni huyu huyu Sophia ambaye chama chake kimekanusha matamshi aliyotatoa mbele ya kadamnasi kuwashambulia wabunge wa kuchaguliwa walio mume na mke – John Malecela na Anne Kilango Malecela.
Ni huyu Sophia mwenye dhamana ndani ya wizara nyeti ya Utawala Bora, yenye wajibu wa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma, iliyo chini ya Ofisi ya Rais.
Ni Sophia ndiye anayewajibika katika kusimamia na kutekeleza kiapo chake cha utii na kumshauri vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa taifa, bila migogoro yoyote.
Ni huyu Sophia, ambaye ndani ya chama chake, amekabidhiwa dhamana ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) - wanaokiamini, kukipenda na kukitumikia chama tawala, yaani CCM.
Ni huyu Sophia aliyedaiwa kumwangushia kipigo, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Janeth Kahama, wakati wa mchakato na kampeni za kumtafuta mwenyekiti wa wanawake hao kwa njia ya kura.
Ni Sophia huyu huyu, aliyewahi kukaririwa na vyombo vya habari akiwatetea wafanyabiashara wakubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kuzua gumzo na kuharibu upepo wa nchi wakati huo.
Sophia Simba, kwangu ni mwanamama anayekurupuka. Ni Waziri asiyejipa muda wa kutafakari na kueleza anachokifahamu. Wakati mwingine nahisi anatumika ama kwa nia ovu au kwa maslahi ya taifa ili kuharibu mwelekeo ama kuwasahaulisha walalahoi kero zinazowakabili.
Ni Sophia, aliyejaribu kucheza ngoma tofauti ya vita dhidi ya ufisadi iliyoanzishwa na viongozi wa vyama vya upinzani kabla ya kupokelewa kwa shangwe wa wakuu wa chama chake, akiwemo rais aliyemteua kushika nafasi ya uwaziri.
Ni Sophia aliyewashangaza wasomi na wasio wasomi, pale alipojiinua na kuishambulia familia ya wanasiasa, akiwemo mkongwe, Mzee Malecela.
Ni huyu Waziri Sophia aliyewaacha vinywa wazi wachambuzi, wajuzi na wananchi wa kawaida pale alipowashambulia kwa tuhuma mbalimbali wanasiasa wenzake.
Ni wapi alipokuwa Sophia kiasi cha kuzikalia tuhuma nzito za wanasiasa hao na kujinasibu kwamba ndani ya chama chao cha CCM hakuna msafi, wote ni mafisadi?
Ni imani yangu kwamba Sophia anahitaji kubanwa ili aanike tuhuma zote anazozifahamu, pengine atalisaidia taifa na kulirejesha kwenye mstari ili walalahoi waone raha na faida ya kuzaliwa juu ya ardhi ya Tanzania.
Pamoja na yote, nina ushauri kwa mkuu wake wa kazi. Kwanza amfukuze kwa sababu amejidhihirisha kwamba hafai kuwa kiongozi wa wanyonge kwa sababu ameshindwa kusimamia mienendo ya watumishi wa umma. Sophia aanze kufuatiliwa, ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Polisi na Usalama wa Taifa. Ni Imani yangu kwamba kuondolewa kwa waziri huyu katika nafasi aliyonayo, kutabadili fikira zangu kwamba analipwa fadhila za mema machache aliyoyatenda wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005
 
Huyu ndie mkono wa kuume wa JK haguswi huyu....kwenye vikao vyao huyu mama ndio anatumika kuwalipua wale ambao wanaonekana ni fitna kwa mtandao!!ndio maana yupo pale ile ni posho yake ya kuwalipua .......wabaya wa JK na mtandao!hana cha zaidi......
 
Sophia simba awa kigezo kwa wa Tanzania wengi hasa wenye huruma na uchumi wa nchi yao ,amekuwa midomoni mwa wanachi wengi kwa ubora wa kusimamia kile anacho kiamini kuwa ni cha ukweli na ni faida kwa taifa.
 
Du nadhani umekosa cha kufanya ukaamua uanzishe mada hii uone reaction!!!!!!!! Pumba tupu
 
Ungekuwa na nyembe karibu, ungeshakuwa marehemu wewe?

jamaa ukifululiza kwenda naye kwenye game ya mpira kwa kama mwezi hivi akiwa shabiki wa timu, mwisho wa mwezi huchelewi kuta keshapungua size... atakuwa amekata vidole, mikono, miguu kwa hasira kwa kila game aliyofungwa goli!! lol
 
Mkuu Spear,
Kuna mtu unamtafuta na atakuja sasa hivi hapa...jiandae na maporomoko ya Same.
 
Sophia simba awa kigezo kwa wa Tanzania wengi hasa wenye huruma na uchumi wa nchi yao ,amekuwa midomoni mwa wanachi wengi kwa ubora wa kusimamia kile anacho kiamini kuwa ni cha ukweli na ni faida kwa taifa.
.
Angalizo, kuna mtu mahali alizungumzia huyu Spear ni nani. Wana JF tuongeze uvumilivu na ustahilivu hata kama post nyingine ni kichevuchefu sio lazima kuzitemea mate just funga macho, endelea na post nyingine zenye akili.

Asante spear kwa kutujuza jinsi Sophia Simba, anavyopanda chati. Naomba jibu maswali haya 11, kwa kuanzia ni chati ipi?, famanua japo kidogo kuhusu hao Watanzania gani? wenye huruma ipi?na uchumi gani? wa nchi yao ipi? wamemuweka vipi midomoni mwao? kwa ubora upi? wa kusimamia kipi? ambacho anachoamini vipi? kuwa ni cha ukweli upi? kwa faida ipi? ya taifa lipi?.
 
Sophia simba awa kigezo kwa wa Tanzania wengi hasa wenye huruma na uchumi wa nchi yao ,amekuwa midomoni mwa wanachi wengi kwa ubora wa kusimamia kile anacho kiamini kuwa ni cha ukweli na ni faida kwa taifa.


Umefanya hivi kumpotosha nani? Mbona watu wote humu tuna akili timamu?
 
Mbili, Selii alisema, "Sophia Simba amesema hapa kuwa Lowassa ni mwanamme namba moja. Ni mwanamme wa shoka. Akimaanisha kwamba wanaume wote akiwamo rais, waziri mkuu, wabunge na madiwani siyo kitu.

Mimi sikubaliani naye. Labda kama mwanamme wa shoka katika masuala mengine," alisema kwa kujiamini.
 
Selelii. Anasema, “aliyoyasema Sophia Simba hapa hayakustahili kutolewa katika kikao hiki. Haya ni maneno yanayopaswa kutolewa kwenye kitchen party. Nimemsikiliza kwa makini, mheshimiwa Simba amezungumza mambo binafsi yanayohusu mtu binafsi,” alisema.

Sophia simba awa kigezo kwa wa Tanzania wengi hasa wenye huruma na uchumi wa nchi yao ,amekuwa midomoni mwa wanachi wengi kwa ubora wa kusimamia kile anacho kiamini kuwa ni cha ukweli na ni faida kwa taifa.
 
Sophia simba awa kigezo kwa wa Tanzania wengi hasa wenye huruma na uchumi wa nchi yao ,amekuwa midomoni mwa wanachi wengi kwa ubora wa kusimamia kile anacho kiamini kuwa ni cha ukweli na ni faida kwa taifa.
.

Spear,
Angalia sana mkuu.
Muda si mrefu utajikuta huko kwenye mistari ya tarabu(mipasho).Huyo sophia simba, watu hawataki kumsikia.Kachoma Msumari kwenye kidonda cha familia husika.

Wenyefamilia wakali kweli kweli.

Ninachojiuliza, kwanini hii familia ya John Malecela wasikubali matokea, kama familia nyingine na kukaa kimya?.Kuna familia ya Mkapa,Familia ya Lowasa na Familia ya RA.Hawa wamekubali matokeo kuwa kweli kuna ufisadi na ndiyo maana wamekaa kimya.

kumsafisha mtu fisadi ni taabu sana.
 
Back
Top Bottom