Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

CCM ni chama kilichozaliwa baada ya TANU kuungana na AFRO SHIRAZ na wapo wanachama waanzilishi. Ukiangalia tarehe alizopatia Kadi Bw.mengi utagundua kuwa ni mwanzilishi wa Chama hicho. Kitu kisicho eleweka hapa ni kwa kuwa Viongozi wa sasa wa CCM ni Viongozi Maslahi. Kama hajamkatia chochote kKatibu huyo Kihiyo hatatambulika katu hata akitoa michango kiasi gani. Hivi sasa kuna CCM Asili, CCM Maslahi na CCM Mtakuja. Mengi yuko kwenye CCM Asili lakini huyo Bw. Kilunde ni Katibu wa CCM Maslahi au Mafisadi kwa hiyo hawako chama kimoja na hawezi kumtambua!!

Umemaliza hapo Mkuu...Hii ni nzuri sana kwa Kumbukumbu!
 
Mengi yupo CCM asili? unatania au upo serious? Yaani Mengi yupo CCM ya Warioba, Salim, Butiku, Mwakawago etc?

Hebu toa tafsiri ya CCM asili
 
Wakati malumbano mbalimbali yanaendelea kuhusu hoja alizotoa Mh Sophia Simba bado kuna mengi aliyoyasema ambayo bado hayako katika public forum.

Hizi ni habari za ndani zilizotujia.

Mh Sophia aliwaambia wabunge wa kamati maalumu inayoongozwa na Mzee Ruksa kuwa hii nchi inayumbishwa na watu wanne ambao ni Speaker Sitta, Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Rostam Aziz na Edward Lowassa. Alisema ni muhimu baada ya bunge kumalizika kamati ikawaita na kuwahoji na kuuliza wanaipeleka wapi nchi yetu.

Waziri Sophia alisema kwa namna zote watu hawa ni wahusika wakuu wa mambo yanavyokwenda sasa hivi kwa hiyo kamati hiyo inayoheshimika iwaite watoe ufafanuzi na waseme wanataka kuifikisha nchi wapi.

Sophia alisema kundi la kina Spika lenye wabunge wanaojinadi kuwa vinara wa kupinga ufisadi wakiongozwa na mpendwa wao mfanyabiashara Reginald Mengi wenyewe sio wasafi hata kidogo.
"Hakuna mtu msafi pale, sema tu serikali ina namna ya kushughulikia mambo yake," alisema.

Alitoa mfano wa mama Anna Kilango kuwa alishakutwa na madawa za kulevya nyumbani kwake kabla ya kuolewa na Mh Malecela. Pia, Jeetu Patel ambaye anasemekana kuwa ni fisadi papa, aliwachangia harusi yao fedha nyingi sana, zaidi ya sh millioni mia mbili hivyo haelewi nani ni fisadi kweli - aliyetoa au aliyepokea.

Alisema Malecela alishajipanga kuwa rais wa Tanzania na mkewe first lady, na kwa kuwa hayo hayakutokea, kelele za mama Kilango sasa hivi ni hasira hizo.

"Ninawaeleza ninyi haya yote ili mnapofuatilia haya mambo ni vizuri mkajua chimbuko lake ili kuweza kuyapatia utatuzi," Sophia aliiambia kamati.

Alimgeukia pia kinara wa wapambanaji Reginald Mengi kuwa magazeti yake yamekuwa yakiandika habari za kuichafua serikali na chama cha CCM.

Alihoji hela mfanyabiashara huyo anazotumia kuzunguka nazo nchi nzima eti vikoba zinatoka wapi? "Wanafikiri zinatoka mfukoni kwa Mengi, lahasha, pesa hizo zinatoka kwa mabalozi hivyo wajue wanashirikiana kuihujumu nchi."

Aliongeza: "Tunafahamu mambo mengi kukaa kimya hakumaanishi hatujui kitu tuna vyombo vya dola vipo makini vina taarifa zote lakini kama serikali, tuna namna ya kushughulikia mambo kwani hii nchi inaongozwa na utawala wa sheria hivyo lazma sheria ifuate mkondo wake."

Sophia alisema ukimfuatilia sana Mengi na utajiri wake utaona kuwa chimbuko lake ni hao hao wahindi anaowatuhumu kila kukicha huku akifikiri hatumjui kuwa yeye sio Mr. Clean hata kidogo.

Aliwaonya wabunge hao wajitenge na Mengi kwani anawapotosha kwa kiasi kikubwa.

Alisema ujinga wa Mengi unaonekana pale anapojitahidi kila kukicha kujifananisha na rais. Anachofanya rais, na yeye eti anafanya. Rais Mengi huyo ameteuliwa na nani? Sophia aliuliza.
 
Mengi yupo CCM asili? unatania au upo serious? Yaani Mengi yupo CCM ya Warioba, Salim, Butiku, Mwakawago etc?

Hebu toa tafsiri ya CCM asili

Mheshimiwa Zitto, nadhani huyu jamaa ameigawa CCM katika vipindi vitatu, ambapo hadi Mengi anajiunga miaka hiyo ya 1977, basi yeye anaita kundi hilo LA ASILIA!

Lakini, kwa habari ya ukomavu, ni wazi Mengi hawagusi hao uliowataja...

After all yeye ni Mfanyabiashara, anaingizwa kwenye siasa kwa nguvu na kwa pesa alizo nazo! -thats my take!
 
huyu mzee huwa mpuuzi sana,
mi huwa namshangaa sana,sijui huwa anatafuta nini?
 
Huyu mama namstahi tu yaani tabia anayoifanya haiendani na yeye mwenyewe alivyo. Lakini President amekosea sana kumchagua maana Huyu mama Historia yake alikuwa anagawa sana sasa iweje apewe Wizara Nyeti???? Tumekwisha yaaani anamshambulia mzee wa watu utafikiri yeye ni mpinzani. Huyu mama ni kibaraka wa Richmonduli. Asante nitalia kwa machuku ya huyu mama Aibu kwa Taifa si yeye
fanya uchunguzi uone kama hajamgawia hata Mzee na ndiyo maana akapata hiyo post!
 
Hizi ni habari za ndani zilizotujia.
Mh Sophia aliwaambia wabunge wa kamati maalumu inayoongozwa na Mzee Ruksa kuwa hii nchi inayumbishwa na watu wanne ambao ni Speaker Sitta, Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Rostam Aziz na Edward Lowassa. Alisema ni muhimu baada ya bunge kumalizika kamati ikawaita na kuwahoji na kuuliza wanaipeleka wapi nchi yetu.
Waziri Sophia alisema kwa namna zote watu hawa ni wahusika wakuu wa mambo yanavyokwenda sasa hivi kwa hiyo kamati hiyo inayoheshimika iwaite watoe ufafanuzi na waseme wanataka kuifikisha nchi wapi.
Sophia alisema kundi la kina Spika lenye wabunge wanaojinadi kuwa vinara wa kupinga ufisadi wakiongozwa na mpendwa wao mfanyabiashara Reginald Mengi wenyewe sio wasafi hata kidogo.
"kwa kiasi kikubwa.
Alisema ujinga wa Mengi unaonekana pale anapojitahidi kila kukicha kujifananisha na rais. Anachofanya rais, na yeye eti anafanya. Rais Mengi huyo ameteuliwa na nani? Sophia aliuliza.

Heeeeeeeeeeeeee!

Hujafa hujaumbika!...Kumbe huyu mama ana Mdomo hivi!..Kweli baraza la mawaziri bongo ni sawa na kundi la taaraabu!

Sasa maneno haya yako huku nje mitaani, na tuamue cha kufanya na hawa watu,... si wanatuongoza sisi?...

Si tumewapa madaraka kwa dhamana?..Tunawaogopa?
 
- I mean usafi aau uchafu wa viongozi wetu hauwezi kuamuliwa na maneno ya mitaani kama ya Sophia, utaamuliwa na facts na ushahidi lakini Oooh! Mwakalinga amepewa Shillingi Millioni 400 na Lowassa, basi hafai tena amepewa kweli ooh! kumbe wote wachafu, this is foolish na ndio maana ninakubali kwamba Sophia ni kichaaa sasa prove otherwise!

Mkuu FMES,

Sijui una maana gani hapo juu? Shauri ya box kunibana, sijafuatilia huu mjadala zaidi ya mchango niliotoa siku ile thread hii ilipoanza.

Kuendelee kuandika majina ya watu wengine ambao hawahusiki na mjadala huu sidhani kama inasaidia kwenye utetezi wako.

Kuna tofauti kubwa kati ya kinachojadiliwa kwenye thread hii na hayo uliyoyaandika ya Mwakalinga. Waziri Sophia ametamka wazi mbele ya vyombo vya habari na mbele ya viongozi wa chama chake, hivyo kama madai yake ni ya uwongo kuna njia nyingi ambazo wahusika wanaweza kuzifuata kuhakikisha majina yao hayachafuliwi.

Hilo la Mwakalinga, linasemwa na wasanii, ambao wanajificha kwenye migomba kabla ya kutamka neno. Kama wanaamini hivyo waseme wazi kama alivyosema Simba naamini huyo Mwakalinga kesho yake atakuwa anapambana nao mahakamani.

Ni muhimu kuweka wazi kwamba ukiachia madai wanayotoa kupitia JF, hakuna kiongozi hata mmoja anayeweza kusimama kwenye vyombo vya habari akasema Mwakalinga kapewa milioni 400 na Lowassa maana hata hao wanaopenyeza hayo maneno wanajua hayana chembe hata ya ukweli na hawako tayari kuona wanaburuzwa mahakamani.

Mwisho, Mwakalinga hana nia wala sababu ya kufadhiliwa na mtu yeyote. Kama ni ubunge basi atajifadhili mwenyewe.

Nafikiri kwenye maandishi yako hapo juu humtendei haki Mwakalinga kwa kuweka statement kama hiyo ambayo inaweza kuwafanya watu ambao hawajafuatilia jambo kama hilo waamini kuna madai kama hayo yametolewa kiwaziwazi.
 
Lunyungu ni msanii na achana naye. Bangi la Amsterdam limeharibu kichwa chake ndio maana anaona maweluwelu na kufikiria mara yuko Tarime, mara Dar, mara Moshi. Bangi lina tabia mbaya sana! Sasa hata kasahau kwamba alishakuwa CCM wakati ule yuko JKT.

Tuna msera mmoja hapa Kyela, akishakoreza bangi lake anaanza kusema ana project kubwa ya kutengeneza ndege ambayo itapaa mwakani. Sisi tunamwita profesa wa bangi!

Mkuu umefika mbali sana na hizi comments na sijajua ni kitu gani kime prompt hizo personality attacks.Bangi ? Msanii ? anyway. Mie huwa nashauri watu ku dwell kwenye hoja na mimi mara zote nikiwa sina cha kujibu huwa naacha kuandika kuliko kumvamia mtu kwa matusi . I am not happy na hizi comments
 
fanya uchunguzi uone kama hajamgawia hata Mzee na ndiyo maana akapata hiyo post!

Yak!!! Please lets stick to the game rules ma'an!!! Hayo ya undani tuyaache kwani si yetu

She has lost it, period!!
 
Mkuu FMES,

Sijui una maana gani hapo juu? Shauri ya box kunibana, sijafuatilia huu mjadala zaidi ya mchango niliotoa siku ile thread hii ilipoanza.

Kuendelee kuandika majina ya watu wengine ambao hawahusiki na mjadala huu sidhani kama inasaidia kwenye utetezi wako.

Kuna tofauti kubwa kati ya kinachojadiliwa kwenye thread hii na hayo uliyoyaandika ya Mwakalinga. Waziri Sophia ametamka wazi mbele ya vyombo vya habari na mbele ya viongozi wa chama chake, hivyo kama madai yake ni ya uwongo kuna njia nyingi ambazo wahusika wanaweza kuzifuata kuhakikisha majina yao hayachafuliwi.

Hilo la Mwakalinga, linasemwa na wasanii, ambao wanajificha kwenye migomba kabla ya kutamka neno. Kama wanaamini hivyo waseme wazi kama alivyosema Simba naamini huyo Mwakalinga kesho yake atakuwa anapambana nao mahakamani.

Ni muhimu kuweka wazi kwamba ukiachia madai wanayotoa kupitia JF, hakuna kiongozi hata mmoja anayeweza kusimama kwenye vyombo vya habari akasema Mwakalinga kapewa milioni 400 na Lowassa maana hata hao wanaopenyeza hayo maneno wanajua hayana chembe hata ya ukweli na hawako tayari kuona wanaburuzwa mahakamani.

Mwisho, Mwakalinga hana nia wala sababu ya kufadhiliwa na mtu yeyote. Kama ni ubunge basi atajifadhili mwenyewe.

Nafikiri kwenye maandishi yako hapo juu humtendei haki Mwakalinga kwa kuweka statement kama hiyo ambayo inaweza kuwafanya watu ambao hawajafuatilia jambo kama hilo waamini kuna madai kama hayo yametolewa kiwaziwazi.

Baho baho baho
 
Huyu mama namstahi tu yaani tabia anayoifanya haiendani na yeye mwenyewe alivyo. Lakini President amekosea sana kumchagua maana Huyu mama Historia yake alikuwa anagawa sana sasa iweje apewe Wizara Nyeti???? Tumekwisha yaaani anamshambulia mzee wa watu utafikiri yeye ni mpinzani. Huyu mama ni kibaraka wa Richmonduli. Asante nitalia kwa machuku ya huyu mama Aibu kwa Taifa si yeye

Unakokosea kwa kudhani wapinzani pekee ndiyo wanatakiwa kushambuliwa . Kesha sema na hayuko juu ya sheria waacha kutufanya wajinga wote wanajua kinacho ongelewa mmoja wao aende mahakamani aombe ufafanuzi maana hata wapinzani ni watanzania na hawahitaji kutukanwa na kudhihakiwa .
 
Hivi kweli unadhani JK anaweza kumwondoa SS? Kama ameshindwa kuwaondoa akina Chenge, Rostam kutoka katika nyadhifa zao CCM atawezajekumwondoa huyo Waziri?
 
FMash
mmi simtetei S.Simba kwa manenu aliyoongea kutokana na yeye ni waziri. Nasimtetei mwana ccm yoyote kwa sasa, me nipo kando na ctaki hata kumtetea mmoja wao, kwani megundua wote ni wachafu, tofauti na wewe unae watetea kina Malecela waziwazi. Nakumbuka ,maneno ya mwalim sanaaa kwa sasa alivyokua akimuita JOHN.
 
Kwanza mi sioni sababu ya Mzee Mengi kuhangaika kujieleza kwa umma juu ya uanachama wake, what for?

Kama ana kadi, na anailipia, hakuna sababu ya kujieleza kote huko!

Whether atakuwa mwanachama au la, i dont see any reason for anyone to make it a loud business!

Mbona mimi hakuna anaenifuatilia?...Wanataka wanachama au wachangiaji?

kwa sababu yeye ni fasadi nyangumi
 
Maneno hayo...waache waje wajisafishe...mwendawazimu keshapayukwa...wanasema penye ulevi pana ukweli.
 
utafikiri ni wamama wamekaa kibarazani wanasutana!? Kumbe ni viongozi wa nchi!! Duh! aibu .
 
Back
Top Bottom