Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Ukweli ni kwamba kwa sasa hii si aibu ya huyu mama any more! Ni aibu ya waliomtuma (i mean kina Rostam, Chenge na Lowassa). Actually amewaharibia badala ya kuwasaidia. Hususan Lowassa huyu mama ameivuruga kwa kiasi kikubwa sana ndoto yake ya kurudi juu kisiasa. Anatakiwa kumkana. Kitu ambacho it is impossible!

Pili amemuharibia sana Kikwete. Kikwete leo nasikia kaenda Misri. lakini sijua akirudi ataficha wapi sura. Ni aibu sana kwa upande wake. Hii ndio timu yake wanaofanya kazi pamoja with common goals! Nadhani itabidi afanye kitu wanachotegemea watu wengi. Kumuomba huyu mama apumzike. This is also impossible!

Mwisho na kubwa zaidi ni aibu kwa taifa, hususan taswira yetu nje imechafuka sana. Imagine wale waliomtunuku Mama malecela tuzo, leo hii wanasikia Waziri anayehusika na usalama wa taifa kamtusi na kumwita fisadi. O boy!

Mwisho hii ni aibu kwa CCM yote. Lakini kwa bahati mbaya hawana aibu hao. Wameshakufa ganzi tayari.

Watanzania tuna bahati mbaya kwa kweli. Poor me!
 
Haya kwa wale watetezi wa Mengi na Chama chenu cha Mafisadi msikie huo ujumbe CCM waliompa Mengi.Tukiwaambia kwamba kama nyie siyo mafisadi basi mkiache hicho Chama mnakuja juu.

Na Tumaini Msowoya

SIKU moja baada ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP Media Reginald Mengi kuthibitisha uanachama wake wa CCM kwa kuonyesha kadi ya mwaka 1977, chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam kimemkana.

Katibu wa CCM mkoani humo Kilunde Ng'enda amesema CCM Dar es Salaam bado haimtambui Mengi kama mwanachama wake vinginevyo akathibitishe ofisini kwake.

Ng'enda alisema pamoja na Mengi kuonyesha kadi hiyo aliyodai imetolewa mwaka 1977, mkoa haumtambui kwa kuwa jina lake haliko kwenye tawi lolote la CCM mkoani humo.

Alisema Mengi anatakiwa kufika ofisini kwake kuthibitisha madai hayo kwa kueleza ni mwanachama wa tawi kwa kuwa hayumo kwenye orodha ya wanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Aje ofisini kwangu ajitambulishe ikiwa yeye ni mwanachama kwani mpaka sasa mkoa hautambui uanachama wake," alisema.

Alisema katika ziara zake za kichama, hajawahi kukutana na jina la Mengi kwenye tawi lolote hali ambayo imemfanya ashidwe kuridhika na maelezo ya Mengi kwamba ni mwanachama wa CCM.

Juzi Mengi alikanusha madai ya CCM kwamba sio mwanachama wake kwa kuonyesha kadi aliyodai kupata mwaka 1977.

Kwa mujibu wa Mengi kadi yake ilitolewa na tawi la Kisutu Aprili 18 mwaka 1977 na kuthibitisha madai hayo kwa kuonyesha barua iliyosainiwa na katibu wa CCM tawi la Kisutu Musa Kambanga.

Mengi alisema maneno ya Kilunde kuwa ametembea kila tawi katika Mkoa wa Dar es Salaam na hajakuta jina lake, ni uzushi na yenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa chama na baadhi ya wanachama katika kupiga vita ufisadi.


Source: Mwananchi 11/7/2009
 
Lakini haya m.at.usi. ndiyo yaliyomsaidia huyu mama kwenye kampeni yake UWT! Alintukana sana mama Kahama kiasi cha kuhatarisha hata ndoa yake. Nafikiri anaamini kuropoka ndiko kulikompa uwaziri pia!
 
kazi ipo ...Mengi unaona madhara ya kukurupuka hayo.wenye chama hawakutambui unang'ang'ana nini?
 
Kwanza mi sioni sababu ya Mzee Mengi kuhangaika kujieleza kwa umma juu ya uanachama wake, what for?

Kama ana kadi, na anailipia, hakuna sababu ya kujieleza kote huko!

Whether atakuwa mwanachama au la, i dont see any reason for anyone to make it a loud business!

Mbona mimi hakuna anaenifuatilia?...Wanataka wanachama au wachangiaji?
 
duh! ccm sasa wanakana wanachama wao? au ndo tusseme mengi hajui taratibu halali za kumwana ccm?
 
Huyu mama namstahi tu yaani tabia anayoifanya haiendani na yeye mwenyewe alivyo. Lakini President amekosea sana kumchagua maana Huyu mama Historia yake alikuwa anagawa sana sasa iweje apewe Wizara Nyeti???? Tumekwisha yaaani anamshambulia mzee wa watu utafikiri yeye ni mpinzani. Huyu mama ni kibaraka wa Richmonduli. Asante nitalia kwa machuku ya huyu mama Aibu kwa Taifa si yeye
 
Mambo ya ndani ya chama zamani yalikuwa yanatatuliwa ndani ya Chama kisha baada ya hapo Mwenyekiti au Kiongozi yeyote anakuja kutoa msimamo! Siku hizi kila mtu ni mwenyekiti na msemaji ndani ya chama! We dont know who to trust any more!
 
Kwanza mi sioni sababu ya Mzee Mengi kuhangaika kujieleza kwa umma juu ya uanachama wake, what for?

Kama ana kadi, na anailipia, hakuna sababu ya kujieleza kote huko!



Whether atakuwa mwanachama au la, i dont see any reason for anyone to make it a loud bisiness!

Mbona mimi hakuna anaenifuatilia?...Wanataka wanachama au wachangiaji?

Kuhusu sababu ya kujieleza hili ni swali zuri sana kwa Mengi

Na kuhusu kuilipia kadi ya chama, atailipiaje wakati wenyewe hawamtambui

Kuhusu kukufuatilia wewe: Wewe nani atakufuatilia wakati siyo fisadi papa wala nyangumi. Wanaofuatiliana ni mafisadi papa na nyangumi
 
hawa wapuuzi; yeye kasema kadi yake ni ya mwaka fulani, ya namba fulani imetolewa Kisutu; huyo mtu wa CCM anatakiwa kusema "hiyo kadi ni yauongo, kadi yenye namba hii haipo, na tawi la Kisutu halikutoa kadi hiyo tarehe na mwaka huo"...

Habari imekwisha; lakini katika wazimu wao wanataka mtu awapigie magoti, awalambe lambe, awamwagie maua na kuwaimbia wimbo wa CCM nambari one.
 
Haya kwa wale watetezi wa Mengi na Chama chenu cha Mafisadi msikie huo ujumbe CCM waliompa Mengi.Tukiwaambia kwamba kama nyie siyo mafisadi basi mkiache hicho Chama mnakuja juu.

"Pole sana mnaoangaika na mambo haya, mimi mpaka sasa sijui niko chama gani, mwaka huu nimetaka kukata kadi mpaka nimeshindwa kuwa niingie chama gani hivyo nimeacha mpaka miaka mitani mingine sioni chama chochote, alafu uzuri ni kwamba haininyimi usingizi wala hainipi chakula wala kupeleka watoto wangu shule, nilicho nacho ni kadi ya ukriso ya kubatizwa"
 
Mfa maji haishi kutapatapa, sisiemu thatha ndo inatapatapa hivyo mpasuko mkubwa unaonekana ndani ya hicho chama.
 
Taib. Wakaze uzi hivyohivyo mpaka kieleweke ili kila mtu hata aliye bubu asikie na kipofu aone.
 
hawa wapuuzi; yeye kasema kadi yake ni ya mwaka fulani, ya namba fulani imetolewa Kisutu; huyo mtu wa CCM anatakiwa kusema "hiyo kadi ni yauongo, kadi yenye namba hii haipo, na tawi la Kisutu halikutoa kadi hiyo tarehe na mwaka huo"...

Habari imekwisha; lakini katika wazimu wao wanataka mtu awapigie magoti, awalambe lambe, awamwagie maua na kuwaimbia wimbo wa CCM nambari one.



MKJJ,
Teh teh teh te te te Hao ndiyo CCM, chama ambacho Mengi anajinasibu nacho. Hivyo inaonyesha kumbe Mengi naye ni kundi la wapuuzi na waongo
 
Jamani mimi ni muda mrefu nilikwishasema huyu mama ni mtambo
 
Wakuu, hata ule mnara wa babeli wakati unakaribia kuanguka palikuwa na watu kama huyu mama!!!

HUyo ndio kiongozi wa wanawake woote wa CCM Tanzania, je anawakilisha hisia zao?
 
Mimi nadhani Mengi is not aware of what he is doing,he don what he wants,thats why kama anakurupukaga flan hiv,kwa maoni yangu mimi naamin kuwa Mzee Mengi ni mnafik,anajipendekeza kwa CCM na JK in particular,sion sababu ya yeye kurumbana na wateule wa JK at the same time ana trust in JK,wana forum nisaidien,inawezekana vp Mengi akosane na Simba,Rostam nk ambao wote ni wateule/watu wa karibu wa jk at the same time anampamba jk,me nadhani kwa hili Mengi anajichanganya,ukienda ndani zaid unaweza kukuta kuna mambo mabaya sana aliyoyafanya thats y anjikomba kwa watawala so anaogopa wanaweza ku mflush out at any time,na kwa kutaka kwake sifa kwa wananchi anajifanya kuwaunga mkono "makamanda" wa ufisad,nionavyo mimi mzee Mengi ni vuguvugu,namshauri achague kuwa barid au moto kama akina sendeka,tabia yake ya kuijipendekeza kwa watawala nad at the same time ku ku kogombana na wateule wa watawala hao hao ni dalili ya unafiki na usalit kwa watanzania anaojinad anapigania maslahi yao na kuwapa misaaad,anafanikiwa kwa hili kwa sababu watanzania ni maskini sana, ana take advantage ya umaskin wa watanzania kuwazunguka,ndio kuwazunguka,ukichunguza kwa makin uatagundua vyombo vya habari vya mengi (ITV) vimeshaanza kumpigia chapuo JK,vipind maalum vya utekelezaji wa ilani ya CCM vinavyo rushwa na ITV ni uthibitisho tosha.
Me namshauri mzee Mengi akae kimya kama walivyofanya akina Jeetu Patel, Manj nk,other wise watanzania wataendelea kujua yeye Mengi ni mtu wa namna gani kama ambavyo mimi naendelea kum define
 
Unajua watu wanashindwa kuelewa hapa ni nini kinaendelea? Hapa huyu bwana mengi ni mfanyabiashara.....sasa jiulize ni wafanyabiashara wangapi wapo ccm na kwa nini? mimi nadhani endapo ccm itaangushwa mwakani basi utasikia hao hao wafanyabiashara wakidai ni wanachama wa chama kitakachokuwa madarakani....hii ni hatari sana kwani kwa utaalamu wa hali ya juu kabisa ni kwamba viongozi wa juu wa serikali wanaongozwa na wafanyabiashara....na yote hii ni kutimiza matakwa yao ya kibiashara....sasa kwa ccm wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe wanaanza kupigana kuhusu chama....mwenye macho na masikio na akili ataelewa na maanisha nini.
 
Unajua watu wanashindwa kuelewa hapa ni nini kinaendelea? Hapa huyu bwana mengi ni mfanyabiashara.....sasa jiulize ni wafanyabiashara wangapi wapo ccm na kwa nini? mimi nadhani endapo ccm itaangushwa mwakani basi utasikia hao hao wafanyabiashara wakidai ni wanachama wa chama kitakachokuwa madarakani....hii ni hatari sana kwani kwa utaalamu wa hali ya juu kabisa ni kwamba viongozi wa juu wa serikali wanaongozwa na wafanyabiashara....na yote hii ni kutimiza matakwa yao ya kibiashara....sasa kwa ccm wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe wanaanza kupigana kuhusu chama....mwenye macho na masikio na akili ataelewa na maanisha nini.

Sasa hapo August ndiyo umesema kitu cha maana. Hawa wafanyabiashara ni wanafiki na waongo. Wanatetea maslahi yao ya kibiashara halafu wanakuja kudai ooh mimi mwanachama wa CCM au ooh mimi napambana na ufisadi, ama ooh wale ni fisadi papa au yule ni fisadi nyangumi.
 
Ah!! Baba yangu unang'ang'ania nini wenyewe hawakutambui sasa cha kujifanya upoteze nguvu zako uongee katika vyombo vya habari wewe mwanachama tokea siku nyingi wapi? acha chama kina wenyewe hicho. Na wewe mpinga mafisadi hapo kama uliandikishwa mwaka huo je waulize swali kila mwaka unachangia chama je Hela zinakwenda wapi? Acha kujipendekeza baba yangu.
 
Back
Top Bottom