Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta hajaanza kulalamikia mambo ovyoooooooo yanayoendelea ndani ya CCM. Ni Sitta huyu aliyekubali madudu mengi kama ya Richmond na Dowens yafumuke bungeni, vinginevyo ingabaki minong'ono tu. Pamoja na kumwengua Sitta, vita alivyovianzisha vinaendelea licha ya juhudi za hao kuwavuta makoti nyuma wasiendelee mbele.

Richmond na Dowans ni turufu za kisiasa, madudu yamo mengi sana, yeye mwenyewe Sitta madudu yake mangapi yaliletwa humu JF?
 
Richmond na Dowans ni turufu za kisiasa, madudu yamo mengi sana, yeye nweyewe Sitta madudu yake mangapi yaliletwa humu JF?

Kwa walio mahiri wa elimu theology, na wenye ilm ya sayansi kwa pamoja wanafikia kukubaliana katika kitu kimoja kwamba binadamu ndani ya fresh body ni dhaifu, ila roho ni kamili kwa wanateologia na kwa wanasayansi pumzi haina mshkeri. Pamoja na mapungufu ya Sitta, tukitumia mizani utaona Sitta mapungufu ni machache kuliko mazuri. Kwa mtazamo huo tunajadili kupata maana ya aliyoongelea Sitta. Vinginevyo walio na madudu mengi yanayozamisha mizani hawataki mambo hayo yaongelewe ila yapelekwe na kuzimwa ndani ya vikao ili jipu lizidi kuvunda.
 
Mkuu CS, anayesema hovyo kuhusu Magamba si Sitta peke yake, bali wako wengi. Wenyewe Magamba wameamua kuwaita wasema ukweli ndani ya chama kile "wanafiki" na wale walioamua kuuchuna ndio wanaonekana wakweli. Sasa idadi ya wanafiki ndani ya Magamba inazidi kuongezeka.

~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~**~

HOFU ya kuondolewa madarakani kwa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao, imezidi kuwakumba viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho kutokana na mwenendo usioridhisha wa utawala wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani Joseph Mungai, amesema endapo viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hawatakuwa makini kuwatumikia watu, chama hicho kitaondolewa madarakani katika uchaguzi ujao.

Mungai ambaye ni mwanasiasa mkongwe wa CCM alisema hayo jana asubuhi wakati akizungumza kuhusu masuala mbalimbali ya nchi kupitia redio moja ya jijini Dar es Salaam.

Alisema ni vema viongozi wakazingatia na kutimiza kile kilichowafanya Watanzania wakakipigia kura, la sivyo watavigeukia vyama vingine vinavyoonyesha siasa nzuri.

"CCM ijifahamu kwamba wananchi ndiyo wanaopiga kura na wanaweza kuitoa madarakani kama haitafanya vizuri; kwa hiyo ni matumaini yangu kwamba viongozi wa chama watakaa wakijua kuwa utendaji wetu ni muhimu kwa kuzingatia mambo mazuri yanayowapendeza Watanzania ili kuendelea kutuchagua," alisema Mungai.

Kuhusu hoja ya kutenganisha biashara na siasa, Mungai alisema haoni maana yoyote kuhusu suala hilo kwani Kikatiba kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila mtu.

"Binafsi nashindwa kuelewa kutenganisha biashara na siasa kwani kugombea ubunge au udiwani ni haki ya kila mtu," alisema Mungai.
Alieleza kuwa cha muhimu ni kwamba anayeunda serikali (Rais) ana haki ya kuweka masharti ya aina ya watu anaotaka kuwa mawaziri.

Kauli ya Mungai, inakuja siku chache tu baada ya kiongozi mwingine wa zamani wa serikali, Joseph Butiku, kutabiri anguko la CCM iwapo itashindwa kukabiliana na hali mbaya ya mmomonyoko wa maadili ndani ya chama na serikalini.

Butiku alikiri kwamba hali na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM ni vya aibu na kutolea mfano wa vitendo vya rushwa, ubabe, matumizi makubwa ya fedha na nguvu za dola katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora kama dalili mbaya kwa chama makini kama hicho.

Hali ya kisiasa ndani ya CCM imekuwa tete kwa miaka ya hivi karibuni ambapo taifa limeshuhudia viongozi wake waandamizi wakishambuliana waziwazi kwa tuhuma katika kile kinachoelezewa kama falsafa ya kuvua gamba.






[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Mungai aibuka, aionya CCM

na Hellen Ngoromera
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]

Joseph Mungai ni mmoja kati ya wanasiasa wazamani ambao nasaha zao hazipaswi kusikilizwa na jamii ya waTanzania hivi leo kwani katika utumishi wake hakuwa na uadilfu wowote bali ubadhilifu na ufisadi uliokithiri sehemu zote alizowahi kutumikia; mfano mmoja ni upotevu wa shlingi billion tatu pale wizara ya elimu alipokuwa waziri na ili kuficha uchafu wake akafanikisha kufukuzwa kwa mhasibu mkuu wa wizara. Huyu bwana hafai na ndio maana wananchi wa Mufindi wanaomfahamu fika walimkataa alipojaribu kuhonga ili ateuliwe kuwa mbunge!! Huyu ni mtu mmoja wakuogopwa kama ugonjwa wa ukoma.
 
Sitta Mnafiki tu na mroho wa madaraka. Kama kweli anaipenda Tanzania na anauchungu nayo, mbona asihame CCM na kujiunga na chama cha uhakika kama Chadema ? Mbona alipokuwa bungeni hivi majizi aliziponda harakati wa vyama vya upinzani wanaopinga ufisadi na kusema ati wanajitafutia umaarufu ??
Natumaini kelele zote anazopiga ni za kutafuta kukimbilia ikuli 2015 - hana lolote huyu jamaa ... kama analo, basi aje CHADEMA ili tuunganishe nguvu !
 
Sitta Mnafiki tu na mroho wa madaraka. Kama kweli anaipenda Tanzania na anauchungu nayo, mbona asihame CCM na kujiunga na chama cha uhakika kama Chadema ? Mbona alipokuwa bungeni hivi majizi aliziponda harakati wa vyama vya upinzani wanaopinga ufisadi na kusema ati wanajitafutia umaarufu ??
Natumaini kelele zote anazopiga ni za kutafuta kukimbilia ikuli 2015 - hana lolote huyu jamaa ... kama analo, basi aje CHADEMA ili tuunganishe nguvu !

Kwani Kikwete ndio mkweli!? Mbona naye alikimbilia kuingia Ikulu kwa kutumia kundi la mafisadi wenyewe walijiita wana mtandao na kutumia mabilioni chungu nzima kununulia kura ndani ya Magamba na pia kumchafua SAS!? CCM kuna yeyote ambaye si mnafiki!? Kama yupo/wapo hebu tuwekeeni jina/majina lake/yao. Ni bora mnafiki ambaye anaamua kusimama na kusema ukweli kutetea maslahi ya nchi kuliko mnafiki ambaye ameamua kuuchuna na kunyamaza kimya huku akiujua ukweli na kunyamaza kwake kunazidi kuiangamiza nchi.
 
Ameumia sana roho huyu Sitta kushindwa na Mwanamke. Mfumo Dume.

Hapa nitaingilia kwa kukumbusha kuwa kwenye uspika, Makamba alisema kuwa nafasi hiyo ilitengwa na CCM kuchukuliwa na mwanamke. Kwa hiyo siyi kuwa alishindwa na mwanamke ila ni kwa vile CCM iliondoa wanaume wote katika kinyang'anyiro kile na kuacha nafasi kwa wanawake tu.

Hata hivyo kwa upande wake Sita naye ana mzigo wake wa kubeba, kwani hata yeye kupata kiti kile ilikuwa ni matokeo ya kubebwa kama ambavyo Makinda alivyobebwa. Inawezekana kuwa ameumizwa na mfumo alioshiriki kuuanzisha kwa kumchagua Spika kwa kutumia makundi. Mwaka ule wa 2005 Sita alikuwa ni mwanamtanado ambao ndio uliomuweka pale, kwa hiyo leo hii baada ya mtandao kugawanyika, na yeye kujikuta nje ya pande lenye nguvu basi ndiyo maana akatupwa. Nadhani wakati akiwa Spika alitakiwa asadie katika kuimarisha demokrasi nchini kwa kuondoa kipengele ambacho kilikuwa kinavipa vyama vya siasa sauti ya kuingilia mambo ya bunge, kwa mfano kutohusisha nafasi ya uspika na vyama vya siasa. Katika mazingira hayo huenda angeweza kugombea tena kama Mbunge Sita, na kuweza kushinda tena kiti kile, lakini aliacha nafasi hiyo kuwa ya kichama, na ndiyo maana kikamtema.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ameumia sana roho huyu Sitta kushindwa na Mwanamke. Mfumo Dume.

Mwanamke yupi? kuwa serious wewe mwanamke!! Hivi hata akili ya mtoto wa primary inaweza amini maneno haya ya huyu faizafoxy? Sitta akushindwa na mwanamke,alishindwa na kambi ya mafisadi pale CCM na hii iko wazi kabisa,aiitaji uwe na Masterz kufahamu hili....
 
Sasa makombora hapo ni yepi? Manake zote ni old news,aseme mapya basi,kha!
 
  • Ahusisha ugonjwa wa Mwakyembe na kulishwa sumu
  • Asema kuengulia kwake uspika mkakati wa mafisadi
  • Alazimika kubadili namba za simu kukwepa vitisho
  • Viongozi CCM wana roho ya kuku, wepesi kubadili mawazo kwa ajili ya pesa
  • Akiri kuifahamu CCJ na anaiongelea vizuri ingawa anakanusha kuhusika uanzishwaji wake
  • Amekubali nguvu ya Chadema ilivyoonyeshwa Igunga na kusifia itikadi zake ila hayuko tayari kuhama CCM

Source: Majira
Sitta haaminiki wana jf sitochoka kusema hili,ametolewa uspika kama alivyoingizwa! Tungemsamehe yote lakini kitendo chake cha kuzima kibabe issue za richmond ndio zinatugharimu hadi sasa hizi kelele za wasilipwe zisingekuwepo! Na alimshushua kihuni Dr slaa na wenzake walipotaka hatua zaidi zichukuliwe! Huyu anapohaidiwa kitu anakuwa mpole akiguswa richmond inaibuka!! Bunge la mwisho ndio kabisaa aliharibu kwa kutetea upuuzi mwingi ikiwemo posho na kuwatukana wapinzani hasa Cdm! Huyu anapigana vita very personal na after single ya richmond ikiisha hamtamsikia kamwe!! Aliasisi ccj then akatosa wenzake dk za mwisho! Mnafiki tu huyu!
 
Sasa makombora hapo ni yepi? Manake zote ni old news,aseme mapya basi,kha!
Hana hata nukta ya kuongeza! Kelele zile zile! Atuambie yeye ndio aliruhusu mjadala wa richmond,je ulipoishia ndio yalikuwa malengo yake? Huyu atakuwa aliuzima baada ya kuhaidiwa kitu na alipoona amegeukwa anaanza tena kulia!!! Kelele za richmond wapige wengine si yeye tumechoka porojo zake zisizo na matokeo mwisho ndio ujinga wa kuilipa dowans mabilioni!
 
Sitta aiogopa CHADEMA
• Akiri inakubalika kwa wananchi kwa kupinga ufisadi

na Waandishi wetu






WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, amesema nguvu ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA) inatishia uhai na utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, waziri huyo ambaye pia aliwahi kuwa Spika alisema: “Mambo kama haya nasema hata kule Igunga CHADEMA walituhangaisha na kujipatia umaarufu wa kukubalika kwa wananchi kutokana na udhaifu wetu na hasa tabia hii ya kuendelea kuwabeba watu wasio waadilifu wenye tuhuma za ufisadi.
“…CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana hawakuwa na mgombea lakini kwenye uchaguzi mdogo wameibuka na kura zaidi ya asilimia 43, wanatumia udhaifu wetu wa tuhuma za ufisadi na ugumu wa maisha halafu wanazijengea hoja wananchi wanawakubali wao. Hapa lazima tujibadilishe na kujipanga upya.”

Alisema nguvu iliyoonyeshwa na CHADEMA katika uchaguzi huo, ilitokana na udhaifu wa CCM ambayo inaendelea kuwakumbatia mafisadi.
Alisema CHADEMA wameweza kutumia udhaifu huo na ugumu wa maisha wa wananchi kuushawishi umma.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kujaza nafasi ya Rostam Aziz aliyejiuzulu kwa madai kwamba amechoshwa na siasa uchwara ndani ya CCM, mgombea wa chama hicho, Dk. Peter Kafumu, alishinda kwa kura 26,484 akifuatiwa na wa CHADEMA, Joseph Kashindye, aliyepata kura 23,260 na Leopold Mahona, wa CUF, kura 2,104.

Sitta alisema katika uchaguzi ujao ndani ya CCM, chama chake kinapaswa kujipanga na kupata safu mpya ya uongozi wenye maadili ili watue mzigo wa mafisadi ambao wanafanya vitendo hata vya kulitia hasara taifa bila kujali, kwani lengo lao ni utajiri.
Alisema mambo si shwari ndani ya CCM, akaonya kwamba endapo chama hicho hakitabadili mfumo na utendaji wake, kitakumbwa na ushindani mkubwa wa kisiasa huko mbele.

“Nadhani unaona hali ya kisiasa inavyozidi kuwa ngumu, wenzetu wa CHADEMA wanatumia mbinu ya umaskini walionao wananchi na hoja ya mafisadi ambayo inazidi kuwajengea umaarufu. Kielelezo tosha ni matokeo ya uchaguzi Igunga ambao CHADEMA walipata aslimia 43. Kumbuka ni mwaka jana tu tumefanya uchaguzi mkuu lakini wananchi wamegeuka,” alisema Sitta.
Waziri Sitta alitumia kipindi hicho kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kwamba hahusiki na uanzishwaji wa chama cha siasa cha CCJ na kudai kuwa yeye ni mwanasiasa na amekuwa akikutana na wanasiasa wenzake wakiwemo wale wa kambi ya upinzani na kujadili mambo mengi, hivyo haoni kuwa huo ni usaliti.

“Unajua ukishakuwa mwanasiasa utakutana na wenzako, wapo wanaokuja tunazungumza na wananiambia huko uliko hakufai njoo upande huu, naomba kukujulisha au kuujulisha umma kuwa mimi ni mwana CCM na nitabaki CCM, lakini ujue kuwa CCM si baba yangu au mama yangu nikiona yamenishinda nitajua cha kufanya,” alisema Sitta.
Hata hivyo, zipo kumbukumbu nyingi zinazoonyesha kuwa Sitta alikuwa miongoni mwa wanasiasa waandamizi ndani ya CCM walioasisi CCJ kwa malengo ya kushindana na CCM na CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Mbali na Sitta, makada wengine wa CCM walioasisi CCJ kwa madai kwamba wanakerwa na mwenendo wa CCM, ni Nape Nnauye, Dk. Harrison Mwakyembe na Fred Mpendazoe.

Miongoni mwao, Mpendazoe ndiye alijitoa mhanga kwa kuondoka CCM na kupoteza ubunge wa Jimbo la Kishapu; lakini CCJ kilipokosa usajili wa kudumu akajiunga na CHADEMA. Baadaye aliandika kitabu na kuwataja aliokuwa nao, ingawa wamekuwa wanakanusha kuhusika na harakati hizo.
Sitta ndiye amekuwa kinara wa kundi lililojipachika jina la “wapambanaji wa ufisadi” ambalo wachambuzi wa siasa wanasema lilijitokeza ili kuuza nguvu ya CHADEMA katika mapambano ya ufisadi.
CHADEMA ndiyo iliyosisi hoja na mapambano ya ufisadi na kwa mara ya kwanza ilianika hadharani orodha ya watuhumiwa ufisadi 11, Septemba 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.

Orodha hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, baada ya Sitta, akiwa Spika wa Bunge, kukataa hoja ya Dk. Slaa kuhusu ufisadi na kutishia kumshtaki kwa maelezo kuwa alikuwa ameghushi vielelezo alivyokuwa navyo.
Hata hivyo, baada ya kuona kasi ya vita ya ufisadi imeshika moto, Sitta na kundi lake, wakiwamo pia Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, na Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, waliibuka na kuanza kushambuliana na makundi mengine ndani ya CCM waliotajwa na Dk. Slaa.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema kwamba nia ya kina Sitta haikuwa kupigana na ufisadi, bali kuendeleza vita ya makundi ndani ya chama chao, na kuipiku CHADEMA katika vita ya ufisadi, ili wananchi waone kwamba hata ndani ya CCM kuna wanaochukia ufisadi.
Baadaye, Rais Jakaya Kikwete amekuja kuitumia hoja ya ufisadi kuwachukulia hatua za kisiasa na kisheria baadhi ya waliotajwa katika orodha hiyo, ingawa naye ni miongoni mwa waliotajwa.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema hatua hiyo ya Rais Kikwete ni propaganda za kisiasa za kutaka kujikosha mbele ya Watanzania, kwani sehemu ya ufisadi unaowahusu hao wanaotuhumiwa ilimhusisha au kumhusu pia yeye, kwani baadhi ya pesa zilizotumika kumwingiza madarakani zilitokana na ufisadi.
Baadhi ya makada ndani ya CCM wamekuwa wanahusisha kauli za Sitta na uchaguzi mkuu ujao, ingawa yeye amesema juzi kwamba hana nia ya urais.

Hata hivyo, inajulikana kwamba Sitta ana kundi lake, na kauli zake zinalenga kuwadhoofisha baadhi ya wanaofikiriwa kuusaka urais ndani ya chama chake, ambao wanadhaniwa kuwa washindani wake au wa kundi lake.
 
Inawezekana kabisa unalosema ni sahihi, lakini chukulia kama ni kweli uyasemayo, utolewe sehemu muhimu kama ile halafu awekwe mwanamke ambae alikuwa ni naibu wako, na wapo wengine wenye "uwezo" zaidi, huoni kuwa huyo mwanamke anazicheza karataka zake vizuri?

Tanzania hii kama uijuavyo, vyeo vidogo tu maofisini, watu wanarogana wanatiliana mafitna, wanafanyiana kila hila, itakuwa pale? Inatakiwa mtu uwe "tough" kufika pale.

Naona kama Makinda kawekwa basi hiyo ndio inayomuuma zaidi Sitta. Inarudi pale pale "Mfumo Dume".

We nawewe unachanganya mambo issu e si kutolewa yeye akawekwa mwanamke ambae alikua naibu wake,bali njia zilozotumika kumuengua ndio issue,wangemuacha yeye na huyo mwanamke washindane kwenye sanduku la kura halafu angeshindwa then aje na malalamika haya ndio issue yako ingekua na mashiko,hapo tungeamini huyu mzee ana nongwa na wanawake lakini sio ule uhuni wa kumuacha mtu anachukua fomu anailipia milioni moja anafanya kampeni masaa machache kabla ya uchaguzi kufanyika ghafla kinapenyezwa ambacho hata ungefanyaje huwezi kukifikia,ni wazi sitta hata angependa asingeweza kujigeuza awe mwanamke kwa muda ule uliobaki na hata angongezewa muda wa mwaka mzima...!!!kama kweli lengo lilikua ni kumuwezesha mwanamke na lilikuwepo kweli tangu mwanzo ccm wangetangaza aidhani kama mh.6 na wanaume wengine wangekubali kupoteza nguvu na fedha zao kuomba nafasi hiyo.ule ni uhuni wa ccm na mafisadi
 
hivi bado kuna watu wanamfuatilia huyu mwehu? just emagine dume zima linakuja kwako kila siku linakulalamikia oooohhh nyumbani kwangu siku hizi pachafu sana mara oohhh mke wangu haogi kabisa siku hizi ooh wanangu hawapendi kuoga/kusoma na stori nyiiiiiiiiiingi za familia yake. ingawa hayakuhusu unampa ushauri lakini kesho anarudi na story hizohizo na wewe bado unapoteza muda wako kumsikiliza....sasa hapo nani mwenye matatizo kati yako na yake...sitta kama unaona ccm pamechafuka hama otherwise nyamaza tumechoka kusikiliza upupu wako, ishi hivyohivyo ndani ya uchafu uliochagua! hizi kelele za mwizi mwizi sasa tunaona ni hadaa wakati mnashirikiana kuitafuna nchi yetu. bahati nzuri sana kwenu ni kuwa mnaongoza nchi ya watu wanaopenda fitina,majungu,uchonganishii etc na ndio maana hapo wanakuona shujaaaaaaaa coz na wewe mulemule.....laiti ningekuwa na uwezo ningeweka plasta hilo domo lako coz nahisi linaniongezea hasira tu hadi natamani kupigana....
 
Back
Top Bottom