Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV


Issue si mfumo dume au la ila ni sera tu za kumtoa. Maana katika hali ya kawaida kabisa ni wazi kwamba Sitta anauwezo kuliko Makinda. Na hii haitokani na kwamba Sitta ni mwanaume au la. Hatuhitaji Profesa kuliiona hili. Bunge la sasa analosimamia Makinda si sawa na bunge alilokuwa anaendesha Sitta....!!! Kwenye ukweli tusiweke suala la mifumo dume au jike.
[h=2] This message is hidden because FaizaFoxy is on your ignore list. [/h] View Post
 
Huwezi kuwa Ndani ya CCM halafu ukajiita wewe MSAFI na kuanza kuwanyooshea vidole wenzako - huo ni unafiki mkubwa sana!!!

Mwandosya, Sitta, Mwakyembe, Nape (PupXXt) wote wanatizama 2015 - na pia wan-beef na kunyimwa sauti katika miaka hii mitano...
 
Huyu SS simuelewielewi vile anajua madudu ya viongozi wake " Viongozi CCM wana roho ya kuku, wepesi kubadili mawazo kwa ajili ya pesa" halafu bado yumo humohumo akisaidiana nao zaidi ya hapo naye ni kiongozi ie waziri, mbunge, mlezi wa Jumuhiya ndani ya chama hicho hicho
 
Alidhani akimwondoa Lowasa kwenye Uwaziri Mkuu yeye angebaki salama wakati ni vyeo waligawana kwa MoU ya wanamtandao? Amebaki JK tu naye chupuchupu 2010 imwondoe kama si nguvu ya dola.
 
najua sitta ana ghadhabu sana. Mfumo ulivyo sasa ndio sababu ya kina sitta, bhanji na wengine kufunguka. Wametendwa hao
 
Kwa walio mahiri wa elimu theology, na wenye ilm ya sayansi kwa pamoja wanafikia kukubaliana katika kitu kimoja kwamba binadamu ndani ya fresh body ni dhaifu, ila roho ni kamili kwa wanateologia na kwa wanasayansi pumzi haina mshkeri. Pamoja na mapungufu ya Sitta, tukitumia mizani utaona Sitta mapungufu ni machache kuliko mazuri. Kwa mtazamo huo tunajadili kupata maana ya aliyoongelea Sitta. Vinginevyo walio na madudu mengi yanayozamisha mizani hawataki mambo hayo yaongelewe ila yapelekwe na kuzimwa ndani ya vikao ili jipu lizidi kuvunda.

Sitta kwa sasa ni kama "Black Mamba" aliyejeruhiwa anajuwa kuwa ama kupona ama kufa na kama ni kifo basi kiwe cha wengi.

Kumbuka, wadhifa wa Uspika wa Bunge ni mkubwa sana katika Tanzania, hata Waziri Mkuu haufiki, ni mhimili mmoja wa Dola kati ya mitatu. Inauma sana kutolewa uspika ukapewa uwaziri. Lazima ajitutumuwe, nna kuhakikishia yumo katika system lakini kwa sasa ni nani zaidi? hakuna.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, amesema nguvu ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA) inatishia uhai na utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, waziri huyo ambaye pia aliwahi kuwa Spika alisema: “Mambo kama haya nasema hata kule Igunga CHADEMA walituhangaisha na kujipatia umaarufu wa kukubalika kwa wananchi kutokana na udhaifu wetu na hasa tabia hii ya kuendelea kuwabeba watu wasio waadilifu wenye tuhuma za ufisadi.
“…CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana hawakuwa na mgombea lakini kwenye uchaguzi mdogo wameibuka na kura zaidi ya asilimia 43, wanatumia udhaifu wetu wa tuhuma za ufisadi na ugumu wa maisha halafu wanazijengea hoja wananchi wanawakubali wao. Hapa lazima tujibadilishe na kujipanga upya.”
Alisema nguvu iliyoonyeshwa na CHADEMA katika uchaguzi huo, ilitokana na udhaifu wa CCM ambayo inaendelea kuwakumbatia mafisadi.
Alisema CHADEMA wameweza kutumia udhaifu huo na ugumu wa maisha wa wananchi kuushawishi umma.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kujaza nafasi ya Rostam Aziz aliyejiuzulu kwa madai kwamba amechoshwa na siasa uchwara ndani ya CCM, mgombea wa chama hicho, Dk. Peter Kafumu, alishinda kwa kura 26,484 akifuatiwa na wa CHADEMA, Joseph Kashindye, aliyepata kura 23,260 na Leopold Mahona, wa CUF, kura 2,104.
Sitta alisema katika uchaguzi ujao ndani ya CCM, chama chake kinapaswa kujipanga na kupata safu mpya ya uongozi wenye maadili ili watue mzigo wa mafisadi ambao wanafanya vitendo hata vya kulitia hasara taifa bila kujali, kwani lengo lao ni utajiri.
Alisema mambo si shwari ndani ya CCM, akaonya kwamba endapo chama hicho hakitabadili mfumo na utendaji wake, kitakumbwa na ushindani mkubwa wa kisiasa huko mbele.
“Nadhani unaona hali ya kisiasa inavyozidi kuwa ngumu, wenzetu wa CHADEMA wanatumia mbinu ya umaskini walionao wananchi na hoja ya mafisadi ambayo inazidi kuwajengea umaarufu. Kielelezo tosha ni matokeo ya uchaguzi Igunga ambao CHADEMA walipata aslimia 43. Kumbuka ni mwaka jana tu tumefanya uchaguzi mkuu lakini wananchi wamegeuka,” alisema Sitta.
Waziri Sitta alitumia kipindi hicho kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kwamba hahusiki na uanzishwaji wa chama cha siasa cha CCJ na kudai kuwa yeye ni mwanasiasa na amekuwa akikutana na wanasiasa wenzake wakiwemo wale wa kambi ya upinzani na kujadili mambo mengi, hivyo haoni kuwa huo ni usaliti.
“Unajua ukishakuwa mwanasiasa utakutana na wenzako, wapo wanaokuja tunazungumza na wananiambia huko uliko hakufai njoo upande huu, naomba kukujulisha au kuujulisha umma kuwa mimi ni mwana CCM na nitabaki CCM, lakini ujue kuwa CCM si baba yangu au mama yangu nikiona yamenishinda nitajua cha kufanya,” alisema Sitta.
Hata hivyo, zipo kumbukumbu nyingi zinazoonyesha kuwa Sitta alikuwa miongoni mwa wanasiasa waandamizi ndani ya CCM walioasisi CCJ kwa malengo ya kushindana na CCM na CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Mbali na Sitta, makada wengine wa CCM walioasisi CCJ kwa madai kwamba wanakerwa na mwenendo wa CCM, ni Nape Nnauye, Dk. Harrison Mwakyembe na Fred Mpendazoe.
Miongoni mwao, Mpendazoe ndiye alijitoa mhanga kwa kuondoka CCM na kupoteza ubunge wa Jimbo la Kishapu; lakini CCJ kilipokosa usajili wa kudumu akajiunga na CHADEMA. Baadaye aliandika kitabu na kuwataja aliokuwa nao, ingawa wamekuwa wanakanusha kuhusika na harakati hizo.
Sitta ndiye amekuwa kinara wa kundi lililojipachika jina la “wapambanaji wa ufisadi” ambalo wachambuzi wa siasa wanasema lilijitokeza ili kuuza nguvu ya CHADEMA katika mapambano ya ufisadi.
CHADEMA ndiyo iliyosisi hoja na mapambano ya ufisadi na kwa mara ya kwanza ilianika hadharani orodha ya watuhumiwa ufisadi 11, Septemba 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.
Orodha hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, baada ya Sitta, akiwa Spika wa Bunge, kukataa hoja ya Dk. Slaa kuhusu ufisadi na kutishia kumshtaki kwa maelezo kuwa alikuwa ameghushi vielelezo alivyokuwa navyo.
Hata hivyo, baada ya kuona kasi ya vita ya ufisadi imeshika moto, Sitta na kundi lake, wakiwamo pia Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, na Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, waliibuka na kuanza kushambuliana na makundi mengine ndani ya CCM waliotajwa na Dk. Slaa.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema kwamba nia ya kina Sitta haikuwa kupigana na ufisadi, bali kuendeleza vita ya makundi ndani ya chama chao, na kuipiku CHADEMA katika vita ya ufisadi, ili wananchi waone kwamba hata ndani ya CCM kuna wanaochukia ufisadi.
Baadaye, Rais Jakaya Kikwete amekuja kuitumia hoja ya ufisadi kuwachukulia hatua za kisiasa na kisheria baadhi ya waliotajwa katika orodha hiyo, ingawa naye ni miongoni mwa waliotajwa.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema hatua hiyo ya Rais Kikwete ni propaganda za kisiasa za kutaka kujikosha mbele ya Watanzania, kwani sehemu ya ufisadi unaowahusu hao wanaotuhumiwa ilimhusisha au kumhusu pia yeye, kwani baadhi ya pesa zilizotumika kumwingiza madarakani zilitokana na ufisadi.
Baadhi ya makada ndani ya CCM wamekuwa wanahusisha kauli za Sitta na uchaguzi mkuu ujao, ingawa yeye amesema juzi kwamba hana nia ya urais.
Hata hivyo, inajulikana kwamba Sitta ana kundi lake, na kauli zake zinalenga kuwadhoofisha baadhi ya wanaofikiriwa kuusaka urais ndani ya chama chake, ambao wanadhaniwa kuwa washindani wake au wa kundi lake.

hapo kwenye red hapo....... pa kuangalia kwa makini sana
 
kwani lazima alikuwa awe spika nchi ina watu wengi wa kushika nafasi hiyo vizuri zaidi yake,hata mimi,tena ni rahisi mno ni kama moderator wa mdahjalo ukishakariri kanuni mwendo mdundo.anachoskitika hawezi kusanya pesa kwa ajili ya kuusaka uraisi 2015 pesheni ua spika kubwa pamoja na bajeti ya bunge,hawezi pata hiyo hela kwa bajeti ya EA ndogo
 
Maneno ya Sitta ni ghiliba kwa watanzania. Yeye siku zote anaona ufisadi wa mapacha watatu tu. Ngoja NEC ijayo ikae tutasikia mengi sana!

Narudia:
Ukiona mtu ndani ya CCM anakomalia jambo la ufisadi fulani basi jua kanyimwa mgao au wanaofaidika na mgao huo ni maadui wake wa kisiasa ndani ya chama PERIOD

Ufisadi ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi na hauishii kwenye Dowans au EPA tu. Hata matumizi ya magari ya kifahari (aliyokuwa anatetea juzi) kwa taifa maskini kama letu ni UFISADI. Ukimsikiliza kwa makini utabaini kuwa yale yalikuwa maneno ya mkosaji na si mtu anayesema ninapigania taifa langu liondokane na ufisadi.

 
Inawezekana kabisa unalosema ni sahihi, lakini chukulia kama ni kweli uyasemayo, utolewe sehemu muhimu kama ile halafu awekwe mwanamke ambae alikuwa ni naibu wako, na wapo wengine wenye "uwezo" zaidi, huoni kuwa huyo mwanamke anazicheza karataka zake vizuri?

Tanzania hii kama uijuavyo, vyeo vidogo tu maofisini, watu wanarogana wanatiliana mafitna, wanafanyiana kila hila, itakuwa pale? Inatakiwa mtu uwe "tough" kufika pale.

Naona kama Makinda kawekwa basi hiyo ndio inayomuuma zaidi Sitta. Inarudi pale pale "Mfumo Dume".

Ukweli ni kwamba Sitta alizidiwa kete na wenzake kwa kumpachika huyu Mama ili kufanikisha agenda zao kwa urahisi. Hakuna kigezo chochote cha maana kilichotumika zaidi ya hicho. Hakuna cha mfumo dume, weledi au uwezo wa kuendesha Bunge kwa manufaa ya Watanzania.
 
mh sitta ameendelea kutoa kauli na malalamiko ambayo kimsingi anaonekana bado anasononeka moyoni baada ya kuukosa u speaker na u pm,ni jambo la kushangaza,hv majuz akizungumza katika kipindi ITV alisema hana nia ya kugombea urais 2015,nilishangaa sana ninavyomfahamu sitta ni mtu ambaye anautamani urais wa nchi kwa namna yoyoye,hii kauli ya kuwa hagombei tena urais,kimsingi mh Sitta kasoma alama za nyakati kwanza amegundua ndani ya CCM hana nguvu yoyote hivyo hakuballiki,na pia umri wake kwa sasa umekwenda mbali,na kubwa zaidi ni uasi wake ndani ya chama mpaka hatua ya kushiriki wake uanzishwaji wa CCJ,baada ya kuona pia kuwa wananchi wamechoka na kauli zake zisizo na mashiko,tegemeo lake kubwa ilikuwa kuungwa mkono na wananchi wengi,mh Mpendazoe alishasema Sitta ni mtu hatari na ameeleza kwa kina jinsi alivyoshiriki uasi ndani ya CCM lkn bado ameendelea kukana kuhusika,mh sitta kwa sasa hana lolote analoweza kumsaidia rais ni bora apumzike alee wajukuu,kimsingi Sitta anautamani urais ila kutokana na vigezo nilivyotaja hapo juu kaanza kajitoa mwenyewe

nawasalisha
 
Hapa nitaingilia kwa kukumbusha kuwa kwenye uspika, Makamba alisema kuwa nafasi hiyo ilitengwa na CCM kuchukuliwa na mwanamke. Kwa hiyo siyi kuwa alishindwa na mwanamke ila ni kwa vile CCM iliondoa wanaume wote katika kinyang'anyiro kile na kuacha nafasi kwa wanawake tu.

Hata hivyo kwa upande wake Sita naye ana mzigo wake wa kubeba, kwani hata yeye kupata kiti kile ilikuwa ni matokeo ya kubebwa kama ambavyo Makinda alivyobebwa. Inawezekana kuwa ameumizwa na mfumo alioshiriki kuuanzisha kwa kumchagua Spika kwa kutumia makundi. Mwaka ule wa 2005 Sita alikuwa ni mwanamtanado ambao ndio uliomuweka pale, kwa hiyo leo hii baada ya mtandao kugawanyika, na yeye kujikuta nje ya pande lenye nguvu basi ndiyo maana akatupwa. Nadhani wakati akiwa Spika alitakiwa asadie katika kuimarisha demokrasi nchini kwa kuondoa kipengele ambacho kilikuwa kinavipa vyama vya siasa sauti ya kuingilia mambo ya bunge, kwa mfano kutohusisha nafasi ya uspika na vyama vya siasa. Katika mazingira hayo huenda angeweza kugombea tena kama Mbunge Sita, na kuweza kushinda tena kiti kile, lakini aliacha nafasi hiyo kuwa ya kichama, na ndiyo maana kikamtema.

Bro! umeandika vizuri sana siyo kama huyu fox ambaye yuko biased na kifisadi kama Vodacom
 
hivi bado kuna watu wanamfuatilia huyu mwehu? just emagine dume zima linakuja kwako kila siku linakulalamikia oooohhh nyumbani kwangu siku hizi pachafu sana mara oohhh mke wangu haogi kabisa siku hizi ooh wanangu hawapendi kuoga/kusoma na stori nyiiiiiiiiiingi za familia yake. ingawa hayakuhusu unampa ushauri lakini kesho anarudi na story hizohizo na wewe bado unapoteza muda wako kumsikiliza....sasa hapo nani mwenye matatizo kati yako na yake...sitta kama unaona ccm pamechafuka hama otherwise nyamaza tumechoka kusikiliza upupu wako, ishi hivyohivyo ndani ya uchafu uliochagua! hizi kelele za mwizi mwizi sasa tunaona ni hadaa wakati mnashirikiana kuitafuna nchi yetu. bahati nzuri sana kwenu ni kuwa mnaongoza nchi ya watu wanaopenda fitina,majungu,uchonganishii etc na ndio maana hapo wanakuona shujaaaaaaaa coz na wewe mulemule.....laiti ningekuwa na uwezo ningeweka plasta hilo domo lako coz nahisi linaniongezea hasira tu hadi natamani kupigana....

Hakika hawa jamaa wanakera sana. Ngoma hii imelia sana muda si mrefu itapasuka.
 
Siasa ni mchezo mchafu, usione kakaa anayasema yote hayo ukafikiri hayumo, yumo alizidiwa tu.
Right to the point, siasa ni kuonyesha umahiri no matter what!!.......nafasi kama ile inamfanya mwanasiasa kuwa juu kwa 5yrs, inamuongezea points kawenye game.
Sita kazidiwa na wahasimu wake lazima imuume.
Hata siku moja Sita hawezi kuwa na dhamira safi.....no way, sio Sita huyu tunayemfahamu. Kama ni maumivu, ni kweli anayo, lakini kwenye porojo zake dhidi ya CCM ni UNAFIKI TU!!
attachment.php
 
Acha majungu. Au umetumwa? Na nani? na Lowassa & co? Unafiki anaujua mwenyewe sitta sisi kwetu la muhimu ni yale anayosema na kutenda. Na sitta kashadhihirisha hilo juu ya kulipwa Dowans. Amesema bila kificho.
Tutolee ujinga wako hapa.
 
Inawezekana kabisa unalosema ni sahihi, lakini chukulia kama ni kweli uyasemayo, utolewe sehemu muhimu kama ile halafu awekwe mwanamke ambae alikuwa ni naibu wako, na wapo wengine wenye "uwezo" zaidi, huoni kuwa huyo mwanamke anazicheza karataka zake vizuri?

Tanzania hii kama uijuavyo, vyeo vidogo tu maofisini, watu wanarogana wanatiliana mafitna, wanafanyiana kila hila, itakuwa pale? Inatakiwa mtu uwe "tough" kufika pale.

Naona kama Makinda kawekwa basi hiyo ndio inayomuuma zaidi Sitta. Inarudi pale pale "Mfumo Dume".

.....utolewe sehemu muhimu kama ile halafu awekwe mwanamke ambae alikuwa ni naibu wako tena ambaye uliwahi kumkemea hadharani kwa dharau kwamba asikurupukie suala la taarifa ya Richmond!!
 
Back
Top Bottom