Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Mshauri awataje majina hao mafisadi, kwanini anamung'unya maneno? Ujasiri ni kutoa list yake ya mafisadi kama ile iliyotolewa Mwembeyanga. Unajua kwanini hathubutu kuwataja kwa majina? kwa sababu hao anaodai ni mafisadi wana rekodi yake full mkoko! Kumbuka hata Sitta uspika alipewa na hao anaodai ni mafisadi. Ni Rostam ndiye aliyesuka mpango Sitta awe Spika ili EL apewe U-PM, ambao Sitta bado unamtesa hadi leo!

We shida yako ni kuwafahamu mafisadi au kusikia sitta akijidhalilisha kwa kurudia list ile ile ya siku zote?, yuko makini. kwenye bold hujasomeka, sentensi inajipinga yenyewe (nadhani ulitaka kupika hoja)
 
Atatokaje naye anagawana na mwenye nyumba pasu pasu? Unadhani U$ 7,0000 kwa mwezi mchezo? hataki nyumba za serikali kang'ang'ania kwenye nyumba ya mtu binafsi ili apate mgao....halafu eti anajifanya muadilifu!

tehe tehe! $70000 hii amekodisha luxury yatch au Kempinski kule serengeti kwa mwezi duh!
 
thumbnail.aspx

Walimu wa watoto hawa ndiyo wenye uchungu na nchi yangu..... they are my heroes!!, the rest need to shut up!!!! and get to work!!
 
Hivi kweli huyu Said Kubenea kanunuliwa na akina RA, EL? ameogopa ile sumu toka Bulgaria nini? lazima uwe na" chuki binafsi" na mafisadi Kama Sitta ili URISK maisha yako otherwise chukua hela jiunge nao.

kwa upande mwingine hii "chuki binafsi" ya Sitta ndiyo nzuri kupambana na ufisadi, tumpe madaraka huyu mzee atawaondoa mafisadi na mfumo wao kwani atakua ana ari na tija zaidi ya kutaka kuwamaliza wenyewe na mfumo wao kuliko wagombea wengine wote ndani ya CCM hata CDM, (Slaa hajamfikia sitta kwa hili)
 
Mie nilishaacha longtime kusoma gazeti la Mwanahalisi, as time goes linaelekea zaidi kuliko uchunguzi...

..Tofauti yake na yale ya Shigongo ni kuwa Mwanahalisi linabase kwenye udaku wa kwenye siasa wakati Shigongo amejikita kwenye udaku wa maisha ya mitaani...
 
mmmh !!! kuwajibika ni msamiati usiotumika kabisa hapa Tanzania hata walimu wa Kiswahili wanashindwa kutolea mifano
 
Sita mnafki sana....Kama yeye anajiona ni msafi kama theluji ndani ya ccm....basi dawa ni kujitoa kwenye uwaziri na hata kenye chama ili aweze kukaa na watakatifu au wasafi kama yeye!!! huwezi kulalamika ooh mafisadi, wezi wamefanya hivi , vile huku unakula nao, wenyewe wakakuteua na ukakubali uteuzi lakini bado unawalalamikia waliokuteua kuwa ni mafisadi! Kama unaona huridhiki na mwenendo mzima BASI lako ni moja tu nayo ni ujitoe katika chama na serikali ili udhihirishe usafi wako na hivyo utatuaminisha kuwa kweeeli Samwel Sitta ni Msafi na sio kuplay game ya unafki unaoufanya sasa!!! Kumbuka Watanzania wa leo sio wale wa zamani; wana uwezo wa kupima, kuchambua na kufanya maamuzi juu ya unafki woote unaouonyesha!!! Tafakari!!!!!!!!!
 
" ndg zangu wana CCM hawa Wapinzani ni wanafiki sana leo hii wanajifanya wanakataa posho ili hali wametosheka sasa mimi nasema kama kweli wanamaanisha wanachosema basi warudishe hela yote waliyo pewa kama posho hapo ndipo tutawaamini ''

Hii ni kauli ilyonifanya nipoteze imani kabisa na SS wangu hata naona bora EL kuliko SS
 
Unafiki mtupu hapa.heading haihusiani na ulichoandika.uzushi mtupu,utaishia kupata aibu..
 
Mie nilishaacha longtime kusoma gazeti la Mwanahalisi, as time goes linaelekea kwenye udaku zaidi kuliko uchunguzi...

Kumbe mwanahalisi limenunuliwa ndiyo maana hivi karibuni limekua na vita na Kikwete na familia yake ikiwa ni njia ya "wamiliki wapya" aka mafisadi kujilinda kisiasa kwa kupotosha umma, kumuogopesha JK, kuzubaisha watu wasahau ya kwao na mbinu nyingine halafu EL analalamika anachafuliwa wakati yeye ndiyo kinara wa siasa hizi chafu actually ndiyo muanzilishi wake. nani mnafiki sasa?
 
Mkuu, naona unaladhimisha habari, heading yako na thread yako vitu wiwili tofauti..

Sitta na Kikwete lao ni mmoja ndiyo maana kamteuwa kuwa waziri
Ukiangalia kwa macho juu juu unaweza ukadhan wapo pamoja, ila kwa Mambo anayoongea Sitta na yale yanayoendelea nyuma ya pazia, naimani kubwa kuwa hawa ni maadui na kaletwa maksudi kwenye uwaziri ili litakalomtokea ionekane JK hausiki, Ref. Mwakyembe, Mwandosya.

Kama Sitta ni Mtu muhimu na wa karibu kwa JK kwanini anaipinga Dowans nje ya vikao vya Cabinet??tena kwenye vyombo vya Habari??kwani huko kwenye vikao vya Cabinet hawawezi kuliongea hili suala wakalimaliza???Its obvious ndani ya vikao hivyo hapewi nafasi na ndo mana kaamua kuongea kupitia vyombo vya habari. Funguka mkubwa.
 
Huyu sitta mimi sina imani naye sana. Yeye kama anataka aonekane ana uchungu basi aungane na kina Slaa.

kama sikosei huyu jamaa alitukana wapinzani live kwenye kikao cha bunge kilichoisha kwamba ni wanafiki sasa anawezaje kujiunga na wanafiki?
 
Sishangai kuna watu humu wanasema Sitta ni mnafiki. Ni kweli,maana mbele ya mafisadi kila anayeongea ukweli ni mnafiki. Hata kusema kuwa ccm ispobadilika 2015 itakuwa na wakati mgumu ni unafiki? Kazi kwenu mafisadi
 
Watu walipiga kelele sana sitta alipotemwa uspika. Leo vipi mnamwita mnafiki? Hapa hapa tulimsifia juu ya utendaji wake bungeni usiwo na upendeleo kwa chama tawala.
Tabia ya mtu hubadilika kiongozi, Sitta Spika sio huyu wa leo, huyu wa leo ni kigeugeu, mnafki, msaliti na mzee kifikra na kimwili, unahitaji nguvu ya ziada kuamini anachokisema.
 
Source: dakika 45.
Kasema mafisadi ambao wako tayari kumtoa roho ndio waliobadili utaratibu wa uchaguzi wa spika.
Anasema walishindwa kushindana naye kwenye box la kura wakaamua kuweka kigezo cha jinsia.
My take: kama JK aliridhia naye ni fisadi

Nikubaliane na huyu mzee kwamba mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya uspika katika chama chake ulitawaliwa na ufisadi. Anataka kutwambia hata mchakato wa kumchagua spika bungeni kulikua na mkono wa hao mafisadi? Huyu mzee amelikosea heshima Bunge itabidi aitwe na ajieleze,na achukuliwe hatua. Lakini itakuwa ni aibu kama chama chake kitashindwa kumchukulia hatua. Huwezi kutuhumu maamuzi ya chama chako namna hii,uongozi wa chama ukabaki unakuchekea.
 
Huyu Sitta ajiandae kufukuzwa uwaziri tu.

Huu siyo muda wa kutafuta ujiko kwa kukemea ufisadi hadharani, tunahitaji hao mafisadi wachukuliwe hatua za kisheria. Sitta anatumiwa na Kikwete ili watu waone kuwa CCM bado kuna watu wenye uchungu. Huwezi ukawa na kadi ya CCM halafu ujifanye unachukia ufisadi, hii ni sawa na kuwa Mkristo lakini humpendi Yesu Kristo.
Kama unasema anachofanya Sitta ni kutoka Kikwette iweje tena ajiandae kufukuzwa uwaziri??
 
wayamalize kwenye vikao vyao au atoke huko ccm, kama unakaa kwenye mfumo unaouweka uchi mbele za watu na una miaka karibia mia na ishirini una faida gani kwa jamii??

hawa jamaa wamekula nyama za watu sasa wanaweweseka

If he is clean basi atoke ccm!!!
 
Back
Top Bottom