Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

habarini wanajamvi?

Nimekuwa nwalimu wa miaka 5 sasa katika mkoa X na shule nayofundisha kwakweli si mbaya sana ina mazingira mazuri kiasi.Lengo la kuja hapa JF ni kuomba ushauri juu ya hatma ya maisha yangu.

Najua kila mtu hajawahi kutosheka juu ya mishahara yao lakini kwa sisi walimu naona hali inazidi kuwa mbaya, Serikali inatukandamiza kwa makato ya siyo ya lazima kama kuchangia mwenge na tunalazimishwa eti mwenge ukija mkoani kwetu lazima walimu tuwepo kuupokea.

kwanini kila kitu mpka sisi walimu tushiriki aiseee, nimechoka kuona kada yangu pendwa imekuwa inadharaulika na serekali kwa kutupiwa kila kitu cha kisiasa matokea yake walimu tumekuwa watu wa mkakati kwa wanasiasa ili kufanikisha azma yao.

Natamani kuacha ualimu ila naogopa wapi ntapata chanzo kingine cha mapato,na sitaki mikopo kabisaa

Naonmbeni ushauri wa wa biashara gani ya kufanya ili niondoke kwenye ualimu

(Sitaki kufungua kijiwe cha tuisheni, walimu tumekuwa tukiona tuisheni kama ni njia pekee ya kujiajiri SITAKIII)

msaada jamani
Kindly consult@mpwanyungu on the subject
 
Nimekuwa nwalimu wa miaka 5 sasa katika mkoa X
Sorry si kwamba nakushushua lakini uko Moro.. Usiniulize nimejuaje..
Samahan najua ww utakua mzoefu hv inawezekana kubadilisha place of domecile katika mkataba wa ajira?
 
Kwanini usijipe kwanza muda ukijichanga mshahara wako kupata mtaji huku pia ukitafuta idea nzuri ya kitu gani ufanye. Kwa sababu biashara nzuri ni ile ya kuifanyia utafiti na kujiridhisha mwenyewe na sio hizi za kuambiwa na watu

sasa shida ni huo mshahara wenyewe unakuta analipwa 710,000 ila makato yote pamoja na CWT, mwenge, halmashauri, makato ya kumtunza mwalimu mkuu akinunua kiroba cha unga na dagaa debe anabaki na 15000

na hapo akiziba pancha baiskelli mara kadhaa anabaki mkiwa.

KATAA UALIMU,NI LAAANA
 
Tulia Sasa mkuu vuta pumzi, hapo cha kufanya kopa benki, baada ya hapo nenda Bayport kopa mpaka moja ya Tatu hakikisha kadi yako mshahara unaingia buku tano tu, baada ya hapo usiache kazi mwenyewe fanya kudoji kazini mwezi mzima bila taarifa utakuta barua ya kufukuzwa kazi juu ya Meza ya mkuu wa shule ndipo lengo lako litakuwa limetimia maana mkopo una Bima kwahiyo watajijua na mwajiri wako na Bayport itakuwa imekula kwao

Fanya biashara ya huduma za kifedha na ufugaji wa kuku kienyeji hutajuta baada ya miaka mitatu pesa yako ya mwezi utakuwa mshahara wa walimu watano wenye TGTS Wasio kuwa na madeni yoyote
Mwalimu mpwayungu vipi pole na aibu za kuumbuliwa jana
 
sasa shida ni huo mshahara wenyewe unakuta analipwa 710,000 ila makato yote pamoja na CWT, mwenge, halmashauri, makato ya kumtunza mwalimu mkuu akinunua kiroba cha unga na dagaa debe anabaki na 15000

na hapo akiziba pancha baiskelli mara kadhaa anabaki mkiwa.

KATAA UALIMU,NI LAAANA
Naoana mpaka makato ya walimu

Obviousily wewe ni ni mwalimu
 
Mpaka mpwayungu village anatoa huo ushauri maana anazijua Kona Kona zote za ualimu

Conclusively am obliged to say that he is a teacher
Hiyo Haina doubt mkuu
Mpwayungu village ni mwalimu ngaxi ya diploma
Screenshot_20230403-182040.jpg
 
Naoana mpaka makato ya walimu

Obviousily wewe ni ni mwalimu

Usikaze mshipa kijana wangu.

najua unatamani kuwa kama mimi Geologist ila ulifeli badae ukatupwa ualimu unateseka na kuhangaika na maisha.

Tuma namba hapa nikutumie hela ya mboga walau uache kula dagaaa na dona kila siku

KATAAA UALIMU NI LAAANAAAA
 
sasa shida ni huo mshahara wenyewe unakuta analipwa 710,000 ila makato yote pamoja na CWT, mwenge, halmashauri, makato ya kumtunza mwalimu mkuu akinunua kiroba cha unga na dagaa debe anabaki na 15000

na hapo akiziba pancha baiskelli mara kadhaa anabaki mkiwa.

KATAA UALIMU,NI LAAANA
Duh! Sio fair. Wanafanya kazi kubwa sana
 
habarini wanajamvi?

Nimekuwa nwalimu wa miaka 5 sasa katika mkoa X na shule nayofundisha kwakweli si mbaya sana ina mazingira mazuri kiasi.Lengo la kuja hapa JF ni kuomba ushauri juu ya hatma ya maisha yangu.

Najua kila mtu hajawahi kutosheka juu ya mishahara yao lakini kwa sisi walimu naona hali inazidi kuwa mbaya, Serikali inatukandamiza kwa makato ya siyo ya lazima kama kuchangia mwenge na tunalazimishwa eti mwenge ukija mkoani kwetu lazima walimu tuwepo kuupokea.

kwanini kila kitu mpka sisi walimu tushiriki aiseee, nimechoka kuona kada yangu pendwa imekuwa inadharaulika na serekali kwa kutupiwa kila kitu cha kisiasa matokea yake walimu tumekuwa watu wa mkakati kwa wanasiasa ili kufanikisha azma yao.

Natamani kuacha ualimu ila naogopa wapi ntapata chanzo kingine cha mapato,na sitaki mikopo kabisaa

Naonmbeni ushauri wa wa biashara gani ya kufanya ili niondoke kwenye ualimu

(Sitaki kufungua kijiwe cha tuisheni, walimu tumekuwa tukiona tuisheni kama ni njia pekee ya kujiajiri SITAKIII)

msaada jamani
Nimejaribu kuliuliza roboti la chatgpt na haya ndio majibu yake

Pole sana kusikia hali yako ya kazi imekuwa ngumu. Hapa kuna baadhi ya ushauri ambao unaweza kuutumia katika kujaribu kubadili hali yako:

Angalia vipaji vyako na ujuzi - Kabla ya kuchagua biashara unayotaka kuanza, angalia kwanza vipaji vyako na ujuzi wako. Kuna biashara nyingi ambazo unaweza kufanya kwa kutumia ujuzi wako kama vile uandishi wa nakala, uchapishaji, uchambuzi wa data, uuzaji mtandaoni, na zaidi.

Fikiria kujifunza ujuzi mpya - Kujifunza ujuzi mpya inaweza kukusaidia kubadili kazi yako au kuanza biashara mpya. Unaweza kuangalia kozi mtandaoni au kuhudhuria mafunzo yaliyoandaliwa katika eneo lako.

Fikiria kuanzisha biashara ndogo - Unaweza kuanza biashara ndogo kwa kutumia ujuzi wako na mtaji mdogo. Kwa mfano, unaweza kuanza kuuza bidhaa au huduma mtandaoni, kufungua duka la vitafunio, kuendesha huduma za ukarabati, nk.

Tafuta fursa za ajira zinazofaa - Unaweza kutafuta kazi nyingine ambazo zinaendana na ujuzi wako na maslahi yako. Angalia tovuti za ajira au tuma maombi ya kazi kwa makampuni yaliyo katika sekta unayopenda.

Tafuta msaada - Unaweza kutafuta msaada kutoka kwa watu wengine, kama vile marafiki, familia, au wataalamu wa kibiashara. Unaweza pia kujiunga na vikundi vya biashara au mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujenga uhusiano na kupata fursa.

Kumbuka, kubadili kazi au kuanza biashara ni jambo la kibinafsi na linahitaji utayari na jitihada. Ni vyema kuweka mipango madhubuti, kuwa na malengo ya wazi, na kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi yoyote.
 
Tulia Sasa mkuu vuta pumzi, hapo cha kufanya kopa benki, baada ya hapo nenda Bayport kopa mpaka moja ya Tatu hakikisha kadi yako mshahara unaingia buku tano tu, baada ya hapo usiache kazi mwenyewe fanya kudoji kazini mwezi mzima bila taarifa utakuta barua ya kufukuzwa kazi juu ya Meza ya mkuu wa shule ndipo lengo lako litakuwa limetimia maana mkopo una Bima kwahiyo watajijua na mwajiri wako na Bayport itakuwa imekula kwao

Fanya biashara ya huduma za kifedha na ufugaji wa kuku kienyeji hutajuta baada ya miaka mitatu pesa yako ya mwezi utakuwa mshahara wa walimu watano wenye TGTS Wasio kuwa na madeni yoyote
bima ya mkopo ni against Kifo na permanent disability,ukiacha au kuachishwa kazi Mkopo unaulipa kama kawaida-Benk husika wakikutafuta na kukupata na ukapelekwa Mahakamani lazima utalipa.
 
Back
Top Bottom