Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

Sitaki Ualimu, nimechoka naombeni ushauri

Ni kwel inakera.ila usiache kazi mdogo wangu.piga kazi na jiongeze na izo bizness nyingine.halafu ukitoa iyo buku tano ya mwenge na kwenda kuupokea mwenge hautapungukiwa chochote.KWA MSISITIZO USIACHE KAZI
Sahihi

Mtaani kunahitaji uzoefu asije akaja huku ,akaaza kutamani kurudi Tena kazini
 
Hii njia niliitumia mwaka 2012 baada ya kuchoka ualimu.so nilikopa NMB,CRDB na Posta Bank..20M in total..nikaenda chuo kikuu X nikasoma Banking and finance nilipomaliza 2015 nikaajiliwa kwenye private company X hadi 2021...nikaacha now Nina migodi yangu ya dhahabu mkoa X...Maisha mazuri sana km ukithubutu...NB nimefanya story iwe fupi japo nimepitia changamoto nyingi mzito
Hongera, ulifanya kazi kwa miaka mingapi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
habarini wanajamvi?

Nimekuwa nwalimu wa miaka 5 sasa katika mkoa X na shule nayofundisha kwakweli si mbaya sana ina mazingira mazuri kiasi.Lengo la kuja hapa JF ni kuomba ushauri juu ya hatma ya maisha yangu.

Najua kila mtu hajawahi kutosheka juu ya mishahara yao lakini kwa sisi walimu naona hali inazidi kuwa mbaya, Serikali inatukandamiza kwa makato ya siyo ya lazima kama kuchangia mwenge na tunalazimishwa eti mwenge ukija mkoani kwetu lazima walimu tuwepo kuupokea.

kwanini kila kitu mpka sisi walimu tushiriki aiseee, nimechoka kuona kada yangu pendwa imekuwa inadharaulika na serekali kwa kutupiwa kila kitu cha kisiasa matokea yake walimu tumekuwa watu wa mkakati kwa wanasiasa ili kufanikisha azma yao.

Natamani kuacha ualimu ila naogopa wapi ntapata chanzo kingine cha mapato,na sitaki mikopo kabisaa

Naonmbeni ushauri wa wa biashara gani ya kufanya ili niondoke kwenye ualimu

(Sitaki kufungua kijiwe cha tuisheni, walimu tumekuwa tukiona tuisheni kama ni njia pekee ya kujiajiri SITAKIII)

msaada jamani
ndugu yangu isiache kazi,buni mradi wowote aidha duka au kilimo na ufugaji,,,sawa mshahara ni mdogo sana,lakini kumbuka unakopesheka kama mfanyakazi wa serikali,bima ya afya unayo na unawekewa mafao ya uzeenu na NSSF au taasisi nyingine,,,cha muhimu usitegemee kipato cha ualimu pekee,,,,so biashara au kilimo kikichanganya,na ukaona changamoto zake na kuzimudu,basi hapo unaweza kuacha kazi,"ukiacha kazi kizembe na mke atakukimbia kizembe"
 
Tulia Sasa mkuu vuta pumzi, hapo cha kufanya kopa benki, baada ya hapo nenda Bayport kopa mpaka moja ya Tatu hakikisha kadi yako mshahara unaingia buku tano tu, baada ya hapo usiache kazi mwenyewe fanya kudoji kazini mwezi mzima bila taarifa utakuta barua ya kufukuzwa kazi juu ya Meza ya mkuu wa shule ndipo lengo lako litakuwa limetimia maana mkopo una Bima kwahiyo watajijua na mwajiri wako na Bayport itakuwa imekula kwao

Fanya biashara ya huduma za kifedha na ufugaji wa kuku kienyeji hutajuta baada ya miaka mitatu pesa yako ya mwezi utakuwa mshahara wa walimu watano wenye TGTS Wasio kuwa na madeni yoyote
Afanye biashara yoyote atakayoipenda, lakini pia shame kutoka huo Mkoa na aende kufanya shughuli ktk Mkoa mwingine.
La sivyo TRA, polisi, nk. hawatamuacha salama

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tuliza akili, linganisha mshahara wako na mkia wa ng'ombe, ukikatwa ng'ombe anakosa balansi na hawezi kukimbia kwa speed kubwa. Ridhika na hicho kidogo ila cheza na mikopo. Ukicheza kwa makini utatoboa Ila kazi usiache.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
AKOPEE MTAJI...aanzishe biashara akiona inamlipaaa aache kazi akaisimamie mwenyeweee! kikiumana kwenye biasharaa bhasi awe mpole tuu... maana anaweza anzisha kilimo au biashara huku ameshaacha kazi vikafail
 
Back
Top Bottom