Bagrameshi
Senior Member
- Jun 22, 2012
- 131
- 43
Habari za muda huu wana JF,
Mimi ni mwalimu wa shule za msingi, nimefanya kazi hii takribani miaka 7 sasa tangu 2009 hadi sasa. Pamoja na juhudi kubwa sana za kusaidia kizazi cha watanzania bado watanzania hasa watawala wameendelea kutudhalilisha walimu badala ya kutusaidia hasa kiuchumi. Hakuna motisha yoyote, tunafanya kazi kwa woga sana, tunaonekana kama panzi wakati ushuda wa walio wengi unaonyesha kuwa watu wengi tumefanikiwa baada ya kupitia mikononi mwa walimu.
Ndugu wana JF, Kilichonisukuma kuandika haya ni kuomba ushauri kwenu kwa sababu kwa sasa mshahara wangu wa mwezi baada ya makato yote ni 430000/= sasa natamani ndani ya miaka 5-10 ijayo niache kazi. Najua humu kuna wana uchumi na wajasiliamali wengi sana. Nipeni ushauri wa kiuchumi namna naweza kuanzisha mambo yangu na nikafanikiwa ndani ya miaka 10 ili nijijenge kiuchumi bila kuteteleka.
Natambua umuhumu wa kazi kama hauna kazi kwa hiyo wadau pamoja na msoto katika elimu naamini inawezekana kuwa na mambo makubwa na kutimiza ndoto zetu.
NAHESIMU MAWAZO YA KILA MMOJA.
asante!!!