Sio kila mwanaume 'anaibiwa' mtoto

Sio kila mwanaume 'anaibiwa' mtoto

Kwa miaka hii kama mwanaume ni mjanja ni vigumu sana kuchomekewa mtoto
Kwa hali ya kawaida mtoto kama si wako lazima utajuwa tu
Yale mambo ya kizamani eti huyu kafanana na mjomba wa mjomba yake yalishapita
Sasa hivi mtoto anatakiwa awe na sura mbili tu
Asipofanana na mama basi afanane na baba au ale pande zote
Sasa unakuta mtoto hafanani na mama pia baba ndio kabisaa hawajaendena kwa lolote hapo lazima hiyo sura itakuwa na mwenyewe tu!
 
Ukiona mtu hadi anaamua kuzaa nje ya ndoa ujue huyo amepitiliza aisee.
Sometimes watu hufunga ndoa na hali wanakuwa bado hawapo tayari kuacha mambo ya ujana ujana.

Sasa wanafunga ndoa ili iwe nini? Si bora awe mwenyewe atmbeshe hadi achoke.....
kuna bidada mmoja nilikuwa siishi kumshangaa pambafff zake
anatembea na rafiki wa mmewe, hadi mara ya mwisho kumuona alikuwa na mimba ya 6mnths ya huyo jamaa
nilikuwa sielewi kabisa akili zake
naona ndoa zinafanywa seheme ya majaribio kama si ya kuondolea nuksi.
 
Huwezi jua..labda ni makubaliano yake na mumewe...wengine hawana huwezo wa kumimbisha wanatumia marafiki zao kiroho safi...

Ila kweli aisee...kubambikiwa ni uzembe...
mtoto akizaliwa utaona mawifi na wakwe wanakagua masikio, macho na vidole...teh teh teh...
Damu nzito haifichiki...

Kwa miaka hii kama mwanaume ni mjanja ni vigumu sana kuchomekewa mtoto
Kwa hali ya kawaida mtoto kama si wako lazima utajuwa tu
Yale mambo ya kizamani eti huyu kafanana na mjomba wa mjomba yake yalishapita
Sasa hivi mtoto anatakiwa awe na sura mbili tu
Asipofanana na mama basi afanane na baba au ale pande zote
Sasa unakuta mtoto hafanani na mama pia baba ndio kabisaa hawajaendena kwa lolote hapo lazima hiyo sura itakuwa na mwenyewe tu!
 
Huwezi jua..labda ni makubaliano yake na mumewe...wengine hawana huwezo wa kumimbisha wanatumia marafiki zao kiroho safi...
Mioyo ya wanaume ione tu ikidunda ndani ya singlend zao
hainaga maamuzi mepesi kama ya wanawake!!!!
hicho ulichokisema ni ngumu sanaa kwa mwanaume
 
Sasa wanafunga ndoa ili iwe nini? Si bora awe mwenyewe atmbeshe hadi achoke.....
kuna bidada mmoja nilikuwa siishi kumshangaa pambafff zake
anatembea na rafiki wa mmewe, hadi mara ya mwisho kumuona alikuwa na mimba ya 6mnths ya huyo jamaa
nilikuwa sielewi kabisa akili zake
naona ndoa zinafanywa seheme ya majaribio kama si ya kuondolea nuksi.
Kuna mtu akiona hii comment yako atafurahi sana. ngoja nimwite lara 1 umeshalala?
 
Ila kweli aisee...kubambikiwa ni uzembe...
mtoto akizaliwa utaona mawifi na wakwe wanakagua masikio, macho na vidole...teh teh teh...
Damu nzito haifichiki...

Na baadhi ya makabila wana DNA test yao ya kiasili,aisee na mtu hachomoki!!
 
Kuna Mtu wa karibu aligundua yeye si mtoto wa familia ile wiki mbili kabla ya ndoa.
Ilianza kwa utani tu, mchumba wake wakati anatizama albam ya familia yao alimwambia jamaa "hapana bana mbona hufanani na ndugu zako wengine, hebu ongea na mama yako vizuri?" Jamaa akachukulia kama utani, lakini at the same time akaanza ku-recall baadhi ya matukio katika familia.

Ile sindano ilimuingia vizuri, siku ya pili akamfuata Mama yake mdogo na kumueleza, baada ya huku na kule akapewa ramani ya aliko Baba yake (biological). Ile anagonga hodi getini akatokea dada mmoja wa makamo na kumwambia "Karibu sana wala huna haja ya kuuliza tumeshajua ulichokuja kuulizia, wewe ni sehemu ya familia yetu". Kukata story alikuja Baba yake na wakaongea siku nzima!!!

Nachotaka kuwaambia Wanawake ambao wanafikiria au wanadhani wanaweza kuficha Biological father wa Mtoto/Watoto wao wanafanya kosa kubwa sana ambalo linaweza kuwagharimu siku moja.

Dunia ya leo na maendeleo ya leo ni ngumu sana kulificha hilo kwa kipindi kirefu.................usije shangaa unaumbuliwa Instagram, Watsapp au kwenye other social network.

Ukiamua kuzaa na Mtu iwe wazi na ajue, ukipata kwa bahati mbaya mwambie mhusika ajue. Usije kujaribu kufanya hilo kwenye ndoa utavuruga familia, mtoto au hata ukoo.

Umeongea kitu kikubwa sana mimi namjua msanii mmoja wa bongo fleva aliwahi kuambiwa kama utani vile mtu anapita barabarani akaambiwa tu 'unamuona yule mzee? ndio baba yako halisi yule' unaweza imagine aliathirika kiasi gani ..
 
Na baadhi ya makabila wana DNA test yao ya kiasili,aisee na mtu hachomoki!!

kabisa kabisa ...kuna watu vidole vyao wanavujua au masikio yao wanayajua.....nasikia kuna makabila ukileta mtoto sio wao ataugua weee hadi watajua.....nilisikia pia wazee wanasema ukimchapa mtoto na akakimbilia nje ujue sio wa kwako..wa kwako atakimbilia ndani....hahaa haa sijui ukweli kiasi gani
 
Umeongea kitu kikubwa sana mimi namjua msanii mmoja wa bongo fleva aliwahi kuambiwa kama utani vile mtu anapita barabarani akaambiwa tu 'unamuona yule mzee? ndio baba yako halisi yule' unaweza imagine aliathirika kiasi gani ..

Unajua Wanawake wanachukulia hili kama jambo dogo lakini lina athari kubwa sana baadaye, fikiria Mtoto au hata Mtu yeyote kwenye familia ajue, sidhani kama siri inaweza kubaki ndani. Unaweza kuona jambo kama la mtoto soon linaweza kuporomosha familia ya Wiyelele na ile ya 'mchepuko' wake.

Ingekuwa suala la 'biological father' ni rahisi hivyo pengine hata mwenyezi Mungu angeweka option ya kutaga mayai, kuatamia na kutotoa!

Mwaka flani nilikuwa natazama DW tv, kuna documentary inamuonesha Mama wa Kijerumani aliyepata mtoto kwa kupandikizwa mbegu za kiume huko Sweden ingawa hakuwa na tatizo lolote la kizazi. Baadaye Mtoto akaja kugundua namna alivyopatikana..................alikuwa frustrated vibaya sana, swali llake ni why Mama yake atumie njia hiyo ambayo imemfanya kutomjua 'Baba yake Mzazi'?
 
Last edited by a moderator:

Kuna mtoto wa kitanzania alitelekezwa hospitali ya mwananyamala.....akawa adopted na wazungu huko Uholanzi..alipokuwa mtu mzima akarudi bongo kuja kutafuta mama yake halisi ili apate 'answers' zinazomsumbua..
 
kabisa kabisa ...kuna watu vidole vyao wanavujua au masikio yao wanayajua.....nasikia kuna makabila ukileta mtoto sio wao ataugua weee hadi watajua.....nilisikia pia wazee wanasema ukimchapa mtoto na akakimbilia nje ujue sio wa kwako..wa kwako atakimbilia ndani....hahaa haa sijui ukweli kiasi gani

Haya mambo yapo,na kuna wengine wanaandaa sherehe kisha mtoto analazwa asipoamka katika muda ambao wameuset wao basi huyo si wao,aisee na hii kitu ina work kabisa. Hiyo ya mtoto kukimbilia ndani ni kweli sababu ndo tabia zao,mtoto wa nyoka ni nyoka.
 
Ivi tatizo Hili lipo kwenye race nyingine? Nahisi Kama waafrika tumezidi ni mtazamo tu.
 
Kwa kweli mwanamme wa kumkataa mtoto,hatokaa apate heshima Yangu hata uwe na hela mpk mashavuni.mpk akili zihame toka chini zinakowazia mpaka juu,....
 
Race nyingine till death ni msamihati...huku kwetu ndoa ni kifungo...ukiingia hakuna kutoka uta fall in and out of love humo humo...kwa wenzetu ndoa kudumu mwaka si kitu kigeni...

Ivi tatizo Hili lipo kwenye race nyingine? Nahisi Kama waafrika tumezidi ni mtazamo tu.
 
Ivi tatizo Hili lipo kwenye race nyingine? Nahisi Kama waafrika tumezidi ni mtazamo tu.

umenikumbusha kuna mhindi mmoja aliniambia hapa TZ waswahili wengi utasikia wanasema 'kwa baba tupo wane na kwa mama tupo sita' akaniambia hasikii hayo kwa wahindi wenzake....ila kwa waswahili kawaida
 
Kuna mmoja huku niliko analea mtoto si wake na anavompenda ni hatari.Ametengana na mama mtoto na huyo mtoto kampeleka kwao moshi akiamini kabisa ni mwanae wa damu..!!nikimuangalia,namuonea hadi huruma.Maana ni anampenda mtoto huyo na mtoto mwenyewe ni wa kiume sasa...Ila wamama wengine ni hatari kwa kweli.
 
Back
Top Bottom