Sio kila mwanaume 'anaibiwa' mtoto

Sio kila mwanaume 'anaibiwa' mtoto

Kwa ishu ya Wiyelele ni nzito na ndiyo maana watu hawakubali uamuzi wake.....kwanza wote walikuwa ndani ya ndoa wakati wanafanya maamuzi ya kupata mtoto wakiendeshwa na kipofu mapenzi.......ingekuwa huyu mtoto walimpata kabla ya hawa wote kuwa ndoani.....kidogo ingepunguza maumivu......ila kitendo cha kuzaa wakati unajua umeoa...umeolewa si swala jepesi.......

Pili mfikilie huyu mwanaume ambae yupo kifua mbele kwa ndugu...jamaa...na marafiki akijidai na binti yake wa pekee....afu leo aambiwe siyo binti yake......unadhani nin atakifanya huyu mwanaume...........
 
Last edited by a moderator:
Kawaida ya wanawake wote tukishatendwa na mwanaume aliyekupa mimba huwa tuna hasira sana na chochote tunaweza kuamua ila ukweliii ubaki tu kila mtoto anayo haki kisheria kumtambua baba yake mzazi hata Kama alimkana mtoto

hata kama anahaki bt kwangu haitakaa ikatokea.. alimkataa leo ajilete nitamtukana matusi yote dunian
 
The Boss naomba urejee kisa hiki kilichowahi kuandikwa katika gazeti la Jitambue na mimi kama mdau wa gazeti hilo nikaja kukiweka hapa;

https://www.jamiiforums.com/mahusia...6-binti-aliyeitoa-jasho-familia-kwa-visa.html

Naomba nikiri kwamba, haya mambo ni magumu tfauti nawatu wanavyofikiria.

Niliwahi kusikia mahali kwamba hapa nchini kuwa baadhi ya makabila ni lazima mke azae nje ya ndoa japo mtoto mmoja ili ile familia ikifanyiwa jambo baya la kuangamiza ukoo kiuchawi ,basi abaki japo mtoto mmoja wa kujenga ukoo mwingine, sasa sijui huo ukoo utatambulika kwa jina lipi, kule mtoto baba halisi wa mtoto alipotokea au jina la ukoo wa huyu baba aliyebambikiwa......

Swala la watoto wa nje ya ndoa waliozaliwa kwa ule mtindo wa kitanda hakizai haramu, wanalindwa sana na mila tangu kale na baba hata akiujua ukweli haruhusiwi kulalamika wala kumsusa, sana sana atapendwa kuliko watoto wote maana atakuwa akilindwa na mama kwa nguvu zote.

Kule Ghana kwa mfano ufalme huwa unarithishwa kwa mjomba, yaani mtoto wa dada wa mfalme, yaani huyu anaaminika ametoka kwenye tumbo la binti wa mfalme, lakini mtoto wa mfalme hawezi kurithi kwa sababu ya hofu ya ufalme kutoka nje ya ukoo, kwani hapa mke wa mfalme haaminiki anaweza kumbambikia mfalme mtoto kutoka ukoo mwingine.....

Ngoja kwanza niishie hapa

Nitarudi
 
Mmmh, inategemea babu.

Ndo umeenda huko duniani, hujapata mtoto, lazima urudi kuulizia.

Mie mwanangu hata kama ni katikati ya bahari, nitamfukua. Bahati ni mwanamke, so 100% nna uhakika na siwezi letewa mamluki bila kujua.

Ila kuna workmate naye ana tatizo kama la wiyelele, mtoto wa kiume around 16yrs. Huwa anampa hela ndogo ndogo kila wakionana, nahisi hata mtoto anahisi kitu.

Hii mada siyo rahisi kiasi hicho. Lazima mtu apime vizuri matokeo ya kujaribu kuweka wazi suala la baba wa mtoto au mtu kudai mtoto aliyemzaa na mke wa mtu.

I would rather consider the baby lost than making an attempt to claim him. Better commit one sin!
 
Ni ngumu sana kujua kama mtoto si wako hasa akifanana na mama yake.

Hamna cha sixth sense wala nini sababu hakuna kitu ambacho kitakufanya uanze kuwaza kuchunguza kama ni wako maana mtakuwa mnaishi vizuri na mke na watoto,unless litokee tukio ambalo lipelekea uwe suspicious otherwise mtaishi miaka yote bila mume kujua.

Possibility za kutokea a suspicious event nazo ni ndogo sababu utakuwa una muamini mke kwahiyo mambo kama haya hata kuya fikiria nafsini mwako utaona ni kufulu.

Binafsi sioni faida ya jamaa kumtaka mwanae.Ukiangalia vizuri hasara ni kubwa mno kuliko faida,yani atakuwa ana jiongezea dhambi ya pili sababu atafuruga hizo familia na kusababisha mpasuko mkubwa sana,bora apotezee tu.
 
Huu ni ukweli mchungu,kila jambo linapofanyika lina matokeo yake,kulipa gharama inahitajika ili kila kitu kiwe sawa.Kinga ni bora kuliko tiba,kuepusha gharama hizi bora kila mtu awe mwaminifu kwa mwenzake. Ukweli haupingiki lazima huyo mtoto atakuwa tofauti kila kitu na wenzake coz naye ana vinasaba vyake kutoka kwa baba yake,na pengine anaweza kuwa baraka au tatizo katika familia husika
 
Mtoto wa nyoka apelekwe kwa nyoka akilelewa na jongoo atasumbua tu

Kuna familia naijua mama alichepuka akaleta mtoto wa njee huwez amin watoto wa baba wa ndoa wanafanana hadi kucha yule wa mchepuko aliyebambikiwa yuko tofaut na wenzie kuanzia tabia hadi mwili

Na mungu alivoumbua watoto halali wana akili mno ila yeye kilaza

Imefika kipindi akawa atambulishwi kama sehemu ya familia
 
Bosi unajikontradikti...wewe si ndio unasemaga kila mtoto alelewe na mama yake?
Au nimekuchanganya na mtu mwingine...
 
wakati angepelekwa kwa baba yake asinge jiona tofauti huko na asingepata 'madhara'
 
I beg to differ...watoto wa nje wanaolelewa na baba wa kubambika wanakuwa na akili si mchezo...

Nina mifano mingi ya watu maharufu ila si vizuri kuwataja humu ntawadhalilisha...

Ila tatizo ndio hilo...uwa wanakuwa sura na tabia tofauti na wenzao...

Mtoto wa nyoka apelekwe kwa nyoka akilelewa na jongoo atasumbua tu

Kuna familia naijua mama alichepuka akaleta mtoto wa njee huwez amin watoto wa baba wa ndoa wanafanana hadi kucha yule wa mchepuko aliyebambikiwa yuko tofaut na wenzie kuanzia tabia hadi mwili

Na mungu alivoumbua watoto halali wana akili mno ila yeye kilaza

Imefika kipindi akawa atambulishwi kama sehemu ya familia
 
Bosi unajikontradikti...wewe si ndio unasemaga kila mtoto alelewe na mama yake?
Au nimekuchanganya na mtu mwingine...

Sawa sawa na mama yake na baba yake halisi
hata kama wanaishi mbali mbali
ninachopinga ni kumuaminisha mtoto baba wake wa kambo ndo baba yake halisi
 
Mmmh, inategemea babu.

Ndo umeenda huko duniani, hujapata mtoto, lazima urudi kuulizia.

Mie mwanangu hata kama ni katikati ya bahari, nitamfukua. Bahati ni mwanamke, so 100% nna uhakika na siwezi letewa mamluki bila kujua.

Ila kuna workmate naye ana tatizo kama la wiyelele, mtoto wa kiume around 16yrs. Huwa anampa hela ndogo ndogo kila wakionana, nahisi hata mtoto anahisi kitu.
labda unataka kuvunja ndo ya watu kwa vile yako umeona inayumba,ingawa unamwona mtoto ni wako dah nimekosa hata la kusema
 
Focus yako nimeipenda umeenda extra mile,inawezekana kweli mwanamke alivyoumbwa Psychologically haoni negative effect ya kumbambikia mwanaume mtoto hapa ndo ninapojiuliza why?wanafikiriaje hawa viumbe?
 
Ndo maana nikasema sio kila mwanaume
wapo wanaoibiwa hawajui but wengine huwa wana kama sixth sense hivi
au strong connection.....labda Pasco aje atusaidie.....

kuna mzee alibambikiwa mtoto.....mtoto wacha augue hadi kuhitaji damu..ikakutwa damu ya baba sio ya mtoto
gruop tofauti hadi baba akajua huyo mtoto sio wake kabambikiwa

Hivi grupu la mtoto ni lazima lifanane na la baba?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom