Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,741
- 92,197
MBINU 7 MAKINI ZA KULEA MTOTO MAZINGIRA YA MJINI
Malezi ya mtoto katika mazingira ya mjini yamekuwa changamoto kubwa kwa wazazi wengi. Mtoto wa Mjini anakua katika dunia yenye mchanganyiko wa tamaduni, mitazamo, teknolojia, mitandao ya kijamii na makundi mbalimbali ya watu.Hii Tofauti na zamani wakati wengi wetu tunakua.
Zama hizi mtoto anaweza kukutana na taarifa na tabia mbalimbali kupitia simu, televisheni, shule, marafiki na mitandao ya kijamii bila mzazi kujua. Kwa hiyo, malezi ya kisasa hayawezi kutegemea ukali pekee. Yanahitaji uelewa wa saikolojia, sosholojia, akili ya kijamii na uelewa wa mazingira.
Na ndio Maana leo Mtibeli nikasema niulete huu mjadala ili wote tujifunze.
Bila kupotezeana muda, Hizi ni mbinu saba muhimu ambazo mzazi anaweza kutumia kumlea mtoto awe mwenye maadili mema katika mazingira ya mjini;
1. JENGA UHUSIANO MZURI NA MTOTO KABLA YA KUWEKA SHERIA.
Nguzo kuu ya familia mi upendo. Na unaposema upendo unazungumzia mahusiano mazuri yanayozingatia ukweli, haki, na akili. Kitibeli zaidi.
Mtoto anayejisikia kupendwa, kusikilizwa na kueleweka huwa rahisi kuongozwa kuliko mtoto anayelelewa kwa hofu pekee. Yaani Kikoloni, kibabe, matusi na vipigo.
Mzazi anapaswa kutenga muda wa kuzungumza na mtoto, kumsikiliza na kumruhusu kuuliza maswali. Mtoto anapofanya kosa, si kila wakati lazima uanze kwa kumuogopesha au kumdhalilisha.
Badala yake, mzazi unaweza kumuuliza:
“Kwa nini umefanya hivi?”
“Umejifunza nini kutokana na kosa hili?”
“Unafikiri ungeweza kufanya nini tofauti?”
"Ulikuwa una wazo gani?"
Kwa mtazamo wa saikolojia, mtoto anayekuwa na uhusiano salama na mzazi huwa na uwezekano mkubwa wa kumjulisha na kuongea na mzazi anapokutana na changamoto.
Mzazi unatakiwa kuwa mtu ambaye mtoto anaweza kumwambia ukweli hata pale anapokuwa amefanya kosa.
2. MFUNDISHE MTOTO KUSOMA WATU NA na MAZINGIRA.
Mtoto wa mjini atakutana na watu wa aina nyingi. Ni muhimu kumfundisha mtoto ujuzi wa kuwasoma na kutambua watu na mazingira. Si kila mtu anayesema mambo mema ana nia nzuri, na si kila mtu anayejionyesha kuwa rafiki ni rafiki wa kweli.
Hivyo, mtoto anahitaji kufundishwa akili ya kijamii. Fid Q aliimba ielewe mitaa ielewe sana. Mfundishe mtoto kitaolojia;
Mfundishe kujiuliza:
“Mtu huyu anataka nini kwangu?”
“Kwa nini ananiambia nifanye hivi?”
“Je, ninajisikia salama nikiwa na mtu huyu?”
“Ninaweza kumwambia mzazi wangu kuhusu jambo hili?”
Hii haimaanishi kumfundisha mtoto kuwa na hofu au kutowaamini watu. Maana yake ni kumjengea uwezo wa kutambua tabia, nia, shinikizo na mazingira hatarishi.
Mtoto mfundishe kukataa jambo ambalo analiona sio sahihi. Kusema hapana bila kujali watu watasema nini au watamuonaje.
3. MFUNDISHE MAADILI KWA VITENDO, SI KWA MANENO PEKEE.
Watoto hujifunza sana kwa kuangalia kuliko kusikiliza. Hili lipo kisaikolojia.
Kila siku nasemaga hapa jambo ambalo wengi tunabishana mpaka kutukanana. Asilimia tisini ya watoto wasio na maadili wamefundishwa na wazazi au walezi wao. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto hujifunza kwa mzazi au mlezi kupitia matendo ya wazazi au walezi kuliko maneno.
Kama mzazi anataka mtoto awe mwaminifu, mzazi naye anapaswa kuonyesha uaminifu.
Kama anataka mtoto aheshimu watu, mtoto anapaswa kuwaona wazazi wakiheshimu wengine.
Kama anataka mtoto awe na huruma, mtoto anapaswa kuona huruma ikitekelezwa nyumbani.
Kwa mfano, mtoto akifanya kosa, mfundishe kulikubali na kulirekebisha. Akimkosea mtu, mfundishe kuomba msamaha. Akiharibu kitu, mfundishe kuwajibika.
Maadili yanapokuwa sehemu ya maisha ya kila siku, mtoto hayabebi kwa sababu anaogopa adhabu; anayabeba kwa sababu yanaanza kuwa sehemu ya utu wake.
4. USIPINGANE NA UTANDAWAZI; MFUNDISHE MTOTO KUJIFUNZA MAMBO CHANYA NA KUCHUJA.
Katika dunia ya leo, ni vigumu kumzuia mtoto kabisa asikutane na mitazamo tofauti.
Atakutana na muziki, filamu, mitandao ya kijamii, marafiki na tamaduni tofauti. Tena bahati iliyombaya trends nyingi huko mitandaoni zimeshikiliwa na machawa, wasanii wakaa uchi na watu wa aina hiyo.
Badala ya kumwambia kila kitu cha nje ni kibaya, mzazi anapaswa kumfundisha mtoto kufikiri.
Mtoto ajifunze kujiuliza:
“Hiki ninachokiona kinanifundisha nini?”
“Je, ni ukweli au ni burudani tuu?”
“Kwa nini mtu anataka niamini hiki?”
“Je, jambo hili linaendana na maadili ninayoamini?”
Hii inajenga uwezo wa mtoto wa kuchambua taarifa na kufanya maamuzi yake mwenyewe.
Lengo la malezi si kumfanya mtoto asione mambo mabaya kabisa. Lengo ni kumfanya awe na uwezo wa kuyaona na kuchagua uadilifu
5. CHAGUA KWA MAKINI MAZINGIRA NA MARAFIKI WA MTOTO
Mtoto haathiriwi na wazazi pekee. Marafiki, shule, majirani, ndugu na mazingira anayokaa nayo vinaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika tabia yake.
Mzazi anapaswa kujua mtoto wake anashirikiana na nani na anatumia muda wake kufanya nini.
Hata hivyo, si lazima kumtenga mtoto na kila mtu mwenye tofauti naye.
Mfundishe kanuni kama hizi;
“Unaweza kuheshimu tofauti za watu bila kuiga kila kitu wanachofanya.”
Katika jamii yenye mchanganyiko wa tamaduni, mtoto anatakiwa kujua kwamba watu wanaweza kuwa na mila, imani, mitazamo na maisha tofauti. Lakini tofauti hizo zisimuondolee uwezo wa kushikilia maadili yake.
6. MPE MTOTO UHURU UNAOAMBATANA NA UWAJIBIKAJI
Mtoto anayefanyiwa kila kitu anaweza kukua bila uwezo wa kufanya maamuzi.
Kadiri mtoto anavyokua, mzazi anapaswa kuongeza uhuru wake hatua kwa hatua.
Mfumo mzuri ni:
Uhuru → Chaguo → Matokeo → Uwajibikaji.
Kwa mfano, mtoto anaweza kupewa uchaguzi wa kufanya kazi yake ya shule kabla au baada ya chakula. Lakini akichelewesha mpaka muda wa kulala, muda wake wa kucheza unaweza kupungua.
Hapo mtoto anajifunza jambo muhimu:
Uhuru unaambatana na wajibu.
Hii humsaidia kufanya maamuzi mazuri hata pale mzazi hayupo.
7. TENGENEZA UTAMADUNI WA FAMILIA WENYE MISINGI ISIYOBADILIKA
Familia inapaswa kuwa na maadili machache ambayo kila mtoto anayajua na kuyaelewa.
Ni muhimu uweke utamaduni wa familia yenu. Baba, mama na watoto.
Msiishi kiholela
Mfano,
Muda wa kula chakula cha jioni lazima muwe wote mezani.
Kuomba kabla ya kula
Mkubwa anatangulia kula ndipo wadogo wafuate.
Wageni wakija watoto baada ya kusalimia waende vyumbani mwao au wasiwepo eneo la sebule.
Usafi na utunzaji wa mali za nyumbani ni jukumu la kila mwanafamilia.
Shida ya mwenzako ni yako. Hata kama kitu ni kidogo vipi mgawane hichohicho.
Baba akiongea hatakiwi kukatizwa, kupingwa.
Kama kuna haja ya mjadala atapingwa siku maalumu ambayo imetengwa kwaajili ya bunge la familia. Ambalo kwa mwezi linaweza kufanyika mara moja. N.k.
Nimechoka.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam