Sinkala (JF Member) kuoa karibuni!

Status
Not open for further replies.
Hii nimeipenda sana hata wale wazazi wanao kataa wakwe dawa yao ndo hiyo hiyo unavimbisha unapewa mzigo bure alafu harusi hulazimishwi.
wewe hata kama mchumbako ni mwislamu nawe mkristo au vice versa halafu wazazi wanatia giza, pachika mimba tu, halafu unatangaza kuwa umepata mchumba mwingine unataka kuoa, wenyewe watanywea
 
Bwana ndo is a life term commitment nadhnai inatakiwa uwe makini sana kabla ya kujicomit kwa wrong person ambaye inabidi kuwa naye maisha yote kwa zuri na baya...mhhhh date mdada kwa miaka walau 15 mtakuwa na watoto walau wawili then unavuta jumla kimya kimya!
hapa powa hata watoto watatu siyo mbaya
sio zile mmekutana miezi sita ndoa then baada ya miezi sita imevunjika, aibu
 
Kesho yake unamletea vito kama mkufu au pete ya Gold anazima fegi wewe unaendeleza libeneke.
au kesho yake unamtoa out ila husiende vile viwanja vyako ulivyovizoea unaweza shangaa kinatokea kimeo uko kinakushika bega, ndoa inasambaratikia bar, ni soo hata kuita wazee kusuluhisha hunakosa ujasiri
 
ahongereke huyo sinkala (maana simfahamu). nilitangaza humu nami natafuta mchumba sijapata response ya maana. yaonyesha humu hakuna totoz.
 
au kesho yake unamtoa out ila husiende vile viwanja vyako ulivyovizoea unaweza shangaa kinatokea kimeo uko kinakushika bega, ndoa inasambaratikia bar, ni soo hata kuita wazee kusuluhisha hunakosa ujasiri

Yaliisha nikumba hayo nikamkana mtu eti dada umenifananisha nini? Vumbi lake acha tu!
 
Mkuu hongera sana
ila wasiliana na mchungaji muondoe lile neno
kwa shida na raha....ile ni laaana...
Wengine baada ya ndoa wanasema raha najipa mwenyewe shida nimemwachia mke/mume wangu...we.........ondoa hilo fasta
send special request else ntakuona....
 
...wanasema binadamu hakamiliki ila kwa mambo matatu,... kuzaliwa, kuoa/kuolewa na kufa...

na wengine wanasema;

... "A man is incomplete until he is married. After that, he is finished!"...

mimi nasema; Sinkala, ...kila la kheri!
 
Uamuzi mzuri na ni wakiume hasaa!
Tujulishane tu tarehe,saa na niwapi ili wana JF 2show up.
 
Una data mkuu? Data zangu zinaonyesha tofauti, wengi wanaoa, unless kama unadefine kuoa ni kwenda kwa sheikh, mchungaji au Padri!!

Kwa data nilizonazo (siyo lazima kila mtu azikubali), wengi wanawowa lakini wanaooa ni wachache mkuu (i.e majority of the people do make love)!
 
Last edited:
ukitoka mitaa ya home tu, unatia pete ya ndoa mfukoni, unabaki kuwa bachelor, unaenda zako mabibo hostel au IFM unatangaza uchumba unachukua kitu kitamu kama asali ya nyuki wadogo, mida ya kurudi home unachukua pete yako unatia kwa kidole unarudi kwa mamsapu na tabasamu
acha uhuni...ukware sio sifa.....

Hongera sinkala kwa maamuzi magumu
 
Nasita kukupa hongera.....unatafuta kero kuowa mazee, uliza waliowa wakuambie ukweli....naona wengi tunasepa hicho kipengele....kwanini msiishi pamoja tu....na hata watoto mkazaa kuliko kujivalisha pingu?

Hongera basi kwa kuwa wengi wamekuambia ila I have warned you with your decision in the first place

Mas

Rafiki acha kumdanganya mwenzako,
 
Pamoja na kukupa hongera zangu na pia pokea shairi hili.
[1]
Owa s'andame hadaa, moyo ukahadaiwa
Owa anaye kufaa, mke mwenye kusifiwa
Owa upate kuzaa, kama ulivyozaliwa
Owa ukijaaliwa, mupendane na mkeo

[2]
Owa aliye na kheri, muandamane kwa dini
Owa yai la johari, litiye nuru nyumbani
Owa mdomo mzuri, ukupambie lisani
Owa ungiye nyumbani, mupendane na mkeo
[3]
Owa moyo wa imani, usozumbua mafuja
Owa usiowe duni, anayeitwa kioja
Owa mtenda wa dini, ndiye mke mwenye haja
Owa utungiwe koja, mupendane na mkeo

[4]
Owa siowe tambara, linukiyalo vibaya
Owa mwanamke jura, mlekeze njema ndia
Owa usiowe sura, kutaka kuzangaliya
Owa mzuri tabiya, mupendane na mkeo
[5]
Owa kijana kitoto, mteshi wa kutekeya
Owa akwandike jito, mwenye kukuhurumiya
Owa usiowe zito, jabali likakwemeya
Owa aliye na haya, mupendane na mkeo

[6]
Owa s'andame uhuni, upate juwa kuzawa
Owa nami natamani, ela sijajaaliwa
Owa utiye chandani, pete uloiteuwa
Owa ujuwe kuowa, mupendane na mkeo
[7]
Owa uvishwe kilemba, na joho na mahazamu
Owa wapate kupamba, ukale twiba na tamu
Owa upambiwe chumba, upate tanganya damu
Owa usijidhulumu, mupendane na mkeo

[8]
Owa kinda la tausi, alo nadhifu mibele
Owa kiini cheusi, chendacho nyuma na mbele
Owa siowe tetesi, apaye watu uwele
Owa aliye lekele, mupendane na mkeo

[9]
Owa ualike watu, wahudhuriye arusi
Owa nawe uwe mtu, mkeo simnakisi
Owa muonyane utu, mukae mutaanasi
Owa mupane mepesi, mupendane na mkeo

[10]
Owa akukubaliye, akuizao siowe
Owa upendane naye, zamani sizo ujuwe
Owa akuridhiyae, mujikubali wenyewe
Owa mukae mutuwe, mupendane na mkeo

[11]
Owa chenye asimini, kikuba cha asiliya
Owa kilo na rihani, na waridi maridhiya
Owa kilicho na shani, na manukato kutiya
Owa ujuwe duniya, mupendane na mkeo

[12]
Owa utukuze cheo, na jina lipate kuwa
Owa apate mkeo, aambiwe meolewa
Owa kama waowao, moyo usiliye ngowa
Owa ujuwe kukuwa, mupendane na mkeo.




Dr Hamza Yosuf Al-Naamani
Doha. Qatar

 
Mkuu yaani bado nafikiria kama vp naweza nikasogeza mbele kabisa 2020 maana ukichelewa kurudi club mtu kanuna yaani we acha tu.

jamani kama JF itakua bega kwa bega nadhani itahamasisha watu kuachana na ukapera, lakini JF isiishie kwenye zawadi tuu, tushirikiane kwenye MAHARI pia kulipa, siku hizi kulipa mahari ni kama biashara, jamani tutaoa kweli?, nadhani tutaishia kujiexpress tu.
 
Bwana ndo is a life term commitment nadhnai inatakiwa uwe makini sana kabla ya kujicomit kwa wrong person ambaye inabidi kuwa naye maisha yote kwa zuri na baya...mhhhh date mdada kwa miaka walau 15 mtakuwa na watoto walau wawili then unavuta jumla kimya kimya!


oooh nooo, khaaa!
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom