Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

Emotions zilivyotapakaa kwenye hii post? Anyway sikumaanisha kumuumiza yeyote, bali kuwa objective.

Why do gays come out?And why straight people don't come out?

Kuna some sort ya kutafuta acceptance kwa wale wa kwanza. Na kwa nini watafute acceptance kama wanaona wako normal?

Ulishawahi kuongea na mwanamke aliyebakwa? Anakuwa emotional over small things.

Kama uko okay for real huwezi kuwa emotional kiasi hiki, sababu kuzaa bila mwenza si ulemavu.
emotions are part of humanity!its normal to symaphathize with other people and having empathy for them au we robot?
 
Econometrician pole kwa kutomfahamu baba yako. Ukweli ni kuwa story yako ndio wanayoipitia watoto wengi sana. Dada yetu mkubwa ana story kama yako. Lakini bahati nzuri yeye alikomaa hadi mama yake akamwambia baba ni nani na yuko wapi. Mwisho wa siku tumemfahamu na tunaishi vizuri sana na dada yetu.

Kinachonoshangaza ni vile wazazi wa kike wanavyowajaza watoto tena umri mdogo sana maneno mabaya kuhusu baba zao. Imagine mtoto wa darasa la pili unamueleza tabia mbaya za baba yake, ili iweje? Unamnyima mtoto haki ya kufurahia utoto wake. Makosa yako na mzazi mwenzako yasikufanye ukampa mtoto mizigo ambayo hsiendani na uwezo wa akili na umri wake. Hapa nao naamini ubinafsi una mapana mengi hata kwa viumbe tulioealeta duniani tunakuwa wabinafsi kwao.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mwanaume ambaye hua nina moyo wa nyama (unapokea furaha na maumivu pia).

Naumia sana kwa mwanaume kumpa Mpenzi wake Mimba n kisha kumtelekeza.If they know impotance of Gender female....??

Unawezae kumpenda mpenzi halafu ukamtenda unyama kiasi cha kumpa ujauzito na kumuacha kama kifaranga cha kuku kweny kundi la mwewe.....?

Kuna hisia za kupendwa/kpenda na hisia za kutamani/kutamaniwa
usimpende mtu kwa 7bu amekupenda mpende kwa kua umempenda pia.Siamini kama mtu amekupenda halafu akakukatili sithadhani.

Pole sana devotha,piga moyo konde mpigani mwanao apate maisha mazuri,kwa huyo baba hata akikubali kuwa na wewe utapata mateso tuu,maana sio responsible katika familia.

Ee Mungu nipe Moyo huu huu wa nyama,wenye utu ndani yake.
 
Umeongea kwa uchungu kilaza. I feel you. Nna rafiki yangu nimeongea nae juzi. Yy ni binti na baba alimpa ujauzito mama ake akiwa anasomea unesi shule ya masista. Yule mama alifukuzwa shule kwa kosa la kupata mimba. Akarudi kijijini kuzaa then baadae akatafuta shule pengne akasoma. Kalea mwanae peke yake.
Big ass kiazi kama unavyomwita alikuja kumtafuta mwanae baada ya kujua kachaguliwa kwenda kusomea udaktari. Huwez amini yule dada alimfukuza baba yake na hata wakikutana barabarani ni shikamoo marahaba no story. Yule dada kwa sasa ni daktari na kaolewa ana watoto wawili. Mzed hata siku ya harusi hakukaribishwa na analalamika wamemuoza binti yake bila kumshirikisha. Watoto wanaokataliwa huwa Mungu anawainua sana baadae.

mkuu to put the records clear mimi sina uchungu wowote kwakuwa sijawai kujutia kutolelewa na kiazi

BTW huyo binti ni mstaarabu sana mpaka shikamoo anampa . .........
 
To be a single is a challenge. I stayed with a man for six good years in a relationship. Fortunately I fell pregnant to him. He told me to abort. Aisee niligoma. Jamaa alikua mbogo na alinitolea maneno mengi sana ya kashfa. Alinitesa sana kipindi cha ujauzito. Kuna wakati usiku nilikua naugua sana but nilikua nahangaika peke yangu usiku kucha yy akiwa kalala pembeni. Kwa neema ya Mungu nilijifungua salama.
Jamaa alinikimbia na kuniacha na mtoto mchanga wa wiki tatu hata arobaini nilikua sijafichikisha. By that time nilikua sina hata kazi masikini ya Mungu. Kula shida,kodi ya nyumba sina. Nakumbuka nilikuja kufukuzwa ninayoishi nikapewa masaa 24 niwe nimehama kama ntakua sijalipa kodi. Nilimweleza mwenzangu akaniambia kopa ukianza kazi utakuja kulipa ila kwa sasa mi sina hela.
Sitasahau jinsi nilivyoumia coz sikuwa na kwa kwenda na mwanamgu. Bahati nzuri kuna rafiki yangu alinikopesha na nilikuja kumlipa baadae nilipopata kazi. Nilimbatiza mwanangu nikiwa sina hata shilingi kumi. Gauni la ubatizo alinunuliwa na rafiki yangu na wasimamizi wa mwanangu ndio walioniandalia chakula. Yy hakutoa hata senti kumi na wala hajui mwanae alivaa nn siku ya kubatizwa.
Ni mengi mno niliyoyapitia lakn kwa neema ya Mungu nimeweza kusimama imara. Binti yangu kwa sasa yuko darasa la pili na nimekua nikimueleza unyama alioufanya baba yake ili atambue kuwa baba ake ni mtu wa aina gani. Sijutii kumweleza ukweli kwan hata akimuuliza baba ake sijali kwan ndiyo aliyoyafanya kwake na kwangu.
Nikimwangalia binti yangu alivyo faraja kwangu huwa nakumbuka mbali sana.

so sad.........by the way sidhani kama ni sahihi kumueleza mtoto hayo unayomueleza mwache ajionee mwenyewe trust me hawa mbuzi hawabadiliki

tena ukizingatia ni mtoto mdogo sana una haribu maisha yake bila ya wewe kujua kunakitu unamjengea ambacho sio kizuri

jitahidi kumlea vizuri kwa nguvu zako zote asihisi utofauti wowote mpaka pale atakapotaka kumjua baba yake ndio umwambie
 
Ni kweli! Badala ya kuyafanyia kazi eti ooh wanawake wengine wabaya wanawajaza maneno watoto! Shame on you hivi mnadhani watoto wajinga si wanaona mambo yanavyokwenda! Una kipato kizuri hutaki kumsidia. akumatambua tu. Ukizeeka au ukaona ana kipao kizuri ndi unamfuata. Akikutolea nje hukawii kuanza oo watoto wa kulelewana na mma wana tabia mbaya Shame on you all mliofanyau mnaotarajiwa kufanya hivy. Be responsible make sure hupati watoto hovyo, kw wanaume hebu jiulize una uwezo waupata watoto wangapi maishani mwako? Chukua tahadhari!

cc

HKigwangalla
 
Last edited by a moderator:
Econometrician pole kwa kutomfahamu baba yako. Ukweli ni kuwa story yako ndio wanayoipitia watoto wengi sana. Dada yetu mkubwa ana story kama yako. Lakini bahati nzuri yeye alikomaa hadi mama yake akamwambia baba ni nani na yuko wapi. Mwisho wa siku tumemfahamu na tunaishi vizuri sana na dada yetu.

Kinachonoshangaza ni vile wazazi wa kike wanavyowajaza watoto tena umri mdogo sana maneno mabaya kuhusu baba zao. Imagine mtoto wa darasa la pili unamueleza tabia mbaya za baba yake, ili iweje? Unamnyima mtoto haki ya kufurahia utoto wake. Makosa yako na mzazi mwenzako yasikufanye ukampa mtoto mizigo ambayo hsiendani na uwezo wa akili na umri wake. Hapa nao naamini ubinafsi una mapana mengi hata kwa viumbe tulioealeta duniani tunakuwa wabinafsi kwao.

Sijamzi maneno mabaya ila namweleza ukweli wa kilichotokea. Na wala sijali hata akimuuliza baba ake kwan ndicho alichokifanya. Simsingizii ila namweleza ukweli binti yake wa kile baba yake alikifanya.
 
Last edited by a moderator:
I am proudly a single parent and i have never regretted my decision to become one. Actually becoming a mother has been one of my greatest achievements so far. Waking up each morning besides my beautiful baby is a true blessing and i always thank God for this beautiful opportunity to be called a mother.

Just to recap a bit about my past.....nakumbuka ilikua mkwa 2010 nilipokutana na huyu kaka and right from the word go i knew he was bad news ila i have always had a thing for "bad boys", huwa niko attracted to such. Basi one thing led to another and all was beautiful & dreamy, everything i would have imagined about him came true. He gave me 6 good months of nothing but pleasure & heaven on earth (hihihihihiii). Anyways to cut the long story short, nikaja gundua i was 2 weeks pregnant surprisingly i was at peace with myself. Right from the word go i knew i wanted to have this baby and one thing i was certain about was that there was no way i was getting this dude involved. So taratibu i started cutting him loose, nikaanza punguza mawasiliano, akitaka tuonane mm nampiga chenga. Kuna kipindi akawa anatamani sana tuonane but mm nikawapa natafuta visingizio, luckily tupo mikoa tofauti & didn't have common friends so interaction was minimal.

Nikiwa almost 9 months pregnant nikakutana na ndugu yake kwa bahati mbaya, huyo ndugu yake si akaenda mwambia jamaa. He flew from wherever he was to where i was to come confirm if i was truly pregnant, tena alinifanyia suprise nisijue kama anakuja. We talked a lot that evening, akaniuliza maswali mengi sana & i never gave him the answers he was looking for. Eventually akarudi zake kwao na life likaendelea. He comes to visit whenever he's around & he supports us as a friend na hadi leo hii sijawahi mwambia kama yy ndo baba wa mtoto wangu.

Ukweli ni kwamba i had my reasons for keeping him at bay about my son's father's identity, hiyo ni siri yangu & i believe that God will understand, hopefully my son will come to understand me when he finally grows up enough to comprehend such things.

Being a single parent has been a blessing in disguise, nimepata breakthroughs za ajabu mno katika shughuli zangu & my life has changed for the best. Lifestyle yangu has changed for good & if i had a second chance at life i wouldn't change a thing about it! I am happy & thankful every single day.

Mnisamehe kwa Kiswaglish changu na story ndefu..hihihihiihihhiii... bottom line is i am a proud parent to the most amazing boy under the sun & would forever be grateful to my "bad boy" for giving me such a beautiful baby, by boy is gonna go places, Mungu atupe uzima tu!

Nimeipenda story yako.

Inshort you are positive about life, thats what others should be.
 
mkuu hatuishi kwa kukariri na huwa binadamu tunatumia vichwa vyetu kufikiri sio kufugia nywele tuu kama wewe unavyofanya

nimeandika hiyo post kwakuwa nimeguswa na koment ya dada yangu aliyekanwa na mume (sitakagi kuliongelea hilo )
binadamu walinielewa (eli 79. zamda .Nandera. and e.t.c) lakini
mbuzi ndio wanaotaka nirudierudie hapa

kwanza nikuonye put my mama out of this she is a genius of her own kind ni msomi ni mrembo na ni mrembo kwelikweli sikui alitoka wapi na yule taira (wanasemaga ndege mjanja ananasa tundu bovu) na amenilelea vizuri kuliko hata ulivyolelewa wewe trust me

mama yangu hajawai kuniambia lolote kuhusu huyu kiazi boya mbuzi kende pi.mbi big fat a.s.s becoz I ddnt show any interest naye wala sijawai kumuulizia na wala sitaki kuuliza mimi ni mtu mzima hata kama walikuwa na ugomvi wao hasira yake ndio anihamishie mimi???????

Tunapiga stori nyingi sana za utotoni nilivyokuwa mtundu n.k hata nilivyoanza kutongoza videmu alikuwa ananishauri vizuri tu bila aibu nakumbuka alikuwa ananiambia
"lets talk like friends nasio kama mtu na mama yake "
elimu aliyonipa ni zaidi ya chuo kikuu

nilichogundua ni kuwa wewe ulimtelekeza mtoto hivyo unaogopa asije akawa na akili kama zangu

hapo kwenye blue
ngoja nikutajie wachache
bill Clinton. 50 cent .mariah carey . B.I.G .p diddy.Armstrong. Tom cruz.jammie fox .jay z .Enrique. jet lee .madonna.Eddie Murphy. Obama. Ronaldhinho.Tupac.kanye west.e.t.c

Dah, kama ukilelewa na single mother unakuwa na matusi namna hii basi kuna tatizo fulani katika malezi. Nimeona single mothers wengi humu ni wajasiri na mashujaa wana determination kuwalea watoto wao vizuri, nashauri wawalee watoto wao wasiwe na hii tabia ya kutoa matusi na kujifanya kijogoo. Mwisho wa siku naona pia kuna character ya kutaka kulipa kisasi au kufidia yale mapungufu ya malezi kwa kujitengenezea mazingira kuwa wewe ni bora zaidi,,, na kuwa kulelewa na single parents ni bora kuliko otherwise,, kitu ambacho kila mtu angependa mtoto alelewe na wazazi wote iwe ndio standard practice.
 
Wanawake na watoto mtegemeeni Mola kama Hajiri aliyemzalia Ibrahimu mtoto Ishmael na kufukuzwa nyumbani
{MWANZO 21:9-20}
 
Soooooo tauching!!! Unaongea maneno ambayo yananiumiza sana moyo wangu, Duh!! Mungu akubariki na akupe nguvu. Iko siku hayo yote utasahau. Mungu ndiye muweza wa yote. Pole sana.

Nashukuru nimemaliza, yaliyobaki ataendeleza mwenyewe na mimi kama mzazi namsaidia pale ninapoona nahitajika si unajua mtoto kwa mama hakui
 
I agree with you 100%. Huwa simwelewi mzazi yeyote anayemweleza mtoto juu ya maovu ya mzazi wake mwingine especially at at tender age. I believe in letting a child form his/her own idea about their parent, sio unamjaza mtoto maneno ya ajabu na kumjengea chuki dhidi ya mzazi wake just because things never worked between the two of you.

Econometrician pole kwa kutomfahamu baba yako. Ukweli ni kuwa story yako ndio wanayoipitia watoto wengi sana. Dada yetu mkubwa ana story kama yako. Lakini bahati nzuri yeye alikomaa hadi mama yake akamwambia baba ni nani na yuko wapi. Mwisho wa siku tumemfahamu na tunaishi vizuri sana na dada yetu.

Kinachonoshangaza ni vile wazazi wa kike wanavyowajaza watoto tena umri mdogo sana maneno mabaya kuhusu baba zao. Imagine mtoto wa darasa la pili unamueleza tabia mbaya za baba yake, ili iweje? Unamnyima mtoto haki ya kufurahia utoto wake. Makosa yako na mzazi mwenzako yasikufanye ukampa mtoto mizigo ambayo hsiendani na uwezo wa akili na umri wake. Hapa nao naamini ubinafsi una mapana mengi hata kwa viumbe tulioealeta duniani tunakuwa wabinafsi kwao.
 
Ok, asante;
Ngoja niseme kidogo tu hapa;

Kwa sababu kadhaa wa kadhaa ikabidi nilianze
Hapo limeshapita tangazo kuwa ........ watoto kwa kuwa wametoka tumboni mwako utajuwa la kufanya...........
Nikaona isiwe tabu, nikajibeba na watoto ni zaidi ya miaka kumi sasa imepita;

Maisha yanaendelea, sijuti kabisa japo nimepita ups and downs kibao,

I thank GOD am happy na maisha yanasonga.

So many things have being said, yangu machache tu, respect and salute u single parents geniveros devota vijance charminglady Zamda Geuka Miss Kim Mamndenyi Babynice NANDERA Victoire msumeno and others.
 
Dah, kama ukilelewa na single mother unakuwa na matusi namna hii basi kuna tatizo fulani katika malezi. Nimeona single mothers wengi humu ni wajasiri na mashujaa wana determination kuwalea watoto wao vizuri, nashauri wawalee watoto wao wasiwe na hii tabia ya kutoa matusi na kujifanya kijogoo. Mwisho wa siku naona pia kuna character ya kutaka kulipa kisasi au kufidia yale mapungufu ya malezi kwa kujitengenezea mazingira kuwa wewe ni bora zaidi,,, na kuwa kulelewa na single parents ni bora kuliko otherwise,, kitu ambacho kila mtu angependa mtoto alelewe na wazazi wote iwe ndio standard practice.

Mbona una generalise mkuu... mie nililelewa na single mom na kwangu ni shujaa... ko ukisema kulelewa na single mom ndio kuna tatizo si kweli
 
Sijamzi maneno mabaya ila namweleza ukweli wa kilichotokea. Na wala sijali hata akimuuliza baba ake kwan ndicho alichokifanya. Simsingizii ila namweleza ukweli binti yake wa kile baba yake alikifanya.

Kwa nini umweleze mtoto mambo yaliyo juu ya uwezo wake? Huoni unamnyima haki ya kufurahia na kuishi kama mtoto?
Mimi naona shida zako na mzazi mwenzako zisikufanye umuumize mtoto kisaikolojia, mtoto wa miaka sita ukimuwleza kuwa baba yake ni m'bwa, hana adabu na hajafanya lolote katika malezi yake ili hali wote mmechangia katika mabaya hayo ni kutomtendea haki mtoto. Mkuze nae atajua tu, lazma ajue kuwa kuna kitu hakiko sawa na aweza kukuuliza au kutafuta mwenyewe ukweli pindi atakapokuwa na uwezo wa kuchanganua mambo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom