duu! umeongea saaana kwa uchungu. Sasa kama mamako alikuficha kuhusu babako na ulivyomkomalia akakwambia na wewe mwenyewe ukachukua hatua kumfata babako akakutolea nje huoni kama mama yako alikuwa na sababu ya kutokwambia toka mwanzo? Unajuaje kama baba yako alimwambia amkome tangu ukiwa tumboni na ndo maana ulivyomkabili akakutimua? unajitwisha mzigo wa kujionea huruma bure tu eti huna mashangazi sijui ndugu zako ni wachache. Hebu kamuulize prof masalakulangwa pale hubert kairuki anaishije maana yeye aliokotwa akakulia mission - hakuna cha baba, mama wala shangazi. Sijawahi kumhoji lakini huwa nahisi anashukuru kwa yote maana asingetupwa uprofesa wake na baraka zingine alizopewa angezisikia redioni tu. Na sisi wengine tungeikosa huduma yake. Nimesikikitka hata ulivyosema unahangaika upate hela labda babako atakukubali. We kaka wewe! hebu acha kujinyanyapaa bwana. Wasamehe hao wazazi wako, tafuta hela ikusaidie wewe na familia yako. Huna upungufu wowote. Watu tumekulia mazingira kama hayo hayo na tumetoka huko tukiwa washindi. Huku nje ya jf tuna-inspire watu wanaona kuna tumaini kwenye maisha. Haijalishi umetokea wapi. Cha msingi uko hapo ulipo, amua kuishi kwa furaha au kwenye kifungo cha vitimbi vya wazazi. Usijidanganye kuwa ungejikuta ndoani hali ingekuwa tofauti. Kuna wenzio wana baba na mama tena wenye uwezo lakini wameharibikiwa kabisa. Sasa kama mamako aligoma kukwambia kuhusu babako na ulivyomjua babako ukaambulia kutimuliwa, hawa watu wangeoana ungekuwa mtoto wa aina gani? Kawaulize watoto/watu wazima walioishi kwenye paa lenye ndoa aina ya kosovo! Usipoteze muda kwenye kuota maisha uliyotaka yawe. Maisha yashakuleta mpaka hapo chukua hatua kuyaboresha.
Halafu ushauri kuwa wamama/wababa wasizae mtoto zaidi ya mmoja na watu tofauti ni mzuri lakini uzoefu wa aina yako haufanani dunia nzima. Kuna mama namjua ana watoto watatu kila mmoja na babake lakini wanae wanapendana sana na wa kwanza ameshaanza maisha yake ya ndoa, wengine bado wanasoma. Kwa hiyo uzoefu wako si wa wengine.
Halafu naamini kina mama huwa na sababu nzuri tu za kutowaambia watoto kuhusu baba zao mpaka wakati wanapoona mtoto amefikia uwezo wa kuujua ukweli hasa kama ni mzito. Sasa imaggine mamako angekwambia ukiwa mdogo kuwa baba yako alikukataa, si ungeathirika sana? Hapo umemfata babako ukiwa mtu mzima umeishia kulia na kuazimia kutafuta hela ili akukubali. Maadam babako ameshajua kuwa hata we umefata, we muache, endelea na mambo yako. Kwani waliofiwa na baba zao wakiwa tumboni wanaishije? Kwa nini wewe unalikuza sana hili jambo?
Kuna wamama wengine ukiwauliza kuhusu baba unawaumiza tu. Huu mfano ninautoa hapa ni wa kweli, ni wa mtu wa karibu kwangu. Huyu alipewa mimba na baba yake mzazi akiwa na miaka 14. Enzi za zamani na sasa kwa wachache mama akavumilia, mtoto akazaliwa mama akamchukua akamlea kama mtoto wake wa mwisho. Yule mtoto aliyenajisiwa na baba akaondolewa pale nyumbani akaenda kuishi mkoani na ndugu. Yule mtoto aliyezaliwa akawa anamwita mama yake dada, na bibi yake sijui mama mkubwa akawa anamwita mama. Baba tu ndo alipatia. Miaka ikaenda, kwa kuwa lile jambo kimila lilikuwa ni laana, tambiko lilifanyika kwa hiyo kuna wajumbe wa tambiko walishindwa kutunza siri. Kwa hiyo binti akiwa kwenye miaka ya 20 akapata nyuuz kuwa yule mamake si mamake, ila hawakumwambia mama yake ni nani. Mtoto akaenda kuanzisha timbwili nyumbani. Mama wa watu kaishia kupoteza tu fahamu na kulazwa. Ikabidi siri iwekwe hadharani ila wakamsihi binti akienda kwa mama yake mzazi aendelee tu kumwita dada maana ile siri hata mume wa dada yake haijui (wakati huo yule dada-mama alikuwa ameshakaa kwenye zaidi ya miaka 10 na watoto watatu.
Hili jambo lilikuwa zito sana kwa binti. Akaanza kujichukia, akawa kahaba na haikupita miaka mitano akawa ameshaambukizwa VVU akafa. Wakati wa msiba wake ndo shemeji yake ambaye ni babake wa kambo wa kambo anajua ukweli kuwa mkewe alizaa na babake. Ile ndoa mpaka leo ipo inakaribia miaka 30. Nia yangu ni kuonyesha tu kuwa mioyo ya watu ina mengi.