Nilipobold red: Hao friends and family ni watu wako, they have nothing to do na paternity ya mtoto. Woriies zako sio za baba wala mtoto, ni zako, wacha na wao wajitengenezee worries zao.
Nilipobold green, ni kweli kabisa. Lakini hicho hicho unakifanya kwa mwanao na baba mtoto, unataka wao waishi kama wewe ulivyopanga, huwezi jua, labda utawafanya waishie njiani bila hata kujua.
Kulelewa na both parrent in relation to parental love ni A, haki ya mtoto/mzazi kumfahamu mzazi/mtoto ni B, havina uhusiano kabisa. Hata baba atamkataa mtoto, ana haki ya kujua ana mtoto, kadhalika kwa mtoto.
Tabu ya baadhi single parent, hasa akina mama(kama mnavyojiita, though sionagi mantiki ya kujiita hivi) ni kuchanganya emotions za mahusiano na mtoto. Hata kama baba ni jambazi/mwehu/kibaka, as long as ndiye aliyeweka mbegu hiyo, tena ukute si kwa kukubaka, basi ana haki sawa na wewe mama ya kufahamu ana mtoto.
Ila kwa kuwa wanawake tumepewa privilege ya kubeba mimba, basi tunadhani ndio waamuzi wa mwisho kwenye uhuasiano wa baba na mtoto, not right at all.
Ni kweli, i will never understand your position kwa sababu unabaka haki ya mtoto in the name of protection. Protection from what? Ni vitu vingapi unaweza kuviprotect? Kwa nguvu gani uliyonayo? Unaweza mzuia mtu asife/kuugua?
Mfano kesho usikie huyo mzazi mwenzio kafa utajisikiaje (siombei hivyo)? Utasubiri mtoto akue ndio ukamwoneshe kaburi la mzaziwe wakati alikuwa na nafasi ya kukutana naye akiwa hai? Sitaki uweke wazi sababu zako, nakupa tu changamoto ya maamuzi yako kwa sabau sikubaliani nayo kabisaaa.