Single mums and dads come this way

Single mums and dads come this way

Kwangu Mimi ilikuwa bahati mbaya na nilipomtaarifu mhusika alikana. Baadaye alikubali lakini kila nilipotaka kujua jinsi tutakavyojipanga kumlea mwanetu mtarajiwa akawa anakwepa. It really broke my heart since sikuwa nafahamu chochote kuhusu yeye na hata home walikuja kujua nikiwa nimetimiza miez 6. Aisee I went through a lot mpaka najifungua. Hakuwa mtu wa kupiga simu kujua tunaendeleaje na hela ya matumizi mpaka atakapojisikia yeye. Mtoto alikuja kumuona akiwa na mwaka na miezi 6 tena baada ya kusogea karibu....changamoto ni nyingi lakini kubwa kwangu ni pale napoulizwa " mama baba yuko wapi? " au anapochukua simu na kujifanya kama vile anaongea na baba yake akiomba aletewe soseji, pipi, matunda n.k. Huwa naumia sana natamani he was there for her. Sijui kama niko sahihi but nimepanga kwenda nyumbani kwao (baba) at least mtoto awatambue ndugu zake pia kufight 4 the last time mwanangu apate mapenzi ya baba na mama, na kama itashindikana will move on with my life

Pls pls pls, lea mwanao jitahidi kumtimizia kile unachoona unauwezo nacho, usimpeleke popote anayemtaka atamfata, mpe elimu nzuri, matunzo unayoyaweza, atakuelewa taratibu, ila naomba kama hutopata mwenza wa maana usiongeze mtoto mwingine. Nina bint mzuri sana kila ninaposali namueka kwenye dua zangu, nampenda kuliko kingine hapa duniani, amemaliza chuo na sasa baba anamtumia ati visenti vya kujikimu hata sielewi ajikimu nini? bint anasema muda wowote akizihitaji atamrudishia, hajamuomba na wala hana shida nazo. Ukienda kuwaona hao ndugu zake watazidi kukudharau, cha mwisho watakachokuuliza ni kwamba kwani wewe ni wa kwanza kuzaa na kuachiwa mtoto? utajibu nini? Daima Ke ni shujaa, onyesha ushujaa wako kwa kulea mwanao. pika hata pumba atakula atashiba na atakuambia asante mama kwa chakula. hiyo ni zawadi yako toka kwa Muumba haijalishi umempataje.
 
Asante Nyumba Kubwa, watu wachache sana wataweza elewa kwann nilifikia maamuzi haya but it was for the best & i don't need to explain to anyone my reasons for doing so. Naelewa fika kwamba ipo siku kijana wangu atataka kujua ukweli kuhusu babake & i pray that when that time comes i will have the courage to explain to him & hopefully atanielewa.

Mhh. Suppose mungu kakuchukua( we are all candidates of death) kijana akiwa bado mdogo?
 
Miss Kim, Mungu akusaidie sifahamu kwa nn umeamua hivyo ila najua umepita mengi sana Pole, mimi pia nina mdogo wangu aliishi na mwanaume akazaa naye watoto wawili baadaye alimkimbia na akaenda kuoa mwanamke mwingine , alikaa kwa miaka saba ndipo alipokuja kuangalia watoto wake, kiukweli watoto walikuwa hawamfaham baba yao walikuwa wanajua mume wangu mm ndiyo baba yao, na kwa bahati mbaya mdogo wangu alifariki, watoto nalea mpk leo, na hasaidii hata senti tano, Mungu ndiye anajua atamhukumu vipi. So Miss Kim Mungu akubariki na usiache kusali ili utakapokuja kuongea na mwanao akuelewe.
 
Pls pls pls, lea mwanao jitahidi kumtimizia kile unachoona unauwezo nacho, usimpeleke popote anayemtaka atamfata, mpe elimu nzuri, matunzo unayoyaweza, atakuelewa taratibu, ila naomba kama hutopata mwenza wa maana usiongeze mtoto mwingine. Nina bint mzuri sana kila ninaposali namueka kwenye dua zangu, nampenda kuliko kingine hapa duniani, amemaliza chuo na sasa baba anamtumia ati visenti vya kujikimu hata sielewi ajikimu nini? bint anasema muda wowote akizihitaji atamrudishia, hajamuomba na wala hana shida nazo. Ukienda kuwaona hao ndugu zake watazidi kukudharau, cha mwisho watakachokuuliza ni kwamba kwani wewe ni wa kwanza kuzaa na kuachiwa mtoto? utajibu nini? Daima Ke ni shujaa, onyesha ushujaa wako kwa kulea mwanao. pika hata pumba atakula atashiba na atakuambia asante mama kwa chakula. hiyo ni zawadi yako toka kwa Muumba haijalishi umempataje.

Soooooo tauching!!! Unaongea maneno ambayo yananiumiza sana moyo wangu, Duh!! Mungu akubariki na akupe nguvu. Iko siku hayo yote utasahau. Mungu ndiye muweza wa yote. Pole sana.
 
Dubwana liliniachisha masomo niko sekondari akaniacha nina mimba ya miezi mi3 bila mawasiliano bila huduma,alivosikia nina mtoto akapiga simu kutoa jina daniel wakati baba yangu RIP nipo hospitali kaota mtu kaja home nakumwambia mwanao kajifungua mtoto wa kiume akasema basi jina lake ni abdulaziz na anatumia hilo na ubini nimempa jina la kakayangu,mwezi wa 4 alikuja anaejifanya ni baba yake akamuulizia mtoto nikamwambia yuko shule akasema ada ya term hii nitakupa mimi siku imefika nampigia hapokei mara aseme yuko mbali mwisho akaniblock nimemchukulia poa kwakuwa sikumuomba wala sikumuita alijileta, yote mema mwanangu yuko form3,nilimuacha mwanangu anasiku6 nikarudi shule sasa hivi nina kazi namsomesha mwanangu na hamjui baba yake . Nashukuru ananipenda sana msg anazonitumia wakati mwingine nasoma nalia anaijua dini kasoma sana qurani haishi kunisisitiza kumtegemea Mungu.Babayake yuko hapo centre police kama mpelelezi,nipo dar tangu august sijamtafuta hata hamu ya kumuona sina.
 
Nimependa spirit yako...
Hukukata tamaa na kulaani...
Hukuchukia wanaume wote...
Na Mungu amekusikia; ni vema kutoacha our past mistakes kutuamulia future...
Kila kitu kinawezekana..
Ni attitude tu...

asante
whatever happens it has reasons
in life there is always second chance
na tunajifunza kutokana na makosa
 
Hakuna mtu anayemwelewa single parent isipokuwa single parent mwenyewe, kudos kwa wababa au wamama wanaolea watoto kama single parent. Mungu awaongezee hekima, nguvu na uwezo wa kukabiliana na majukumu. Siku zote kumbuka kumlea mtoto bila kumwonyesha mabaya ya mzazi mwenzako, usimuingize mtoto kwenye kesi zako na kumjenga akue na chuki moyoni. Mwache mpaka atakapofika umri wa kuelewa (miaka 18), utamuelewesha kwa hekima.
I salute you single parents. geniveros, devota vijance, charminglady, Zamda Geuka, Miss Kim

Thanks much for your appreciation, for sure hata sielewi nawezaje kumlea pekeyangu. Mtu akiniuliza kiukweli hataamini na kunielewa. Ila kwa Kudra za Mwenyezi Mungu tunaishi tena maisha mazuri tu ambayo hatukosi basic needs...
 
Last edited by a moderator:
Freedom of expression and i believe that you are both entitled to it, so nyie ongeeni tu coz mnatumia sheria zilizotungwa na binadamu kuwahumu wenzenu. You will never understand my position and it is not in my place to make you guys comprehend my situation. Cha msingi ni kwamba the people i call friends & family walinielewa toka mwanzo na walieshimu maamuzi yangu juu ya maisha ya mwanangu. Ukitaka kila mtu aishi kama watu wengine waishivyo wapo watakao ishia njiani. Wapo wanaolelewa na both parents but they have never known the true meaning of parental love. Proudly single parent!

Ubinafsi....
Dhuluma...ni kinyume na haki za binadamu....
Huyu mtoto will never be at peace maisha yake yote....hata akiweza kufanikiwa kimaisha....atabaki na pengo ulilomwekea kwa makusudi....

Kongosho umemaliza....
Malezi sio uwezo wa kiuchumi pekee....
 
I am not worried about his future coz if you are a christian the bible says in Jeremiah 29:11 "For I know the plans I have for you," declares the Lord, "plans to prosper you and not to harm you, plans to give you hope and a future."

My boy's future is secure with or without me.

Mhh. Suppose mungu kakuchukua( we are all candidates of death) kijana akiwa bado mdogo?
 
Najaribu kukueleza ukweli tu...
Mimi ni nimelelewa na single parent (mama)....najua...naelewa!!!
Ninajua hisia za mtoto kwa mzazi....najua!!!
Sio ishu ya uhuru wa kuongea wala nini....ishu ni kwamba umepora haki za watu wawili ukajimilikisha....kwa sababu unazoona wewe ni nzuri! Yawezekana ulichojenga kwa miaka 20 kikaja kumwagika siku moja tu...unaamini dogo atakuja kukulewa...labda ataelewa...or may be not!

Sipingi wala kukukatisha tamaa kuwa single parent....it takes a lot!

Freedom of expression and i believe that you are both entitled to it, so nyie ongeeni tu coz mnatumia sheria zilizotungwa na binadamu kuwahumu wenzenu. You will never understand my position and it is not in my place to make you guys comprehend my situation. Cha msingi ni kwamba the people i call friends & family walinielewa toka mwanzo na walieshimu maamuzi yangu juu ya maisha ya mwanangu. Ukitaka kila mtu aishi kama watu wengine waishivyo wapo watakao ishia njiani. Wapo wanaolelewa na both parents but they have never known the true meaning of parental love. Proudly single parent!
 
Dubwana liliniachisha masomo niko sekondari akaniacha nina mimba ya miezi mi3 bila mawasiliano bila huduma,alivosikia nina mtoto akapiga simu kutoa jina daniel wakati baba yangu nipo hospitali kaota mtu kaja home na mwanao kajifungua mtoto wa kiume akasema basi jina lake ni abdulaziz na anatumia hilo na ubini nimempa jina la kakayangu,mwezi wa 4 alikuja anaejifanya ni baba yake akamuulizia mtoto nikamwambia yuko shule akasema ada ya term hii nitakupa mimi siku imefika nampigia hapokei mara aseme yuko mbali mwisho akaniblock, yote mema mwanangu yuko form3,nilimuacha anasiku6 nikarudi shule sasa hivi nina kazi namsomesha mwanangu na hamjui baba yake . Nashukuru ananipenda sana msg anazonitumia wakati mwingine nasoma nalia.Babayake yuko hapo centre police kama mpelelezi,nipo dar tangu august sijamtafuta hata hamu ya kumuona sina.

pole sana aisee kuna wanaume mbwa kabisa
mi nashukuru kwa kweli nilikua naingia wa tatu chuo
yaani mi nna mimba na mwingine akadai ana mimba yule binti akajipeleka kwao mkaka fasta dada
ukabila ukatake place akaoa msichana akadanganya ana mimba ya miezi mitano walivyooana tu mwezi febr. aprli kajifungua mtoto mhindi pure akaua mtoto yule dada ndoa ina migogoro mpaka bas
anabaki na majuto tuu
 
Nilipobold red: Hao friends and family ni watu wako, they have nothing to do na paternity ya mtoto. Woriies zako sio za baba wala mtoto, ni zako, wacha na wao wajitengenezee worries zao.

Nilipobold green, ni kweli kabisa. Lakini hicho hicho unakifanya kwa mwanao na baba mtoto, unataka wao waishi kama wewe ulivyopanga, huwezi jua, labda utawafanya waishie njiani bila hata kujua.

Kulelewa na both parrent in relation to parental love ni A, haki ya mtoto/mzazi kumfahamu mzazi/mtoto ni B, havina uhusiano kabisa. Hata baba atamkataa mtoto, ana haki ya kujua ana mtoto, kadhalika kwa mtoto.

Tabu ya baadhi single parent, hasa akina mama(kama mnavyojiita, though sionagi mantiki ya kujiita hivi) ni kuchanganya emotions za mahusiano na mtoto. Hata kama baba ni jambazi/mwehu/kibaka, as long as ndiye aliyeweka mbegu hiyo, tena ukute si kwa kukubaka, basi ana haki sawa na wewe mama ya kufahamu ana mtoto.

Ila kwa kuwa wanawake tumepewa privilege ya kubeba mimba, basi tunadhani ndio waamuzi wa mwisho kwenye uhuasiano wa baba na mtoto, not right at all.

Ni kweli, i will never understand your position kwa sababu unabaka haki ya mtoto in the name of protection. Protection from what? Ni vitu vingapi unaweza kuviprotect? Kwa nguvu gani uliyonayo? Unaweza mzuia mtu asife/kuugua?

Mfano kesho usikie huyo mzazi mwenzio kafa utajisikiaje (siombei hivyo)? Utasubiri mtoto akue ndio ukamwoneshe kaburi la mzaziwe wakati alikuwa na nafasi ya kukutana naye akiwa hai? Sitaki uweke wazi sababu zako, nakupa tu changamoto ya maamuzi yako kwa sabau sikubaliani nayo kabisaaa.

Freedom of expression and i believe that you are both entitled to it, so nyie ongeeni tu coz mnatumia sheria zilizotungwa na binadamu kuwahumu wenzenu. You will never understand my position and it is not in my place to make you guys comprehend my situation. Cha msingi ni kwamba the people i call friends & family walinielewa toka mwanzo na walieshimu maamuzi yangu juu ya maisha ya mwanangu. Ukitaka kila mtu aishi kama watu wengine waishivyo wapo watakao ishia njiani. Wapo wanaolelewa na both parents but they have never known the true meaning of parental love. Proudly single parent!
 
pole sana aisee kuna wanaume mbwa kabisa
mi nashukuru kwa kweli nilikua naingia wa tatu chuo
yaani mi nna mimba na mwingine akadai ana mimba yule binti akajipeleka kwao mkaka fasta dada
ukabila ukatake place akaoa msichana akadanganya ana mimba ya miezi mitano walivyooana tu mwezi febr. aprli kajifungua mtoto mhindi pure akaua mtoto yule dada ndoa ina migogoro mpaka bas
anabaki na majuto tuu

Dah.wanaume achana nao kabisa.
 
Halafu hajajua tu, marginal utility is real.

The more unamnyima mtoto nafasi ya kuonana na baba yake, the more anakuwa troubled na kutaka kumjua. Lakini akishamjua na kumuona ni mtu wa kawaida, wala anaweza asiwe na habari naye, hasa watoto wa kiume.

Mtoto kuja kuelewa baada ya miaka 20 ni A, lakini memmory uliyompokonya ya utoto wake ni B.

Nikupe mfano: Mwanamme mtu mzima kanywa viagra akitegemea mpenzi wake anakuja. For some reason mpenzi hajaja, viagra imefanya kazi haswaaa. Yule mtu anazidiwa, anatoka nje na kukuta binti wa miaka 18, bikra, anaamua kumbaka ili kujinusuru na kweli yule baba anapona. Familia ya binti inagundua kitendo hicho, inamuuliza mwanamme, anakubali kuwajibika kwa kumuoa na binti anaridhia kuolewa.

Je hiyo ni justification ya binti kubakwa? Kovu la kihisia/saikolojia litapona? Utajuaje limepona na halijaathiri maisha ya binti ya kimapenzi?

Kuna mambo hayana majibu marahisi, let nature take care of its course. Ulinzi wa binadamu una limitation, kuna vitu viko nje ya uwezo wetu kabisa.

Najaribu kukueleza ukweli tu...
Mimi ni nimelelewa na single parent (mama)....najua...naelewa!!!
Ninajua hisia za mtoto kwa mzazi....najua!!!
Sio ishu ya uhuru wa kuongea wala nini....ishu ni kwamba umepora haki za watu wawili ukajimilikisha....kwa sababu unazoona wewe ni nzuri! Yawezekana ulichojenga kwa miaka 20 kikaja kumwagika siku moja tu...unaamini dogo atakuja kukulewa...labda ataelewa...or may be not!

Sipingi wala kukukatisha tamaa kuwa single parent....it takes a lot!
 
  • Thanks
Reactions: RR
I rest my case, some battles are best fought in silence. And just so you know my decision was never based on emotions, it was a well thought decision which has worked out for the best of everyone. Nikutakie siku njema mpendwa.

Nilipobold red: Hao friends and family ni watu wako, they have nothing to do na paternity ya mtoto. Woriies zako sio za baba wala mtoto, ni zako, wacha na wao wajitengenezee worries zao.

Nilipobold green, ni kweli kabisa. Lakini hicho hicho unakifanya kwa mwanao na baba mtoto, unataka wao waishi kama wewe ulivyopanga, huwezi jua, labda utawafanya waishie njiani bila hata kujua.

Kulelewa na both parrent in relation to parental love ni A, haki ya mtoto/mzazi kumfahamu mzazi/mtoto ni B, havina uhusiano kabisa. Hata baba atamkataa mtoto, ana haki ya kujua ana mtoto, kadhalika kwa mtoto.

Tabu ya baadhi single parent, hasa akina mama(kama mnavyojiita, though sionagi mantiki ya kujiita hivi) ni kuchanganya emotions za mahusiano na mtoto. Hata kama baba ni jambazi/mwehu/kibaka, as long as ndiye aliyeweka mbegu hiyo, tena ukute si kwa kukubaka, basi ana haki sawa na wewe mama ya kufahamu ana mtoto.

Ila kwa kuwa wanawake tumepewa privilege ya kubeba mimba, basi tunadhani ndio waamuzi wa mwisho kwenye uhuasiano wa baba na mtoto, not right at all.

Ni kweli, i will never understand your position kwa sababu unabaka haki ya mtoto in the name of protection. Protection from what? Ni vitu vingapi unaweza kuviprotect? Kwa nguvu gani uliyonayo? Unaweza mzuia mtu asife/kuugua?

Mfano kesho usikie huyo mzazi mwenzio kafa utajisikiaje (siombei hivyo)? Utasubiri mtoto akue ndio ukamwoneshe kaburi la mzaziwe wakati alikuwa na nafasi ya kukutana naye akiwa hai? Sitaki uweke wazi sababu zako, nakupa tu changamoto ya maamuzi yako kwa sabau sikubaliani nayo kabisaaa.
 
Anyway, kila mtu ana maamuzi yake, lakini ulitakiwa kuwashirikisha baba na mtoto pia nao wapime kama kufahamiana kwao kutawadhuru, ni haki ya msingi ya binadamu. Kumbuka hakuna mtu anaweza kujipa mimba mwenyewe, kama huwezi hili then why hili jingine unadhani unaweza?

Cheers!

I rest my case, some battles are best fought in silence. And just so you know my decision was never based on emotions, it was a well thought decision which has worked out for the best of everyone. Nikutakie siku njema mpendwa.
 
Miss Kim, sababu za kutomshirikisha mzazi mwenzio zaweza kuwa na mantiki sana kwako, lakini zisiwe na mantiki yeyote kwa mtoto na babake.

Wewe ni nani hadi uwaamulie muda wa kufahamiana? You are not God, kusema unapanga kila kitu.

Juzi nasoma mambo ya haki za watoto, ni pamoja na kuwafahamu wazazi wake wa asili, hata kama wewe ni mama yake, bado huna haki ya kumfanya mtoto asijuane na baba yake.

We mwache itokee bahati mbaya akatangulia kufa ilhali mtoto na baba hawajuani. Atatuongezea idadi ya machokoraa mtaani.

Kutomwonyesha mtoto baba yake ni ushetani uliopitiliza.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom